Uchaguzi 2020 CHADEMA hawaaminiki, tuwapime kwa ishu ya Korona tu tutapata picha

Uchaguzi 2020 CHADEMA hawaaminiki, tuwapime kwa ishu ya Korona tu tutapata picha

Kuna mtu alikuwa anasunguka ulaya anasema mamia ya watanzania wanakufa lakini leo anafanya kampeni, anapanda mwendokasi, anakwenda kariakoo sokoni , manzese kwenye mitumba, mlimani city na kote kwenye mikusanyiko lakini havai barakoa ukifikiria alikwepa kwenda kwenye kesi yake akisema anajiweka karantini kwa kifupi walipanga kuichafua nchi bila kujali madhara yake
Alienda kuonana na ndugu wa marehemu wa watu waliyokufa kwa corona hapa Tz.
 
Wapinzani hawana misimamo na ndio maana wanajikuta wanapinga kila jambo tu,sasa ndio kama hili la Corona yani mtu anapiga kelele weee kwamba sijui watu wanakufa kimya kimya lakini hata yeye haamini jilo suala.
 
Hapo ndio mahali tuna kosea tuna sahau kuwa hata Chadema ina ongozwa na wanadamu wenye miili yenye damu na nyama kama CCm tu. Ukisha kuwa mwanadamu makosa yana weza fanyika tu, kuwa hukumu kwa kosa kama hilo na kusahau hayo mengine mema walio tufungua macho sio sahihi sana. Mtu yeyote yule ana weza fanya uamuzi ukawa sahihi au ukawa na dosari so ni vizuri kukubali makosa pale tunapo kosea na kujirekebisha.
 
Nenda kasome tena kuhusu wajibu na majukumu ya mbunge halafu ndio urudi hapa
Nonsense I dully understand the three arms of government and its core functions....lakini sio wajibu wake kama vile wanafanya wabunge wenu kugonga meza tuu na chorus zawo Ndiyooooooooo!!!!!!!
 
Mimi point yangu ambayo nilikuwa nafafanua hapa ni kwamba suala la Magufuli kusema kuwa Corona ni virus dhaifu ambae huwa anayeyuka kwenye joto haikuwa ni scientific fact bali ilikuwa ni porojo.

Yes ni poroja na kwa sababu sisi Watanzania kufikiri huwa ni kitu cha mwisho mtu hawezi kufikiri zaidi................. na huyo huyo uliyemtaja huwa ana porojo anadhani kila mtu akili yake imedumaa just take simple kuwaambia wafanyabiashara wadogo ile card ya 20k inaweza kukopa bank bima and so...................... Mtu unabaki like seriously? kitu hakina hata jina yaani anyway Mungu atusimamie kwa kweli.
 
Wanabodi,

Sina lengo la kuishambulia CHADEMA ila Kuna mambo yananitatiza kuhusu kuaminika kwao.

Sote tunajua timbwili walilolianzisha bungeni kuhusu korona mpaka kufikia kijikarantini kibabe. Wakati wenyewe wanajikaranti, wapiga kura wao walikuwa wanapambana uraiani kutafuta mkate wao wa kila siku.

Ila nikawaza, hivi kweli hawa wanauchungu na wapiga kura wao? Hivi hawa wanajua wapiga kura wao wanatafutaje riziki zao? Jibu nikalipata kuwa hawana uchungu na wapiga kura wao. Mgombea wao akiwa huko ughaibuni aliwasapoti kwa 💯%.

Wakati wabunge wa CHADEMA wakijikarantini, wenzao wa CCM walisimama kidete bila kuogopa kufa kuwapigania wapiga kura wao na watanzania kwa ujumla. Mbaya zaidi, CHADEMA iliwafukuza wabunge waliokataa mpango huo dhalimu. Ninashangaa wakijiita chama cha demokrasia, hamna kitu hapo.

Kama hayo hayatoshi, nilidhani CHADEMA watapiga kelele kuzitaka mamlaka zihairishe uchaguzi kwani kuna gonjwa la hatari la korona. Aah wapi, mwenyekiti aliyekuwa anavaa Kama ninja au Batman pamoja na sauti ya Lissu kutoka Tena sijui mji gani huko ubelgiji sasa wanakusanya watu, no social distance no facial masks. Wakihojiwa wanasema korona ipo, sasa watu hawa Kama wanaamini hivyo, si watakuwa wauwaji hawa?

Anyway, nimegundua nini ujue? Jamaa wanamkubali sana jembe JPM kwa vitendo ila wanamkataa kwa maneno. Matendo yao yanamkubali sana bwana mkubwa na ndio maana nikaandika uzi huu:

Uchaguzi 2020 - Zikiwa zimebaki siku 20, wapinzani wanashindana huku akili na mioyo yao ikiamini mshindi ni Magufuli

Tuwakatae wapinzani kwani wamejidhihirisha kuwa sio waaminifu.

Tarehe 28 kura zote kwa John Magufuli, mbunge na diwani wa CCM.

Amani Msumari.

Tanga.
Nimefurahi kuona Rais Magufuli amepita humuhumu akiwa Kawe
 
Back
Top Bottom