PreGE2025 CHADEMA haitoweza kushiriki uchaguzi ndani ya miaka mitano ikiwemo wa mwaka huu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sasa ina maana hawana tena hoja? Watafanya nini? Walitaka kugombea ubunge na udiwani wamekosa mwana na maji ya moto.

View attachment 3301525
Sasa kunachaguzi tena hapo.si watangaze tu mshindi.Wampe chauma viti viwili Cuf vitatu ACt vitano Updp wawape madiwani watoni mchezo uishe hamna haja yakuharibu pesa za Watazania.Nadhani hakuna Chama Ambacho kitakataa kwa mgawanyo huo.
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.

Kanuni hizo zinasainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na (INEC) jijini Dodoma. “Chama cha Chadema ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025, hakitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.” amesema Kailima. Awali, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika alisema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda kusaini kanuni hizo.

Mnyika kupitia mtandao wa kijamii wa X na baadaye katika mazungumzo kwa simu na Mwananchi leo Aprili 12, 2025 amesema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda Dodoma kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Alipoulizwa ni kwa nini hajateua mwakilishi Mnyika amesema: “Ni vyema mkaandika kwamba sijakwenda wala sijateua mtu. Habari kubwa sasa hivi ni katibu mkuu, sitakwenda kusaini wala sijateua mtu." Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU,UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK, UDP.
View attachment 3301510
Huo ndio ukweli,
na hivyo ndivyo kanuni na sheria za uchaguzi zinavyosema gentleman, na sio muujiza :pedroP:
 
NI KHERI KULIKO NDUGU ZETU KWENDA KUULIWA MAPORINI.

Thread 'DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!' Pre GE2025 - DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!
 
Ndo mana mie kuna muda naphtali shida sana kuwaamini Waislam. Ukimwona Kailima anavyoswali alafu ukiangalia anavyoshiriki kufanya huu upuuzi unasema tu hakuna dini pale.
Mambo ya kailima muhukumu yeye sio dini yake.tumia jukwaa vizuri comrade.
 
Sipigi kura rais anajulikana, hamna haja ya kufanya kampeni Wala kutumia gharama za kijinga kisa uchaguzi pesa zote waelekeze kwenye mambo ya msingi, maana wameshajiteua na rais anajulikana hivyo hamna haja ya uchaguzi
Kale kasungura kadogo lazima wakagawane kwa hiyo maigizo ya hako kasungura kuruka ruka lazima yafanyike
 
Afadhali Mwaka huu hakuna watu kuuawa na kujeruiwa na kupewa kesi za kisiasa hii ni kwa upande wa Tanzania bara

Huko visiwani mwendo utakua ni uleule Jusa anaujua
 
Mimi sijaelewa kabisaaa .ina Maana chadema ndiyo chama pekee chenye akili kuwazidi vyame vingine 22?

Kuna mambo mengine ya kistajabisha kwa kweli!!

Unasema unahamasisha uasi??? Hivi hamna lugha nyengine ya kutumia zaidi ya Hiyo? Mfano : unahamasisha maamdamano,mabadiriko,fujo,etc!! Neno uasi ni neno baya!! Shetani alihamasisha uasi mbinguni akaishia kuangushwa Duniani pamoja na Wale malaika mataila waliyomsikiliza!!
Mbona Mwl Nyerere alilitamka na halikuchukuliwa unavyofikiria? Bullshit
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.

Kanuni hizo zinasainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na (INEC) jijini Dodoma. “Chama cha Chadema ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025, hakitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.” amesema Kailima. Awali, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika alisema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda kusaini kanuni hizo.

Mnyika kupitia mtandao wa kijamii wa X na baadaye katika mazungumzo kwa simu na Mwananchi leo Aprili 12, 2025 amesema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda Dodoma kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Alipoulizwa ni kwa nini hajateua mwakilishi Mnyika amesema: “Ni vyema mkaandika kwamba sijakwenda wala sijateua mtu. Habari kubwa sasa hivi ni katibu mkuu, sitakwenda kusaini wala sijateua mtu." Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU,UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK, UDP.
View attachment 3301510
Zamani niliamini muislamu safi ni yule mwenye sijda usoni. Siku hizi nimegundua hata kuhiji wanaenda kina mwijaku
 
Back
Top Bottom