SoC01 CHADEMA ina Matatizo 4 Makubwa na la 5 Ni Kubwa Zaidi: Nani ataiokoa?

Stories of Change - 2021 Competition

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Na. M. M. Mwanakijiji

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinataka kukiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani na hivyo kishike hatamu za uongozi wa taifa letu. Katika kufikia lengo hilo CHADEMA kimetumia mbinu mbalimbali na kushiriki chaguzi mbalimbali kuanzia ngazi za chini kabisa hadi kwenye nafasi ya Urais. Kimejaribu kuweka wagombea katika nafasi ya Urais, Ubunge, Udiwani na kwa muda kiliweza kujipatia waumini na wafuasi wengi ambao walikuwa tayari kukifanya kuwa chama mbadala.

Pamoja na mbinu, mikakati, na njia mbalimbali za kujaribu kuiondoa CCM madarakani CHADEMA haipo katika nafasi ya kukaribia kushika hatamu za uongozi wa taifa letu. Wanachama, mashabiki, wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wanapoangalia yaliyotokea Zambia, Malawi, Senegal, Malaysia na sehemu nyingine duniani ambapo vyama vya upinzani viliweza kuingia madarakani na kushika uongozi wanajikuta na maswali mengi. Wanajiuliza hawa wamewezaje? Kwanini haitokei Tanzania, tuna tatizo gani, kwanini kizingiti kilichopo hakivukiki?

Majibu ya Haraka
Wapo wanaotoa majibu ya haraka na mengine yanaonekana hata hayajafikiriwa vizuri. Majibu mawili mara nyingi yanatolewa na wale wanaojaribu kuelezea kwanini CHADEMA haijaweza kuindia madarakani. Kwanza, wanatuambia ni kukosekana kwa Katiba Mpya na la pili ni kutokuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi. Ndani ya hayo mawili ni hoja kuwa sheria zilizopo, mifumo na taasisi zote zilizopo hazifanyi kazi kwa uhuru na hivyo haviitendei haki CHADEMA. Hoja hizi ni za kujipa faraja tu na kutafuta udhuru; siyo sababu hasa.

Kama chama cha siasa na taasisi ya kisiasa naomba kutoa mapendekezo kuwa endapo CHADEMA haitajitathmini (self-assessment) uwezekano wa chama hiki pendwa na kongwe cha upinzani kushika madaraka unaendelea kusogea mbali kila baada ya uchaguzi mkuu. Ni katika muktadha huo naomba kuchokoza tathmini hii. Kwa maoni yangu (ambayo hayakuombwa) naamini CHADEMA haitoweza kushika madaraka Tanzania hadi pale itakapoweza kuyashughulikia matatizo yafuatayo.

1. Kimepoteza Ajenda Yake Kuu Inayokitofautisha
Mojawapo ya matatizo makubwa ya kisiasa ya CHADEMA ni kukosekana kwa ajenda kuu ya kisera na kiitikadi ambayo itakuwa tofauti na ajenda za chama tawala. Kama tutakavyoona hapa chini tatizo hili linatokena na matatizo mengine. CHADEMA wakati wa Kikwete (2005-2015) naweza kusema ilikuwa katika kilele cha siasa zake; naweza kuziita ni zama zake za dhahabu (golden age) kwani ni wakati huu tofauti yake na CCM ilikuwa wazi, bayana, na kamili.

Ajenda kuu ya CHADEMA wakati ule ilikuwa ni kupinga ufisadi. Mafanikio makubwa kwa chama hicho ilikuwa ni kuweza kuwashawishi Watanzania kuwa kulikuwepo na tatizo kubwa la ufisadi na kuwa ufisadi huo usingeweza kutenganishwa na CCM. Kufuatia kufunuliwa kwa orodha ya mafia wa Tanzania (Tanzanian mafia gang) na baadaye orodha ya mafisadi CCM kwa mara ya kwanza ilijikuta katika kujitetea (on defense). Tunakumbuka ilifikia mahali pa CCM kuja na wazo la “kujivua gamba” na kama wengi tulivyohisia jitihada hizo hazikuweza kuisafisha CCM. Chadema ilikuwa inaenda kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 ikiwa na nguvu ya hoja, itikadi, mwelekeo na mapendekezo mbadala.

2. Kimekuwa Chama cha Wasomi na Wenye Uwezo
Tatizo la pili na ninaamini linaenda kuwa kubwa sana sasa hivi na inawezekana ni mazao ya utawala wa Rais Magufuli (2015-2021) ni kuwa CHADEMA imeenda kuwa na mvuto zaidi kwa wasomi na watu wenye ukwasi wa kimaisha (elites and affluent individuals). Hili linaonekana sana katika aina ya hoja za kisiasa zinazotolewa na CHADEMA sasa hivi. Hatari ya hili ni kuwa CHADEMA kinatoka kuwa chama cha wanyonge na kuwa chama cha matajiri na wenye ukwasi. Tumeona jinsi gani taasisi za wasomi na watu maarufu ambao wamejitokeza mara kwa mara sasa kuitetea CHADEMA kiasi cha kwamba ile dhana ya kuwa chama ni cha kikabila inaenda kufa na sasa kinaenda kuwa chama cha matajiri na wasomi.

Swali la ni chama cha aina gani, cha nani, na kwanini CHADEMA inataka kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 linaanza kujibiwa kwa jibu linalotisha na kukatisha tamaa.

3. CHADEMA inafanana sana kimuundo na kimfumo na CCM.
Mojawapo ya matatizo ya kimsingi ya vyama vyetu vya upinzani ikiwemo CHADEMA ni kuwa kimuundo na mfumo kinafanana mno na CCM. Hili linamatokeo ya kiCCM. Mojawapo ya matokeo mabaya ya kurudi kwa mfumo wa vyama vingi nchini ni kuwa vyama vyetu vya kisiasa vilijikuta (bila kutafakari sana) kuchukua na kuiga kwa kiasi kikubwa muundo wa CCM. Ninalolizungumzia hapa kubwa ni jinsi gani mfumo wa “Kamati Kuu” ya chama na “Sekretariati ya chama” kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuweza kufuta na kuvunja maamuzi ya chini. Hili linaweza kuonekana ni sahihi lakini matokeo yake ni kuwa chama kinakuwa ni cha kitaifa kiutawala.

Ningeweza kutoa mifano michache hapa ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo yaliacha machungu mengi kwa wanachama, mashabiki na wapenzi wake. Lakini sitofanya hivyo kwa sababu wafuatiliaji wote wa siasa za nchi yetu wanaweza kukumbuka mifano hii. Kwa kadiri ya kwamba mifumo na utendaji wa CHADEMA unafanana na chama chenye miundo ya kisoshalisti kama CCM basi CHADEMA haitoweza kuepuka matokeo ya miundo hiyo. Kwa CHADEMA upungufu huu una madhara makubwa kwa sababu haina dola. CCM inaweza kusimamia miundo yake kwa sababu imeshika dola.

4. CHADEMA inaitegemea mno CCM kuweza Kuingia Madarakani.
Jambo hili niliwahi kuliandika miaka kadhaa huko nyuma. Kwa bahati mbaya bado halijabadilika. CHADEMA imekuwa siyo chama cha upinzani bali chama cha ushauri wa chama tawala. Na hili naweza kusema linagusa hata vyama vingine vya upinzani ambavyo vimegeuka kuwa wakosoaji na washauri wa CCM. Mara kadhaa tunashuhudia vyama vya upinzani vikiishauri serikali ifanye “hili” au “ifanye lile” na ikitokea serikali imefanya basi wapinzani wanajipongeza kuwa “tuliwashauri” na serikali isipofanya wapinzani wanaona “hawasikilizwi”.

Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuandika makala ya “siyo jukumu la CHADEMA kuikosoa CCM ili Ijisahihishe na Kutawala Vizuri ” (Aprili 18, 2011, Jamiiforums). Makala ile ilionesha vizuri zaidi tatizo hili la CHADEMA na ninaamini miaka kumi baadaye bado CHADEMA hawajajua nafasi yao. CHADEMA wanabembeleza kila kukicha CCM iwatengenezee Katiba Mpya, wanalilia kila siku CCM isimamie uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, wananung’unika kila siku serikali ya CCM isitumie polisi vibaya n.k Yaani, wanataka CCM itengeneze mazingira bora ya jinsi ya kuondolewa madarakani! Na isipofanya hivyo CHADEMA na wapinzani wengine wanalalamika! Hili ni tatizo kubwa sana kwa CHADEMA na upinzani.

Upinzani wa Tanzania unasubiri, unaombea, na kukaa chini kusubiri CCM iwabadilishe sheria, katiba, na kanuni mbalimbali ili ifanye kuwa rahisi kwa upinzani kufanya shughuli zao. Yaani, wanataka papa ajilete mwenyewe chunguni, ajikatie ndimu na kujipaka chumvi, pilipili, na mdalasini halafu ajiweke mwenyewe chunguni ili akaangwe kwa mafuta yake!

5. CHADEMA Imepoteza Kuaminika
Matokeo ya matatizo hayo 4 yanasababisha tatizo kubwa zaidi; kutokuaminika. Chama cha Siasa mtaji wake mkubwa ni wananchi wake. Wananchi wanaoweza kuwaamini kuwapa ridhaa ya kushika madaraka au kuambatana nanyi kuhakikisha watawala wanashindwa kutawala. Kuna matukio kadhaa makubwa yametokea nchini miaka hii michache ambayo yangetokea sehemu nyingine duniani upinzani ungeonesha nguvu yake. Sasa hivi, ukiondoa mikutano midogo ya ndani CHADEMA haina ushawishi wa kile ambacho kilikuwa ni gumzo kubwa wakati wa JK: “People’s Power”. Ndio maana nasema wakati ule ulikuwa ni wa kipekee kwa CHADEMA; walitikisa na kutetemesha nchi kweli kweli.

Leo hii sijui ni kiongozi gani anaweza kuitisha People’s Power kutaka Mwenyekiti atolewe bila ya masharti! Uongozi mzima wa upinzani na mashabiki wao wanasubiri hisani ya Rais ili kesi ya Mbowe isiendelee. Yaani, Mwenyekiti wa chama cha upinzani yuko jela kwa madai ya ughaidi na wanachama na wapenzi wake wanakunywa chai na kulala vitandani vyao kwa amani, na maaskofu na marafiki wanamtembelea tu Ukonga na kurudi kwenye magodoro yao ya kunesanesa!

Mambo haya manne naam matano yanakifanya chama hiki kikongwe kiwe katika hali ngumu zaidi ya kisiasa na kisipoangalia kinaweza kujikuta kinaanza kufutika pole pole katika medani za siasa za Tanzania. Hadi pale uongozi wa chama hicho utajichunguza, utaangalia ni wapi uliteleza, na utatoa majibu ya kwanini unastahili kuaminiwa wataendelea kuonekana kama chama maslahi tu. Ni lazima CHADEMA ijiangalie ni jinsi gani inaweza kujibadilisha kimiundo na kiitikadi ili kiweze kurudi na kuwa chama kweli cha wanyonge na kuwa kimbilio la wananchi.

Lakini kubwa zaidi ni lazima CHADEMA ni lazima irudi na kujiuliza je ni nini cha kufanya ili kiaminike tena? Je, kinaweza vipi kujenga umma wake ili wakisema tuandamane watu wanakuja kweli. Kubwa zaidi ni kurudisha imani kwa wanachama na wapenzi wake. Kuna wengine wanaoweza kupuuzia hoja hizi kwa sababu zimetolewa na mimi; lakini kama Waingereza wanavyosema “hata saa mbovu iko sahihi mara mbili kwa siku”. Ukweli wa hoja zangu hautegemei kabisa kama nawaunga mkono au la; au kwamba tuliachana njia mwaka 2015 kwa sababu ya mojawapo ya hoja nilizotoa hapo juu na bado sijaona ni kwa jinsi gani watu kama mimi tunaotaka mabadiliko ya kweli Tanzania tunaweza kurudi na kuiunga mkono CHADEMA ikiendelea kuwa na mitazamo ile ile, miundo ile ile na matatizo yale yale yaliyokifikisha hapa kilipo. Wengi wetu hatuwezi kuiunga mkono CCM kama chama cha siasa kwani bado tunatambua ni tatizo kubwa zaidi kwa nchi yetu; lakini hatutasita kumuunga mkono mtu ambaye tunaamini anaweka maslahi ya Tanzania na watu wake mbele zaidi kuliko kitu kingine.

Je, mtu huyo anaweza kupatikana tena CHADEMA? Je, mtu huyo anaweza kupatikana chama kingine? Je, matatizo haya niliyoyasema kuhusu CHADEMA yanaweza kuwa ndio matatizo ya upinzani jinsi ulivyo kwa sasa? Inawezekana labda yapo matatizo mengine makubwa zaidi ambayo hata sijathubutu kuyataja?

Mwisho
 
Upvote 17
Kimsingi ni kuwa katika mazingira ya nchi yetu na hasa ukisikiliza hoja za upinzani kwa ujumla wake zilivyo sasa ni kuwa CCM iweke mazingira ya kusaidia upinzani ufanye kazi yake vizuri.
Kwa hiyo unataka wapinzani wajitoe muhanga kama Taliban, au?
 
....Naunga Mkono Hoja

Kwa mfano haikuwa sahihi kwa CHADEMA kumfanya Edward Lowasa kuwa mgombea Urais kwa sababu kwa miaka mingi waliwahi kutuaminisha kuwa ni fisadi (imefanya wananchi wawaine kama ni wachumia tumbo tu na hawana agenda yenye msimamo)

CHADEMA ijitafakari sana na iepuke maamuzi ya watu wachache na upendeleo.
Kwani uchaguzi ule bila wizi wa NEC na washirika wao, nani alishinda?
 
Mods, mbona mmeweka kitufe kimoja tu cha
'up vote' ?

Em pia tuwekee cha 'down vote'
kwa ajili ya uzi kama huu wa huyu
Mzee Mwanakijiji
 
Hiyo sasa ni mada mpya na mimi siyo msemaji
Lakini tayari umesema "...haikuwa sahihi CHADEMA kuweka Lowassa kama mgombea urais..."

Ni vzr basi ungeenda mbele zaidi utueleze mshindi halali wa ule uchaguzi kabla ya wizi wa kura
 
Mshindi halali hutangazwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 
Uchambuzi katika uzi wako umechambua zaidi kwa mtazamo wa kulinganisha nyakati ie Kikwete na Magufuli
Wakati wa Kikwete yeye alihakikisha siasa ni kupambana kwa hoja na kumpa nafasi mwananchi aamue upande ndio maana Chadema kwa wakati ule ilikua ndio golden age yao ndio maana baada ya hapo Magufuli hakutaka namna hiyo ya siasa yeye ikawa ni kusifiwa mwenyekiti na serikali yake ndio maana wakati huu Chadema wanapotea
Kwa uchambuzi wa muundo wa vyama hapo ni sawa karibu vyama vyote Tanzania inayofanana labda kwa ACT kidogo wamejaribu kutofautisha kofia ya mwenyekiti na Raisi. Shida ya huu mfumo wa kisoshalisti ni kama ulivyosema unapunguza nguvu ya wanachama katika maamuzi zaidi kutegemea viongonzi na kamati za vyama
Kwa mtazamo wangu suala la kuwa na mifumo na taasisi bora na za kueleweka bado ni muhimu sana mustakabali wa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla, kwa dunia ya sasa tunahitaji taasisi na mifumo huru inayojisimamia na kusimamiana bila kuingiliana ie suala la katiba itakayoleta time huru ya uchaguzi, kupunguza mamlaka ya muhimili wa utendaji kuingilia muhimili mingine. Ukisema kuwa CCM haihitaji kuwa na time huru ya uchaguzi au katiba mpya ambayo ni bora Mimi naona hata hao CCM hawako kwaajili ya maendeleo ya nchi na wananchi Bali wao wanaajenda yao binafsi ndio maana vijana na wasomi hawakubaliani na CCM na hata waliopo huko ni kwaajili ya matumbo yao Sasa hatari yake ndio kuua uzalendo wa nchi yetu
 
Chadema ili kuchukua madaraka nchi hii kinatakiwa kije na sera ya mfumo wa elimu kwa miaka 20 au zaidi ijayo wenye kulenga upatikanaji wa ajira kwa wananchi.
Pia waje na sera yenye nguvu ya kuifanya Tanganyika iwe nchi na Zanzibar iwe nchi.
 
Mojawapo ya mambo ambayo CHADEMA inahitaji kuyafanyia kazi ni kuuza sera zake zaidi kuliko malalamiko yake. Wananchi watakiwa wajue ni nini hasa chadema inataka kukifanya ambacho kitakuwa tofauti na CCM na kwanini inachotaka kufanya kitakuwa bora kuliko kinachofanywa na watawala wa sasa. Mfano wako katika elimu ni jambo mojawapo.
 
Eh..
Uchambuzi katika uzi wako umechambua zaidi kwa mtazamo wa kulinganisha nyakati ie Kikwete na Magufuli
Wakati wa Kikwete yeye alihakikisha siasa ni kupambana kwa hoja na kumpa nafasi mwananchi aamue upande ndio maana Chadema kwa wakati ule ilikua ndio golden age yao ndio maana baada ya hapo Magufuli hakutaka namna hiyo ya siasa yeye ikawa ni kusifiwa mwenyekiti na serikali yake ndio maana wakati huu Chadema wanapotea
Kwa uchambuzi wa muundo wa vyama hapo ni sawa karibu vyama vyote Tanzania inayofanana labda kwa ACT kidogo wamejaribu kutofautisha kofia ya mwenyekiti na Raisi. Shida ya huu mfumo wa kisoshalisti ni kama ulivyosema unapunguza nguvu ya wanachama katika maamuzi zaidi kutegemea viongonzi na kamati za vyama
Kwa mtazamo wangu suala la kuwa na mifumo na taasisi bora na za kueleweka bado ni muhimu sana mustakabali wa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla, kwa dunia ya sasa tunahitaji taasisi na mifumo huru inayojisimamia na kusimamiana bila kuingiliana ie suala la katiba itakayoleta time huru ya uchaguzi, kupunguza mamlaka ya muhimili wa utendaji kuingilia muhimili mingine. Ukisema kuwa CCM haihitaji kuwa na time huru ya uchaguzi au katiba mpya ambayo ni bora Mimi naona hata hao CCM hawako kwaajili ya maendeleo ya nchi na wananchi Bali wao wanaajenda yao binafsi ndio maana vijana na wasomi hawakubaliani na CCM na hata waliopo huko ni kwaajili ya matumbo yao Sasa hatari yake ndio kuua uzalendo wa nchi yetu
hivi kweli uliishi wakati wa Kikwete au ulikuwa hufuatilii kilichokuwa kinatokea wakati ule? Naelewa kwanini kuna wapinzani walisema wanammiss Kikwete.
 
Kiwango chako cha uchambuzi si cha level za watanzania waliowengi. Kiwango chako ni cha kimataifa na cha weledi wa hali ya juu unaohitaji utulivu mkubwa wa kifikra na kiakili kama uliokuwa nao.

Nimekusoma vema na nimekuelewa vizuri. Umeongea hoja ambazo kuzielewa mtu inabidi ajitoe katika akili na mawazo ya siasa za ushindani na ujuaji na atazamie uhalisia wa mambo.

Mimi nimekusoma na kukupata vema kabisa na nimeelewa na kujifunza. Ila nimekuwa so disappointed na comments za vijana hapa ambazo majority wamejipump hasira zisizo za ulazima sababu ya kupenda majibizano na ushindani wa siasa za kushindana na sio za ujenzi wa kitaifa.

Anyways, tuliombee taifa hiki kizazi kijue direction.
 
Ni sawa mkuu umenena , nimekuunga mkono na mengine , sijakuunga mkono . kwanza utawala wa awamu ya tano chini ya serikali ya magufuri ulikandamiza upinzani kwa ya juu sana Uhuru wa kutoa maoni na kuikoa serikali ilionekana kama msaliti anayetumiwa mabepari, raia wakaaminishwa na wakaamini. Pili pale mizizi ya chadema na upinzani ilikatwa kabisa, kupigwa marufuku mikutano ya hadhara na bunge lisiwe live. Tatu mwimbi la kuhama na kuhamia chama tawala, makanda na viongozi wakuu wa chadema na upinzani. Kujifua nyasifa na ubunge na kuhamia ccm , na kwenda kupewa lidhaa ya kugombea ubunge, na kushinda tena ubunge. Hii ilikua ishara mbaya sana kwa upinzani na kwa mwananchi, ambayo waliitaji mabadiliko.
 
Kuna watu kila uchwao wanalalamikia serikal kuminya demokrasia lkn kila uchwao wao ndio wa mwanzo kuminya demokrasia jamvin
 
Chadema isitegemee upendeleo wowote kutoka CCM. Na wasirudie makosa yale yale ya kuwapokea wanaCCM na kuwapa vyeo.
 
Back
Top Bottom