Wakati ule upinzani unaanza kuchipukia ktk miaka ile ya 1990's nakumbuka Baba wa Taifa alitoa kauli kuwa hawezi kukubali nchi ikaangukia mikononi mwa MBWA. Lakini kwa mazingira tuliyopo hivi sasa nafikiri imefika wakati wa kutokukubali tena nchi yetu iwe mikononi mwa FISI.
Nahisi hii ingalikuwa ni kauli thabiti kutoka mdomoni mwa Baba wa Taifa ktk mazingira ya kisiasa ya sasa, ijapokuwa mjane wake kahongwa kwa tausi 25, pasipo kuzingatia misimamo yake wala umri wa mjane aliokuwa nao hivi sasa. Na hata pia umuhimu wa hao tausi ktk maisha yake ya sasa ya uzee wake.