PreGE2025 CHADEMA haitoweza kushiriki uchaguzi ndani ya miaka mitano ikiwemo wa mwaka huu

PreGE2025 CHADEMA haitoweza kushiriki uchaguzi ndani ya miaka mitano ikiwemo wa mwaka huu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
JPM alisingiziwa mabaya mengi sana
20250408_000956.jpg
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.

Kanuni hizo zinasainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na (INEC) jijini Dodoma. “Chama cha Chadema ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025, hakitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.” amesema Kailima. Awali, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika alisema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda kusaini kanuni hizo.

Mnyika kupitia mtandao wa kijamii wa X na baadaye katika mazungumzo kwa simu na Mwananchi leo Aprili 12, 2025 amesema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda Dodoma kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Alipoulizwa ni kwa nini hajateua mwakilishi Mnyika amesema: “Ni vyema mkaandika kwamba sijakwenda wala sijateua mtu. Habari kubwa sasa hivi ni katibu mkuu, sitakwenda kusaini wala sijateua mtu." Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU,UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK, UDP.
View attachment 3301510
Mpumbavu sana huyu.
Laiti angejua anayopanga Mungu wetu asingeropoka haya.
Sisi tunaipenda Tanzania kuliko kitu chochote kile ikiwemo vyama vya siasa.
 
Kwani sini ni sheria ilivyo mkuu,mnataka kuishi kwenye nchi isiyokua na sheria eti.HAPANA
Na ndiyo maana watu wanataka mabadilko ya kweli. Kuweka sheria za kipuuzi kwa lengo tu la kulinda maslahi yako, badala ya maslahi ya wengi; ni ubinafsi wa kijinga.
 
Hichi kipengele cha kusaini kilikuwepo miaka yote?
 
Wewe ebu twambie mtaishije bhasi?
Kivipi? Kwani ni lazima chadema ishiriki uchaguzi ndo ukubarike kimataif a?Kuna vyama 23 vimesaini.sijajua ni taasisi Gani Ina uhalali wa kuitetea chadema kama taasisi hiyo ni ya haki?
 
Mimi kuna saa huwa siwaelewi Chadema. Kuacha kushiriki leo ni kosa sana. Walitakiwa washiriki halafi waendelee na kampeni ya NO REFORMS NO ELECTION.
Huenda inge leta pressure kwa wezi wa kura. Sasa wamejtoa Ccm wame baki burudani
Kujitoa ndo vyema, nchi wameivua nguo kimataifa , kumbuka cdm ndo chama kikuu cha upinzani, kugomea uchaguzi sio sura nzuri hasa dunian huko tunakojinasibu tuna democrasia, kushiriki uchaguz inamaana tunakubali mambo yako shwari ! Ngoja misaada ianze kukata !
 
Na sigda (sajda) anayo kabisa.....Mungu wetu ana huruma sana
Watu kama Tundu Lissu hawapaswi kuwa kwenye ngazi ya maamuzi ya mwisho ya kitu chochote. Ni watu wa kutumwa tu au kuchambua mambo/issues
 
Kwa mantiki hiyo kufanya kampeni na uchaguzi nikuchezea rasilimali za watanzania
Kailima ateue jina moja kwa nafasi ya Rais Ili kuokoa muda na fedha
 
Waliosema mama 2025 hatapita wako wapi?
 
Back
Top Bottom