Mkuu Freeland, kwanza asante kuchangia uzi wangu huu, nakiri kuufahamu umuhimu wa kufuata sheria taratibu na kanuni, na hizi zinatungwa ili kuhakikisha haki inatendeka!. Lakini kwa Chadema kwenye katiba yao wameainisha taratibu za nidhamu ili kutoa haki, kwenye uendeshaji kesi na kufikia maamuzi, taratibu hizi zimewekwa kando na kutolewa maamuzi ya kiimla na vikao visivyo na mamlaka!, yaani katika kufikia uamu za haki, katiba imewekwa pembeni, watu wanyongwe tuu!, ila inapolalia kwao kwamba hili ni kosa la kustahili kunyonga, ndipo sasa Chadema inakuja mbio mbia na katiba yao kuwa sasa ile adhabu ya kunyonga itekelezwe kwa mujibu wa katiba!. What a double standard?!.
Kama hiyo katiba ipo, kwa nini haikufuatwa wakati wa kumhukumu Zitto, lakini leo ameshindwa kesi, vimbelembele hao mbio kwenye katiba!.
Nasisitiza kufuatwa kwa taratibu, sheria na kanuni za haki!.
Pasco