Umoja wa kitaifa ni jambo la msingi sana kwenye ujenzi wa Taifa. Taifa la Tanzania limefanikiwa pakubwa sana kuwa na umoja wa kitaifa.
Ni kweli umoja wa kitaifa ni muhimu
Lakini panapotokea chama cha siasa ambacho kwa maslahi binafsi kinataka kutengenisha umoja wa kitaifa, lazima kichukiwe na wananchi.
Of course ni lazima kichukiwe. Chama Cha Mapinduzi - CCM ndicho kinachoharibu umoja huu kwa sababu ya uroho wa madaraka na ili kubaki madarakani, kinatumia hila zote ikiwemo kuua na kuumiza wanaowapinga, kuharibu chaguzi (rigging elections) kwa kutumia serikali na vyombo vya dola. Chama cha namna hii, hakiwezi kupendwa na watu na ndivyo ilivyo kwa CCM...
Ni kweli kila nchi inahitaji upinzani ili kuwa kama kioo kwa chama tawala. Lakini sio upinzani unaotishia na kupinga kila jambo linalofanywa na chama tawala.
Ni kama vile hujui hata dhana ya chama tawala na chama kilicho nje ya serikali (chama pinzani) na jinsi inavyofanya kazi..
Tangu lini chama tawala kikaunga mkono hoja za vyama vilivyo nje ya serikali? Unadhani hakijipendi siyo?
Viceversa yake ni kuwa, ni vigumu na haiwezekani kabisa chama kinachoongoza serikali/dola kukubaliwa na kuungwa mkono na chama kilicho nje ya serikali kwa sababu dhanà na maana nzima ya "chama tawala" na "chama cha upinzani" inajengwa katika dhana ya tofauti ya migongano ya KISERA na ITIKADI na MIPANGO...
Kwa dhana hii, chama tawala kikikosolewa sera na mipango na itikadi yake, basi chenyewe kitatafsiri kama ni shambulizi ya kuvunja umoja wa kitaifa na kitatumia kila njia haramu kujilinda...!!
Kupinga, ujenzi wa miradi mikakati, shule, hata sera na mipango madhubuti kwa taifa.
Huu ni UONGO wa mchana kweupe na bahati mbaya umeshindwa kuupaka rangi vizuri uongo huu ili ufanane na ukweli japo kidogo...!!
CHADEMA hawapingi haya na wananchi wanaelewa hivyo....
CHADEMA na sisi wengine tusio wanaCHADEMA tunachopinga na kutokukubaliana ni njia za utekelezaji wa miradi hii ambayo msingi wake ni ubovu wa vipaumbele (priorities) vya nchi kwa wananchi...
Hiki kimesababisha CHADEMA kujenga uhasama kwa wananchi. Kwa ufupi kimechukiwa.
Huu ni UONGO mwingine wa mchana kweupe...!!
Unapiga propaganda zilizoshindikana kufanya kazi kwa muda mrefu na kuikoa CCM. Ukisemacho hakipo na situation is contrary...
CHADEMA ni adui wa CCM na serikali....
Kinyume chake ni kuwa CHADEMA ni rafiki, mtetezi na tegemeo la wananchi wanyonge...
Na huu ndio msingi wa HOFU na WOGA wa CCM/serikali/dola kiasi cha kuanza kuitumia dola kwa maana ya (polisi, TISS, magereza, mahakama na DPP) vibaya kuumiza na kunyanyasa wananchi wote wasiowaunga mkono...!!