CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

tumekuelewa mheshimiwa pasco,kwanza ungewauliza ratiba yao ya uchaguzi vipi?internal democracy,viongoz wate wa kitaifa wanang`ang`ania madaraka kwa uroho wa ruzuku,sasa kwa style hii watafika kweli,
 
Kadri siku zinavyozidi kusonga, chadema nayo inazidi kupukutika, wanachama wanaikimbia, mashabiki wanaikimbia, wananchi wanaisusia. Inabakibkatika kaeneo kadogo cha arusha mjini na moshi mjini. Yamesemwa mengi kuwa hii ni saccos, nk lakini mimi nasema hiki chama cha kaskazini

Mtaji wa CCM ni ukanda wa pwani.
 
Tatizo la Pasco katika ulimwengu wake huwa anadhani mawazo yake ndio mamlaka na hakuna mtu mwenye ruhusa ya kupingana na mawazo yake.
 
Pasco, bila kujali itikadi zako za kisiasa, umezungumza ukweli mtupu. Kwa hali ilivyo kwa sasa, hata mimi nimekata tamaa na CDM. Napata hisia kuwa 2015 ni CCM tena, sadly! Natamani mtu aniambie kwa nini nisikate tamaa na CDM kuchukua dola 2015; mtu aniambie kama hali ndo ilivo sasa chamani kwa nini tuamini kuwa itabadilika na kuleta ushindani wa kweli 2015.

2015 bado ntapigia kura CDM lakini si kwa sababu ni chama bora bali kwa sababu CCM ni chama kibaya zaidi. Heri zimwi lisilotujua, kwani litujualo linatumaliza.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Nakuunga mkono Mia kwa Mia mkuu Pasco, huwezi kushindwa mfululizo na kujiona bado una nguvu.

Tuliwahi kuwashauri hawa jamaa kuwa wajitahidi kuwa na ofisi ngazi ya wilaya na kuajiri makatibu wa wilaya watakaokuwa wanalipwa mshahara na chama badala ya kuwa na viongozi wa kujitolea ambao ukifika wakati wa uchaguzi CCM inawanunua, au wengine wanaficha fomu za wagombea CCM inapita bila kupingwa. At least CHADEMA ingeanzia hata ngazi ya mkoa kuwa na makatibu wa kuajiriwa, wenye JOB SECURITY kwenye kazi ya chama, ambao wanatumwa kokote, watafanya kazi za chama kama Pasco anavyofanya kazi za PPR. Kutegemea watu wanaojitolea ni udhaifu ambao CCM wanautumia toka 1995 kwa kuweka watu wao ndani ya vyama vya siasa. Mwisho mnabakia kuwaita wasaliti huku mnasahau kuwa njaa ndio iliwatuma.

Mwisho nasema kutegemea kurusha helikopta katika sehemu ambazo haukuwa na matawi kama kalenga ni TOP DOWN APPROACH, hakuna chama kimefanikiwa duniani kwa hii approach. Grassroot system ndio njia pekee, weka matawi ngazi za chini, wape mamlaka wajiongoze. Kusubiri Slaa na Mbowe waje kwenye operation Sangara ni siasa za kizamani, acheni matawi yafanye operation dagaa ili sangara akija akute kuna samaki wengine pia.

Unadhani hawaelewi umuhimu wa grass-root approach?Wanauelewa sana tatizo linakuja kwenye utekelezaji wake maana kuwaambia hawa waheshimiwa wa makao makuu waelekeze kiasi kikubwa cha fedha mikoani,wilayani na hata mashinani ili kuimarisha CHADEMA kwenye ngazi za chini kabisa ni sawa na kuwashauri viongozi wa serikali ya chama tawala kuwa TANESCO ijiendeshe kama shirika binafsi ili liweze kujiendesha kwa ufanisi na kwa faida jambo hawatakubali kulifanya hata iweje kwasababu wanajuwa fika kwamba dili zao nyingi zitaharibika
 
Pasco, bila kujali itikadi zako za kisiasa, umezungumza ukweli mtupu. Kwa hali ilivyo kwa sasa, hata mimi nimekata tamaa na CDM. Napata hisia kuwa 2015 ni CCM tena, sadly! Natamani mtu aniambie kwa nini nisikate tamaa na CDM kuchukua dola 2015; mtu aniambie kama hali ndo ilivo sasa chamani kwa nini tuamini kuwa itabadilika na kuleta ushindani wa kweli 2015.

2015 bado ntapigia kura CDM lakini si kwa sababu ni chama bora bali kwa sababu CCM ni chama kibaya zaidi. Heri zimwi lisilotujua, kwani litujualo linatumaliza.

Mungu Ibariki Tanzania
Mkuu Msengapavi, I've loved this!.

Kuna thread niliweka humu nikawapa Chadema data kuwa tulipokuwa watu milioni 42, eligible voters walikuwa ni milioni 30!, waliojindikisha kupiga kura ni milioni 20!, waliopiga kura ni milioni 8!, JK akachaguliwa na watu milioni 6!, hao milioni 2 ndio wakachagua opposition!.

Kwenye website ya CCM, inajitapa ina wanachama milioni 6!, na JK kachaguliwa na kura milioni 6!. The gap between eligible voters, milioni 30!, na walioichagua CCM, milioni 6!, ni milioni 24!, that should have been ndio owe target ya Chadema!.

Reseach zimeishafanyika kwa nini watu wenye umri wa kujiandikisha kupiga kura, hawajiandikishi!, kwanini watu wanajiandikisha, halafu hawapigi kura?!, ukifanikiwa tuu kuyashika haya makundi mawili, CCM Gone!. Hivyo Chadema wakashindwa kupanga vipaumbele vyake kati ya visibility na reaching out the masess!, badala ya ku concentrante on reaching out, Chadema wakajikita zaidi kwenye visibility, kuonekana, kuandamana, kushout kwa loud voice rushwa, ufisadi, CCM hiki, CCM kile, as if hiki ndicho Watanzania wanalichotaka!.

Baada ya ushindi mnono wa 2010, Chadema sasa inapata ruzuku ya kutosha kabisa to operate its mass media!, kuwa na redio yake, kuwa na TV yake na kuwa na magazeti yake!, (TZ Daima ni la Mbowe). Wakati CCM ikitumia TV ya Taifa, Redio ya taifa na redio yake, Magazeti ya serikali, magazeti ya wapambe wao, na gazeti lao, priority ya Chadema ikawa ni kununua magari ya M4C, kununua PA, kukodisha chopa za Ndesa, na kufanya mikutano!. Watu wenye time ya kuhudhuria mikutano ndio wale wale kundi la wale milioni 8 waliojitokeza, hao milioni 22 have never been reached!. Kama Chadema inge invest kwenye mass media ingewafikia wengi zaidi kuliko washangaa chopa!.

Nilipowaambia hawajipanga, na kuwaeleza wajipange wapi, wenzetu wako bize kufanya yale ya kuonekanika!. Hata hivyo kupanga ni kuchagua!, Chadema made its choices na lazima kuyakubali matokeo ya priorities zao and ether live with it and be doomed forever, or change for the better and make a diference!.
Kuendelea kuisupport Chadema despite all the odds is the most paromount thing to do!.

Nakubaliana na wewe!.

Pasco.
Pasco
 
Chadema ni chama makini kimejipanga kuchukuwa dola.
 
Pasco uwa nazikubali arguments zako nyingi,ebu shauri kwa haya matumizi ya vyombo vya dola yaliyokithiri CHADEMA inaweza kupitia wapi?lafu nyingi zinachezwa wakati wa uchaguzi ni bora uwashauri CHADEMA la kufanya,pili believe me,kitu cha muhimu kwa CHADEMA kujipanga ni kufuatilia kwa makini na kusimamia uboreshaji wa daftari la kupigia kura ili wote wenye sifa za kupiga kura wawe kwenye daftari ilo,kwa maoni yangu kama ilo litafanyika, 2015 patachimbika,kwa sasa wengi walio kwenye ilo daftari kama ambavyo wengi wamewahi kusema ni conservatives,wafia chama na wengi wao kwa umri walio nao na upeo wao hata ujipange vipi,hata ufanye kampeni kampeni usiku kucha,uzunguke na chopa wiki mbili,ni sawa na kumpigia mbuzi jita ukitegemea kuwa atatingisha mkia,kama wasemavyo wenzatu you can not teach an old dog new tricks.Nakubaliana na PASCO Chalinze imejaa watu wa design hiyo,hata ufanye kampeni vipi,ni vigumu kueleweka,japo kushindwa kuko palepale ,mimi sishauri CHADEMA ijiondoe kwenye uchaguzi wa CHALINZE
 
Pasco umelenga pale ninapopazungumzia kila mara. Pamoja na mtiririko mzuri wa Dr. kwa mfumo uliopo wa kuwapokea wanachama kutoka vyama vingine na kuwapa vyeo sio sahihi kabisa kwani inawavunja moyo makamanda ambao hujitoa mhanga usiku na mchana kueneza itikadi na sera za CDM.

Kampeni za juu - chini katika mazingira haya haziwezi kuleta ushindi kwa CDM. Pamoja na kutokujipanga mapema kwa chaguzi zozote viongozi wa juu ni bora na ni vema wangehamasisha wanachi kwa mtindo tofauti. Hata vipeperushi vingesaidia kuliko helikopta. Na wale viongozi wachache waliopo sehemu husika wapewe mamlaka kamili ya kusimamia na kuendesha kampeni kwani wanafahamika na wanawafahamu wananchi wa sehemu husika. Hata wakisema hapa hatutashinda viongozi waichukulie hiyo hali na kuachana na kampeni watumie mbinu mbadala wa kuwaamsha wananchi wa sehemu husika.

Sisi huku kwenye msing tunakatishwa tamaa kwa sababu hatupati ripoti zozote kutoka juu zenye maelekezo ya nini tufanye tuweze kuwaaminisha wanachi kwamba CDM italeta mabadiliko chanya ktk nchi hii. Kuna sehemu tunashia kufungua misingi na matawi lakini uhai wa chama hauendelezwi kwa sababu ya viongozi kukosa maelekezo kutoka juu.

Hiki chama nakipenda sana lakini kuna namna kinaonyesha kimekosa mwelekeo. Viongozi toeni mikakati ya kuamsha ari ya wananchama na wananchi kwa jumla.

Swala la umwagaji damu linaweza kutokea pale ambapo yule ambaye ameshindwa analazimisha kushinda!
 
Pasco uchambuzi wako yakini ila jipange kuvumilia dhoruba!
 
Last edited by a moderator:
Pasco uchambuzi wako yakini ila jipange kuvumilia dhoruba!
 
Last edited by a moderator:
Pasco,
Ushaurii wako ni mzuri kwa Chadema kuuzingatia.
Ila kuna mambo ya msingi pia umeyaachaa na ningependaa kuyajadili.
Safari ya upinzania kuuondoa madarakani chama tawala na serikali yake sio lelemama na kwa kiasi cha kuridhisha chadema wameianzaa vema. Matokeo ya uchaguzi mkuu 2010 ni alama muhimu ya safari hiyo.
Kuna maeneo muhimu sana ambayo chadema imefanikiwaa kuisimamia serikali na kutoa upinzani unaonekana na kutoa matumaini kwa umma na hilo ndo moja ya jambo la msingi sana katika kujenga siasa za ushindani katika taifa lolote la demokrasia hapa duniani.
Tumeshuhudia chadema kupitia bunge pamoja na uchache wake ikiweza kutoa michango ya haja yenye kuchochea uwajibikajii nchini na hatimaye hata kuigwaa na CCM wenyewe ndani ya bunge na kwenye mikutano yao ya kisiasa.
Tukio la kutengeneza katiba mpya linaloendelea kwa sasa ni moja ya hoja muhimu iliyopigiwaa chapua na chadema katika uchaguzi mkuu 2010 na kuungwa mkono na makundi mbali mbali na hatimaye watawala wakakubali kuridhiaa zezi hilo.
Uzoefuu siasa za upinzani katika mataifa ya kiafrika yana hulka moja kuu ambayo ni MTAWALA NA CHAMA TAWALA KUWA NA MGUVU KUBWAA NA HATA WAKATI MWINGINE KUWA JUU YA SHERIA!
Mapambano ya kupungunguza na hata nkuondoa nguvu hiyooo yahitaji mikakati mingi tofauti yenye kujitoaa na uvumilivuu wa hali ya juu (fuatiliaa siasa za kenya pamoja na ubepari wa viongozi wa siasa za upinzani)
Tanzania ni nchi ya kijamaa iliyorukia ubeparii bila mfumo rasmi huku watawala wakiwa ni wamiliki wa kila kitu mpaka WATU WAKE!!!
 
Pasco uwa nazikubali arguments zako nyingi,ebu shauri kwa haya matumizi ya vyombo vya dola yaliyokithiri CHADEMA inaweza kupitia wapi?lafu nyingi zinachezwa wakati wa uchaguzi ni bora uwashauri CHADEMA la kufanya,pili believe me,kitu cha muhimu kwa CHADEMA kujipanga ni kufuatilia kwa makini na kusimamia uboreshaji wa daftari la kupigia kura ili wote wenye sifa za kupiga kura wawe kwenye daftari ilo,kwa maoni yangu kama ilo litafanyika, 2015 patachimbika,kwa sasa wengi walio kwenye ilo daftari kama ambavyo wengi wamewahi kusema ni conservatives,wafia chama na wengi wao kwa umri walio nao na upeo wao hata ujipange vipi,hata ufanye kampeni kampeni usiku kucha,uzunguke na chopa wiki mbili,ni sawa na kumpigia mbuzi jita ukitegemea kuwa atatingisha mkia,kama wasemavyo wenzatu you can not teach an old dog new tricks.Nakubaliana na PASCO Chalinze imejaa watu wa design hiyo,hata ufanye kampeni vipi,ni vigumu kueleweka,japo kushindwa kuko palepale ,mimi sishauri CHADEMA ijiondoe kwenye uchaguzi wa CHALINZE

Kwa watu walioamua nguvu ya dola haitaambulia kitu. Ila ndio hapo DR. Slaa anasema damu inaweza ikamwagika! Watajaribu kuiba lakini kama wananchi waliamua kuupa upinzani kura hawatafanikiwa. Mfano jimbo la Kawe na Ubungo 2010 walijaribu weeee wakakwama. Hata mimi sishauri CDM ijitoe Chalinze maadamu wameshampata mgombea.
 
Vipi kuhusu kauli ya Dr Slaa iliyosema "damu lazima imwagike"?

Kumbuka mhe rais Kikwete alitoa hiyo kauli kama mwenyekiti wa CCM, na Dr Slaa alitoa hiyo kauli yake kama katibu mkuu wa CHADEMA. Haya nambie unasemaje kuhusu kauli ya babu?
Sheria ifuate mkondo wake. Wote wawili washitakiwe ili mahakama itoe tafsiri ya kauli zao na impact yake katika jamii.
 
Pasco umelenga pale ninapopazungumzia kila mara. Pamoja na mtiririko mzuri wa Dr. kwa mfumo uliopo wa kuwapokea wanachama kutoka vyama vingine na kuwapa vyeo sio sahihi kabisa kwani inawavunja moyo makamanda ambao hujitoa mhanga usiku na mchana kueneza itikadi na sera za CDM.

Kampeni za juu - chini katika mazingira haya haziwezi kuleta ushindi kwa CDM. Pamoja na kutokujipanga mapema kwa chaguzi zozote viongozi wa juu ni bora na ni vema wangehamasisha wanachi kwa mtindo tofauti. Hata vipeperushi vingesaidia kuliko helikopta. Na wale viongozi wachache waliopo sehemu husika wapewe mamlaka kamili ya kusimamia na kuendesha kampeni kwani wanafahamika na wanawafahamu wananchi wa sehemu husika. Hata wakisema hapa hatutashinda viongozi waichukulie hiyo hali na kuachana na kampeni watumie mbinu mbadala wa kuwaamsha wananchi wa sehemu husika.

Sisi huku kwenye msing tunakatishwa tamaa kwa sababu hatupati ripoti zozote kutoka juu zenye maelekezo ya nini tufanye tuweze kuwaaminisha wanachi kwamba CDM italeta mabadiliko chanya ktk nchi hii. Kuna sehemu tunashia kufungua misingi na matawi lakini uhai wa chama hauendelezwi kwa sababu ya viongozi kukosa maelekezo kutoka juu.

Hiki chama nakipenda sana lakini kuna namna kinaonyesha kimekosa mwelekeo. Viongozi toeni mikakati ya kuamsha ari ya wananchama na wananchi kwa jumla.

Swala la umwagaji damu linaweza kutokea pale ambapo yule ambaye ameshindwa analazimisha kushinda!

Ujumbe huu umfikie Dr.W.Slaa freeman Mbowe Tumaini Makene, john Myika
 
Back
Top Bottom