PreGE2025 CHADEMA haitoweza kushiriki uchaguzi ndani ya miaka mitano ikiwemo wa mwaka huu

PreGE2025 CHADEMA haitoweza kushiriki uchaguzi ndani ya miaka mitano ikiwemo wa mwaka huu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Vyama vyote 18 vilosaini huu utopolo wamehongwa hela na CCM yenyewe ili wasaini maana wanajua ni CCM "B" au Mamluki wa CCM na hawataweza kushinda Uchaguzi hata mara 1. Kiufupi hao ni wasindikizaji na vibaraka wa CCM tu!!!
😂😂😂😂😂😂
 
Toka lini Tanzania imewahi kuwa na uchaguzi?....
Kailima anachekesha sana....aamke dunia imebadilika sana....alafu uzuri hapo alipo alikuwepo mtu na baada yake atakuja mtu..maisha yataendelea tu...
 

Attachments

  • VID-20250413-WA0002.mp4
    19.4 MB
Mwaka huu, Raisi atakuwa mwanaume
Naona mama ana weweseka! Tùnajua aliingia kwa mlango wa nyuma pale mtangulizi wake ku-rest in peace baada ya dhuluma kubwa ya uonevu, ukandamizaji na dhuluma kwa Wapinzani. Sasa ameona ubavu wa kupambana na kina Lissu na Heche hana! Solution ni KUWAMBIKIA VIONGOZI WA CHADEMA KESI ZA UHAINI NA KUWAFUTA WASIGOMBEE KUPITIA TUME YA CCM YA UCHAGUZI....!!!
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.

Kanuni hizo zinasainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na (INEC) jijini Dodoma. “Chama cha Chadema ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025, hakitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.” amesema Kailima. Awali, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika alisema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda kusaini kanuni hizo.

Mnyika kupitia mtandao wa kijamii wa X na baadaye katika mazungumzo kwa simu na Mwananchi leo Aprili 12, 2025 amesema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda Dodoma kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Alipoulizwa ni kwa nini hajateua mwakilishi Mnyika amesema: “Ni vyema mkaandika kwamba sijakwenda wala sijateua mtu. Habari kubwa sasa hivi ni katibu mkuu, sitakwenda kusaini wala sijateua mtu." Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU,UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi,

Tangu 2020, hawajashiriki uchaguzi na bado wapo. Maza akishapata kile snachokitafuta kwa udi na uvumba atakuja na mazungumzo. Atawatafuta yeye mwenyewe.

Chadema na CCM ni kama Simba na Yanga kwenye mpira. CCM wasifikiti kuwa Chadema itakufa au kupotea kama vile NCCR, CUF au TLP.
 
Huu uchafuzi tunaoita uchaguzi ni Bora kabisa kutokushiriki hizi comedy za Tume ya CCM ya uchaguzi, kama uchaguzi tu wa serikali za mitaa wameharibu na kuuchafua kiasi kile sembuse uchaguzi Mkuu? Bila mageuzi huu uchaguzi ni batili
 
Vyama vyote 18 vilosaini huu utopolo wamehongwa hela na CCM yenyewe ili wasaini maana wanajua ni CCM "B" au Mamluki wa CCM na hawataweza kushinda Uchaguzi hata mara 1. Kiufupi hao ni wasindikizaji na vibaraka wa CCM tu!!!
Ila ACT wanashangaza Sana.
Wamesaini, halafu nao wanalaani kukamatwa kwa Lissu.
ACT ni wanafiki sana.
 
Mkurugenzi katoa BOKO, atuombe radhi watanzania.
 
May be an image of 1 person and text that says 'eastafrica fri RADIO HABARI CHADEMA YAKOSA SIFA KUSHIRIKI UCHAGUZI f EastAfricaTV/EastAfricaRadio'

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.
Kanuni hizo zinasainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na (INEC) jijini Dodoma.
Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU,UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK, UDP. chanzo:EastAfricaTV
 
Na ndiyo maana watu wanataka mabadilko ya kweli. Kuweka sheria za kipuuzi kwa lengo tu la kulinda maslahi yako, badala ya maslahi ya wengi; ni ubinafsi wa kijinga.
Sheria gani CHADEMA mnataka iwe upande wenu? Ilo litakua Taifa la hovuo sana kua wanapitisha sheria kisa kundi flani linatanufaika
 
Back
Top Bottom