Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Bila kusahau Ikulu itajaa wachaga na watu wa kaskazin tu.Yaan mungu atuepushe mbali na hiki chama kuchukua Dola.
cdm wakipewa nchi hatutaruhusiwa kumsema raisi.hatutaruhusiwa kufanya mikakati ya uchaguzi kabla ya uchaguzi.hatutaruhusiwa kwenda mahakamani mahakama zitafungwa kwenye utawala huu.kwasababu katiba ya cdm yenyewe hazitambui haki ya mtu kwenda mahakamani.

mahakama zote zitafungwa tutahukumiwa na kamati za cdm tu.
 
Naomba kujua chama ambacho kimeacha mlango wazi kwa mwanachama kukishitaki mahakamani?naamini hakuna chama kinahitaji kupoteza muda na wanachama wake mahakamani badala ya kwenda ku-preach sera na malengo kwa wananchi.
 
Mleta mada ameleta mada ya kijinga.

CHADEMA haiwezi kuleta udikteta kwani tayari tunaishi kwenye udikteta unaosimamiwa na CCM.

Unajaribu kuwatisha watu ambao hawatishiki tena.

Kama ni kupigwa mabomu ya machozi, CHADEMA wanaongoza.

Kama ni kubambikiwa kesi lukuki, hata za kuitwa magaidi, CHADEMA wanaongoza.

Kama ni kupigwa na polisi na wapenzi na wanachama wao kuuwawa pia, CHADEMA wanaongoza.

Niseme nini tena ili juha kama huyu mleta mada aache kuleta mada za kipumbavu?

Ni Watanzania gani hao mnaodhani wanadanganyika na tisha-toto hizi za kijinga?
Moderator na Invisible tafadhali muwe mnatuepusha na wazushi kama hawa, wanaotaka kupotosha ukweli, kwamba nchi imefika pabaya, na udikteta huu umeletwa rasmi na CCM.

Uthibitisho ni Sheria ya Makosa ya Mtandao ambayo inakiuka Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayothibitisha haki ya Uhuru wa Maoni, Kujieleza, Kutafuta na Kusambaza taarifa muhimu kwa jamii.

Sasa bloggers nao watafunga mdomo?
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi!.
Preamble: Chadema ni Chama cha Kimokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!, hii thread ni ya swali tuu, Hivi Chadema ilivyo, bado haijakabidhiwa nchi, inatoa maamuzi ya kiimla Jee Chadema Ikikabidhiwa Nchi hapo October 2015!, Hakuna Hatari ya Uwezekano wa Kuigeuza nchi yetu kuwa ni nchi ya Utawala wa Kidikteta?!. Pasco
Pasco
Wanabodi, hili swali niliwahi kuliuliza kule nyuma, ila kilichotokea katika mchakato mzima wa kumkaribisha Lowassa ndani ya Chadema, ndio muendelezo wa huu udikiteta niliuozungumzia hapa, na sasa ni dhahiri Chadema inakwenda kuchukua nchi October kupitia Lowassa, hivyo sasa for sure Tanzania tunakwenda kuongozwa na chama cha kidikteta, na kiukweli Lowassa ni kiongozi dikteta wa ukweli, ila pia nakubaliana na hii hoja yangu kuwa Tanzania kwa hapa tulipofikia, tunahitaji chama cha kidikteta na rais dikteta kama Lowassa ambaye atakuwa ni benevolent dictator kufanya mambo yaende.

Ingekuwa kama huu udikiteta wa viongozi wa Chadema, isingewezekana kwa mwanachama mpya anapokelewa leo, kesho anakwenda kuchukua fomu za urais ambazo zilipaswa kutolewa na Katibu Mkuu wa chama, lakini kufuatia Lowassa kukaribishwa kidikiteta, Katibu Mkuu nae akaamua kuleta udikiteta wake kugoma kutoa fomu, Mwenyekiti dikteta akautumia udikiteta wake, kupoka majukumu ya Katibu Mkuu, na kutoa fomu yeye!, Katibu Mkuu atake asitake!, anune asinune!, asuse asisuse!, fomu zikatolewa!.

Kiukweli mwanzo niliukasirikia udikiteta huu kwa jinsi ulivyoshughulikia suala la Zitto nikiamini alionewa!, lakini leo nimefarijika baada ya kujiridhisha kuwa kumbe huu udikiteta wa Chadema, ni msumeno unakata kote kote, kama upanga wa makali kuwili!, unao opatare bila ubaguzi, kama upanga huu au msumeno huu, ulimkata Zitto na kuishia kujitimkia zake, sasa umemkumba Katibu Mkuu ambaye ameamua kununa na kususa, then huu ni udikiteta wa haki bin haki, hauna double standards, yaani uamuzi wa kupiga mapanga shwa... Zitto alipoleta za kuleta, akapigwa panga shwa... Mwamba Lowassa alipopiga hodi Chadema, kuna watu wakataka kugoma kumfungulia mlango eti tuu kwa vile yuko kwenye listi ya mafisadi wa Chadema, ule ule udikiteta ukasaidia, mlango ukafunguliwa kinguvu, Lowassa akaruhusiwa kuingia, na sasa ndio mgombea wa Chadema na UKAWA!, maadamu nyie mliko Chadema unaujua udikiteta huu, dawa iliyobakia sio kususa, ni ama mjinyamazie tuu na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku, au tumieni haki yenu ya kidemokrasia ya fungasheni na ondokeni!.

Japo maamuzi ya kidikiteta sometimes sio mazuri, lakini kiukweli kwenye hili la Lawassa, udikiteta huu ni mzuri, kwa sababu ndio utakaisaidia Chadema kuingia ikulu.

Tena namsisitizia Rais Lowassa akifika tuu Magogoni,

  1. Kazi ya kwanza ni kuipurura CCM malizo zake zote ilizozikwapua kwa umma wa Watanzania na kujimilikisha, hivyo CCM itabaki landless, penniless na poweless hivyp kujifia zake natural death!.
  2. Kazi ya pili, ni kuzirudisha zile nyumba zote za umma viongozi wa CCM walizijigawia wakisimamiwa na Fisadi John Pombe Magufuli ambaye alizigawa hadi kwa vimada wake!.
  3. Kazi ya tatu ni kuwapandisha kizimbani mafisadi wote, wakiwemo wa EPA, na wale mafisadi wawili waliokuwa wapangaji wa ile nyumba nyeupe!.
  4. Fisadi wa kwanza kwa kufanya biashara ikulu ile kinga ya kutokushitakiwa inahusu kutokushitakiwa kwa kutekeleza majukumu ya urais, kwa vile kufanya biashara ikulu sii miongoni mwa makumu ya urais, then kinga ile haihusiki na wanashitakika!.
  5. Wa pili ni kwa kupageuza pale 'patakatifu' petu kugeuka ni pango la walanguzi!, tena hadi kesi ya tule tujizawadi twa suti 3 za Seville itatinga mahakamani,
  6. Nyingine nyingi zitafuatia...

Na kwa jinsi baadhi ya watu walivyomtesa rais wetu huyu, akiingia kuna watu sijui watakomaje!.

Pasco
 
Wanabodi!.

Preamble: Chadema ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!, hii thread ni ya swali tuu, Hivi Chadema ilivyo, bado haijakabidhiwa nchi, inatoa maamuzi ya kiimla Jee Chadema Ikikabidhiwa Nchi hapo October 2015!, Hakuna Hatari ya Uwezekano wa Kuigeuza nchi yetu kuwa ni nchi ya Utawala wa Kidikteta?!. Pasco

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayofuatia misingi ya sheria, taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977.

Katiba ndio sheria mama, kila kitu kuhusiana na shughuli yoyote ndani ya JMT ni kwa mujibu wa Katiba!. Sheria yoyote, kanuni yoyote na taratibu yoyote, inayokwenda kinyume cha katiba ni batili!.

Katiba yetu imeweka utaratibu wa kutafuta haki ndani ya JMT ni kupitia mhimili wa mahakama. Vyama vyote vya siasa nchini, viko kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa!.

Kwenye sheria ya vyama hivyo, vyama kabla ya kusajiliwa, vinapaswa kuwasilisha katiba ya chama hicho na kupitiwa na wanasheria, ikukutwa iko sawa kwa mujibu wa katiba ya nchi, ndipo chama hicho hupewa usajili wa muda, kisha usajili wa kudumu!.

Hivyo ndivyo Chadema ilivyofanya ule mwaka 1992. Uliwasilisha katiba safi ya kidemokrasia yenye ukomo wa vipindi vya uongozi, kuwa ni vipindi viwili tuu, na wanachama wa Chadema walikuwa wako huru kufuata sheria za nchi!.

Mwaka 2006, Chadema ilifanya mabadiliko ya katiba, katika mabadiliko hayo, kile kipengele cha ukomo wa madaraka, kilinyofolewa kinyemela bila kujadiliwa popote!, hivyo marekebisho yaliwasilishwa kwa msajili wa vyama, hayakuwa tena na kipengele hicho cha ukomo, na kiliyeyuka bila muhtaasari wa kikao chochote kilichokijadili kipengele hicho!, hivyo marekebisho yaliyowasilishwa kwa msajili, kipengele hicho hakikuwepo, as if kimejadiliwa na kufikia uamuzi kiondolewe!, wakati kiukweli, hakikujadiliwa popote na yeyote bali kilinyofolewa tuu kinyemela, na katiba iliyowasilishwa mwaka 2006 hakikuwepo tena!.

Lengo la watungaji wa katiba mama ya Chadema, lilikuwa zuri, kwa uongozi wa Chadema kuwa na ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ili kupokezana vijiti ili kuzuia uongozi wa kisultani!. Mwaka huo wa 2006, wakaingia wajanja fulani!, wakakinyofoa kipengele kile, sasa uongozi wa Chadema hauna ukomo!. Yaani ni uongozi wa maisha mpaka kiongozi atakapoamua mwenyewe kuwa sasa amechoka!.

Mabadiliko hayo ya katiba ya Chadema ya mwaka 2006, pia yalipenyeza kipengele kinachomzuia mwanachama wa Chadema, kupeleka kesi yoyote mahakamani kukishitaki chama!. Hi ni kipengele cha kidikteta kuminya haki, na kiko kinyume cha katiba ya JMT, ambayo inasisitiza chombo pekee cha kutoa haki ndani ya JMT ni mahakama!. Kwa kipengele hiki, Chadema imejijengea himaya yake ya kidikteta ndani ya JMT ambayo haiutambui mhimili wa mahakama!. Na mwanachama ukipeleka jambo lolote mahakamani, ukishindwa, hapo ndipo mwisho wa uanachama wako wa Chadema!.

Sasa nawauliza wanasheria na watetezi wa haki za binaadamu, hivi mwana Chama wa Chadema akikosa haki ndani ya chama chake akaitafute wapi?!.

Kama Chadema hivi tuu ni chama na bado hakijapewa dola, kimepenyeza vifungu vya kidikteta na kinyume cha katiba kwa kutoutambua mhimili wa mahakama, jee kikipewa nchi hiyo October, si ni kina uwezekano kabisa wa kuisimamisha kabisa katiba yenyewe na kutangaza utawala wa kiimla na kidikiteta jumla?!.

Hili la Katiba ya Chadema, nimewahi kulizungua hapa na nilishutumiwa sana na kunyooshewa vidole kuwa mimi ni CCM!.

Leo nimelikumbuka na kulizungumzia hapa, kufuatia mwanachama fulani wa Chadema, kupoteza uanachama wake, simply kwa kosa la kutafuta haki yake kwenye vyombo halali vya kutoa haki!.

Kwa udikiteta huu, na unaokwenda kinyume cha katiba ya nchi, enyi members wa jf wenye uelewa na sheria na katiba, ndio mnataka kutueleza ni i kuhusiana na Chadema katika kufuata sheria taratibu na kanuni?!.

Nalirudia swali la msingi, Katiba ya Chadema ni "Unconstitutional" Jee ni Batili?. Na Chadema Ikipewa Nchi, Hakuna Hatari Kugeuka Dikteta?!.

Pasco.

NB. Kwa msisitizo: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa!, hajawahi kujiunga na chama chochote cha siasa, wala hana mpango wowote wa kujiunga na chama chochote, kwa lengo la lolote, bali ni political commentator, ambaye anazungumzia jambo lolote, kuhusu chama chochote. Sio mfuasi, mshabiki, wa kambi yoyote, au kiongozi yoyote, bali kama Mtanzania mwingine yoyote, kuna watu anaowakubali kijamii, kiuchumi na kisiasa, na siku ya kupiga kura, atapiga kura kuchagua kiongozi.

Update 1.

Mkuu MwanaHaki, kwanza asante kwa post hii, uzi huu unaelekea post 100, hii ndio posti ya kwanza kuijibu kwa sababu ndio post pekee iliyojikita kwenye subject matter!, na kufuatia post hii, nimeipeleka kule juu ili wenye kuhitaji kuujua ukweli, waujue ukweli, tuwaache hawa wajinga wajinga waendelee kupiga porojo!.

Hii sio mara ya kwanza kulizungumzia hili la Katiba ya Chadema kunyofolewa kipengele hicho cha ukomo wa madaraka!. Nilipouliza mwanzo nilijibiwa hivi.

Soma kwa makini hapo kwenye bold!, kisha tazama hapa kama ulivyoshauri, tena ni scanned copy na sio soft copy!
Suala hili lilifafanuliwa vyema na JJ Mnyika kama hivi.

Majibu ya Mnyika anasema 2006 walitunga katiba mpya!, taarifa iliyopo ofisi ya Msajili sio katiba mpya bali ni marekebisho ya Katiba!.

Yaani Chadema imewasilisha marekebisho ya katiba yenye kifungu ambacho kimenyofolewa kinyemela, hakikujadiliwa popote, yaani katiba ya 2004 imeweka ukomo wa vipindi viwili vya uongozi, katiba ya 2006 ikavinyofoa kinyemela na sasa uongozi wa Chadema ni for life!. Excuse ya kuhalalisha uharamia huu, ni kuiita katiba ya 2006 ni katiba mpya!. Katika constitutional making process zote za kutunga katiba mpya, katiba ya zamani hujadiliwa kipengele kwa kipengele, na ndipo katiba mpya hutungwa. Hakuna mahali popote kipengele hiki cha ukomo wa kipindi cha uongozi, kilijadiliwa!, kwa lugha rahisi, kipengele hiki kili 'just vanish into thin air!.

Na kipengele kinachokiuka katiba ya JMT ni hiki.

x. CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi nawanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama.

Pasco
Nafanya rejea kuhusu muktadha wa udikiteta ndani ya nchi ambao Chadema inauspicious kelele kupitia UKUTA na Udikiteta halisi uliomo ndani ya Chadema, jee tuishauri Chadema kuondoa kwanza boriti kwenye jicho lake ndipo lifuate kibanzi kwenye jicho la mwenzie? !.

Au mkuki ni kwa nguruwe tuu?!.

Nashauri katika utekelezaji wa kuuvunja huu UKUTA Mkuu nje, Chadema pia ivunje vile vikuta vyake vidogo vya ndani by practising what you preach! .
Jumapili Njema.
Pasco
 
Hapo ndo unafiki wa pasco unapoaanza mtu akisimamia katiba mnasema dikitetor akishidwa kusimamia mnaanza ooh hakuna uwajibikaji.
je mnataka wafanye nini?
Mkuu JME, hapa nazingatia sana ulichosema kuhusu mtu akisimamia katiba kuhusu dhana ya udikiteta! .

Pasco
 
Wanabodi, hili swali niliwahi kuliuliza kule nyuma, ila kilichotokea katika mchakato mzima wa kumkaribisha Lowassa ndani ya Chadema, ndio muendelezo wa huu udikiteta niliuozungumzia hapa, na sasa ni dhahiri Chadema inakwenda kuchukua nchi October kupitia Lowassa, hivyo sasa for sure Tanzania tunakwenda kuongozwa na chama cha kidikteta, na kiukweli Lowassa ni kiongozi dikteta wa ukweli, ila pia nakubaliana na hii hoja yangu kuwa Tanzania kwa hapa tulipofikia, tunahitaji chama cha kidikteta na rais dikteta kama Lowassa ambaye atakuwa ni benevolent dictator kufanya mambo yaende.

Ingekuwa kama huu udikiteta wa viongozi wa Chadema, isingewezekana kwa mwanachama mpya anapokelewa leo, kesho anakwenda kuchukua fomu za urais ambazo zilipaswa kutolewa na Katibu Mkuu wa chama, lakini kufuatia Lowassa kukaribishwa kidikiteta, Katibu Mkuu nae akaamua kuleta udikiteta wake kugoma kutoa fomu, Mwenyekiti dikteta akautumia udikiteta wake, kupoka majukumu ya Katibu Mkuu, na kutoa fomu yeye!, Katibu Mkuu atake asitake!, anune asinune!, asuse asisuse!, fomu zikatolewa!.

Kiukweli mwanzo niliukasirikia udikiteta huu kwa jinsi ulivyoshughulikia suala la Zitto nikiamini alionewa!, lakini leo nimefarijika baada ya kujiridhisha kuwa kumbe huu udikiteta wa Chadema, ni msumeno unakata kote kote, kama upanga wa makali kuwili!, unao opatare bila ubaguzi, kama upanga huu au msumeno huu, ulimkata Zitto na kuishia kujitimkia zake, sasa umemkumba Katibu Mkuu ambaye ameamua kununa na kususa, then huu ni udikiteta wa haki bin haki, hauna double standards, yaani uamuzi wa kupiga mapanga shwa... Zitto alipoleta za kuleta, akapigwa panga shwa... Mwamba Lowassa alipopiga hodi Chadema, kuna watu wakataka kugoma kumfungulia mlango eti tuu kwa vile yuko kwenye listi ya mafisadi wa Chadema, ule ule udikiteta ukasaidia, mlango ukafunguliwa kinguvu, Lowassa akaruhusiwa kuingia, na sasa ndio mgombea wa Chadema na UKAWA!, maadamu nyie mliko Chadema unaujua udikiteta huu, dawa iliyobakia sio kususa, ni ama mjinyamazie tuu na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku, au tumieni haki yenu ya kidemokrasia ya fungasheni na ondokeni!.

Japo maamuzi ya kidikiteta sometimes sio mazuri, lakini kiukweli kwenye hili la Lawassa, udikiteta huu ni mzuri, kwa sababu ndio utakaisaidia Chadema kuingia ikulu.

Tena namsisitizia Rais Lowassa akifika tuu Magogoni,

  1. Kazi ya kwanza ni kuipurura CCM malizo zake zote ilizozikwapua kwa umma wa Watanzania na kujimilikisha, hivyo CCM itabaki landless, penniless na poweless hivyp kujifia zake natural death!.
  2. Kazi ya pili, ni kuzirudisha zile nyumba zote za umma viongozi wa CCM walizijigawia wakisimamiwa na Fisadi John Pombe Magufuli ambaye alizigawa hadi kwa vimada wake!.
  3. Kazi ya tatu ni kuwapandisha kizimbani mafisadi wote, wakiwemo wa EPA, na wale mafisadi wawili waliokuwa wapangaji wa ile nyumba nyeupe!.
  4. Fisadi wa kwanza kwa kufanya biashara ikulu ile kinga ya kutokushitakiwa inahusu kutokushitakiwa kwa kutekeleza majukumu ya urais, kwa vile kufanya biashara ikulu sii miongoni mwa makumu ya urais, then kinga ile haihusiki na wanashitakika!.
  5. Wa pili ni kwa kupageuza pale 'patakatifu' petu kugeuka ni pango la walanguzi!, tena hadi kesi ya tule tujizawadi twa suti 3 za Seville itatinga mahakamani,
  6. Nyingine nyingi zitafuatia...

Na kwa jinsi baadhi ya watu walivyomtesa rais wetu huyu, akiingia kuna watu sijui watakomaje!.

Pasco
Bandiko hili linazungumzia faida za udikiteta.

Pasco
 
Kwani Udikteta una tatizo gani? Kwangu mimi poa tu kama udikteta ndiyo utakao tutoa hapa tulipo kwenye dimbwi la Umaskini, ujinga, Unyonge n.k basi na iwe hivyo!

Jamii zote Duniani zina lengo moja la kuboresha na kutatua matatizo ya Wananchi wake ila njia za kufika huko ndio hutofautiana, hivyo kama CHADEMA wakiwa Madikteta kwanza mimi kwangu hata kama wakifuta Chaguzi nchini powa tu cha muhimu nchi iende na iondoke hapa tulipo, cha muhimu hawa watawala wa sasa hivi Kikwete, Pinda &Co. wauwaji wa maalbino na Mungu awalaani waondoke hilo ndiyo muhimu!
Mkuu Kijakazi, naomba kuutumia ujumbe wako huu kuhusu udikiteta uwafikie wana UKUTA! .

Pasco
 
Pasco umetoka povu sana nchi yetu inhitaji viongozi wenye element za udiketa tusingwe wahi kusikia milion kumi za kununua mboga wala nyoka mwenye makengez wat cdm did whether is unconstitutional or nt let them do tanzania inahitaji viongozi kama haw wanareact mapema then it's over tuko nyuma sana hizi porojo za watu kama pasco ndo zinaidumaza hii nchi
Mkuu the boss 23, kumbe taifa letu linahitaji viongozi wenye elements za udikiteta, waambie hawa jamaa zetu ili hitaji ili lieleweke kwao.

Pasco
 
Pasco

uchambuzi uliotoa kuhusu shida ya katiba ya Chadema na usimamiaji wa Katiba husika haujazingatia kiini cha migogoro ndani ya Chadema na namna chama kinavyotumia miongozo yake kutanzua hiyo migogoro.

Hivi, andiko hili ulobandika hapa, unataka tuamini ati ni hao waliofukuzwa pekee ndio wanafahamu kuhusu kunyofolewa kwa vifungu vya katiba ya Chadema peke Yao?

ndio kusema maelfu ya wanachadema waliobaki Hawajui lolote kuhusu vifungu tajwa?

Jipya lingine ninaloliona kwenye post yako ni kuwa: Chadema wanafanya makosa kama sio dhambi kusimamia misingi ya chama chao, hivi sio Pasco huyuhuyu anayewakemea CCM WANAPOSHINDWA kusimamia misingi ya chama chao? Ama Pasco unafikiri CCM wakianza kusimamia misingi yao Leo hii, utasema CCM wanaongoza ki-dikteta?

Nauliza tu!
Mkuu 50Thebe, ni kweli CCM wanaongoza kidikteta! .

Pasco
 
Wanabodi!.

Preamble: Chadema ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!, hii thread ni ya swali tuu, Hivi Chadema ilivyo, bado haijakabidhiwa nchi, inatoa maamuzi ya kiimla Jee Chadema Ikikabidhiwa Nchi hapo October 2015!, Hakuna Hatari ya Uwezekano wa Kuigeuza nchi yetu kuwa ni nchi ya Utawala wa Kidikteta?!. Pasco

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayofuatia misingi ya sheria, taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977.

Katiba ndio sheria mama, kila kitu kuhusiana na shughuli yoyote ndani ya JMT ni kwa mujibu wa Katiba!. Sheria yoyote, kanuni yoyote na taratibu yoyote, inayokwenda kinyume cha katiba ni batili!.

Katiba yetu imeweka utaratibu wa kutafuta haki ndani ya JMT ni kupitia mhimili wa mahakama. Vyama vyote vya siasa nchini, viko kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa!.

Kwenye sheria ya vyama hivyo, vyama kabla ya kusajiliwa, vinapaswa kuwasilisha katiba ya chama hicho na kupitiwa na wanasheria, ikukutwa iko sawa kwa mujibu wa katiba ya nchi, ndipo chama hicho hupewa usajili wa muda, kisha usajili wa kudumu!.

Hivyo ndivyo Chadema ilivyofanya ule mwaka 1992. Uliwasilisha katiba safi ya kidemokrasia yenye ukomo wa vipindi vya uongozi, kuwa ni vipindi viwili tuu, na wanachama wa Chadema walikuwa wako huru kufuata sheria za nchi!.

Mwaka 2006, Chadema ilifanya mabadiliko ya katiba, katika mabadiliko hayo, kile kipengele cha ukomo wa madaraka, kilinyofolewa kinyemela bila kujadiliwa popote!, hivyo marekebisho yaliwasilishwa kwa msajili wa vyama, hayakuwa tena na kipengele hicho cha ukomo, na kiliyeyuka bila muhtaasari wa kikao chochote kilichokijadili kipengele hicho!, hivyo marekebisho yaliyowasilishwa kwa msajili, kipengele hicho hakikuwepo, as if kimejadiliwa na kufikia uamuzi kiondolewe!, wakati kiukweli, hakikujadiliwa popote na yeyote bali kilinyofolewa tuu kinyemela, na katiba iliyowasilishwa mwaka 2006 hakikuwepo tena!.

Lengo la watungaji wa katiba mama ya Chadema, lilikuwa zuri, kwa uongozi wa Chadema kuwa na ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ili kupokezana vijiti ili kuzuia uongozi wa kisultani!. Mwaka huo wa 2006, wakaingia wajanja fulani!, wakakinyofoa kipengele kile, sasa uongozi wa Chadema hauna ukomo!. Yaani ni uongozi wa maisha mpaka kiongozi atakapoamua mwenyewe kuwa sasa amechoka!.

Mabadiliko hayo ya katiba ya Chadema ya mwaka 2006, pia yalipenyeza kipengele kinachomzuia mwanachama wa Chadema, kupeleka kesi yoyote mahakamani kukishitaki chama!. Hi ni kipengele cha kidikteta kuminya haki, na kiko kinyume cha katiba ya JMT, ambayo inasisitiza chombo pekee cha kutoa haki ndani ya JMT ni mahakama!. Kwa kipengele hiki, Chadema imejijengea himaya yake ya kidikteta ndani ya JMT ambayo haiutambui mhimili wa mahakama!. Na mwanachama ukipeleka jambo lolote mahakamani, ukishindwa, hapo ndipo mwisho wa uanachama wako wa Chadema!.

Sasa nawauliza wanasheria na watetezi wa haki za binaadamu, hivi mwana Chama wa Chadema akikosa haki ndani ya chama chake akaitafute wapi?!.

Kama Chadema hivi tuu ni chama na bado hakijapewa dola, kimepenyeza vifungu vya kidikteta na kinyume cha katiba kwa kutoutambua mhimili wa mahakama, jee kikipewa nchi hiyo October, si ni kina uwezekano kabisa wa kuisimamisha kabisa katiba yenyewe na kutangaza utawala wa kiimla na kidikiteta jumla?!.

Hili la Katiba ya Chadema, nimewahi kulizungua hapa na nilishutumiwa sana na kunyooshewa vidole kuwa mimi ni CCM!.

Leo nimelikumbuka na kulizungumzia hapa, kufuatia mwanachama fulani wa Chadema, kupoteza uanachama wake, simply kwa kosa la kutafuta haki yake kwenye vyombo halali vya kutoa haki!.

Kwa udikiteta huu, na unaokwenda kinyume cha katiba ya nchi, enyi members wa jf wenye uelewa na sheria na katiba, ndio mnataka kutueleza ni i kuhusiana na Chadema katika kufuata sheria taratibu na kanuni?!.

Nalirudia swali la msingi, Katiba ya Chadema ni "Unconstitutional" Jee ni Batili?. Na Chadema Ikipewa Nchi, Hakuna Hatari Kugeuka Dikteta?!.

Pasco.

NB. Kwa msisitizo: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa!, hajawahi kujiunga na chama chochote cha siasa, wala hana mpango wowote wa kujiunga na chama chochote, kwa lengo la lolote, bali ni political commentator, ambaye anazungumzia jambo lolote, kuhusu chama chochote. Sio mfuasi, mshabiki, wa kambi yoyote, au kiongozi yoyote, bali kama Mtanzania mwingine yoyote, kuna watu anaowakubali kijamii, kiuchumi na kisiasa, na siku ya kupiga kura, atapiga kura kuchagua kiongozi.

Update 1.

Mkuu MwanaHaki, kwanza asante kwa post hii, uzi huu unaelekea post 100, hii ndio posti ya kwanza kuijibu kwa sababu ndio post pekee iliyojikita kwenye subject matter!, na kufuatia post hii, nimeipeleka kule juu ili wenye kuhitaji kuujua ukweli, waujue ukweli, tuwaache hawa wajinga wajinga waendelee kupiga porojo!.

Hii sio mara ya kwanza kulizungumzia hili la Katiba ya Chadema kunyofolewa kipengele hicho cha ukomo wa madaraka!. Nilipouliza mwanzo nilijibiwa hivi.

Soma kwa makini hapo kwenye bold!, kisha tazama hapa kama ulivyoshauri, tena ni scanned copy na sio soft copy!
Suala hili lilifafanuliwa vyema na JJ Mnyika kama hivi.

Majibu ya Mnyika anasema 2006 walitunga katiba mpya!, taarifa iliyopo ofisi ya Msajili sio katiba mpya bali ni marekebisho ya Katiba!.

Yaani Chadema imewasilisha marekebisho ya katiba yenye kifungu ambacho kimenyofolewa kinyemela, hakikujadiliwa popote, yaani katiba ya 2004 imeweka ukomo wa vipindi viwili vya uongozi, katiba ya 2006 ikavinyofoa kinyemela na sasa uongozi wa Chadema ni for life!. Excuse ya kuhalalisha uharamia huu, ni kuiita katiba ya 2006 ni katiba mpya!. Katika constitutional making process zote za kutunga katiba mpya, katiba ya zamani hujadiliwa kipengele kwa kipengele, na ndipo katiba mpya hutungwa. Hakuna mahali popote kipengele hiki cha ukomo wa kipindi cha uongozi, kilijadiliwa!, kwa lugha rahisi, kipengele hiki kili 'just vanish into thin air!.

Na kipengele kinachokiuka katiba ya JMT ni hiki.

x. CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi nawanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama.

Pasco
Nadhani chadema pamoja na kuwa kilishakufa kinapaswa kifutwe kwa sababu kinakiuka kaitiba ya JMT
 
Pasco kumbe ulishalidadisi hili kitambo, shikamoo blaza
 
bw pasco tanzania inahitaji kiongozi dikteta ili kurudisha misingi ya azimio la arusha​,
Mkuu Prince asante kwa taarifa hii kuhusu hitaji la kiongozi dikiteta na ni kweli dikiteta John Pombe Joseph Magufuli anarudisha misingi ya Azimio la Arusha, hivyo tuungane wote kuwashangaa wana UKUTA? !.
Pasco
 
Pasco, unaweza kuwa na hoja ya maana, lakini kwa maoni yangu, naona unaiwasilisha vibaya; na au kwa nia mahususi kwako binafsi, yenye lengo maalum ambalo haliwezi kutusaidia sana kama taifa, bali kuwaondoa watu katika hoja ya msingi-kwamba katika muktadha huu wewe Pasco wa JF unaweza kuwa unafanya "spinning". Wewe mwenyewe unafahamu kwamba Chadema kama chama cha siasa kisheria na kikatiba inayo haki ya kujiwekea utaratibu wake maalum kwa wanachama wake.

Pasco, wewe unafahamu kwamba kujiunga na chama au kikundi chochote ni sawa na kuingia mkataba, na kwenye mkataba huwa kuna kipengele kinachoeleza ni wapi au ni namna gani mtashughulikia mgongano au kutoelewana iwapo itatokea hivyo. Suala la kuzuia mwanachama kukimbilia kortini na badala yake kusisitiza kumaliza suala hilo ndani ya vikao vya chama haiwezi kuwa udikiteta hata kidogo kiasi cha wewe kuanza kuvuruga maoni ya wanaopinga kuzuia mikutano ya kisiasa ambayo imeruhusiwa na katiba ya nchi.
 
Mkuu 50Thebe, ni kweli CCM wanaongoza kidikteta! .

Pasco

Mkuu Pasco

Heshima kwako.

Mbona unaninukuu namna hii? Mchango wangu ule ulikuwa kwenye context nyingine ambayo napata ukakasi ikiwa naweza kurudia kuandika content ile ile kwa context ya sasa.

Pengine niseme hivi: takribani miezi 12 sasa tumeshuhudia mabadiliko makubwa sana kupindukia kwenye siasa zetu hususani kwenye eneo la ideology za vyama hivi (ingawa haipo wazi sana). Kwa mfano, waliolaani ufisadi kiasi cha kuombea tupate raisi dikteta sasa wanalaani udikteta. Waliotuhumiwa kwa ufisadi sasa wameunda chombo (mahakama ya mafisadi - wahujumu wa uchumi). Bila shaka wataunda chombo maalumu kitakachochunguza namna uhujumu uchumi unavyofanyika badala ya polisi na PCCB. Hivyo kuna contrast kubwa sana ya maisha ya siasa zetu toka mara ya mwisho nilipotupia maoni yangu haya.

Kwa muhtasari huu na swali lako kwamba: CCM inatawaliwa kidikteta ama lah? Maoni yangu ni kwamba CCM haitawaliwi kidikteta. Tunachoshuhudia ni usimamizi wa sheria, kanuni na taratibu zikiwamo 'presidential decree' ndio zinatumiwa na serikali ya CCM. Wakati mwingine najiuliza ikiwa Mh Raisi Magufuli anatumia katiba tofauti na ile iliyotumika wakati wa muhula wa Mh Raisi Kikwete.

Nihitimishe kwamba: CCM hawaongozi nnchi kidikteta. Bali safari hii wameonesha kusimamia sheria, kanuni na taratibu kwa umadhubuti zaidi. Na pale miongozo hii inakwama tayari wametuonesha kwamba wanaweza kutumia 'presidential decree' ili kupata matokeo.

Nawasilisha.
 
Labda ni bora tuwe na Serikali ya Kidikteta, ili watu wanyooke, wawajibike, waache kugeuza kila kitu DILI!

Ukienda Polisi, akikamatwa mtu, hawamwulizi kama ana hatia. Wanauliza ana pesa kiasi gani ili wamuachie. Askari wanashirikiana na majambazi. HATUNA Jeshi la Polisi linalostahili kuitwa Jeshi la Polisi.

Ukienda Hospitali, mgonjwa - haswa mjamzito - anaulizwa ana pesa kiasi gani, ili aweze kupata huduma stahiki. Asiye na pesa atajifungulia hapo hapo chini, sakafuni, na kama sio siku yake ya kuitwa na Yehova, atapona. La sivyo MTAZIKA! Wauguzi na madaktari wameigeuza kazi yako kuwa ajira!

Ukienda Mahakamani, hapo laana tupu. Mtu amekamatwa na ushahidi umetimia, lakini nduguze "wanamweka sawa" Hakimu. Kesi itakapoanza kusikilizwa kuna kitu kinaitwa Preliminary Hearing, ambapo Waendesha Mashtaka (Mawakili wa Serikali) ndio wanapaswa kusema iwapo watuhumiwa ana kesi ya kujibu au la. Baada ya hapo, kesi inaahirishwa ili Hakimu apitie vielelezo vya State Attorneys. Kesi inaporudi kuanza kusikilizwa, Hakimu anasema ushahidi hautoshi, kwa hiyo bora Mahakama isipoteze muda na fedha za serikali. Mtuhumiwa anachoropoka.

Wizarani huko ni balaa! Wanajipangia masurufu kwenye kasma za Semina, Warsha, Makongamano, ambayo yote ni HEWA. Pia kuna wafanyakazi HEWA, ambao ni wale waliostaafu, waliofariki, waliopunguzwa, n.k. Wanaendelea kulipwa na TAMISEMI inalijua hili. Hata HAZINA nako wanajua.

Sasa mnaitaka Serikali LEGELEGE ya CCM au mnaitaka Serikali DIKTETA ya CHADEMA, itakayofuta ufedhuli wote huu?

Kuna mengi sijayasema.... yanakera MNO!
Mkuu MwanaHaki hapa umesema kweli kuhusu serikali ya kidikteta japo wakati ukiandika haya ilitarajiwa Chadema ndio washinde na kuendesha udikiteta huu, maadam CCM ndio iliyoshinda na kuuendesha udikiteta ule ule ambao Chadema ingeuendesha, kuna ugumu gani Chadema kumsupport Dikiteta Mzalendo John Pombe Joseph Magufuli? .

Mkuu Pasco, u dikteta sio jambo la kusifiwa likitoka chama chochote. Nafikiri JPM sio Dikteta , nadhani ameona nchi haina nidhamu ya kazi na wanasiasa pia hawana nidhamu ya sheria wala kazi. Nashauri Raisi ajikite kuwatumikia wananchi ila pia awaruhusu wanasiasa wafanye siasa maana ni kazi yao na sheria zinawaruhusu. Ukitaka mtu àheshimu sheria lazima wewe pia uwe mfano wa kwanza wa kuheshimu sheria. Nafikiri Rais wetu ataliona hili jambo kwa mwanga ulio bora maana anachofanya kwa watanzania ni chema ila aache wengine nao watimize wajibu wao
 
Nadhani chadema pamoja na kuwa kilishakufa kinapaswa kifutwe kwa sababu kinakiuka kaitiba ya JMT

kufutwa ndo suluhisho la kutatua suala la
udikteta? hivi kama na wewe ndo umetoa
mchango ktk post hii tuna safar ndefu sana
ktk elimu yetu kilikufa chadema magufuli
kura milion 8 chadema wanafuata milion
kura milion 6 halafu kilikufa.
 
Back
Top Bottom