Hebu twende darasani taratibu. Chama cha siasa ni kundi ama kikundi cha watu wanaotumia umoja wao kutaka ama kuongoza nchi kwa namna chama hicho kinavyojipambanua.
Kama ni hivyo ni lazima chama kiwe kina mfumo wa kuanzishwa yaani vyama havizuki bali kuna mifumo ya kuanzishwa kwake. Chama Rwandese Patriotic Front (RPF) kilianzishwa baada ya vita vya wanyarwanda kumalizika. Lakini CCM ilianzishwa baada ya kuviua vyama vya Afro Shirazi Party (ASP) na Tanganyika African National Union (TANU). Lakini wakati CCM inaanzishwa tayari TANU na ASP vilishakuwa ni vyama dola kwenye nchi zao.
Uchama dola ni ile hali ambapo chama cha siasa kilichopo kinachukuliwa kwa hiyari ama lazima kwamba ni chama cha Taifa. Kabla ya ya Mwaka 1992 ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi, CCM ilikuwa ni chama dola. Lakini baada ya hapo CCM ilikoma kuwa chama dola ingawa chenyewe kinatamani kuendelea kuwa chama dola.
Enzi CCM kilipokuwa chama dola kila sehemu kuliwa kuna matawi ya chama hicho. Jeshini, kwenye taasisi za elimu, masokoni, maofisini, mitaani huko kote chama ndicho kilikuwa ni sheria ilikuwa ni CCM. Kuna watu walipata vyeo vya kijeshi kwa kuwa tu walikuwa waenezaji wazuri wa itikadi za CCM majeshini. Leo hii CCM SIO CHAMA DOLA hata kama kinatamani kuwa hivyo.