Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Mkuu MwanaHaki hapa umesema kweli kuhusu serikali ya kidikteta japo wakati ukiandika haya ilitarajiwa Chadema ndio washinde na kuendesha udikiteta huu, maadam CCM ndio iliyoshinda na kuuendesha udikiteta ule ule ambao Chadema ingeuendesha, kuna ugumu gani Chadema kumsupport Dikiteta Mzalendo John Pombe Joseph Magufuli? .

Pasco
Ha ha haaaa

Yaani CHADEMA waisapoti CCM? Political goal yao itamezwa mkuu.
 
Nchi yetu,bila kutawaliwa kidikiteta hataenda,hapa ilipofikia hakuna mwenye Kauai ya mwisho,mafisadi wanalindwa,waauwaji wa alubinyo hawashughulikiwi ipasavyo,wataalumu wetu wamegeuka wanasiasa baada ya kuona ndipo mahali pa kuwatoa fasta kimaisha,wafanyabiashara wakubwa wamegeuka viongozi wa kisiasa kukwepa kulipa kodi,na kufanya biashara haramu .afu useme uitawale tanzania kawaida kawaida tu,
Mkuu By Hair, kumbe nchi yetu bila kutawaliwa kidikiteta mambo hayendi!, hii inamaanisha ili Tanzania twende mbele udikiteta ni lazima! ,sasa hizi kelele za UKUTA ni za nini? .

Pasco
 
Ha ha haaaa

Yaani CHADEMA waisapoti CCM? Political goal yao itamezwa mkuu.
Vyama vyote vina the same political goals kuingia ikulu, ili kwenda kutekeleza some political objectives zilizoorodheshwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama husika. Wananchi wamekikataa Chadema na kuipa CCM, kupitia kwa Magufuli, na alipoingia tuu kwa kuona ilani ya uchaguzi ya Chadema ni mzuri akaamua kuitelekeza, jee kuna ubaya gani Chadema kumsupport Dikiteta Mzalendo John Pombe Joseph Magufuli kwa kuitelekeza ilani ya Chadema? . Kama political objectives ni Ikulu, Chadema wameisha ikosa Ikulu lakini wamepatiwa fursa ya ilani yao kutekelezwa kwa udikiteta ule ule ule ambao wangeutekeza wao, sasa kwanini wasimsupport Dikiteta Magufuli kwa kuyafanya yale yale waliyotaka kuyafanya kama tungewapa ridhaa, sasa huyu mwenye ridhaa ndio anayafanya hayo, kwa nini Chadema wasimsupport? . Au huu udikiteta wafanye Chadema tuu ndio sawa, udikiteta akifanya mwingine. ...UKUTA! .

Pasco
 
Vipi bado unataka tuendelee kujadili uzi huu ?
Hatuujadili uzi huu bali naijadili hoja ya udikiteta uliomo ndani ya uzi huu nikionyesha michango ya ma masupporter wa Chadema humu walivyokuwa wakiunga mkono udikiteta wa Chadema, lakini leo ndio hawa hawa wanaibuka kupinga udikiteta wa Magufuli huku lengo likiwa lile lile!.

What a double Standard, udikiteta ukifanywa na Chadema sawa! ,ukifanywa na Magufuli unageuka nongwa hadi kuundiwa UKUTA! .

Pasco
 
What a double Standard, udikiteta ukifanywa na Chadema sawa! ,ukifanywa na Magufuli unageuka nongwa hadi kuundiwa UKUTA! .
Pasco
Kwa hiyo unataka kusema JPM anafanya udikteta?
 
Hakuna udikteta mzuri.
Udikteta ni ubinafsi na uroho wa kutukuzwa.

Ndio maana watawala hawapendi kusikia hilo neno likitajwa kwa kuhusishwa na utawala wao. Hakuna anayependa kuitwa dikteta.
Ni sifa mbaya sana. Na hata wapizani walipokuwa wanataja kuwa anatakiwa rais dikteta hawakumaanisha kwa sifa za dikteta. Walimaanisha rais anayesimamia sheria na katiba kwa haki bila kubagua watu kwa dini zao, itikadi zao za kisiasa ,rangi zao ,makabila yao na kanda zao.

Madikiteta siku zote wana hulka ya ubaguzi ,ubinafsi ,ukatili, Ubwana mkubwa.
Ili uwe dikteta ni Lazima utumie dola kwenye siasa.

Ili uwe dikteta ni lazima ubague watu kwenye madaraka.

Ili uwe dikteta ni lazima uwaweke ndugu na marafiki wa karibu kwenye nafasi za uongozi ndani ya serikali na ndani ya vyombo vya dola.
Ili uwe dikteta ni Lazima uweka marafiki na ndugu kwenye vyombo vya sheria na bunge ili uweze kudhibiti au kuondoa kabisa mihimili mingine ya nchi.

Ili uwe dikteta ni lazima uzibe midomo ya wale wanaokosoa na kumulika utawala wako.

Ili uwe dikteta ni lazima uchague watu wako wa karibu kusimamia uchumi na hata biashara na mikataba mikubwa.

Ili uwe dikteta ni lazima umtoe kwenye serikali kila anayepingana na mawazo yako. Ili uwe dikuteta ni lazima uwe na uwezo wa kuteua kila mkuu wa idara na taasisi na uweke ndugu na watu wako wa karibu na ukigundua kuwa kuna asiye wa kwako basi unamuondoa mara moja.

Ili uwe dikteta ni lazima uchague watawala wa ngazi za chini wasiofuata sheria.

Ili uwe dikteta mzuri na utimize malengo yako ya udikteta ni lazima ubadilishe katiba ili ufute mfumo wa kidemokrasia na haki za binadam. Hii itasaidia kutawala watu wanaojua kuwa mfumo uliopo ni wa kidikteta na rais dikteta. Vinginevyo usipoweka mfumo na katiba ya kidikteta unaweza ukajikuta unapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kuishia jela baada ya muda wako kuisha.

Chadema waliamua kubadili katiba ili waendane na mfumo wao unaitwa wa kidikteta. Nadhani walifanya hivyo kutokana na kuona jinsi watu wanavyotafuta madaraka ndani ya chama kwa lengo la kukikabidhi chama mikononi mwa CCM. Wenye chama waliona jinsi vijana waliokua wanapata umaarufu walivyokuwa wanatumika kukihujumu chama ili kisambaratike kama walivyofanya NCCR mageuzi.
Wazee wa chadema waliliona hili na kumwamini Mbowe zaidi aendelee kukiongoza chama. Na hii imesaidia mpaka leo Chadena kipo na uchaguzi wa mwaka Jana kilijizolea kura mil.6 tena baada ya uchaguzi uliosimamiwa na Mwenyekiti wa CCM na tume yake ya uchaguzi. Uchaguzi uliojawa rafu na jazba,vitisho na ukorofi wa kila aina toka CCM.

Najiuliza hivi kama Magufuli asingepata urais je, angechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM?
Je,ni demokrasia kweli ndani ya Chama cha mapinduzi iliyosababisha Mh. Magufuli kuwa mwenyekiti wa Chama?
Jibu ni hapana !
CCM inamkabidhi rais wa nchi chama ili aweze kukibeba chama ki uchumi, kisiasa na kijamii kwa kupitia mgongo wa serikali na nguvu ya dola?
Ukishakuwa mwenyekiti na rais inakua ni vigumu wapinzani wako kukosoa chama bila kukutaja na wanapokutaja wanaadhibiwa kwa kumtaja Rais wa nchi na amiri jeshi mkuu.?
Kwenye nchi ya kidemokrasia inabidi uwe mvumilivu mana pia ni mwenyekiti wa chama kama walivyo wengine. Ukipoteza uvumilivu utajikuta muda wote unatumia madaraka ya urais tu na vyomvo vya dola hata kwenye mambo ya kulumbana kisiasa kama mwenyekiti.
 
Tuache unafiki udicteta ni aina ya uongozi. Hitler asingekuwa dictator ujeruman isingefika hapo. So tanzania tunahitaji uongoz ulio serious. Watu wanaiba pesa hakuna hatua. Tuache ushabiki kipofu.
Mkuu Tanzania Leo, nakubaliana na wewe kuwa Tanzania tulipofika tulihitaji Udikteta na tumeupata. Sasa UKUTA unalalamikia nini? !.
Pasco
 
kwani udikteta ndoo kitu kipya au? jaribu kuangalia nchi zote ambazo zimepiga hatua kubwa kimaendeleo ni mfumo upi wanatumia kuendesha dola,kwa ufupi ni kwamba katika democrasia kuna makona mengi yanayochelewesha uwajibikaji hivyo ili nchi iendelee ktk kulinda maslahi ya wengi lazima iwe na elements za udikteta kwahiyo udikteta hauepukiki kwa nchi kupiga hatua za kimaendeleo!!!!!!!!
Udikteta kwa Maendeleo. .naunga mkono hoja
 
Mkuu Tanzania Leo, nakubaliana na wewe kuwa Tanzania tulipofika tulihitaji Udikteta na tumeupata. Sasa UKUTA unalalamikia nini?
Pasco

UKUTA unalalamika haya hapa chini:

Wanabodi,

Naomba kuanza na angalizo: Ukosoaji wowote, utaofanywa kwa kinachofanywa na serikali yetu, kama unatolewa in good faith, kwa nia ya kujenga na sio kubomoa, huu ni ukosoaji mzuri na ni very heathy kwa serikali yoyote yenye nia ya dhati ya kufuata katiba na kuheshimu utawala wa sheria!, kinyume cha hapo ni udikiteta!.

Kitendo cha Mkuu mmoja wa mihimili ya dola, kuingilia haki, uhuru na mamlaka za mihimili mingine, sio kukiuka ile kanuni ya Checks and Balances and The Separation of Powers?!.

Nimehamasika Kuanzisha uzi huu, kufuatia mjadala wa ami ya rais kuzuia safari za nje, pia imewakumba watumishi wa bunge na watumishi wa mahakama!.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Sio kila anayelipwa na fedha za umma ni mtumishi wa serikali!, hata vyama, watumishi wote wa vyama vya siasa, kikiwemo Chadema, wanalipwa kwa fedha za umma kupitia ruzuku, hawa sio watumishi wa umma!.

Kuna kanuni za uendeshaji wa serikali zote dunia nzima, ambapo kuna mihimili mitatu, seikali bunge na mahakama!, rais wa nchi ni mkuu wa mhimili mmoja tuu wa serikali, mkuu wa bunge ni spika na mkuu wa mahakama ni Jaji Mkuu!. Kitendo cha rais wa nchi kutoa amri ya kutosafiri kwa watumishi wa bunge na mahakama bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi ni rais kuingilia uhuu na madaraka ya vyombo hivi, huku ni kwenda kinyume cha utawala bora!, mimi nakuita ni sehemu tuu ya udikiteta wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli!, kitendo cha watu wanaojua the principle of separation of powers, hawakupaswa kulinyamazia hili!.

Kwa vile katazo la rais kuzui safari za nje bila kibali, limetolewa kwa nia njema ili kuzuia safari za nje zisizo na manufaa kwa taifa, rais alipaswa kuwaita Spika na Jaji Mkuu, ili spika na yeye atoe amri kama hiyo kwa wabunge na watumishi wa bunge kuomba kibali kwa Spika kupitia kwa Katibu wa Bunge, na watumishi wa mahakama, kuomba kibali kwa Jaji Mkuu kupitia kwa Msajili wa Mahakama ili ami ya rais iwahusu watumishi wa serikali tuu ikiwa ni seikali kuu na serikali za mitaa. Wabunge wapate vibali ofisi ya bunge na watumishi wa mahakama wapate vibali vya mahakama ili kuepusha kuingilia majukumu kati ya mihimili hii!.

Naomba kuwasilisha.

Heri ya Mwaka Mpya.
Pasco
 
Mkuu Pasc
Vyama vyote vina the same political goals kuingia ikulu, ili kwenda kutekeleza some political objectives zilizoorodheshwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama husika. Wananchi wamekikataa Chadema na kuipa CCM, kupitia kwa Magufuli, na alipoingia tuu kwa kuona ilani ya uchaguzi ya Chadema ni mzuri akaamua kuitelekeza, jee kuna ubaya gani Chadema kumsupport Dikiteta Mzalendo John Pombe Joseph Magufuli kwa kuitelekeza ilani ya Chadema? . Kama political objectives ni Ikulu, Chadema wameisha ikosa Ikulu lakini wamepatiwa fursa ya ilani yao kutekelezwa kwa udikiteta ule ule ule ambao wangeutekeza wao, sasa kwanini wasimsupport Dikiteta Magufuli kwa kuyafanya yale yale waliyotaka kuyafanya kama tungewapa ridhaa, sasa huyu mwenye ridhaa ndio anayafanya hayo, kwa nini Chadema wasimsupport? . Au huu udikiteta wafanye Chadema tuu ndio sawa, udikiteta akifanya mwingine. ...UKUTA! .

Pasco

Mkuu Pasco.

Kwamba ni CHADEMA pekee ndio sana mamlaka ya kujiendesha kidikteta hapa Tanzania ni hoja kubwa. Ki-academician hii ni hoja ya masomo ya PhD.

Itoshe kusema: inasikitisha sana kuona CHADEMA wanaumizwa na Magufuli anayezingatia sheria. Jambo ambalo CHADEMA walilipigia kelele sana. Ukitazama namna chama hiki kilivyosimamia sheria zake hususani ile safisha safisha ya wasaliti na masalia, inashtua na kustaajabisha iweje waone vibaya pale Magufuli anavyosafisha mianya rushwa, uzembe na ufisadi kwenye serikali ya awamu ya tano. Vile ambavyo wewe Pasco umeshangaa, nami nimeshangaa vivyo hivyo. Hapo ndipo yanaibuka maswali mengi ya msingi kuhusu Uzalendo wa Viongozi wa CHADEMA (maana sijasikia wamebadili katiba yao). Moja ya maswali ni je viongozi wa CHADEMA wanasimamia nini hasa ikiwa hawaungi mkono utekelezaji wa maono yao ya Tanzania ya mabadiliko waliyoainisha kwenye election manifesto yao ya 2015?

Bila shaka hata lile neno lao maarufu la tulianza na mungu, tupo na mungu na tutamaliza na mungu sasa limeingia shombo. Maana Mungu mwenyewe atashindwa achague nini cha kubariki kinachofanywa na CHADEMA. Abariki sala na maombi ya kupata Raisi dikteta? Ama abariki maombi ya kumzuia Raisi dikteta asifanye kazi zake za Uraisi?

Well, safari ya CHADEMA kujipatia identification (utambulisho) wake bado mbichi sana.

Wasalaam
 
Hakuna udikteta mzuri.
Udikteta ni ubinafsi na uroho wa kutukuzwa.

Ndio maana watawala hawapendi kusikia hilo neno likitajwa kwa kuhusishwa na utawala wao. Hakuna anayependa kuitwa dikteta.
Ni sifa mbaya sana. Na hata wapizani walipokuwa wanataja kuwa anatakiwa rais dikteta hawakumaanisha kwa sifa za dikteta. Walimaanisha rais anayesimamia sheria na katiba kwa haki bila kubagua watu kwa dini zao, itikadi zao za kisiasa ,rangi zao ,makabila yao na kanda zao.

Madikiteta siku zote wana hulka ya ubaguzi ,ubinafsi ,ukatili, Ubwana mkubwa.
Ili uwe dikteta ni Lazima utumie dola kwenye siasa.

Ili uwe dikteta ni lazima ubague watu kwenye madaraka.

Ili uwe dikteta ni lazima uwaweke ndugu na marafiki wa karibu kwenye nafasi za uongozi ndani ya serikali na ndani ya vyombo vya dola.
Ili uwe dikteta ni Lazima uweka marafiki na ndugu kwenye vyombo vya sheria na bunge ili uweze kudhibiti au kuondoa kabisa mihimili mingine ya nchi.

Ili uwe dikteta ni lazima uzibe midomo ya wale wanaokosoa na kumulika utawala wako.

Ili uwe dikteta ni lazima uchague watu wako wa karibu kusimamia uchumi na hata biashara na mikataba mikubwa.

Ili uwe dikteta ni lazima umtoe kwenye serikali kila anayepingana na mawazo yako. Ili uwe dikuteta ni lazima uwe na uwezo wa kuteua kila mkuu wa idara na taasisi na uweke ndugu na watu wako wa karibu na ukigundua kuwa kuna asiye wa kwako basi unamuondoa mara moja.

Ili uwe dikteta ni lazima uchague watawala wa ngazi za chini wasiofuata sheria.

Ili uwe dikteta mzuri na utimize malengo yako ya udikteta ni lazima ubadilishe katiba ili ufute mfumo wa kidemokrasia na haki za binadam. Hii itasaidia kutawala watu wanaojua kuwa mfumo uliopo ni wa kidikteta na rais dikteta. Vinginevyo usipoweka mfumo na katiba ya kidikteta unaweza ukajikuta unapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kuishia jela baada ya muda wako kuisha.

Chadema waliamua kubadili katiba ili waendane na mfumo wao unaitwa wa kidikteta. Nadhani walifanya hivyo kutokana na kuona jinsi watu wanavyotafuta madaraka ndani ya chama kwa lengo la kukikabidhi chama mikononi mwa CCM. Wenye chama waliona jinsi vijana waliokua wanapata umaarufu walivyokuwa wanatumika kukihujumu chama ili kisambaratike kama walivyofanya NCCR mageuzi.
Wazee wa chadema waliliona hili na kumwamini Mbowe zaidi aendelee kukiongoza chama. Na hii imesaidia mpaka leo Chadena kipo na uchaguzi wa mwaka Jana kilijizolea kura mil.6 tena baada ya uchaguzi uliosimamiwa na Mwenyekiti wa CCM na tume yake ya uchaguzi. Uchaguzi uliojawa rafu na jazba,vitisho na ukorofi wa kila aina toka CCM.

Najiuliza hivi kama Magufuli asingepata urais je, angechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM?
Je,ni demokrasia kweli ndani ya Chama cha mapinduzi iliyosababisha Mh. Magufuli kuwa mwenyekiti wa Chama?
Jibu ni hapana !
CCM inamkabidhi rais wa nchi chama ili aweze kukibeba chama ki uchumi, kisiasa na kijamii kwa kupitia mgongo wa serikali na nguvu ya dola?
Ukishakuwa mwenyekiti na rais inakua ni vigumu wapinzani wako kukosoa chama bila kukutaja na wanapokutaja wanaadhibiwa kwa kumtaja Rais wa nchi na amiri jeshi mkuu.?
Kwenye nchi ya kidemokrasia inabidi uwe mvumilivu mana pia ni mwenyekiti wa chama kama walivyo wengine. Ukipoteza uvumilivu utajikuta muda wote unatumia madaraka ya urais tu na vyomvo vya dola hata kwenye mambo ya kulumbana kisiasa kama mwenyekiti.
Basi wapinzani kipindi kile wasingesema hii nchi inamuitaji Rais dikteta Maan udikteta una maana moja tu ya kutojari utu wa mtu. MI nawaona wapinzani nao ni wanafiki tu
 
Siku wakijifunza kujikosoa wenyewe ndio tutaamini kwenye kauli zao. Chadema haitaki kukosolewa kwavile tu hawana dola. Huwezi kuona mapro Chadema wakija na hoja za kuikosoa Chadema ili kijiandae vyema kuchukua dola. Wananchi wajifunze kudai haki zao nje ya mfumo wa sasa wakisiasa uliojaa ulaghai mzito.
 
CHADEMA kinavunja Katiba ya TANZANIA wazi wazi, si Mbowe, si Lisu, si Heche, si Saa nane, Si Kileo, si Mnyika, waliothubutu kuilinda Katiba ya Nchi.. Chadema kimekataza kwa mwanachama wake kutafuta Haki mahakamani, pale anapoona Haki yake imeminywa katika Chama.. Ukienda mahakamani unafukuzwa uanachama wako(unajifuta).... Hakuna mtu yoyote ndani ya Chadema anaweza kusimama kukosoa hili..

Hapo ndio utajua Chadema ni wachumia tumbo tu.. Sio wapo kupigania maslahi ya wanyonge.. Nani aliweka hiki kipengere katika katiba ya Chadema.. Ya kuvunja Katiba ya Nchi..
 
Back
Top Bottom