Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo: Ukosoaji wowote, utaofanywa kwa kinachofanywa na serikali yetu, kama unatolewa in good faith, kwa nia ya kujenga na sio kubomoa, huu ni ukosoaji mzuri na ni very heathy kwa serikali yoyote yenye nia ya dhati ya kufuata katiba na kuheshimu utawala wa sheria!, kinyume cha hapo ni udikiteta!.
Kitendo cha Mkuu mmoja wa mihimili ya dola, kuingilia haki, uhuru na mamlaka za mihimili mingine, sio kukiuka ile kanuni ya Checks and Balances and The Separation of Powers?!.
Nimehamasika Kuanzisha uzi huu, kufuatia mjadala wa ami ya rais kuzuia safari za nje, pia imewakumba watumishi wa bunge na watumishi wa mahakama!.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Sio kila anayelipwa na fedha za umma ni mtumishi wa serikali!, hata vyama, watumishi wote wa vyama vya siasa, kikiwemo Chadema, wanalipwa kwa fedha za umma kupitia ruzuku, hawa sio watumishi wa umma!.
Kuna kanuni za uendeshaji wa serikali zote dunia nzima, ambapo kuna mihimili mitatu, seikali bunge na mahakama!, rais wa nchi ni mkuu wa mhimili mmoja tuu wa serikali, mkuu wa bunge ni spika na mkuu wa mahakama ni Jaji Mkuu!. Kitendo cha rais wa nchi kutoa amri ya kutosafiri kwa watumishi wa bunge na mahakama bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi ni rais kuingilia uhuu na madaraka ya vyombo hivi, huku ni kwenda kinyume cha utawala bora!, mimi nakuita ni sehemu tuu ya udikiteta wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli!, kitendo cha watu wanaojua the principle of separation of powers, hawakupaswa kulinyamazia hili!.
Kwa vile katazo la rais kuzui safari za nje bila kibali, limetolewa kwa nia njema ili kuzuia safari za nje zisizo na manufaa kwa taifa, rais alipaswa kuwaita Spika na Jaji Mkuu, ili spika na yeye atoe amri kama hiyo kwa wabunge na watumishi wa bunge kuomba kibali kwa Spika kupitia kwa Katibu wa Bunge, na watumishi wa mahakama, kuomba kibali kwa Jaji Mkuu kupitia kwa Msajili wa Mahakama ili ami ya rais iwahusu watumishi wa serikali tuu ikiwa ni seikali kuu na serikali za mitaa. Wabunge wapate vibali ofisi ya bunge na watumishi wa mahakama wapate vibali vya mahakama ili kuepusha kuingilia majukumu kati ya mihimili hii!.
Naomba kuwasilisha.
Heri ya Mwaka Mpya.
Pasco