Chadema imekosa hoja za kupambana na CCM na kwa mantiki hii wamekubali matokeo mapema

Tufahamishe chama dola kinakuwaje? Maana labda hatujui.
 
Huwezi kunipumbaza Ccm ni chama dola na kinatumia dola vizuri kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Ccm.
Hebu twende darasani taratibu. Chama cha siasa ni kundi ama kikundi cha watu wanaotumia umoja wao kutaka ama kuongoza nchi kwa namna chama hicho kinavyojipambanua.

Kama ni hivyo ni lazima chama kiwe kina mfumo wa kuanzishwa yaani vyama havizuki bali kuna mifumo ya kuanzishwa kwake. Chama cha Rwandese Patriotic Front (RPF) kilianzishwa baada ya vita vya wanyarwanda kumalizika. Lakini CCM ilianzishwa baada ya kuviua vyama vya Afro Shirazi Party (ASP) na Tanganyika African National Union (TANU). Lakini wakati CCM inaanzishwa tayari TANU na ASP vilishakuwa ni vyama dola kwenye nchi zao.

Uchama dola ni ile hali ambapo chama cha siasa kilichopo kinachukuliwa kwa hiyari ama lazima kwamba ni chama cha Taifa. Kabla ya ya Mwaka 1992 ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi, CCM ilikuwa ni chama dola. Lakini baada ya hapo CCM ilikoma kuwa chama dola ingawa chenyewe kinatamani kuendelea kuwa chama dola.

Enzi CCM kilipokuwa chama dola kila sehemu kuliwa kuna matawi ya chama hicho. Jeshini, kwenye taasisi za elimu, masokoni, maofisini, mitaani huko kote chama ndicho kilikuwa ni sheria ilikuwa ni CCM. Kuna watu walipata vyeo vya kijeshi kwa kuwa tu walikuwa waenezaji wazuri wa itikadi za CCM majeshini. Leo hii CCM SIO CHAMA DOLA hata kama kinatamani kuwa hivyo.
 
N
Nakuonea huruma sana. Ila sio kosa lako, kosa ni kuwa upo Chadema. Chama dola ni ni chama kinachotawala nchi maana kinasimamia masuala yote ya serikali.
 
N

Nakuonea huruma sana. Ila sio kosa lako, kosa ni kuwa upo Chadema. Chama dola ni ni chama kinachotawala nchi maana kinasimamia masuala yote ya serikali.u
Jionee huruma mwenyewe sio mimi. Chama dola mara nyingi kilikuwa enzi zile za Ushoshalisti na Ukomunisti duniani. Hamuwezi kuwa na mfumo wa vyama vingi hapo hapo mkawa na chama dola.

Kwenye mfumo wa chama dola hairuhusiwi kwenda kinyume na chama hicho na hata maamuzi ya Serikali yanaweza kubatilishwa na vikao vya chama hata kama ni kinyume cha sheria. Wewe ulikuwepo wakati ule hadi mahakamani kulikuwa na matawi ya CCM?
 
CCM imeshindwa kuongoza nchi, badala ya kupambana na maadui wa taifa umasikini, ujinga na maradhi wao wanapambana na CHADEMA.

Mmesahau! 1.5 trillion zilitafunwa na majizi CCM
 
Kawape hilo darasa makamanda wa ufipa. Hivi mtajenga ofisi kweli maana baada ya October hata ruzuku itakuwa ishu.
 
Eti Kigogo 2014 amekuwa source of info!

CCM ingekuwa inapambana kwa hoja tusingesikia rais akiwatishia wasimamizi wa tume ya uchaguzi kuwa anawalipa yeye mshahara. Tusingeona mabox ya kura yakitolewa vituoni kwenda kujazwa kura za ccm. Tusingeona uhayani na ukatili wa wazi kwenye chaguzi zetu, tena kwa uratibu wa vyombo vya dola ili ccm watangazwe washindi. Hicho chama kizee kina hoja gani ya kushindwa kupambana nazo? Kama ni miradi ya umeme, barabara nk ndio hoja za kubaki madarakani, leo hi weupe wa south Afrika wangekuwa bado madarakani.
 
Nyie mliojenga Ofisi ndiyo hawa wapima mapapai. Ofisi zinawasaidia nini kama kila siku ni kutoa matamko yanayopingana!!??
Hakuna mtu aliyepima mapapai. Ila sampuli za papai,fenesi, oil na mbuzi zilipelekwa kama mtego ili kujua ufanisi wa maabara.
 
Hakuna mtu aliyepima mapapai. Ila sampuli za papai,fenesi, oil na mbuzi zilipelekwa kama mtego ili kujua ufanisi wa maabara.
Hizo sampuli za mapapai zilitokana na samaki nguru ama mapapai. Unapopima sampuli si ndiyo unapima papai lenyewe? Kwa nini mantiki ndogo tu huwa zinawasumbua!!

Au huji neno sampuli linamaanisha kuwa ni sehemu ya kitu kinachopimwa? Yaani ukipimwa damu ikikutwa na UKIMWI wewe uliyetoa ile damu utakuwa huna UKIMWI au siyo wewe ndiye utakuwa umepimwa?
 
Hizo sampuli za mapapai zilitokana na samaki nguru ama mapapai. Unapopima sampuli si ndiyo unapima papai lenyewe. Kwa nini mantiki ndogo tu huwa zinawasumbua!!
Kwani yalipimwa mapapai kumi? Au sampuli ilichukuliwa kwenye papai moja? Lakini hoja ya msingi ni kujua ufanisi wa maabara ya taifa.
 
Weka ushahidi hapa rais akiwatisha watumishi wa tume ya uchaguzi.
 
Usiilinganishe ccm na hao vichaa wa siasa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…