Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Tundu Lissu, akiongozana na viongozi wengine wa CHADEMA, Mhe. John Heche, Mhe. Amani Golugwa, na Mhe. Godbless Lema, walikutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tine Tonnes, katika makazi ya balozi Oysterbay, Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Lissu na ujumbe wake walijadili msimamo wa chama cha CHADEMA wa "No Reform No Election" na umuhimu wa Jumuiya za Kimataifa kusaidia Tanzania kuwa na mfumo wa uchaguzi wa haki, wazi, na wa kuaminika.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Balozi Tonnes alimuhakikishia Mhe. Lissu kuwa Norway itaendelea kuwa rafiki wa Tanzania katika kudumisha demokrasia na maendeleo.
Soma, Pia