SoC01 CHADEMA ina Matatizo 4 Makubwa na la 5 Ni Kubwa Zaidi: Nani ataiokoa?

Stories of Change - 2021 Competition

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Na. M. M. Mwanakijiji

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinataka kukiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani na hivyo kishike hatamu za uongozi wa taifa letu. Katika kufikia lengo hilo CHADEMA kimetumia mbinu mbalimbali na kushiriki chaguzi mbalimbali kuanzia ngazi za chini kabisa hadi kwenye nafasi ya Urais. Kimejaribu kuweka wagombea katika nafasi ya Urais, Ubunge, Udiwani na kwa muda kiliweza kujipatia waumini na wafuasi wengi ambao walikuwa tayari kukifanya kuwa chama mbadala.

Pamoja na mbinu, mikakati, na njia mbalimbali za kujaribu kuiondoa CCM madarakani CHADEMA haipo katika nafasi ya kukaribia kushika hatamu za uongozi wa taifa letu. Wanachama, mashabiki, wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wanapoangalia yaliyotokea Zambia, Malawi, Senegal, Malaysia na sehemu nyingine duniani ambapo vyama vya upinzani viliweza kuingia madarakani na kushika uongozi wanajikuta na maswali mengi. Wanajiuliza hawa wamewezaje? Kwanini haitokei Tanzania, tuna tatizo gani, kwanini kizingiti kilichopo hakivukiki?

Majibu ya Haraka
Wapo wanaotoa majibu ya haraka na mengine yanaonekana hata hayajafikiriwa vizuri. Majibu mawili mara nyingi yanatolewa na wale wanaojaribu kuelezea kwanini CHADEMA haijaweza kuindia madarakani. Kwanza, wanatuambia ni kukosekana kwa Katiba Mpya na la pili ni kutokuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi. Ndani ya hayo mawili ni hoja kuwa sheria zilizopo, mifumo na taasisi zote zilizopo hazifanyi kazi kwa uhuru na hivyo haviitendei haki CHADEMA. Hoja hizi ni za kujipa faraja tu na kutafuta udhuru; siyo sababu hasa.

Kama chama cha siasa na taasisi ya kisiasa naomba kutoa mapendekezo kuwa endapo CHADEMA haitajitathmini (self-assessment) uwezekano wa chama hiki pendwa na kongwe cha upinzani kushika madaraka unaendelea kusogea mbali kila baada ya uchaguzi mkuu. Ni katika muktadha huo naomba kuchokoza tathmini hii. Kwa maoni yangu (ambayo hayakuombwa) naamini CHADEMA haitoweza kushika madaraka Tanzania hadi pale itakapoweza kuyashughulikia matatizo yafuatayo.

1. Kimepoteza Ajenda Yake Kuu Inayokitofautisha
Mojawapo ya matatizo makubwa ya kisiasa ya CHADEMA ni kukosekana kwa ajenda kuu ya kisera na kiitikadi ambayo itakuwa tofauti na ajenda za chama tawala. Kama tutakavyoona hapa chini tatizo hili linatokena na matatizo mengine. CHADEMA wakati wa Kikwete (2005-2015) naweza kusema ilikuwa katika kilele cha siasa zake; naweza kuziita ni zama zake za dhahabu (golden age) kwani ni wakati huu tofauti yake na CCM ilikuwa wazi, bayana, na kamili.

Ajenda kuu ya CHADEMA wakati ule ilikuwa ni kupinga ufisadi. Mafanikio makubwa kwa chama hicho ilikuwa ni kuweza kuwashawishi Watanzania kuwa kulikuwepo na tatizo kubwa la ufisadi na kuwa ufisadi huo usingeweza kutenganishwa na CCM. Kufuatia kufunuliwa kwa orodha ya mafia wa Tanzania (Tanzanian mafia gang) na baadaye orodha ya mafisadi CCM kwa mara ya kwanza ilijikuta katika kujitetea (on defense). Tunakumbuka ilifikia mahali pa CCM kuja na wazo la “kujivua gamba” na kama wengi tulivyohisia jitihada hizo hazikuweza kuisafisha CCM. Chadema ilikuwa inaenda kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 ikiwa na nguvu ya hoja, itikadi, mwelekeo na mapendekezo mbadala.

2. Kimekuwa Chama cha Wasomi na Wenye Uwezo
Tatizo la pili na ninaamini linaenda kuwa kubwa sana sasa hivi na inawezekana ni mazao ya utawala wa Rais Magufuli (2015-2021) ni kuwa CHADEMA imeenda kuwa na mvuto zaidi kwa wasomi na watu wenye ukwasi wa kimaisha (elites and affluent individuals). Hili linaonekana sana katika aina ya hoja za kisiasa zinazotolewa na CHADEMA sasa hivi. Hatari ya hili ni kuwa CHADEMA kinatoka kuwa chama cha wanyonge na kuwa chama cha matajiri na wenye ukwasi. Tumeona jinsi gani taasisi za wasomi na watu maarufu ambao wamejitokeza mara kwa mara sasa kuitetea CHADEMA kiasi cha kwamba ile dhana ya kuwa chama ni cha kikabila inaenda kufa na sasa kinaenda kuwa chama cha matajiri na wasomi.

Swali la ni chama cha aina gani, cha nani, na kwanini CHADEMA inataka kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 linaanza kujibiwa kwa jibu linalotisha na kukatisha tamaa.

3. CHADEMA inafanana sana kimuundo na kimfumo na CCM.
Mojawapo ya matatizo ya kimsingi ya vyama vyetu vya upinzani ikiwemo CHADEMA ni kuwa kimuundo na mfumo kinafanana mno na CCM. Hili linamatokeo ya kiCCM. Mojawapo ya matokeo mabaya ya kurudi kwa mfumo wa vyama vingi nchini ni kuwa vyama vyetu vya kisiasa vilijikuta (bila kutafakari sana) kuchukua na kuiga kwa kiasi kikubwa muundo wa CCM. Ninalolizungumzia hapa kubwa ni jinsi gani mfumo wa “Kamati Kuu” ya chama na “Sekretariati ya chama” kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuweza kufuta na kuvunja maamuzi ya chini. Hili linaweza kuonekana ni sahihi lakini matokeo yake ni kuwa chama kinakuwa ni cha kitaifa kiutawala.

Ningeweza kutoa mifano michache hapa ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo yaliacha machungu mengi kwa wanachama, mashabiki na wapenzi wake. Lakini sitofanya hivyo kwa sababu wafuatiliaji wote wa siasa za nchi yetu wanaweza kukumbuka mifano hii. Kwa kadiri ya kwamba mifumo na utendaji wa CHADEMA unafanana na chama chenye miundo ya kisoshalisti kama CCM basi CHADEMA haitoweza kuepuka matokeo ya miundo hiyo. Kwa CHADEMA upungufu huu una madhara makubwa kwa sababu haina dola. CCM inaweza kusimamia miundo yake kwa sababu imeshika dola.

4. CHADEMA inaitegemea mno CCM kuweza Kuingia Madarakani.
Jambo hili niliwahi kuliandika miaka kadhaa huko nyuma. Kwa bahati mbaya bado halijabadilika. CHADEMA imekuwa siyo chama cha upinzani bali chama cha ushauri wa chama tawala. Na hili naweza kusema linagusa hata vyama vingine vya upinzani ambavyo vimegeuka kuwa wakosoaji na washauri wa CCM. Mara kadhaa tunashuhudia vyama vya upinzani vikiishauri serikali ifanye “hili” au “ifanye lile” na ikitokea serikali imefanya basi wapinzani wanajipongeza kuwa “tuliwashauri” na serikali isipofanya wapinzani wanaona “hawasikilizwi”.

Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuandika makala ya “siyo jukumu la CHADEMA kuikosoa CCM ili Ijisahihishe na Kutawala Vizuri ” (Aprili 18, 2011, Jamiiforums). Makala ile ilionesha vizuri zaidi tatizo hili la CHADEMA na ninaamini miaka kumi baadaye bado CHADEMA hawajajua nafasi yao. CHADEMA wanabembeleza kila kukicha CCM iwatengenezee Katiba Mpya, wanalilia kila siku CCM isimamie uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, wananung’unika kila siku serikali ya CCM isitumie polisi vibaya n.k Yaani, wanataka CCM itengeneze mazingira bora ya jinsi ya kuondolewa madarakani! Na isipofanya hivyo CHADEMA na wapinzani wengine wanalalamika! Hili ni tatizo kubwa sana kwa CHADEMA na upinzani.

Upinzani wa Tanzania unasubiri, unaombea, na kukaa chini kusubiri CCM iwabadilishe sheria, katiba, na kanuni mbalimbali ili ifanye kuwa rahisi kwa upinzani kufanya shughuli zao. Yaani, wanataka papa ajilete mwenyewe chunguni, ajikatie ndimu na kujipaka chumvi, pilipili, na mdalasini halafu ajiweke mwenyewe chunguni ili akaangwe kwa mafuta yake!

5. CHADEMA Imepoteza Kuaminika
Matokeo ya matatizo hayo 4 yanasababisha tatizo kubwa zaidi; kutokuaminika. Chama cha Siasa mtaji wake mkubwa ni wananchi wake. Wananchi wanaoweza kuwaamini kuwapa ridhaa ya kushika madaraka au kuambatana nanyi kuhakikisha watawala wanashindwa kutawala. Kuna matukio kadhaa makubwa yametokea nchini miaka hii michache ambayo yangetokea sehemu nyingine duniani upinzani ungeonesha nguvu yake. Sasa hivi, ukiondoa mikutano midogo ya ndani CHADEMA haina ushawishi wa kile ambacho kilikuwa ni gumzo kubwa wakati wa JK: “People’s Power”. Ndio maana nasema wakati ule ulikuwa ni wa kipekee kwa CHADEMA; walitikisa na kutetemesha nchi kweli kweli.

Leo hii sijui ni kiongozi gani anaweza kuitisha People’s Power kutaka Mwenyekiti atolewe bila ya masharti! Uongozi mzima wa upinzani na mashabiki wao wanasubiri hisani ya Rais ili kesi ya Mbowe isiendelee. Yaani, Mwenyekiti wa chama cha upinzani yuko jela kwa madai ya ughaidi na wanachama na wapenzi wake wanakunywa chai na kulala vitandani vyao kwa amani, na maaskofu na marafiki wanamtembelea tu Ukonga na kurudi kwenye magodoro yao ya kunesanesa!

Mambo haya manne naam matano yanakifanya chama hiki kikongwe kiwe katika hali ngumu zaidi ya kisiasa na kisipoangalia kinaweza kujikuta kinaanza kufutika pole pole katika medani za siasa za Tanzania. Hadi pale uongozi wa chama hicho utajichunguza, utaangalia ni wapi uliteleza, na utatoa majibu ya kwanini unastahili kuaminiwa wataendelea kuonekana kama chama maslahi tu. Ni lazima CHADEMA ijiangalie ni jinsi gani inaweza kujibadilisha kimiundo na kiitikadi ili kiweze kurudi na kuwa chama kweli cha wanyonge na kuwa kimbilio la wananchi.

Lakini kubwa zaidi ni lazima CHADEMA ni lazima irudi na kujiuliza je ni nini cha kufanya ili kiaminike tena? Je, kinaweza vipi kujenga umma wake ili wakisema tuandamane watu wanakuja kweli. Kubwa zaidi ni kurudisha imani kwa wanachama na wapenzi wake. Kuna wengine wanaoweza kupuuzia hoja hizi kwa sababu zimetolewa na mimi; lakini kama Waingereza wanavyosema “hata saa mbovu iko sahihi mara mbili kwa siku”. Ukweli wa hoja zangu hautegemei kabisa kama nawaunga mkono au la; au kwamba tuliachana njia mwaka 2015 kwa sababu ya mojawapo ya hoja nilizotoa hapo juu na bado sijaona ni kwa jinsi gani watu kama mimi tunaotaka mabadiliko ya kweli Tanzania tunaweza kurudi na kuiunga mkono CHADEMA ikiendelea kuwa na mitazamo ile ile, miundo ile ile na matatizo yale yale yaliyokifikisha hapa kilipo. Wengi wetu hatuwezi kuiunga mkono CCM kama chama cha siasa kwani bado tunatambua ni tatizo kubwa zaidi kwa nchi yetu; lakini hatutasita kumuunga mkono mtu ambaye tunaamini anaweka maslahi ya Tanzania na watu wake mbele zaidi kuliko kitu kingine.

Je, mtu huyo anaweza kupatikana tena CHADEMA? Je, mtu huyo anaweza kupatikana chama kingine? Je, matatizo haya niliyoyasema kuhusu CHADEMA yanaweza kuwa ndio matatizo ya upinzani jinsi ulivyo kwa sasa? Inawezekana labda yapo matatizo mengine makubwa zaidi ambayo hata sijathubutu kuyataja?

Mwisho
 
Upvote 17
Ala sasa hutaki? siyo maandamano tu ni hamasa ya wananchi. Hivi wewe huoni tatizo kuwa kiongozi mkongwe wa chama kikubwa cha upinzani analala rumande na wanachama na mashabiki wanarudi kwenye vyumba vyao na kulala na kunywa chai asubuhi? Halafu kuna watu wanasema ni kama "Mandela" seriously? Unajua makaburu hawakuweza kukaa kwa amani kwa kadiri ya kwamba Mandela alikuwa kisiwa cha Robben.
Mzee rudi maktaba kafanye tafiti upya.
Mtu makini hawezi kupima muitikio wa wanachama kwa maaandamano(kumbuka chama chako cha CCM na serikali yako inaamini maandamano ya wapinzani ni uhaini)

Huyo Mbowe na wenzake waliwahi kubambikiwa kesi na CCM yako na kuhukumiwa kwenda jela au kulipa 350M na waliochanga hizo fedha na kuwatoa gerezani ni wananchi, sasa kama unamaanini Chadema hakina watu kwasababu watu hawaandamani inabidi tena nisisitize 'uzee huja na mengi'.

Narudia tena, Mzee rudi maktaba au piga kimya tu kama ulivyoshona mdomo enzi za ngosha mwenzako.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mawazo yako hayapishani na wanaccm wenzako.
Badala wa
waboreshe maisha ya watu wao ni kuhangaika na upinzani kila siku na kubuni tozo kila siku.
Ingia tena kwenye jukwaa la stories of change. Uangalie wenzako wakina Lady Furahia na Mr Mbagaa walivyoandika madini kuntu. Huchoki kusoma
Sasa wewe kwa uelewa wako mdogo, nani anahangaika na vyama wakati anaona maisha ya kiuchumi yalivyopamba moto.
Sasa hayo uliyoyasema ingekuwa nchi ina upinzani wenye nguvu unafikiri watu wangeendelea kulilia pembeni? Hao viongozi wa upinzani wanakula nyama kutoka wapi"? wananunua vitunguu na mafuta kutoka wapi? hayo machungu wao hawayaoni? Kuna nchi bei ya mkate na vitunguu ziliweza kusababisha matatizo makubwa kwa watawala...
 
Nani aendeshe uchaguzi "huru na haki"? Ili kiwe nini? Nadhani unashindwa kuelewa hoja yangu. Ni kuwa kukosekana kwa uhuru na haki katika uchaguzi ingekuwa ndio sababu kubwa ya kwanini CHADEMA isimame kuiondoa CCM madarakani. Yaani, wao CHADEMA ndio wangeweza kuja kutengeneza mazingira ya kuwa uchaguzi huru na wa haki. CCM ina maslahi gani ya kupatikana kwa uchaguzi huru na wa haki; ili kiwe nini?
Sasa Chadema wachukue mbinu gani ili kuwepo na tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya?

Vurugu?
Fujo?
Mapambano ya silaha?

CCM wanapenda madaraka kuliko Chadema wanavyopenda madaraka ni kama vile ambavyo tajiri anapenda kuendelea kuwa tajiri kuliko masikini anavyopenda kuwa tajiri.
 
Nadhani unashindwa kuelewa hoja yangu; hivyo vyote vinatakiwa kuwa chachu ya upinzani kutaka kuingia madarakani. Political pluralism is not a gift from the ruling government. Yote uliyoyasema kuanzia 1-4 inatakiwa iwe sababu ya kuchochea upinzani. Nadhani watu wanasahau kuwa CCM siyo kama vingine vya siasa duniani; CCM inajiona ni 'caretaker' wa Tanzania. Sasa, kiruhusu mazingira bora ya kufanyika kwa siasa ili kiwe nini? Hivi, unafikiri CCM hawahofii kutokuwa madarakani?
Kama unalijua hilo kwa nini unadhani chama kinachoshindwa kwa 'kuvunjwa mbavu' (kila kukicha kwa kukabiliwa na kesi na wanachama wake kuumizwa kwa sababu ya kufanya siasa ambayo ndiyo kazi ya chama cha siasa) ndicho chenye udhaifu? Kwa nini usianze kwa kusema mfumo tulio nao wa kufanya siasa unakibeba chama kimoja dhidi ya vingine?
 
....Naunga Mkono Hoja

Kwa mfano haikuwa sahihi kwa CHADEMA kumfanya Edward Lowasa kuwa mgombea Urais kwa sababu kwa miaka mingi waliwahi kutuaminisha kuwa ni fisadi (imefanya wananchi wawaine kama ni wachumia tumbo tu na hawana agenda yenye msimamo)

CHADEMA ijitafakari sana na iepuke maamuzi ya watu wachache na upendeleo.
Peter, umetoa mfano mzuri; kwa mfano Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ingetatuaje tatizo la Lowassa na lile kundi la "ulipo tupo"?
Kama unalijua hilo kwa nini unadhani chama kinachoshindwa kwa 'kuvunjwa mbavu' (kila kukicha kwa kukabiliwa na kesi na wanachama wake kuumizwa kwa sababu ya kufanya siasa ambayo ndiyo kazi ya chama cha siasa) ndicho chenye udhaifu? Kwa nini usianze kwa kusema mfumo tulio nao wa kufanya siasa unakibeba chama kimoja dhidi ya vingine?
Hiyo ndiyo point yangu; na kila mpinzani Tanzania amelielewa tangu 1995. Mfumo na taratibu zote zilitengenezwa kulinda mfumo wa chama kimoja. Sasa ukishalielewa hilo unafanyaje siasa? Je, unaomba CCM iuonee huruma upinzani? Unaomba CCM iongeze ruzuku kwa upinzani? Maana hasa ya upinzani ni hii; kutambua mabovu ya chama tawala na kuwa tayari kuyabadilisha wao wakiingia madarakani; siyo waombe chama tawala kifanyefanye urahisi kidogo ili upinzani uingie madarakani. Bado hujanipata. Siyo jukumu la CCM kusaidia upinzani kama vile siyo jukumu la upinzani kusaidia CCM itawale vizuri. Sivyo?
 
Sasa Chadema wachukue mbinu gani ili kuwepo na tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya?

Vurugu?
Fujo?
Mapambano ya silaha?

CCM wanapenda madaraka kuliko Chadema wanavyopenda madaraka ni kama vile ambavyo tajiri anapenda kuendelea kuwa tajiri kuliko masikini anavyopenda kuwa tajiri.
Ndiyo swali la msingi hapa; jibu ni rahisi ni lazima waaminike kwa wananchi wengi zaidi kuliko chama tawala. Matokeo ya kuaminika huku yanaweza kuonekana kwenye chaguzi na harakati za kisiasa.
 
UPUUZI MTUPU! Msukule wa maccm. Wapuuzi kama wewe ambao hamna msimamo ni moja ya matatizo makubwa sana ya nchi yetu.
Na. M. M. Mwanakijiji

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinataka kukiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani na hivyo kishike hatamu za uongozi wa taifa letu. Katika kufikia lengo hilo CHADEMA kimetumia mbinu mbalimbali na kushiriki chaguzi mbalimbali kuanzia ngazi za chini kabisa hadi kwenye nafasi ya Urais. Kimejaribu kuweka wagombea katika nafasi ya Urais, Ubunge, Udiwani na kwa muda kiliweza kujipatia waumini na wafuasi wengi ambao walikuwa tayari kukifanya kuwa chama mbadala.

Pamoja na mbinu, mikakati, na njia mbalimbali za kujaribu kuiondoa CCM madarakani CHADEMA haipo katika nafasi ya kukaribia kushika hatamu za uongozi wa taifa letu. Wanachama, mashabiki, wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wanapoangalia yaliyotokea Zambia, Malawi, Senegal, Malaysia na sehemu nyingine duniani ambapo vyama vya upinzani viliweza kuingia madarakani na kushika uongozi wanajikuta na maswali mengi. Wanajiuliza hawa wamewezaje? Kwanini haitokei Tanzania, tuna tatizo gani, kwanini kizingiti kilichopo hakivukiki?

Majibu ya Haraka
Wapo wanaotoa majibu ya haraka na mengine yanaonekana hata hayajafikiriwa vizuri. Majibu mawili mara nyingi yanatolewa na wale wanaojaribu kuelezea kwanini CHADEMA haijaweza kuindia madarakani. Kwanza, wanatuambia ni kukosekana kwa Katiba Mpya na la pili ni kutokuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi. Ndani ya hayo mawili ni hoja kuwa sheria zilizopo, mifumo na taasisi zote zilizopo hazifanyi kazi kwa uhuru na hivyo haviitendei haki CHADEMA. Hoja hizi ni za kujipa faraja tu na kutafuta udhuru; siyo sababu hasa.

Kama chama cha siasa na taasisi ya kisiasa naomba kutoa mapendekezo kuwa endapo CHADEMA haitajitathmini (self-assessment) uwezekano wa chama hiki pendwa na kongwe cha upinzani kushika madaraka unaendelea kusogea mbali kila baada ya uchaguzi mkuu. Ni katika muktadha huo naomba kuchokoza tathmini hii. Kwa maoni yangu (ambayo hayakuombwa) naamini CHADEMA haitoweza kushika madaraka Tanzania hadi pale itakapoweza kuyashughulikia matatizo yafuatayo.

1. Kimepoteza Ajenda Yake Kuu Inayokitofautisha
Mojawapo ya matatizo makubwa ya kisiasa ya CHADEMA ni kukosekana kwa ajenda kuu ya kisera na kiitikadi ambayo itakuwa tofauti na ajenda za chama tawala. Kama tutakavyoona hapa chini tatizo hili linatokena na matatizo mengine. CHADEMA wakati wa Kikwete (2005-2015) naweza kusema ilikuwa katika kilele cha siasa zake; naweza kuziita ni zama zake za dhahabu (golden age) kwani ni wakati huu tofauti yake na CCM ilikuwa wazi, bayana, na kamili.

Ajenda kuu ya CHADEMA wakati ule ilikuwa ni kupinga ufisadi. Mafanikio makubwa kwa chama hicho ilikuwa ni kuweza kuwashawishi Watanzania kuwa kulikuwepo na tatizo kubwa la ufisadi na kuwa ufisadi huo usingeweza kutenganishwa na CCM. Kufuatia kufunuliwa kwa orodha ya mafia wa Tanzania (Tanzanian mafia gang) na baadaye orodha ya mafisadi CCM kwa mara ya kwanza ilijikuta katika kujitetea (on defense). Tunakumbuka ilifikia mahali pa CCM kuja na wazo la “kujivua gamba” na kama wengi tulivyohisia jitihada hizo hazikuweza kuisafisha CCM. Chadema ilikuwa inaenda kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 ikiwa na nguvu ya hoja, itikadi, mwelekeo na mapendekezo mbadala.

2. Kimekuwa Chama cha Wasomi na Wenye Uwezo
Tatizo la pili na ninaamini linaenda kuwa kubwa sana sasa hivi na inawezekana ni mazao ya utawala wa Rais Magufuli (2015-2021) ni kuwa CHADEMA imeenda kuwa na mvuto zaidi kwa wasomi na watu wenye ukwasi wa kimaisha (elites and affluent individuals). Hili linaonekana sana katika aina ya hoja za kisiasa zinazotolewa na CHADEMA sasa hivi. Hatari ya hili ni kuwa CHADEMA kinatoka kuwa chama cha wanyonge na kuwa chama cha matajiri na wenye ukwasi. Tumeona jinsi gani taasisi za wasomi na watu maarufu ambao wamejitokeza mara kwa mara sasa kuitetea CHADEMA kiasi cha kwamba ile dhana ya kuwa chama ni cha kikabila inaenda kufa na sasa kinaenda kuwa chama cha matajiri na wasomi.

Swali la ni chama cha aina gani, cha nani, na kwanini CHADEMA inataka kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 linaanza kujibiwa kwa jibu linalotisha na kukatisha tamaa.

3. CHADEMA inafanana sana kimuundo na kimfumo na CCM.
Mojawapo ya matatizo ya kimsingi ya vyama vyetu vya upinzani ikiwemo CHADEMA ni kuwa kimuundo na mfumo kinafanana mno na CCM. Hili linamatokeo ya kiCCM. Mojawapo ya matokeo mabaya ya kurudi kwa mfumo wa vyama vingi nchini ni kuwa vyama vyetu vya kisiasa vilijikuta (bila kutafakari sana) kuchukua na kuiga kwa kiasi kikubwa muundo wa CCM. Ninalolizungumzia hapa kubwa ni jinsi gani mfumo wa “Kamati Kuu” ya chama na “Sekretariati ya chama” kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuweza kufuta na kuvunja maamuzi ya chini. Hili linaweza kuonekana ni sahihi lakini matokeo yake ni kuwa chama kinakuwa ni cha kitaifa kiutawala.

Ningeweza kutoa mifano michache hapa ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo yaliacha machungu mengi kwa wanachama, mashabiki na wapenzi wake. Lakini sitofanya hivyo kwa sababu wafuatiliaji wote wa siasa za nchi yetu wanaweza kukumbuka mifano hii. Kwa kadiri ya kwamba mifumo na utendaji wa CHADEMA unafanana na chama chenye miundo ya kisoshalisti kama CCM basi CHADEMA haitoweza kuepuka matokeo ya miundo hiyo. Kwa CHADEMA upungufu huu una madhara makubwa kwa sababu haina dola. CCM inaweza kusimamia miundo yake kwa sababu imeshika dola.

4. CHADEMA inaitegemea mno CCM kuweza Kuingia Madarakani.
Jambo hili niliwahi kuliandika miaka kadhaa huko nyuma. Kwa bahati mbaya bado halijabadilika. CHADEMA imekuwa siyo chama cha upinzani bali chama cha ushauri wa chama tawala. Na hili naweza kusema linagusa hata vyama vingine vya upinzani ambavyo vimegeuka kuwa wakosoaji na washauri wa CCM. Mara kadhaa tunashuhudia vyama vya upinzani vikiishauri serikali ifanye “hili” au “ifanye lile” na ikitokea serikali imefanya basi wapinzani wanajipongeza kuwa “tuliwashauri” na serikali isipofanya wapinzani wanaona “hawasikilizwi”.

Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuandika makala ya “siyo jukumu la CHADEMA kuikosoa CCM ili Ijisahihishe na Kutawala Vizuri ” (Aprili 18, 2011, Jamiiforums). Makala ile ilionesha vizuri zaidi tatizo hili la CHADEMA na ninaamini miaka kumi baadaye bado CHADEMA hawajajua nafasi yao. CHADEMA wanabembeleza kila kukicha CCM iwatengenezee Katiba Mpya, wanalilia kila siku CCM isimamie uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, wananung’unika kila siku serikali ya CCM isitumie polisi vibaya n.k Yaani, wanataka CCM itengeneze mazingira bora ya jinsi ya kuondolewa madarakani! Na isipofanya hivyo CHADEMA na wapinzani wengine wanalalamika! Hili ni tatizo kubwa sana kwa CHADEMA na upinzani.

Upinzani wa Tanzania unasubiri, unaombea, na kukaa chini kusubiri CCM iwabadilishe sheria, katiba, na kanuni mbalimbali ili ifanye kuwa rahisi kwa upinzani kufanya shughuli zao. Yaani, wanataka papa ajilete mwenyewe chunguni, ajikatie ndimu na kujipaka chumvi, pilipili, na mdalasini halafu ajiweke mwenyewe chunguni ili akaangwe kwa mafuta yake!

5. CHADEMA Imepoteza Kuaminika
Matokeo ya matatizo hayo 4 yanasababisha tatizo kubwa zaidi; kutokuaminika. Chama cha Siasa mtaji wake mkubwa ni wananchi wake. Wananchi wanaoweza kuwaamini kuwapa ridhaa ya kushika madaraka au kuambatana nanyi kuhakikisha watawala wanashindwa kutawala. Kuna matukio kadhaa makubwa yametokea nchini miaka hii michache ambayo yangetokea sehemu nyingine duniani upinzani ungeonesha nguvu yake. Sasa hivi, ukiondoa mikutano midogo ya ndani CHADEMA haina ushawishi wa kile ambacho kilikuwa ni gumzo kubwa wakati wa JK: “People’s Power”. Ndio maana nasema wakati ule ulikuwa ni wa kipekee kwa CHADEMA; walitikisa na kutetemesha nchi kweli kweli.

Leo hii sijui ni kiongozi gani anaweza kuitisha People’s Power kutaka Mwenyekiti atolewe bila ya masharti! Uongozi mzima wa upinzani na mashabiki wao wanasubiri hisani ya Rais ili kesi ya Mbowe isiendelee. Yaani, Mwenyekiti wa chama cha upinzani yuko jela kwa madai ya ughaidi na wanachama na wapenzi wake wanakunywa chai na kulala vitandani vyao kwa amani, na maaskofu na marafiki wanamtembelea tu Ukonga na kurudi kwenye magodoro yao ya kunesanesa!

Mambo haya manne naam matano yanakifanya chama hiki kikongwe kiwe katika hali ngumu zaidi ya kisiasa na kisipoangalia kinaweza kujikuta kinaanza kufutika pole pole katika medani za siasa za Tanzania. Hadi pale uongozi wa chama hicho utajichunguza, utaangalia ni wapi uliteleza, na utatoa majibu ya kwanini unastahili kuaminiwa wataendelea kuonekana kama chama maslahi tu. Ni lazima CHADEMA ijiangalie ni jinsi gani inaweza kujibadilisha kimiundo na kiitikadi ili kiweze kurudi na kuwa chama kweli cha wanyonge na kuwa kimbilio la wananchi.

Lakini kubwa zaidi ni lazima CHADEMA ni lazima irudi na kujiuliza je ni nini cha kufanya ili kiaminike tena? Je, kinaweza vipi kujenga umma wake ili wakisema tuandamane watu wanakuja kweli. Kubwa zaidi ni kurudisha imani kwa wanachama na wapenzi wake. Kuna wengine wanaoweza kupuuzia hoja hizi kwa sababu zimetolewa na mimi; lakini kama Waingereza wanavyosema “hata saa mbovu iko sahihi mara mbili kwa siku”. Ukweli wa hoja zangu hautegemei kabisa kama nawaunga mkono au la; au kwamba tuliachana njia mwaka 2015 kwa sababu ya mojawapo ya hoja nilizotoa hapo juu na bado sijaona ni kwa jinsi gani watu kama mimi tunaotaka mabadiliko ya kweli Tanzania tunaweza kurudi na kuiunga mkono CHADEMA ikiendelea kuwa na mitazamo ile ile, miundo ile ile na matatizo yale yale yaliyokifikisha hapa kilipo. Wengi wetu hatuwezi kuiunga mkono CCM kama chama cha siasa kwani bado tunatambua ni tatizo kubwa zaidi kwa nchi yetu; lakini hatutasita kumuunga mkono mtu ambaye tunaamini anaweka maslahi ya Tanzania na watu wake mbele zaidi kuliko kitu kingine.

Je, mtu huyo anaweza kupatikana tena CHADEMA? Je, mtu huyo anaweza kupatikana chama kingine? Je, matatizo haya niliyoyasema kuhusu CHADEMA yanaweza kuwa ndio matatizo ya upinzani jinsi ulivyo kwa sasa? Inawezekana labda yapo matatizo mengine makubwa zaidi ambayo hata sijathubutu kuyataja?

Mwisho
 
Mawazo yako hayapishani na wanaccm wenzako.
Badala wa
waboreshe maisha ya watu wao ni kuhangaika na upinzani kila siku na kubuni tozo kila siku.
Ingia tena kwenye jukwaa la stories of change. Uangalie wenzako wakina Lady Furahia na Mr Mbagaa walivyoandika madini kuntu. Huchoki kusoma
Sasa wewe kwa uelewa wako mdogo, nani anahangaika na vyama wakati anaona maisha ya kiuchumi yalivyopamba moto.
Labda hujui uhusiano wa sera za chama cha siasa na uundwaji wa mifumo ya kisiasa na kiutawala. Chama kinaposhinda uchaguzi kinaenda kutekeleza sera zake. Sasa haya yote unayosema yanapendekezwa kutekelezwa yataenda kutekelezwa na sera za chama gani?
 
UPUUZI MTUPU! Msukule wa maccm. Wapuuzi kama wewe ambao hamna msimamo ni moja ya matatizo makubwa sana ya nchi yetu.
Nakubali ni upuuzi; sasa jaribu basi kuonesha ubora wa mawazo yako. CHADEMA inatakiwa ifanye nini ili iisaidie CCM kuondoka madarakani? Au CCM ifanye nini ili CHADEMA iweze kuingia madarakani? Nasubiri usiandike upuuzi kama nilioandika mimi.
 
Waaminike mara ngapi wewe!!!! Kama hawaaminiki na Watanzania kwanini maccm WANAPORA chaguzi? Kwanini maccm wanahofia Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ili Uchaguzi nchini iuwe wa HAKI na HURU? Hebu tuondolee uuuzi wako hapa!!!

Ndiyo swali la msingi hapa; jibu ni rahisi ni lazima waaminike kwa wananchi wengi zaidi kuliko chama tawala. Matokeo ya kuaminika huku yanaweza kuonekana kwenye chaguzi na harakati za kisiasa.
 
KAKURUPUKA huyu Mkuu kuandika ujinga wake.

Kama unalijua hilo kwa nini unadhani chama kinachoshindwa kwa 'kuvunjwa mbavu' (kila kukicha kwa kukabiliwa na kesi na wanachama wake kuumizwa kwa sababu ya kufanya siasa ambayo ndiyo kazi ya chama cha siasa) ndicho chenye udhaifu? Kwa nini usianze kwa kusema mfumo tulio nao wa kufanya siasa unakibeba chama kimoja dhidi ya vingine?
 
Kabla hujawa MSUKULE wa maccm usingeshindwa kulijibu swali hili lakini tangu ulipoamua kujitoa UFAHAMU umekuwa ZERO BRAIN.

Nakubali ni upuuzi; sasa jaribu basi kuonesha ubora wa mawazo yako. CHADEMA inatakiwa ifanye nini ili iisaidie CCM kuondoka madarakani? Au CCM ifanye nini ili CHADEMA iweze kuingia madarakani? Nasubiri usiandike upuuzi kama nilioandika mimi.
 
UPUUZI MTUPU! Msukule wa maccm. Wapuuzi kama wewe ambao hamna msimamo ni moja ya matatizo makubwa sana ya nchi yetu.
Na wewe ni mchaga wa chadema?[emoji23][emoji1787]
 
Kabla hujawa MSUKULE wa maccm usingeshindwa kulijibu swali hili lakini tangu ulipoamua kujitoa UFAHAMU umekuwa ZERO BRAIN.
Nakubali miye zero nielimishe basi katika ubora wa uzero wangu...
 
Endelea kuwa MSUKULE wa maccm ili kusaka TEUZI. Miaka 6 ya kujikomba kama mchumia tumbo bado wanakukwepa kwenye TEUZI.
Nakubali miye zero nielimishe basi katika ubora wa uzero wangu...
 
Narudia tena endelea kuwa MSUKULE wa maccm. Umedharaulika sana baada ya kujijengea heshima kubwa sana katika jamii ya Watanzania. Usidhani Watanzania ni wajinga.
Ni rahisi kutukana giza kuliko kuwasha kibatari....
 
Narudia tena endelea kuwa MSUKULE wa maccm. Umedharaulika sana baada ya kujijengea heshima kubwa sana katika jamii ya Watanzania. Usidhani Watanzania ni wajinga.
Itakuwa ni udhaifu mkubwa kudhania aliyekushinda kwa hoja amekushinda jwa sababu ni mwanaccm.
 
Back
Top Bottom