#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ameshangaa serikali kusema chanjo ya corona itakuwa ya hiari na amemtaka rais Samia kutangaza chanjo hiyo kuwa ya lazima na kila mtu lazima achanjwe.

My take.
Mwendazake Charles Mbowe hakuchanjwa?
Rwanda walikochanjwa mwazoni kabisa mwa mwaka 2020 chanjo zao zimewasaidia nini ? Mbona Rwanda wametangaza lockdown tena?
Mbowe hajifunzi kitu hapo?

Screenshot_20210719-154932_millardayo.jpg
 
Na huo ndio ukweli!!

Mzazi gani hua anaulizwa kama mtoto achomwe chanjo ya surua/ pepopunda??!

Huu ugonjwa haujapata kiongozi serious wa kushughulika nao hapa Tanzania. Kama alivokua Mwendasake...huyu nae kaja na maneno kibwena!
 
Chanjo gani ?

Pfzier maybe...

Hizi nyingine sina Imani nazo..... Nadhani tunataka Chanjo Bora na sio Bora Chanjo.
 
Lazima kivipi yaani?

Ulazima wa chanjo utasababisha Wananchi kuichukia Serikali yao.

Suala la Afya ya mtu sio Mali ya wanasiasa ni hiyari ya mtu kuamua.

Kama ambavyo suala la Katiba Mpya kuwa ni Mali ya Wananchi ndivyo ilivyo kwa chanjo ya Uviko.

Kuna mahala ifike wakati tuwaachie Wananchi wenyewe waamue ama kupitia maoni yao au iitishwe kura ya maoni kabla ya wanasiasa kushinikiza baadhi ya Agenda zao bila kupata ridhaa ya watu.
 
Mbowe anakwenda kubaya kabisa ama labda akili zake zimebadilishwa na chanjo aliyochomwa kule Dubai

Hapa amebakiza kusema " ndoa za jinsia moja ziwe za lazima kwa kila ukoo wa wamachame"
 
Ya kuwadunga mambumbu
Peleka ujinga wako Lumumba. Kama serikali haijui nini cha kufanya ifunge domo kuliko kuagiza kitu isichojua umuhimu wake. Na mbumbumbu wa dizaini yako ndio mliotufikisha hapa kwa kugawia Lijiwe mitano tena
 
Hivi Tanzania tunafuata United Nation Human rights?

Human rights are rights inherent to all human beings, regardless of race, sex, nationality, ethnicity, language, religion, or any other status.

Human rights include the right to life and liberty, freedom from slavery and torture, freedom of opinion and expression, the right to work and education, and many more.
 
Mzee Mbowe pumzika ubaki mshauri wa chama, CHADEMA ina hazina ya damu changa wenye akili nyingi sana tu wakipewa nafasi. Nchi ngapi duniani zimefanya chanjo ya COVID iwe lazima?
 
Mbowe huenda ana nia nzuri lakini bahati mbaya sio watu wote wana mtazamo sawa juu ya Covid-19 achia tu hizo chanjo zake...
 
Back
Top Bottom