CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

wanabodi,

haya ninayoyaandika hapa, yanatoka ndani kabisa ya moyo wangu na ninaandika kwa uchungu!, kwa mtu yoyote ambaye alikuwa na matumaini ya labda 2015, tunaweza kupata mabadiliko, akiangalia hii trend ya chadema inayokwenda nayo sasa, atakubaliana na mimi, kuwa the trend is not good at all!, 2015 is just around the corner!, i'm afraid, by the time chadema ita realize imefanya nini, ilipasw kufanya nini, sasa inafanya nini, na 2015 itafanya nini!, it will be too little too late!, huu ni ukweli mchungu sana kumeza,kuwa chadema haikujipanga (jana), chadema hijajipanga (leo), chadema haijipangi (kesho), na amini nawaambieni!, chadema haitajipanga (2015), hivyo huu ni ukweli mchungu kweli kweli kumeza kuwa 2015, ni ccm tena!.

tangu 2010, chadema hamkujipanga!.
mara baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2010, uliofufua kwa kiwango kikubwa matumaini ya uwezekano wa chadema kuchukua nchi, 2015, mimi ni miongoni mwa wana jf wa mwanzo kutinga viwanja vya bunge dodoma, kuwapongeza baadhi ya makamanda waliokata vigogo wa ccm!, nikatoa tathimini yangu kuwa kwenye baadhi ya maeneo, chadema imeshinda uchaguzi, sio kwa sababu ilijipanga vizuri!, no!, nikasema chadema imeshinda uchaguzi katika baadhi ya maeneo kwa sababu tuu ccm imechokwa; chadema haijajipanga!. Hapa chadema niliwaambia hivi


hakuna ubishi kuhusu kitakachompata yoyote atakayeteta ukosoaji wa chadema humu jukwaani, na mimi ndicho kilichonikuta, na miongoni mwa walionijibu uzi wangu huo, ni katibu mkuu wa chadema, dr. Wibrod silaa, alinijibu hivi

kiukweli baada ya jibu hili, mimi nikaishia kuwa mdogo tuu kama piriton, ukijumlisha na comments wa wengine, kwa kweli nilikuwa kama sisimizi!.

Hii maana yake ni nini, chadema wakiambiwa hawasikii!, kwenye uzi huo, hoja kuu nilisema chadema isiendelee kutegemea kutwaa majibo kwa sababu tuu ccm imechokwa!, ili chadema ishinde kihalali very good clear and sweet victory, ni pale wananchi wanapokuwa wamehasika na kufanya informed decision kuwa tunaichagua chadema kwa sababu hizi, hizi na hizi, hivyo chadema lazima ije na mkakati, itafanya nini kinyume cha kinachofanywa na serikali ya ccm!.

ccm imechokwa:
kwenye uzi huo nilisema ccm imekuwa ikishda chaguzi mbalimbali sio kwa sababu inapendwa sana!, no way, nilisema ccm imekuwa ikishinda chaguzi nyingi kutokana na mazoea, huku iki take advantage ya ignorance ya watanzania, hawana chagua kwa "choice" ya kushindanisha sera, wanachagua kwa "shibe" ya leo!, yeyote atakayekushibisha leo, huyo ndie!, hata kama atakulaza tena njaa miaka mitano ijayo, na ikifika, kama kawaida atarudi tena na t-shirt na kofia na ile shibe ya siku moja!, tutaichagua tena!, kama sio ignorance ni nini?!.

Kwenye uzi huo nilipendekeza dawa ya kuitibu ccm iliyochokwa kama ifuatavyo

hakuna mwana ccm yoyote aliyekanusha kuchokwa kwa ccm, lakini haukupita muda, hiyo dose niliyoipendekeza ilidungwa ccm!, wala sijitambi kuwa ccm inafuatilia jf, au ndio chanzo cha mabadiliko hayo chanya, ukiona mbeba pakacha linavunja, ukamshtua mbebaji kuwa pakacha linavuja, akasimama kivulini na kuliziba kisha akaendelea na safari yake!, wewe unaweza kujiaminisha kuwa nimemsaidia yule mbeba paka kumtaarifu kuvuja kwa pakacha lake!, kumbe ukweli ni kuwa mbemba pakacha ulijua pakacha linavuja lakini akapanga ngoja afike kivulini ndipo alitue kuliba na kupumzika kidogo!, hivyo useme usisema mabadiliko yangekuja!.

Kufuatia mabadiliko ya sasa ya ccm, 2015, chadema isitegemee majimbo ya ubwete wa ccm chovu, na tena isipokuwa makini na baadhi ya wabunge wake haswa wale "vichaa!", ccm inaweza kuwapokonya, only save kwa baadhi ya maeneo ambayo machalii wa kipande hiyo, vichaa ndio huwa machaguo yao,hivyo kwa kadri unavyozidi kuwa kichaa ndivyo unavyozidi kupendwa na kukubalika!.

uso kwa uso na dr. Slaa!.
niliwahi kwenda ofisini kwa dr. Slaa for official visit, wakati huo nikiwa utumwani kwenye utumwa fulani, hivyo unapokuwa mtumwa, ukitumwa mahali, unawakilisha kile ulichotumwa na bwana wako aliyekutuma, hivyo sijihesabu kama mimi nilionana na dr. Slaa!.

Siku tulionana rasmi na kwa nafasi, ni pale tulipokutana tuu mahali, sote tukiwa safarini, tukatokea kujipumzisha mahali na kupata mlo, hivyo kukutana kwa bahati!.

Kwa vile mimi ni mwandishi, kwanza nilimkabili, na kuamsalimia huku nikitanguliza kuomba radhi, maana mahali hapo ni privacy ya mtu, na watu wako na watu wao, hivyo mwandishi kupenyeza penyeza pua its uncalled for!, ila nikakaribishwa!.

Nakumbuka vuzuri nilimweleza resevations zangu kwa "chadema kutokujipanga" na haswa kuhusu utaratibu wake wa kupata wagombea!.
Nilisema nimenote wengi wa wagombea wao, ni wagombea sadakalawe!, baada ya kukosa kwenye ile sadalawe ya kule, then hukimbilia huku na ndivyo dr. Alivyoingia chadema. Nikasema huwezi kushinda uchaguzi na kushika dola kama hauna able people behind!. Nikashauri, kama kweli chadema kina nia ya dhati ya kushika dola 2015, hakiwezi kushika dola kwa kuwategemea wagombea wanaopatikana kwa game of chance!. Lazima chadema ifanye "head hunting" na ikikosa "able people", ifanye hata grooming kabla na sio kusubiria "makapi" ya ccm!. Kusema ukweli, alinieleza a very fine na promising strategies, ikiwemo msimamo wake binafsi kuhusu kugombea tena urais 2015!, hivyo mimi ni mmoja wa watu wachache sana wanaujua msimamo wa dr. Slaa kwenye kugombea urais 2015 from horsed mouth!. (naomba nisiutaje humu kwa sababu mazungumzo yetu yalikuwa informal hivyo ni off the record).

chadema haijajipanga!.
matokeo mabaya chadema katika baadhi ya chaguzi ndogo za ubunge na udiwani, ni uthibitisho kuwa chadema bado haijajipanga!. Hata ushindi wa chadema arumeru kwa kijana nasari, umechangiwa na support ya vita vya ccm ndani kwa ndani kulikomoa chaguo la yule "jamaa yangu". Kama wengi mtakuwa na maswali, chadema ijipange kwenye nini, mnaweza kunitembelea hapa nimeeleza kila kitu!.

chadema hamjipangi!.
hata baada ya kipigo kitakatifu cha kalenga, kuna kitu nimewashauri chadema kuhusu uchaguzi wa jimbo la chalinze!, ili chadema kujionyesha chenyewe ni kidume, au kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi, bado itang'ang'ana na kuendelea kutumbukiza pua chalinze!, angalau kwa kalenga picha ilikuwa haisomeki sana!, chalinze ndio maeneo ya strong hold ya wale vobonde niliowazungumzia kule ambao ndio mtaji wa ccm!.

Uchaguzi kama vita!, ukijijua huwezi kushinda, ule msemo wa "no retreat, no surrender" wa "ku
pigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike!" huo ndio huo unaitwa "ushujaa!" alikufa vitani akiipigania nchi yeke!, mkiisha malizika wote, adui atapata walk over victory kuitwaa nchi yenu yote kugeuka mateka!. Wapiganaji makini ni wale wakishajipima na kujiona hawawezi, hurudisha majeshi nyuma (retreat) na kujipanga upya!.
Chadema wakikubali ku retreat na kujipanga upya, wata boost kidogo morali ya wapiganaji wake, kiliko kuendelea kupeleka vikosi vyake vitani na kuishia kuwa wiped!.

na kwa 2015!, chadema haitajipanga!.
kwa maoni yangu, bunge hili maalum, likifuatiwa na kikao cha bunge, then kura ya maoni, then uchaguzi wa serikali za mitaa!, then uchaguzi wa ndani wa chadema (uongozi uliopo madarakani kwa mujibu wa katiba ya chadema, umalizika mwaka huu baada ya kuuongezea mwaka mmoja!, katiba ya chadema haikutoa any possibility ya extra extension, japo uongozi wa chadema unaweza kumuandikia msajili na kulitaja bunge maalum ni "force majeure" hivyo kutofanya uchaguzi wake wa ndani kihalali kabisa!". Ndipo ufuate uchaguzi mkuu, huku kuna ile pending case!!. Kikweli kabisa, my honest opinion, kwa time iliyobakia kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, mambo yaliyopo mbele ya chadema ni too much! Kwa chadema kujipanga and the time is too little too late!, hivyo naiona wazi kabisa ccm ikirudi kujichukulia nchi kama imeokota!.

hitimisho: Chadema na "karma!"
namalizia kwa kusisitiza, chadema zingatieni sana hii kitu inaitwa "karma", msiidharau kabisa!, karma is real!.
do the right thing or else!.

Poleni kwa ya kalenga!.

Jipangeni

pasco
nb. Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa!, bali ni mtazamaji mzuri tuu wa hii game la siasa kazi yake ikiwa kutazama tuu!, na kueleza, na kutoa ushauri wa bure!.


du! Hii analysis nimeikubali ni ya kweli, mimi ni mwanaccm ila kiukweli naipenda chadema na ni mojawapo ya wanaccm tuliokuwa na imani kubwa kuwa cdm itakomboa hii nchi, ila sasa kiukweli tumekata tamaaa na matokeo yake ndo kama tunavyoshuhudia
cdm inahitaji kuuchukua huu ushauri kama ulivyo na kuufanyia kazi sambamba na sawia!
 
Naunga mkono CHADEMA kushiriki uchaguzi mdogo wa chalinze kwa sababu zifuatazo
1. ni fursa ya upinzani kuelezea sera zake kwa umma
2. ni fursa ya kujijenga kisiasa kwa changuzi mbali mbali zijazo
3. ni ukomavu kuonyesha inakubalika hata kwa kuweza kusimamisha mgombea eneo husika (fuatilia rekodi ya vyama vinavyoshindwa kusimamisha mgombea maeneo mbali mbali kwa kukosaa mtandao na hata kuungwa mkono katika hatua za awali)
4. ni uwanja muhimu wa kuichachafyaa serikali na chama tawala
5. ni fursaa pekee (kwa aina ya mgombea wa chama tawala uhusiano wake na mtawala) kuelezeaa mapungufu ya kiungozi ya mtawala moja kwa mojaaa.
 
Mimi ninaamini chadema walijipanga, lazima walikuwa na mikakati kam ambayo tumekwisha ishuhudia hasa hiyo ya M4C na operesheni nyingine nakadhalika lakini ukweli ni kwamba matokeo ya mikakati hiyo hayakuwa n aushawishi mkubwa na wakudumu mpk sasa!chadema wanatakiwa kufanya tathimini upya na kuja na njia mbadala(mikakati) ya kujiokoa katika muda huu mfupi!ikumbukwe kwamba mikakati yoyote ya kuijenga chadema inaenda sambamba na mikakati ya ccm ya kuibomoa au kuidhoofisha chadema ndani na nje ya chadema yenyewe!

Watanzania wengi wanaonekana kuchoshwa au kukata tamaa na mambo ya siasa,ni kama hawaoni namna ambavyo wanasiasa wanaweza kuwaleta mabadiliko hivyo wanajiweka pembeni kweny mambo ya siasa na hasa upigaji kura na uongozi wa vyama vya upiznani kuanzia kwnye ngazi za chini,wengi tunazungumza hapa kwenye majukwaa kama haya au kutegemea wengine wawe mstari wa mbele lkn ni wangapi tupo mstari wa mbele ktk siasa za mtaani au kwenye kata zetu,matokeo yake ni kuona kuwa watu ni wale wale wa ccm wakijihusisha na siasa za jana, leo na kesho ndio ha hao wanapiga kura na kufanya maamuzi ya nani atwae dola, ndio hao hao wanapata orientation za siasa!

Pamoja na ugumu wa kupata wafuasi wa wazi wa vyama vya upinzani na kufanya siasa za upinzani katika mazingira magumu haya ya utawala wa ccm lazima chadema itumie mbinu mbadala vinginevyo itakuwa historia tu,ugumu usiwe sababu ya kukata tamaa bali uwe chachu ya kusonga mbele kimkakati zaidi!
 
Hiki chama ni sawa na kundi la misukule hawajui walipo,hawelewi walipotoka wala hawajitambui wanakokwenda, kushabikia chadema lazima uwe na akili za kobe.
Kweli we ni chuki
 
Tatizo la Chadema ukiwakosoa wanakuona adui sielewi kwanini wanaendelea kutumia helikopta kwenye kila chaguzi kwani gharama wanazotumia ni nyingi ukilinganisha na gharama ambazo wangetumia kujenga mtandao ngazi ya chini.
wanachama wengi hawaijui hata Chadema tunaweza kusema wengi ni washabiki ni ukweli usiopingika Chadema inaitaji mwenyekiti mwenye mawazo mampya kwani mazingira ya mwaka 2010 ni tofauti na 2015 ccm watakuja na mgombea mwingine na hoja za ufisadi pamoja bado upo lakini hazitakuwa na nguvu kama za wakati ule
kuna sehemu kama lushoto chadema wana nguvu lakini wanakosa sapoti toka juu ndio maana tunasikia mgombea anashindwa lakini baadae ananyang'anywa ushindi bila chama kusema chochote huu ni udhaifu mwingine wa chadema si ajabu wakashindwa kusimamisha wagombea kwenye majimbo mengine sababu hawajajenga nguvu inayotakiwa kwenye mizizi ya wananchi wananchi wengi wa Tanzania hawaingii kwenye mitandao ukweli ccm imechokwa lakini chadema wameshindwa kutumia nafasi hii kwa faida yao
 
Naunga mkono CHADEMA kushiriki uchaguzi mdogo wa chalinze kwa sababu zifuatazo
1. ni fursa ya upinzani kuelezea sera zake kwa umma
2. ni fursa ya kujijenga kisiasa kwa changuzi mbali mbali zijazo
3. ni ukomavu kuonyesha inakubalika hata kwa kuweza kusimamisha mgombea eneo husika (fuatilia rekodi ya vyama vinavyoshindwa kusimamisha mgombea maeneo mbali mbali kwa kukosaa mtandao na hata kuungwa mkono katika hatua za awali)
4. ni uwanja muhimu wa kuichachafyaa serikali na chama tawala
5. ni fursaa pekee (kwa aina ya mgombea wa chama tawala uhusiano wake na mtawala) kuelezeaa mapungufu ya kiungozi ya mtawala moja kwa mojaaa.

Nakuunga mkono asilimia 100. Ikizingatiwa kwamba mwaka 2010 hawakuweka mgombea katika jimbo hilo na ccm wakapeta na kuzoa kura asilimia 90.
 
Kwangu mimi siku zote Pasco ni chizi tuh au futuhi,lakin leo nimeshangaa chizi kuandika vitu vya msingi kama hivi,umemaliza dose au???

Msalimie Nikupateje...
 
Last edited by a moderator:
Chadema kwa kuwa kalenga walishinda kwenye viunga vya kanisa nawashauri chalinze wakashinde viunga vya misikitin,si wameyataka wenyewe??

Waache yawakute
 
Tatizo la Chadema ni kuamini kwamba wamekubalika na wananchi na kwamba 2015 watatinga ilkulu.Hiyo ni ndoto ya mchana na ni ukweli mchungu kuupokea.Viongozi wa Chadema ni wenye jaziba na wasiopenda ushauri wa mtu yeyote yule hasa ushauri huo ukiwa na mwelekeo wa kuwakosoa.Chadema jipangeni!
 
Chadema wanaponzwa na kiburi,ubabe na ubishi hii lazima iendelee kuwatesa chadema ni chama cha watu fulani hao ndiyo wenye maamuzi nacho.
 
ngololo.jpg
 
Mkuu Msengapavi, I've loved this!.

Kuna thread niliweka humu nikawapa Chadema data kuwa tulipokuwa watu milioni 42, eligible voters walikuwa ni milioni 30!, waliojindikisha kupiga kura ni milioni 20!, waliopiga kura ni milioni 8!, JK akachaguliwa na watu milioni 6!, hao milioni 2 ndio wakachagua opposition!.

Kwenye website ya CCM, inajitapa ina wanachama milioni 6!, na JK kachaguliwa na kura milioni 6!. The gap between eligible voters, milioni 30!, na walioichagua CCM, milioni 6!, ni milioni 24!, that should have been ndio owe target ya Chadema!.

Reseach zimeishafanyika kwa nini watu wenye umri wa kujiandikisha kupiga kura, hawajiandikishi!, kwanini watu wanajiandikisha, halafu hawapigi kura?!, ukifanikiwa tuu kuyashika haya makundi mawili, CCM Gone!. Hivyo Chadema wakashindwa kupanga vipaumbele vyake kati ya visibility na reaching out the masess!, badala ya ku concentrante on reaching out, Chadema wakajikita zaidi kwenye visibility, kuonekana, kuandamana, kushout kwa loud voice rushwa, ufisadi, CCM hiki, CCM kile, as if hiki ndicho Watanzania wanalichotaka!.

Baada ya ushindi mnono wa 2010, Chadema sasa inapata ruzuku ya kutosha kabisa to operate its mass media!, kuwa na redio yake, kuwa na TV yake na kuwa na magazeti yake!, (TZ Daima ni la Mbowe). Wakati CCM ikitumia TV ya Taifa, Redio ya taifa na redio yake, Magazeti ya serikali, magazeti ya wapambe wao, na gazeti lao, priority ya Chadema ikawa ni kununua magari ya M4C, kununua PA, kukodisha chopa za Ndesa, na kufanya mikutano!. Watu wenye time ya kuhudhuria mikutano ndio wale wale kundi la wale milioni 8 waliojitokeza, hao milioni 22 have never been reached!. Kama Chadema inge invest kwenye mass media ingewafikia wengi zaidi kuliko washangaa chopa!.

Nilipowaambia hawajipanga, na kuwaeleza wajipange wapi, wenzetu wako bize kufanya yale ya kuonekanika!. Hata hivyo kupanga ni kuchagua!, Chadema made its choices na lazima kuyakubali matokeo ya priorities zao and ether live with it and be doomed forever, or change for the better and make a diference!.
Kuendelea kuisupport Chadema despite all the odds is the most paromount thing to do!.

Nakubaliana na wewe!.

Pasco.
Pasco


Pasco,umeweka analysis yako vizuri,ila kuna issues ndogo ndogo ambazo haujazifanyia reaserch ya kutosha au haujaamua kuyaweka bayana tukayaona.

Je,unadhani Serikali yetu ya CCM imekubali vyama vingi kwa moyo mmoja?
Je,unadhani Serikali yetu itakubali watanzania japo asilimia 70 iwe imejiandikisha by 2015.
Je,unadhani Serikali itakubali kuwe na uchaguzi HURU na HAKI?
Je,TUME zetu zote mbili zinazohusiana na Chaguzi,zinaweza kuwa HURU na HAKI kwenye utendaji wake?

Kama tukiweza kupata majibu ya haya na kila mtoa RUSHWA TUME hizi zikatoa adhabu stahiki basi UPINZANI waweza kuwika na hapa nimesema UPINZANI sababu HAKI na UHURU hauchagui vyama vya UPINZANI,bali vyote vinamatatizo yanayoshabihiana kwenye suala la upatikanaji wa HAKI na UHURU wa kukipigia chama cha UPINZANI.
 
Samaki mkunje akiwa angali mbichi!. Siasa za kilaghai haziwezi kupambana na uharisia wa kisiasa nchini.

Pasco acha "kupotosha" wanaJf. CHADEMA ni chama makini na kimejiandaa kuchukua nchi 2015, come rain or shine!.

CHADEMA haliwezi kuwa ni sikio la kufa bali ni sikio ambalo limeisha kufa muda mrefu na kilichobaki ni maziko.

Soma maelezo hapa chini ya Katibu Mkuu wa CHADEMA akiwaambia washabiki, wapenzi na wanachama wa CHADEMA.



Unaweza kusoma hii thread kupitia hapa,
Wewe ni mlevi wa pombe za kienyeji huwa nakudharau sana
 
Chadema kwa kuwa kalenga walishinda kwenye viunga vya kanisa nawashauri chalinze wakashinde viunga vya misikitin,si wameyataka wenyewe??

Waache yawakute
Tapeli la gesi ndani ya Nyumba!!!!! mabomba yamefika kinyerezi wewe tapeli tayari kuanza kutumia kama vipi jiue
 
Hivi Pasco,wajua huko vijijini wengi hawajui haki zao za msingi?Tunaoenda vijijini tunaelewa mengi kuliko mlioko mijini.Kama mtu ananyang'anywa ardhi kwa kumtishia kumuweka ndani na bila hiari anakubali kuitoa ardhi kwa watendaji ili mabwana wakubwa wenye pesa zao wa hodhi maeneo yenye rutuba.

Kama haya hawayajui,je haki za vyama vingi watazijua?Kuna wakati nilikuambia kazi ya waandishi wahabari hasa wewe uliyesoma sheria ni kuelimisha UMMA wa watanzania ambao haki zao za kisheria zilizoainishwa kwenye KATIBA hawazijui,mmefikia wapi?Je,kweli utakuwa na HAKI ya kuwalaumu CDM wakati hata wewe nafasi yako haujaitendea HAKI?
 
Back
Top Bottom