Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Inashangaza sana na inatia huruma, dunia nzima ipo katika wimbi zito la kupambana na ugonjwa wa Covid-19. Ugonjwa ambao umeua watu zaidi ya laki moja dunia nzima.
Wanasiasa na wafuasi wa Chadema wanakesha mitandaoni kuiombea vibaya nchi yao ipate maambukizi ili chama tawala kionekane kilishindwa kuchukua hatua. Je huu ni uungwana?
Wanadiriki kupost picha ya maiti ikichukuliwa na wahudumu wa afya kuonyesha sasa mlipuko upo katika hali mbaya. Lakini hata kama ni kweli walipaswa kupost na kutoa maelezo ambayo sio ya kufitinisha kwamba hatua stahiki hazichukuliwi.
Hawajiulizi swali moja kubwa kwamba ugonjwa huu haubagui na watu ambao wako katika hatari ya kuupata ni watu wasio na uwezo.
Mimi binafsi nilitarajia wawe pamoja na serikali kuonyesha mshikamano katika kupambana na hili janga. Lakini wao siku nzima ni kuombea mabaya tu hasa wanaombea idadi ya reported cases ziwe nyingi. Na hii itawsaidia nini?
Mimi nilidhani wao kwa miaka hii mitano ya serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli wangepambanua nini ameshindwa kutekeleza katika ilani yake ya Chama ili ndio ziwe ajenda za kumkabili kisiasa,lakini sio kumuombea mabaya ili Covid -19 iuwe watanzania wengi ili waanze kumzodoa.
Labda sababu jamaa amepiga kazi tena ambazo zinaonekana kwa macho ndio maana wamekosa ajenda za kumkabili, zaidi ya maneno ya kitoto kama amejificha Chato kukwepa Covid -19.
Walianza na kisingizio cha zuio la kisiasa eti limewaporomosha kisiasa. Lakini yeye alizuia ile mikutano ambayo for publick interest ingezuia watu wasijengewe Mabarabara,zahanati na vituo vya afya,Mradi kama JNHHP, madaraja kama wami na busisi to kigongo n.k.
Na zuio hili alilifanya kwa mujibu wa wa katiba kama ibara ya 30(1) ya katiba ya JMT inavyo ainisha. Na ndio maana kuna mdau aliwaambia kama kama hili zuio ni udikteta basi nendeni HC mkaweke petition,wote walifyata mkia.
Na bahati nzuri aliruhusu siasa kwenye majimbo ili wasimwingilie na afanye maendeleo kwa manufaa ya umma.
Leo hii wamebakiza kuombea mabaya kwa nchi yao,na kuibua kilio cha tume huru wakati miaka yote ipo huru na wanashinda ubunge na madiwani. Inasikitisha sana kuwa na Chama cha namna hii.