SoC01 CHADEMA ina Matatizo 4 Makubwa na la 5 Ni Kubwa Zaidi: Nani ataiokoa?

Stories of Change - 2021 Competition

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Na. M. M. Mwanakijiji

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinataka kukiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani na hivyo kishike hatamu za uongozi wa taifa letu. Katika kufikia lengo hilo CHADEMA kimetumia mbinu mbalimbali na kushiriki chaguzi mbalimbali kuanzia ngazi za chini kabisa hadi kwenye nafasi ya Urais. Kimejaribu kuweka wagombea katika nafasi ya Urais, Ubunge, Udiwani na kwa muda kiliweza kujipatia waumini na wafuasi wengi ambao walikuwa tayari kukifanya kuwa chama mbadala.

Pamoja na mbinu, mikakati, na njia mbalimbali za kujaribu kuiondoa CCM madarakani CHADEMA haipo katika nafasi ya kukaribia kushika hatamu za uongozi wa taifa letu. Wanachama, mashabiki, wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wanapoangalia yaliyotokea Zambia, Malawi, Senegal, Malaysia na sehemu nyingine duniani ambapo vyama vya upinzani viliweza kuingia madarakani na kushika uongozi wanajikuta na maswali mengi. Wanajiuliza hawa wamewezaje? Kwanini haitokei Tanzania, tuna tatizo gani, kwanini kizingiti kilichopo hakivukiki?

Majibu ya Haraka
Wapo wanaotoa majibu ya haraka na mengine yanaonekana hata hayajafikiriwa vizuri. Majibu mawili mara nyingi yanatolewa na wale wanaojaribu kuelezea kwanini CHADEMA haijaweza kuindia madarakani. Kwanza, wanatuambia ni kukosekana kwa Katiba Mpya na la pili ni kutokuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi. Ndani ya hayo mawili ni hoja kuwa sheria zilizopo, mifumo na taasisi zote zilizopo hazifanyi kazi kwa uhuru na hivyo haviitendei haki CHADEMA. Hoja hizi ni za kujipa faraja tu na kutafuta udhuru; siyo sababu hasa.

Kama chama cha siasa na taasisi ya kisiasa naomba kutoa mapendekezo kuwa endapo CHADEMA haitajitathmini (self-assessment) uwezekano wa chama hiki pendwa na kongwe cha upinzani kushika madaraka unaendelea kusogea mbali kila baada ya uchaguzi mkuu. Ni katika muktadha huo naomba kuchokoza tathmini hii. Kwa maoni yangu (ambayo hayakuombwa) naamini CHADEMA haitoweza kushika madaraka Tanzania hadi pale itakapoweza kuyashughulikia matatizo yafuatayo.

1. Kimepoteza Ajenda Yake Kuu Inayokitofautisha
Mojawapo ya matatizo makubwa ya kisiasa ya CHADEMA ni kukosekana kwa ajenda kuu ya kisera na kiitikadi ambayo itakuwa tofauti na ajenda za chama tawala. Kama tutakavyoona hapa chini tatizo hili linatokena na matatizo mengine. CHADEMA wakati wa Kikwete (2005-2015) naweza kusema ilikuwa katika kilele cha siasa zake; naweza kuziita ni zama zake za dhahabu (golden age) kwani ni wakati huu tofauti yake na CCM ilikuwa wazi, bayana, na kamili.

Ajenda kuu ya CHADEMA wakati ule ilikuwa ni kupinga ufisadi. Mafanikio makubwa kwa chama hicho ilikuwa ni kuweza kuwashawishi Watanzania kuwa kulikuwepo na tatizo kubwa la ufisadi na kuwa ufisadi huo usingeweza kutenganishwa na CCM. Kufuatia kufunuliwa kwa orodha ya mafia wa Tanzania (Tanzanian mafia gang) na baadaye orodha ya mafisadi CCM kwa mara ya kwanza ilijikuta katika kujitetea (on defense). Tunakumbuka ilifikia mahali pa CCM kuja na wazo la “kujivua gamba” na kama wengi tulivyohisia jitihada hizo hazikuweza kuisafisha CCM. Chadema ilikuwa inaenda kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 ikiwa na nguvu ya hoja, itikadi, mwelekeo na mapendekezo mbadala.

2. Kimekuwa Chama cha Wasomi na Wenye Uwezo
Tatizo la pili na ninaamini linaenda kuwa kubwa sana sasa hivi na inawezekana ni mazao ya utawala wa Rais Magufuli (2015-2021) ni kuwa CHADEMA imeenda kuwa na mvuto zaidi kwa wasomi na watu wenye ukwasi wa kimaisha (elites and affluent individuals). Hili linaonekana sana katika aina ya hoja za kisiasa zinazotolewa na CHADEMA sasa hivi. Hatari ya hili ni kuwa CHADEMA kinatoka kuwa chama cha wanyonge na kuwa chama cha matajiri na wenye ukwasi. Tumeona jinsi gani taasisi za wasomi na watu maarufu ambao wamejitokeza mara kwa mara sasa kuitetea CHADEMA kiasi cha kwamba ile dhana ya kuwa chama ni cha kikabila inaenda kufa na sasa kinaenda kuwa chama cha matajiri na wasomi.

Swali la ni chama cha aina gani, cha nani, na kwanini CHADEMA inataka kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 linaanza kujibiwa kwa jibu linalotisha na kukatisha tamaa.

3. CHADEMA inafanana sana kimuundo na kimfumo na CCM.
Mojawapo ya matatizo ya kimsingi ya vyama vyetu vya upinzani ikiwemo CHADEMA ni kuwa kimuundo na mfumo kinafanana mno na CCM. Hili linamatokeo ya kiCCM. Mojawapo ya matokeo mabaya ya kurudi kwa mfumo wa vyama vingi nchini ni kuwa vyama vyetu vya kisiasa vilijikuta (bila kutafakari sana) kuchukua na kuiga kwa kiasi kikubwa muundo wa CCM. Ninalolizungumzia hapa kubwa ni jinsi gani mfumo wa “Kamati Kuu” ya chama na “Sekretariati ya chama” kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuweza kufuta na kuvunja maamuzi ya chini. Hili linaweza kuonekana ni sahihi lakini matokeo yake ni kuwa chama kinakuwa ni cha kitaifa kiutawala.

Ningeweza kutoa mifano michache hapa ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo yaliacha machungu mengi kwa wanachama, mashabiki na wapenzi wake. Lakini sitofanya hivyo kwa sababu wafuatiliaji wote wa siasa za nchi yetu wanaweza kukumbuka mifano hii. Kwa kadiri ya kwamba mifumo na utendaji wa CHADEMA unafanana na chama chenye miundo ya kisoshalisti kama CCM basi CHADEMA haitoweza kuepuka matokeo ya miundo hiyo. Kwa CHADEMA upungufu huu una madhara makubwa kwa sababu haina dola. CCM inaweza kusimamia miundo yake kwa sababu imeshika dola.

4. CHADEMA inaitegemea mno CCM kuweza Kuingia Madarakani.
Jambo hili niliwahi kuliandika miaka kadhaa huko nyuma. Kwa bahati mbaya bado halijabadilika. CHADEMA imekuwa siyo chama cha upinzani bali chama cha ushauri wa chama tawala. Na hili naweza kusema linagusa hata vyama vingine vya upinzani ambavyo vimegeuka kuwa wakosoaji na washauri wa CCM. Mara kadhaa tunashuhudia vyama vya upinzani vikiishauri serikali ifanye “hili” au “ifanye lile” na ikitokea serikali imefanya basi wapinzani wanajipongeza kuwa “tuliwashauri” na serikali isipofanya wapinzani wanaona “hawasikilizwi”.

Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuandika makala ya “siyo jukumu la CHADEMA kuikosoa CCM ili Ijisahihishe na Kutawala Vizuri ” (Aprili 18, 2011, Jamiiforums). Makala ile ilionesha vizuri zaidi tatizo hili la CHADEMA na ninaamini miaka kumi baadaye bado CHADEMA hawajajua nafasi yao. CHADEMA wanabembeleza kila kukicha CCM iwatengenezee Katiba Mpya, wanalilia kila siku CCM isimamie uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, wananung’unika kila siku serikali ya CCM isitumie polisi vibaya n.k Yaani, wanataka CCM itengeneze mazingira bora ya jinsi ya kuondolewa madarakani! Na isipofanya hivyo CHADEMA na wapinzani wengine wanalalamika! Hili ni tatizo kubwa sana kwa CHADEMA na upinzani.

Upinzani wa Tanzania unasubiri, unaombea, na kukaa chini kusubiri CCM iwabadilishe sheria, katiba, na kanuni mbalimbali ili ifanye kuwa rahisi kwa upinzani kufanya shughuli zao. Yaani, wanataka papa ajilete mwenyewe chunguni, ajikatie ndimu na kujipaka chumvi, pilipili, na mdalasini halafu ajiweke mwenyewe chunguni ili akaangwe kwa mafuta yake!

5. CHADEMA Imepoteza Kuaminika
Matokeo ya matatizo hayo 4 yanasababisha tatizo kubwa zaidi; kutokuaminika. Chama cha Siasa mtaji wake mkubwa ni wananchi wake. Wananchi wanaoweza kuwaamini kuwapa ridhaa ya kushika madaraka au kuambatana nanyi kuhakikisha watawala wanashindwa kutawala. Kuna matukio kadhaa makubwa yametokea nchini miaka hii michache ambayo yangetokea sehemu nyingine duniani upinzani ungeonesha nguvu yake. Sasa hivi, ukiondoa mikutano midogo ya ndani CHADEMA haina ushawishi wa kile ambacho kilikuwa ni gumzo kubwa wakati wa JK: “People’s Power”. Ndio maana nasema wakati ule ulikuwa ni wa kipekee kwa CHADEMA; walitikisa na kutetemesha nchi kweli kweli.

Leo hii sijui ni kiongozi gani anaweza kuitisha People’s Power kutaka Mwenyekiti atolewe bila ya masharti! Uongozi mzima wa upinzani na mashabiki wao wanasubiri hisani ya Rais ili kesi ya Mbowe isiendelee. Yaani, Mwenyekiti wa chama cha upinzani yuko jela kwa madai ya ughaidi na wanachama na wapenzi wake wanakunywa chai na kulala vitandani vyao kwa amani, na maaskofu na marafiki wanamtembelea tu Ukonga na kurudi kwenye magodoro yao ya kunesanesa!

Mambo haya manne naam matano yanakifanya chama hiki kikongwe kiwe katika hali ngumu zaidi ya kisiasa na kisipoangalia kinaweza kujikuta kinaanza kufutika pole pole katika medani za siasa za Tanzania. Hadi pale uongozi wa chama hicho utajichunguza, utaangalia ni wapi uliteleza, na utatoa majibu ya kwanini unastahili kuaminiwa wataendelea kuonekana kama chama maslahi tu. Ni lazima CHADEMA ijiangalie ni jinsi gani inaweza kujibadilisha kimiundo na kiitikadi ili kiweze kurudi na kuwa chama kweli cha wanyonge na kuwa kimbilio la wananchi.

Lakini kubwa zaidi ni lazima CHADEMA ni lazima irudi na kujiuliza je ni nini cha kufanya ili kiaminike tena? Je, kinaweza vipi kujenga umma wake ili wakisema tuandamane watu wanakuja kweli. Kubwa zaidi ni kurudisha imani kwa wanachama na wapenzi wake. Kuna wengine wanaoweza kupuuzia hoja hizi kwa sababu zimetolewa na mimi; lakini kama Waingereza wanavyosema “hata saa mbovu iko sahihi mara mbili kwa siku”. Ukweli wa hoja zangu hautegemei kabisa kama nawaunga mkono au la; au kwamba tuliachana njia mwaka 2015 kwa sababu ya mojawapo ya hoja nilizotoa hapo juu na bado sijaona ni kwa jinsi gani watu kama mimi tunaotaka mabadiliko ya kweli Tanzania tunaweza kurudi na kuiunga mkono CHADEMA ikiendelea kuwa na mitazamo ile ile, miundo ile ile na matatizo yale yale yaliyokifikisha hapa kilipo. Wengi wetu hatuwezi kuiunga mkono CCM kama chama cha siasa kwani bado tunatambua ni tatizo kubwa zaidi kwa nchi yetu; lakini hatutasita kumuunga mkono mtu ambaye tunaamini anaweka maslahi ya Tanzania na watu wake mbele zaidi kuliko kitu kingine.

Je, mtu huyo anaweza kupatikana tena CHADEMA? Je, mtu huyo anaweza kupatikana chama kingine? Je, matatizo haya niliyoyasema kuhusu CHADEMA yanaweza kuwa ndio matatizo ya upinzani jinsi ulivyo kwa sasa? Inawezekana labda yapo matatizo mengine makubwa zaidi ambayo hata sijathubutu kuyataja?

Mwisho
 
Upvote 17
Hiyo hoja namba 4."inategemea sana ccm kuingiza madarakani"hivi hapo unamaanisha nini.yaani mshindani akubali mpinzani wake kumsaidia amtoe madadakani wakati yeye anayataka?labda huko huko ccm kuwe na mamluki wengi au upande wa vyombo vya ulinzi naa usalama waamue ndio cdm inaweza angalu lakini hivi hivi bado sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vile MATAGA wanawahi kwenye uzi wako kuja kukupigia kura za kishindo!😁😁😁
2021041122000.jpg
 
Uendeshwe uchaguzi huru na haki halafu ndiyo tuone kama tathmini yako ni sahihi,
Katika uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa, sisi tulio vijijini tulishuhudia wagombea wa chadema wa kila aina, siyo matajiri au wenye uwezo tu bali wa kila aina hasa wenye uelewa na uthubutu, Kishindo hicho cha kuwa na wagombea kila mahali ndicho kilifanya kuingiliwa kwa uchaguzi huo - wote tunajua kilichotokea.

Kwenye uchaguzi mkuu sote tunajua chadema ilivyosimamisha wagombea wa kila aina, na kishindo hicho ndicho kilifanya mkuu kufanya uchaguzi kama tulivyouona kinyume hata na ahadi zake kuwa uchaguzi ungekuwa huru na haki.

Kuhusu kuikosoa na kuishauri CCM, Chadema wanachofanya ni kuikosoa na kuishauri serikali siyo ccm, na hili ni tatizo la watu wengi kudhani kuwa seikali ni ccm na ccm ni serikali, Kwa hiyo Chadema wanafanya kazi yao vizuri, hii ni nchi yetu sote huwezi kuona mambo yanaenda vibaya ukaacha kukosoa eti kisa ukikosoa watajirekebisha! Kwani usipokosoa na yakaharibika zaidi si wote tunaumia?
 
Pumba

Ajenda ya ccm ni nini hadi kipigiwe kura? Kuongeza tozo na mikopo ya benk ya dunia? Kujenga matundu ya vyoo mashuleni nchi nzima?

Polisi tanzania wamechukua nafasi ya ccm

Ccm tanzania kimekufa kama chama cha siasa

Chadema wamevuka hatua ya kupambana na ccm kwa sasa wanapambana na polisi

Ccm wamepotezwa na chadema hadi wamekabidhi chama na shughuli za siasa kwa polisi.

Hebu kuwa na adabu kwa chadema kwa hatua waliyofikia ni kubwa sana.

Chama kipo madarakani toko 1961 leo kinajinasibu kujenga matundu ya vyoo mashuleni na unashangilia aibu hii
 
1. Katiba Bora na tume huru siyo vitu vya kubeza kwa serious person. It is as if kutokuwa na katiba bora (= sheria nzuri) na tume huru ndiko kunafanya vyama vya siasa vifanye siasa nzuri na kujenga vyama vyao wakati katika uhalisi kuna'distabilise political pluralism'. What a joke!
2. Kutokuwa na usawa katika kufanya siasa.
3. Kama kufanya siasa au kukusanyika kwa lengo la kufanya siasa ni kuvunja sheria.
4. Kama kufanya siasa ni kwa wale tu waliochaguliwa kwenye maeneo yao - inakuwaje kwa vyama ambavyo vingeweza kupata wanachama wapya katika maeneo mengine, lakini kwa kuwa na katazo kama hilo havipati? Huko nako unaona ni sawa tu na wa kulaumiwa ni wale wanaoathirika na katazo hilo?
5. Wachambuzi wengi wa the operating political system in the country lack critical/intelligent/smart thinking. Hivyo, uchambuzi wao ni biased na hauongelei matatizo halisi ya kufanya siasa, bali matatizo ya pembeni yasiyoimarisha demokrasia ya vyama vingi.
6. Inabidi tuamue ama kuwa na mfumo wa chama kimoja, then vyama vya upinzani havina nafasi ya kufanya siasa; ama kuwa na mfumo wa vyama vingi ambapo vyama vyote vya siasa vina fursa sawa za kufanya siasa sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ili mradi havivunji sheria za nchi).
 
Uzi wako ni wakitopolo sana. Siwezi kukupigia kura.
Ngoja nikawape wanaojielewa.
Nyama sasa hivi ni 8500 kutoka 6000.
Hiyo 8500 bado wife hajanunua mafuta, nyanya na vitunguu. Si 10,000 tayari.
Tunakabiliwa na matatizo mengi sana ktk hii nchi.
 
Hiyo hoja namba 4."inategemea sana ccm kuingiza madarakani"hivi hapo unamaanisha nini.yaani mshindani akubali mpinzani wake kumsaidia amtoe madadakani wakati yeye anayataka?labda huko huko ccm kuwe na mamluki wengi au upande wa vyombo vya ulinzi naa usalama waamue ndio cdm inaweza angalu lakini hivi hivi bado sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kimsingi ni kuwa katika mazingira ya nchi yetu na hasa ukisikiliza hoja za upinzani kwa ujumla wake zilivyo sasa ni kuwa CCM iweke mazingira ya kusaidia upinzani ufanye kazi yake vizuri.
 
Uendeshwe uchaguzi huru na haki halafu ndiyo tuone kama tathmini yako ni sahihi,
Katika uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa, sisi tulio vijijini tulishuhudia wagombea wa chadema wa kila aina, siyo matajiri au wenye uwezo tu bali wa kila aina hasa wenye uelewa na uthubutu, Kishindo hicho cha kuwa na wagombea kila mahali ndicho kilifanya kuingiliwa kwa uchaguzi huo - wote tunajua kilichotokea.

Kwenye uchaguzi mkuu sote tunajua chadema ilivyosimamisha wagombea wa kila aina, na kishindo hicho ndicho kilifanya mkuu kufanya uchaguzi kama tulivyouona kinyume hata na ahadi zake kuwa uchaguzi ungekuwa huru na haki.

Kuhusu kuikosoa na kuishauri CCM, Chadema wanachofanya ni kuikosoa na kuishauri serikali siyo ccm, na hili ni tatizo la watu wengi kudhani kuwa seikali ni ccm na ccm ni serikali, Kwa hiyo Chadema wanafanya kazi yao vizuri, hii ni nchi yetu sote huwezi kuona mambo yanaenda vibaya ukaacha kukosoa eti kisa ukikosoa watajirekebisha! Kwani usipokosoa na yakaharibika zaidi si wote tunaumia?
Nani aendeshe uchaguzi "huru na haki"? Ili kiwe nini? Nadhani unashindwa kuelewa hoja yangu. Ni kuwa kukosekana kwa uhuru na haki katika uchaguzi ingekuwa ndio sababu kubwa ya kwanini CHADEMA isimame kuiondoa CCM madarakani. Yaani, wao CHADEMA ndio wangeweza kuja kutengeneza mazingira ya kuwa uchaguzi huru na wa haki. CCM ina maslahi gani ya kupatikana kwa uchaguzi huru na wa haki; ili kiwe nini?
 
Yani imani ya wanachama inapimwa kwa muitikio wa maandamano 🤣 🤣 🤣

Mzee umeisha, uzee wako unamaliza uwezo wa kupambanua mambo.

Ala sasa hutaki? siyo maandamano tu ni hamasa ya wananchi. Hivi wewe huoni tatizo kuwa kiongozi mkongwe wa chama kikubwa cha upinzani analala rumande na wanachama na mashabiki wanarudi kwenye vyumba vyao na kulala na kunywa chai asubuhi? Halafu kuna watu wanasema ni kama "Mandela" seriously? Unajua makaburu hawakuweza kukaa kwa amani kwa kadiri ya kwamba Mandela alikuwa kisiwa cha Robben.
 
1. Katiba Bora na tume huru siyo vitu vya kubeza kwa serious person. It is as if kutokuwa na katiba bora (= sheria nzuri) na tume huru ndiko kunafanya vyama vya siasa vifanye siasa nzuri na kujenga vyama vyao wakati katika uhalisi kuna'distabilise political pluralism'. What a joke!
2. Kutokuwa na usawa katika kufanya siasa.
3. Kama kufanya siasa au kukusanyika kwa lengo la kufanya siasa ni kuvunja sheria.
4. Kama kufanya siasa ni kwa wale tu waliochaguliwa kwenye maeneo yao - inakuwaje kwa vyama ambavyo vingeweza kupata wanachama wapya katika maeneo mengine, lakini kwa kuwa na katazo kama hilo havipati? Huko nako unaona ni sawa tu na wa kulaumiwa ni wale wanaoathirika na katazo hilo?
5. Wachambuzi wengi wa the operating political system in the country lack critical/intelligent/smart thinking. Hivyo, uchambuzi wao ni biased na hauongelei matatizo halisi ya kufanya siasa, bali matatizo ya pembeni yasiyoimarisha demokrasia ya vyama vingi.
6. Inabidi tuamue ama kuwa na mfumo wa chama kimoja, then vyama vya upinzani havina nafasi ya kufanya siasa; ama kuwa na mfumo wa vyama vingi ambapo vyama vyote vya siasa vina fursa sawa za kufanya siasa sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ili mradi havivunji sheria za nchi).
Nadhani unashindwa kuelewa hoja yangu; hivyo vyote vinatakiwa kuwa chachu ya upinzani kutaka kuingia madarakani. Political pluralism is not a gift from the ruling government. Yote uliyoyasema kuanzia 1-4 inatakiwa iwe sababu ya kuchochea upinzani. Nadhani watu wanasahau kuwa CCM siyo kama vingine vya siasa duniani; CCM inajiona ni 'caretaker' wa Tanzania. Sasa, kiruhusu mazingira bora ya kufanyika kwa siasa ili kiwe nini? Hivi, unafikiri CCM hawahofii kutokuwa madarakani?
 
Uzi wako ni wakitopolo sana. Siwezi kukupigia kura.
Ngoja nikawape wanaojielewa.
Nyama sasa hivi ni 8500 kutoka 6000.
Hiyo 8500 bado wife hajanunua mafuta, nyanya na vitunguu. Si 10,000 tayari.
Tunakabiliwa na matatizo mengi sana ktk hii nchi.
Sasa hayo uliyoyasema ingekuwa nchi ina upinzani wenye nguvu unafikiri watu wangeendelea kulilia pembeni? Hao viongozi wa upinzani wanakula nyama kutoka wapi"? wananunua vitunguu na mafuta kutoka wapi? hayo machungu wao hawayaoni? Kuna nchi bei ya mkate na vitunguu ziliweza kusababisha matatizo makubwa kwa watawala...
 
uwe unalala mapema na kuchelewa kuamka maana hiyo miguu inapata sana shida kubeba hicho kichwa
Unatakiwa kujibu hoja kwa hoja siyo vihoja. Najua siyo kila mtu anauwezo wa kufanya hivyo.
 
Chadema wamevuka hatua ya kupambana na ccm kwa sasa wanapambana na polisi

Huku ni kuvuka au kuporomoka?
 
Unatakiwa kujibu hoja kwa hoja siyo vihoja. Najua siyo kila mtu anauwezo wa kufanya hivyo.
Tangu uanze kujibiwa kwa hoja umekuwa unatoka from bad to worse

pumzisha bichwa hilo lisilo na akili ni mzigo kwa miguu hiyo
 
namba 6 ukabila namba 7 mwenyekiti hataki kuondoka achaguliwe mwingine ni yeye tuu
 
....Naunga Mkono Hoja

Kwa mfano haikuwa sahihi kwa CHADEMA kumfanya Edward Lowasa kuwa mgombea Urais kwa sababu kwa miaka mingi waliwahi kutuaminisha kuwa ni fisadi (imefanya wananchi wawaine kama ni wachumia tumbo tu na hawana agenda yenye msimamo)

CHADEMA ijitafakari sana na iepuke maamuzi ya watu wachache na upendeleo.
 
Back
Top Bottom