Bro itakuwa hujui siasa au tuseme kazi ya Siasa, hii ni ajira kama zilivyo ajira zingine maana hata muuza maziwa ya ng'ombe huongeza maji, inawezekana hujui kwa nini, ni kuchelewesha au kuzuia maziwa kuharibika haraka, japo mteja hupiga makelele.
Sasa chama chochote kilicho kwenye benchi cha siasa ni lazima kiongeze maji na maji haya ni kulinda chama kisidumae kutokana na wale waliopo serikalini wanatenda mazuri na kuonekana ni chama bora kinachofaa kuongoza milele japo wana mabaya.
Hivo basi nyinyi mliopo kwenye mabenchi ni lazima mupinge na kuponda jambo lolote lile linalofanywa na chama tawala bila ya vurugu wala ugomvi, hilo mnalolipinga iwe lipo sawa au halipo sawa - Mnapinga chochote kwa hoja na propaganda zilizosheheni vinogesho.
Si wamejenga madaraja na mazuri tu na mabasi ya mwendo kasi na faida ya mtumiko inaonekana basi hapo hapo unatakiwa upige kwa silaha zote na uponde vibaya mno, unaweza kusema zimetumika hela nyingi sana ambazo zingefaa kujenga mahospitali miko yote tena mahospitali ya kisasa yenye mashine zinazohitajika na vifaa vya kiuchunguzi.
Madaraja yaliyojengwa yamejengwa kwa kiwango cha chini na yameanza kubomoka na hatayachukua muda mrefu nchi imeingia hasara na yatahitaji kufanyiwa ukarabati baada ya kila miaka mitano wewe utasema kila siku.
Reli hii SGR haijafikia hata miaka miwili tayari reli zimeanza kulegalega na ukipanda ile behewa inavyotingishika ni balaa na kuna sehemu imeharibiwa na maji yaliyokatisha kutokana na mvua, wameijenga ile reli na hawakuifanyia misingi imara badhi ya tunnel kwenye milima zimeanza kufanya ufa taifa limeingia hasara kubwa sana kwani mkandarasi ni wa kiwango cha chini na inasemekana hajawahi kujenga reli ya aina hizi na zenye urefu, ile reli sasa inatishia maisha ya Watanzania.
Hio ndio siasa hakuna wala usijaribu kuisifu serikali ikiwa wewe ni chama pinzani, never! Bora ukae kimya kuliko kusifu ukisifu kidogo tu umeshaharibu kila kitu kwani chama kilichopo madarakani kitaitumia sentensi hio kuzidi kukudumaza.