CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

Kwanza mimi sio mwanachama wa CHADEMA. Kanuni za uchambuzi, hasa inapokuja suala la prediction, mchambuzi anatakiwa aseme maneno ambayo mtu mwengine anaweza kusema hapana, yaani falsification. Hili umepatia. Lkn prediction hiyo lazima itokane na masuala ya kweli (real/true). Kwa bahati mbaya hapa siku zote huwa unakosea. Inakuwa vigumu mtu kukuelewa na hoja zako kwa mazingira ya sasa ya kisiasa. Hebu jitahidi unapofanya uchambuzi uwe sober na impartial. Inapendeza mtu anaposoma uchambuzi ambao umefuata kanuni; vinginevyo unakuwa chapwa.
Z
 
Mimi nasema ukweli wote toka moyoni. NAKUUNGA MKONO PASCO! Upinzani umenichosha kabisa sasa. Kila siku sisi tu ndo tunategwa na kuingia mtogoni kama MAZUZU! ccm ina strong system na kama tunataka kuwaondoa lazima kwanza tukubali hilo, kisha tuwena mikakati madhubuti yenye uhalisia kuwakabili. Ninaanza kuwa na mashaka na uhalisia wa real identity ya viongozi wa upinzani. Je! Nikweli hawa ni wapinzani au wako kwenye mission ya kukamata tu watu akili ili mambo yaende?????? Le me stop here!
 
Anzisha Chama ukajipange uwe mfano kwa Chadema...
 
Kupambana na ccm au police?

Ikiwa nikupambana wapambane na nani?
 
Toa suggestion
 
Mkuu Zawadin, kuna tofauti kati ya mtafiti, mchambuzi na mtazamaji.
Mtafiti ni researcher, huyu ndiye anatakiwa kufanya utafiti wa kisayansi, research na ndie anayetakiwa kutumia kanuni za scientific research zikiwemo
plausible major and minor to reach a logical conclusion that can be based on a well founded "major and minor". Mimi sio mtafiti.

Mchambuzi ni mtu yoyote mbobezi kwenye neno husika hivyo anafanya uchambuzi wa kisomi na ki weledi kutokana na elimu na long experience ya uzoefu wa muda mrefu. Mimi sio mchambuzi.

Mimi ni mtazamaji tuu wa hii game of politics na kuripoti kile ninachokiona, hivyo sifanyi predictions bali natoa trends za kile ninachokiona kufuatia observation yangu kwenye issue husika.

Hii issue niliyoizungumza humu ni ukweli mtupu, nothing but the truth with objectivity, impartiality na balance. Siegemei upande wowote.
P
 
Najionea porojo tu ungekuja na hiyo namna ya kujipanga ningekuelewa otherwise naona unafiki tu na kujikosha..
Angalia tumewashauri nini Chadema since time immemorial soma tarehe ya bandiko uangalie tulishauri nini


P
 
Hii issue niliyoizungumza humu ni ukweli mtupu, nothing but the truth with objectivity, impartiality na balance. Siegemei upande wowote.
Hapa ndio nilipopasemea. Unaposema ni ukweli unatakiwa uwe mkweli. Hivi katika mazingira ya siasa za leo unaweza kusema chama cha upinzani hakijajipanga wakati hakuna mazingira wezeshi ya kufanya hivyo? Mkuu hivi sasa vyama vya upinzani, kwa mawazo yako, vinawezaje kujipanga wakati vimefungwa miguu na mikono? Sitarajii katika siasa za kistaarabu vyama vianzishe vurugu. Kama hiyo si njia sahihi, na kwa sasa labda wafanye hivyo, basi havina namna ya kujipanga; na kwa hili hawastahili lawama.
 
Mayalla ndo shida ya humu JF wadau wanafurai kuitukana Serikali tu lakini ukiandika ukweli kuhusu mapungufu ya Upinzani basi ni kuambulia matusi tu,Upinzani Nchini bado upo kwenye mkwamo wa masafa marefu
 
Wew na Mayalla sijui malaya P mlitakiwa muwepo siku ile pale msamvu Dadeek yaani
 
Moja kati ya matatizo yetu watanzania ni kuongea nje ya uhalisia wa maisha yetu ya kila siku
Nyie kwenye tasnia yenu muko huru mumejipangaje? kama sio kuacha kujiingiza kwenye vile ambavyo mtawala hapendi kusikia... Leo unataka vyama vya upinzani vijipange... Na wao wameamua kuwaiga nyie wa tasnia ya Habari kuachana na kile mtawala hapendi.... Watawala Wamekata majina, yaliobakia upinzani umeamua kuyaondoa yote isiwe tabu

CCM OYEEE
 
Hakuna kitu ambacho hawakukijua.

Trends zote tumewawekea humu tangu awamu ya 5 inaingia madarakani.


Hiki kinachoendelea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ni cha mtoto, funga kazi ni uchaguzi Mkuu wa 2020

P
 
unashauri tupigane ?
 
mayala mbona umebadilika sana baada ya kuitwa bungeni?
Unaweza kukumbuka niliitwa lini Bungeni na ukalinganisha na hoja za bandiko hili?.
Kwa kukusaidia tuu, bandiko hili ni la mwezi Machi 2014 nikiizungumzia jinsi ambavyo Chadema haijajipanga kwa Uchanguzi wa serikali za mitaa ile
2014 na uchaguzi mkuu wa 2015.

Niliitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge, April 1918, miaka 4 baada ya bandiko hili.

Hoja zangu katika bandiko hili bado ni zile zile, Chadema haikujiandaa ipasavyo kwa Uchanguzi wa Serikali za Mitaa, Chadema haijajiandaa kwa succession plan ya uchaguzi wake wa ndani, at the same time Chadema ilipaswa kujiandaa kwa Uchanguzi Mkuu wa 2020 kwa head hunting able candidates, the time is just too little too late.

Matokeo it's going to loose big time.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…