CHADEMA haya mnayoyafanya ndio yalipelekea tukaletewa Hayati Magufuli

Mwangwi wa kilio cha uoga cha CCM wazidi kuchekesha, MWE.
 
Kweli kaanza vizuri, tatizo Kuna wanaccm wanamuundia zengwe
 
Nani alikudangaja baada ya chadema kusema kuna ufisadi magufuli alikuja kumaliza ufisadi? Unajua zilipokwenda trilion 1.3 kwenye ripoti ya CAG (prof Assad enzi zile)? unajua ni ma trillion mangapi yamepigwa kwenye idara mbali mbali katika ripoti ile? Unajua kwanini madini hayakaguliwi na CAG? Actually uliongezeka mara 10 ya kipindi cha mtangulizi wake.

Kwanini unatumia neno TUKALETEWA inamaana sisi kama nchi hatuko huru kuamua nani awe raisi na nani asiwe raisi bali watu wachache wa ccm ndo wanaamua nchi hii nani awe raisi.
 
Mbowe anawatesa sana, Kwanini hamjifunzi waliojaribu kupambana nae karibu wote wameshakata ringi mwingine kakata moto

Makonda hoi
Sabaya mali ya nyampala huko jera
Mwendazake kakata moto
Mambo sasa hata hajulikani kama bado yupo kazini au amestaafu

Na wengine wengi,...
 
Vitu hivi haviji kwa hisani. Hupiganiwa na hata baadhi hupoteza maisha na mali.

Mama ni diplomat na democrat . Hatataka achafuliwa kama wafuasi wa Ccm wanavyotamani atumie nguvu.
 
Chadema ni chama cha umma sio cha mwenyekiti. Mkikosea spana ziko pale pale.
 
Kwa hii comment Nchi bado mko wajinga wengi sana kwahiyo huamini kwamba umaskini pia unachangiwa kwa mi VYEO ya hovyo hovyo unajua wanatumia kiasi Gani duh
 

Tuchukulie uko sahihi haya unayosema, kwa sasa Cdm/Lisu hawasikilizwi, je wasidai katiba mpya kwa sababu anayesikilizwa ni mama tu? Mbona wakati wa Magufuli pia tuliambiwa anasikilizwa kuliko wapinzani, hapo tushike lipi? Mkuu mbona umeumia cdm kudai katiba mpya bila hata kutoa mapendekezo wafanyeje, zaidi ya kutaka wampe mama muda bila hata time frame? Ww kwa mtazamo wako, ni lini mama atakuwa tayari ndio katiba ianze kudaiwa?
 
Tukiachana na mahaba ya chama hivi kwa hali ya nchi sasa ukizingatia tulipotoka dai la kwanza ilifaa kuwa katiba mpya? tena kwa kuweka rehani amani yetu?
Jamani tuna majeraha muacheni mama atuponye....wakati vijana wanakosa ajira, wakati tunawekewa VRF za kiuonevu na watumishi kunyimwa nyongeza wengine walikimbilia dubei, hawajui tulopitia sisi tusioweza hata kukimbilia malawi. Tumeanza vizuri na mama wasimtibue.
 
Jitu kama Mdude katolewa jela Tu kaanza matusi hapo hapo kwa waliomtoa..
Bangi tupu
Halafu ni kiongozi eti chadema

Hebu punguza munkari, mdude sio kiongozi, alipewa nafasi ya kuongea kama muhamasishaji, na lengo ni kujua watu wa aina zote wanaiongeleaje katiba. Au ulitaka wapewe nafasi wasomi tu, wachungaji tu bila kuchanganya na wahuni? Unapozungumza jambo la kijamii utakutana na watu wa aina zote, hivyo uvumilivu ni jambo la msingi. Sasa ww hata uvumilivu umekushinda kisha unawapangia cdm wafanye ili kuwafurahisha ccm?
 
m
Tatizo tunaamini kuwa huru ni HISANI ya Mtawala
Mngeyaongea na kuyaishi haya wakati wa Magufuli ningewaona wanaume kweli. mbona mlikimbia kama uhuru sio hisani?
 
Mkuu umezungumza point ambayo nimekuwa nikiisema sana hapa jukwaani Chadema hawataweza kwenda mbele kwa kutumia mawazo yaleyale ya Mwenyekiti wa kudumu, waruhusu mtu mwingine alete changamoto zingine.
 
Eti tija ya Taifa hebu badilisheni Mwenyekiti wa tokea enzi za Pontio Pilato.
 
Agenda ya Katiba mpya ni ya muhumu sana,lakini anayedai Katiba Mpya hana nia njema yaani anataka kutumia hiyo Katiba mpya kupata madaraka. Na anayeyekataa Katiba hana nia njema anataka kutumia Katiba iliyopo kubaki madarakani. Tatizo hili ndiyo lilivuruga mchakato wa Katiba mpya wakati wa JK.

Yule mzee JK alikuwa na nia njema kabisa akitoka madarakani awe ametuachia Katiba iliyobora lakini wanasiasa wa CCM na Upinzani(UKAWA) wakavuruga ule mchakato kwa sababu ya kupigania maslahi yao badala ya maslahi ya nchi.

Mama tokea mwanzo akiongea tu unaona nia yake ya kutuachia Katiba iliyobora kabisa lakini CCM na Upinzani (CHADEMA) watamvuraga kama walivyomvuruga JK na hakuna Katiba itakayopatika sana sana tutaiingiza nchi kwenye vurugu za kisiasa kwa maslahi ya wanasiasa.

Wanasiasa wa CCM na Upinzani acheni upumbavu wenu,wenye akili tunawachora lakini wapumbavu akina Mdude Nyagali na Sabaya watatumika kutuletea vurugu zisizo na msingi.
 
Hawa chadema wanatuvunja moyo 2015 niliwapigia kura 2020 pia lkn kwa hya mazingaombwe yao itawagharimu
 
Naunganmkono hoja. Chadrma ni kikundi cha wahuni. Yaan hata jiwe hajapasuka tumbo tayar nchi washaleta fujo.
Kwa kweli kwa hili tuko na mama.

Kwanza katiba si hitaji la wananchi ni hitaji la chadema washinde uchaguzi waende ikulu.

Hatukubali.
Wabinafsi sana hawa, yani mama asikamilishe miradi, asiboreshe maslahi ya watumishi, asiboreshe maisha ya wananchi...pesa awape wao wakatuandikie makorokocho huko in the name of katiba mpya. Na ukizingatia mama hajakataa kasema tumpe tu muda.
Kama wamemiss posho wavumilie tu, mbona sisi tumevumilia hali ngumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…