CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

Kumbe wewe hunijui?!. Basi kwako na wengine wasionijua, mimi ndiye ninayetoa fedha zangu mfukoni, kuigharimia Chadema kujiendesha!, hivyo nina mamlaka yote 100% kujua kila kitu Chadema inachofanya!.

Pasco
Pasco katika ubora wake
 
Last edited by a moderator:
Nafanya Rejea kwa seke seke ya CUF,jee Chadema wako imara? . Kwa 2015 Chadema hawakujipanga, jee kwa 2020 watajipanga? .
Paskali
 
Nafanya Rejea kwa seke seke ya CUF,jee Chadema wako imara? . Kwa 2015 Chadema hawakujipanga, jee kwa 2020 watajipanga? .
Paskali
Wenda wanasubiri uchaguzi wa mihemko tena Mkuu.


Kumchagua mtu kwa kumwelewa nini anakuletea na kumchagua mtu kimihemko vitu tofauti.
 
binadamu wameubwa na kuchwa kwa ajili ya kuweka nywele tu wakati wengine nywele si mhimu sana ila kwenye kichwa kuna ubongo ambao unahifadhi kumbukumbu na kujua mazuri na mabaya,hv ww kama una akili timamu kichwani mwako unaweza kusema kauli kama hiyo kuwa chadema hawajajipanga kwa uchaguzi ina maana kama siasa zinafanywa za upande mmoja upande wa pili wasubili hadi wakati wa uchaguzi hiyo kweli inaingia akilini!kwa kauli yako hiyo ruhusu kila mwezi ruhusu siku moja tu wao wafanye kila cku uone mziki wake!yaani kama lowassa apite tu bila kuongea kitu utaona mafuriko!uoga umewazidi igeni mfano kwa musure mzee wa msoga!
 
Nafuatilia kwa karibu, hii movement ya viongozi wa Chadema huhamia CCM, kama ina uhusiano wowote na Chadema kutokujipanga.

P.
 
CHADEMA wanapitia wakati magumu sana.

Tusubiri tuone wataibuka namna gani, maana wanajificha sana kwenye neno "USALITI" na "WASALITI"
 
Mkuu 50thebe, ni kweli Chadema inapitia wakati mgumu kabisa kuliko kipindi kingine chochote.

Paskali

Hakika

CHADEMA kama taasisi, wanachama, wapenzi, viongozi na hata waandamizi wake sidhani kama walipata kufikiri kuwa wangepitia hatua wanazopitia wakati huu.

Jambo la kustaajabisha, tena la kustaajabisha zaidi ni namna wana CHADEMA wanavyoelekeza shutuma na lawama zao kwa Mwenyekiti wa CCM Mh Magufuli. Maajabu kabisa. Ndugu zetu hawa hawaoni kabisa kwamba wao ndio waasisi wa anguko lao wenyewe.

Mkuu paskal Mayalla wewe ni shahidi. Hapa nchini mwetu vyama vya upinzani havijawahi kupata wepesi wa kukabiliana na CCM. Wakili Lamwai na wenzake walikuwa karibu waiangushe CCM mwaka 1995/96 wakiongozwa na Mh Mrema. Tuliona namna NCCR-Mageuzi ilivyopoteana baada ya uchaguzi ule. Bila shaka watangulizi wa CHADEMA waling'amua kwamba haiwezekani kuing'oa CCM kwa kutumia makapi ya CCM.

Fast forward, kazi ya Dr Slaa kuijenga CHADEMA hususani ujio wa kitu alichokiita "inteligensia ya chama" kilifanikiwa sana kuidhoofisha CCM. From no where, CHADEMA ikakumbatiana na Mh Lowassa. Miaka miwili (2) ya uwepo wa Mh Lowassa ndani ya chama hiki, hakuna anayejua tena ni nini chama hiki kimekusudia kufikia. Watoto wa mjini wanasema 'wamepoteana'.

Mbaya zaidi badala ya chama hiki kuketi kitaasisi na kujitafakari wapi kimeboronga na kifanye vipi kurejesha hadhi na uimara wake, tunasikia malalamiko kuhusu kukandamizwa na CCM. Ni lini CCM iliviacha vyama vya upinzani kufanya kazi za siasa vitakavyo? Waliwezaje waliofikisha CHADEMA kwenye chama kikuu cha upinzani na wanashindwaje waliopo kutunza hadhi hii?

Chama cha demokrasia na maendeleo kitaendelea kupitia wakati huu mgumu kwa muda mrefu ujao, mpaka pale viongozi waandamizi wenye kushikilia maamuzi watakapokiri kuwa wanapaswa kujiongeza ili waweze kushindana kisiasa na CCM.
 
Matokeo ya kushindwa Chadema, sasa ndio yatawaamsha wengi kuwa Chadema haikujipanga, haijipangi, na haitajipanga!, its very unfortunately, kufikia 2020, Chadema will be reduced to almost nothing, hivyo uchaguzi wa 2020 ndio utakuwa rasmi kwa Chadema ni bye bye!.
P
 
Wanabodi,

Haya ninayoyaandika hapa, yanatoka ndani kabisa ya moyo wangu na ninaandika kwa uchungu!, kwa mtu yoyote ambaye alikuwa na matumaini ya labda 2015, tunaweza kupata mabadiliko, akiangalia hii trend ya Chadema inayokwenda nayo sasa, atakubaliana na mimi, kuwa the trend is not good at all!, 2015 is just around the corner!, I'm afraid, by the time Chadema ita realize imefanya nini, ilipaswa kufanya nini, sasa inafanya nini, na 2015 itafanya nini!, it will be too little too late!, huu ni ukweli mchungu sana kumeza, kuwa Chadema Haikujipanga (jana), Chadema Haijajipanga (leo), Chadema Haijipangi (kesho), na amini nawaambieni!, Chadema Haitajipanga (2015), hivyo huu ni ukweli mchungu kweli kweli kumeza kuwa 2015, ni CCM Tena!.

Tangu 2010, Chadema Hamkujipanga!.
Mara Baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2010, uliofufua kwa kiwango kikubwa matumaini ya uwezekano wa Chadema kuchukua nchi, 2015, mimi ni miongoni mwa wana jf wa mwanzo kutinga viwanja vya Bunge Dodoma, kuwapongeza baadhi ya makamanda waliokata vigogo wa CCM!, nikatoa tathimini yangu kuwa kwenye baadhi ya maeneo, Chadema imeshinda uchaguzi, sio kwa sababu ilijipanga vizuri!, no!, nikasema Chadema imeshinda uchaguzi katika baadhi ya maeneo kwa sababu tuu CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!. hapa Chadema niliwaambia hivi


Hakuna ubishi kuhusu kitakachompata yoyote atakayeteta ukosoaji wa Chadema humu jukwaani, na mimi ndicho kilichonikuta, na miongoni mwa walionijibu uzi wangu huo, ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibrod Silaa, alinijibu hivi

Kiukweli baada ya jibu hili, mimi nikaishia kuwa mdogo tuu kama piriton, ukijumlisha na comments wa wengine, kwa kweli nilikuwa kama sisimizi!.

Hii maana yake ni nini, Chadema wakiambiwa ukweli, badala ya kusikiliza hoja na kuzifanyia kazi, wao ndio kwanza wana react na hawasikii!, kwenye uzi huo, hoja kuu nilisema Chadema isiendelee kutegemea kutwaa majimbo kwa sababu tuu CCM imechokwa!, ili Chadema ishinde kihalali very good clear and sweet victory, ni pale wananchi wanapokuwa wamehamasika na kufanya informed decision kuwa tunaichagua Chadema kwa sababu hizi, hizi na hizi, hivyo Chadema lazima ije na mkakati, itafanya nini tofauti na kinachofanywa na serikali ya CCM, ili wanaoichagua, wajione wanachagua chama mbadala.

CCM Imechokwa:
Kwenye uzi huo nilisema CCM imechokwa lakini imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali sio kwa sababu inapendwa sana!, no way, nilisema CCM imekuwa ikishinda chaguzi nyingi kutokana na mazoea, huku iki take advantage ya ignorance ya Watanzania, hawana choice to choose from kwa kushindanisha sera, kutokana na ujinga, na umasikini uliotopea, wengi wa wapiga kura, hawanauwezo wa kushindanisha sera, wala kujua wanachagua kwa sababu gani, bali wanachagua kwa "shibe" ya leo!, yeyote atakayekushibisha leo, huyo ndie!, hata kama atakulaza tena njaa miaka mitano ijayo, na ikifika, kama kawaida atarudi tena na T-shirt na kofia na ile shibe ya siku moja!, tutaichagua tena!, kama sio ignorance ni nini?!.

Kwenye uzi huo nilipendekeza dawa ya kuitibu CCM iliyochokwa kama ifuatavyo

Hakuna mwana CCM yoyote aliyekanusha kuchokwa kwa CCM, lakini haukupita muda, hiyo dose niliyoipendekeza ilidungwa CCM!, wala sijitambi kuwa CCM inafuatilia jf, au ndio chanzo cha mabadiliko hayo chanya, ukiona mbeba pakacha linavunja, ukamshtua mbebaji kuwa pakacha linavuja, akasimama kivulini na kuliziba kisha akaendelea na safari yake!, wewe unaweza kujiaminisha kuwa nimemsaidia yule mbeba paka kumtaarifu kuvuja kwa pakacha lake!, kumbe ukweli ni kuwa mbemba pakacha ulijua pakacha linavuja lakini akapanga ngoja afike kivulini ndipo alitue kuliziba na kupumzika kidogo!, hivyo useme usisema mabadiliko yangekuja!.

Kufuatia mabadiliko ya sasa ya CCM, 2015, Chadema isitegemee majimbo ya ubwete wa CCM chovu, na tena isipokuwa makini na baadhi ya wabunge wake haswa wale "vichaa!", CCM inaweza kuwapokonya, only save kwa baadhi ya maeneo ambayo machalii wa kipande hiyo, vichaa ndio huwa machaguo yao,hivyo kwa kadri unavyozidi kuwa kichaa ndivyo unavyozidi kupendwa na kukubalika!.

Uso kwa Uso na Dr. Slaa!.
Niliwahi kwenda ofisini kwa Dr. Slaa for official visit, wakati huo nikiwa utumwani kwenye utumwa fulani, hivyo unapokuwa mtumwa, ukitumwa mahali, unawakilisha kile ulichotumwa na bwana wako aliyekutuma, hivyo sijihesabu kama mimi nilionana na Dr. Slaa!.

Siku tulionana rasmi na kwa nafasi, ni pale tulipokutana tuu mahali, sote tukiwa safarini, tukatokea kujipumzisha mahali na kupata mlo, hivyo kukutana kwa bahati!.

Kwa vile mimi ni mwandishi, kwanza nilimkabili, na kuamsalimia huku nikitanguliza kuomba radhi, maana mahali hapo ni privacy ya mtu, na watu wako na watu wao, hivyo mwandishi kupenyeza penyeza pua its uncalled for!, ila nikakaribishwa!.

Nakumbuka vuzuri nilimweleza resevations zangu kwa "Chadema kutokujipanga" na haswa kuhusu utaratibu wake wa kupata viongozi wake na wagombea!.
Nilisema nimenote wengi wa wagombea wao, ni wagombea sadakalawe!, baada ya kukosa kwenye ile sadalawe ya kule, then hukimbilia huku na ndivyo Dr. alivyoingia Chadema. Nikasema huwezi kushinda uchaguzi na kushika dola kama hauna able people behind!. Nikashauri, kama kweli Chadema kina nia ya dhati ya kushika dola 2015, lazima kitayarishe watu, by investing in people, hakiwezi kushika dola kwa kuwategemea wagombea wanaopatikana kwa game of chance!. Lazima Chadema ifanye "head hunting" ya able people na ikikosa "able people", ifanye hata spotting na grooming from grassroot, ili ijenge kada yake ya viongozi iliyowalea na kuwakuza kichadema, ambao hawa watakuwa ni waaminifu na tegemeo lake, na sio kusubiria "makapi" ya CCM!.

Kusema ukweli, Dr. Slaa alinieleza a very fine na promising strategies, zikiwemo succession plan, pia alinieleza msimamo wake binafsi kuhusu kugombea tena urais 2015!, hivyo mimi ni mmoja wa watu wachache sana wanaujua msimamo wa Dr. Slaa kwenye kugombea urais 2015 from the horses mouth!. (Naomba nisiutaje humu kwa sababu mazungumzo yetu yalikuwa informal hivyo ni off the record).

Chadema Haijajipanga!.
Matokeo mabaya Chadema katika baadhi ya chaguzi ndogo za ubunge na udiwani, ni uthibitisho kuwa Chadema bado haijajipanga!. Hata ushindi wa Chadema Arumeru kwa kijana Nasari, umechangiwa na support ya vita vya wenyewe kwa wenyewe CCM ndani kwa ndani kulikomoa chaguo la yule "jamaa yangu". Kama wengi mtakuwa na maswali, Chadema ijipange kwenye nini, mnaweza kunitembelea hapa nimeeleza kila kitu!. Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...

Chadema Hamjipangi!.
Hata baada ya kipigo kitakatifu cha Kalenga, kuna kitu nimewashauri Chadema kuhusu uchaguzi wa Jimbo la Chalinze!, ili Chadema kujionyesha chenyewe ni kidume, au kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi, bado itang'ang'ana na kuendelea kutumbukiza pua Chalinze!, angalau kwa Kalenga picha ilikuwa haisomeki sana!, Chalinze ndio maeneo ya strong hold ya wale vibonde niliowazungumzia kule ambao ndio mtaji wa CCM!. Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze: CHADEMA Muungeni mkono mgombea ...

Uchaguzi kama vita!, ukijijua huwezi kushinda, ule msemo wa "no retreat, no surrender" wa "kupigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike!" huo ndio huo unaitwa "ushujaa!" alikufa vitani akiipigania nchi yeke!, mkiisha malizika wote, adui atapata walk over victory kuitwaa nchi yenu yote na nyinyi nyote kugeuka mateka!. Wapiganaji makini ni wale wakishajipima na kujiona hawawezi, hurudisha majeshi nyuma (retreat) na kujipanga upya!.
Chadema wakikubali ku retreat na kujipanga upya, wata boost kidogo morali ya wapiganaji wake, kiliko kuendelea kupeleka vikosi vyake vitani na kuishia kuwa wiped!.

Na Kwa 2015!, Chadema Haitajipanga!.
Kwa maoni yangu, Bunge hili Maalum, likifuatiwa na kikao cha Bunge, then kura ya maoni, then uchaguzi wa serikali za mitaa!, then uchaguzi wa ndani wa Chadema (uongozi uliopo madarakani kwa mujibu wa katiba ya Chadema, umalizika mwaka huu baada ya kuuongezea mwaka mmoja!, katiba ya Chadema haikutoa any possibility ya extra extension, japo uongozi wa Chadema unaweza kumuandikia Msajili na kulitaja Bunge Maalum ni "force majeure" hivyo kutofanya uchaguzi wake wa ndani kihalali kabisa!". Ndipo ufuate uchaguzi mkuu, huku kuna ile pending case!!. Kikweli kabisa, my honest opinion, kwa time iliyobakia kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, mambo yaliyopo mbele ya Chadema ni too much! kwa Chadema kujipanga and the time is too little too late!, hivyo naiona wazi kabisa CCM ikirudi kujichukulia nchi kiurahisi kama imeokota!.

Hitimisho: Chadema na "Karma!"
Namalizia kwa kusisitiza, Chadema katika kupanga mambo yenu, zingatieni sana hii kitu inaitwa "Karma", msiidharau kabisa!, karma is real!.
Do the right thing or else!.

Poleni kwa ya Kalenga!.

Jipangeni

Paskali

NB. Paskali, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa!, bali ni mtazamaji mzuri tuu wa hii game la siasa kazi yake ikiwa kutazama tuu!, na kueleza, na kutoa ushauri wa bure!.
Rafiki yangu paschal Mbowe anajipangaje kwa mfano hajui ata theory moja ya mapinduzi/mageuzi duniani acheni kufanya maisha mapesi hivyo na kuiona elimu haina maana hasa zama hizi
 
Sasa Chadema inaanza kujipanga kwa kuonyesha ukomavu kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kuwashughulikia wanaoitwa wasaliti, ambapo katika kuushughulikia usaliti wa Zitto, Kitila na Mwigamba, walitumia ujinga!, lakini katika kushughulikia usaliti wa Kubenea na Komu, busara imetumika, Sisemi kuwa safari hii busara imetumika kwa sababu tuu ya Komu being Mkaskazini, bali safari hii busara imetumika, kwa sababu sasa Chadema inakuwa more mature, ule ujinga ujinga katika issue ya Zitto ulikuwa ni utoto tuu, na ujana, sasa inamature katika utu uzima.

Hongera sana Chadema for maturity, sasa mnaanza kujipanga, ila not for 2020, its too little too late, wanaoondoka waachwe wajiondokee, kazi ya kuijenga upya Chadema ya kuendeleza opposition, iendelee katika hatua za awali kwa ajili ya 2025.

P.
 
Sasa Chadema inaanza kujipanga kwa kuonyesha ukomavu kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kuwashughulikia wanaoitwa wasaliti, ambapo katika kuushughulikia usaliti wa Zitto, Kitila na Mwigamba, walitumia ujinga!, lakini katika kushughulikia usaliti wa Kubenea na Komu, busara imetumika, Sisemi kuwa safari hii busara imetumika kwa sababu tuu ya Komu being Mkaskazini, bali safari hii busara imetumika, kwa sababu sasa Chadema inakuwa more mature, ule ujinga ujinga katika issue ya Zitto ulikuwa ni utoto tuu, na ujana, sasa inamature katika utu uzima.

Hongera sana Chadema for maturity, sasa mnaanza kujipanga, ila not for 2020, its too little too late, wanaoondoka waachwe wajiondokee, kazi ya kuijenga upya Chadema ya kuendeleza opposition, iendelee katika hatua za awali kwa ajili ya 2025.

P.

Naam

Binafsi nimefurahi pia kuona CHADEMA inajifunza kwa vitendo kuachia "ngano na magugu" viote pamoja. Hekima hii imefika kwa kuchelewa. Walau imefika. Ni jambo jema
 
Baada ya Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni super man, nimemkumbuka naomba nimdurusu kidogo, niliwaji kusema nini humu kumhusu mtu huyu.

P.
 
Back
Top Bottom