Uchaguzi 2020 CHADEMA inakuwaje mtu anagombea Kiti cha Ubunge wa Jimbo na Viti Maalumu kwa mpigo na anashinda vyote? Kwanini asigombee moja?

Sofia Simba wakati akiwa mwenyekiti wa UWT alipendekeza kuwa mbunge wa viti maalum awakilishe miaka isiyozidi kumi (vipindi viwili), yaani agombee ubunge wa jimbo baada ya miaka mitano ya viti maalum na asiposhinda agombee tena jimbo baada ya miaka 10 ya viti maalum. Asiposhinda hapo basi astaafu kupisha wenzake kwenye viti maalum. Wenzake wakampinga hoja yake ikashindwa.
 
Na Halima Mdee kafanya hivyo hivyo.

Maana yake ni kuwa hawa jamaa hawategemei hata kidogo kwamba watashinda kwenye hayo majimbo. Wanajua CCM inayarudisha. Hivyo wamejiwahi kwenye kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum ili angalao warejee mjengoni.

Sifa ya chama kupata viti maalum inategemea na idadi ya wabunge itakaowapata kwenye majimbo - at least wasipungue 10, idadi ambayo chadema ni ngumu kuipata.
 

Ni kweli ccm inaweza kuyarudisha, ila sio kwa kura, bali kwa kupitia mamlaka ya urais yanayotumika vibaya.
 
Wacha wakatane halafu waanze kurogana, maana maccm hayawezi kuachiana hata chupa ya maji ya kunywa.
 
Tofautisha kusifia na kusema ukweli. Mathalani mwakani Mungu akipenda JNHPP inakamilika wewe hautafaidi huo umeme?

Hata umeme wa wakoloni naufaidi, na shule ya msingi niliyosoma hapa Dar ilijengwa na wakoloni.
 
Hata umeme wa wakoloni naufaidi, na shule ya msingi niliyosoma hapa Dar ilijengwa na wakoloni.
Ndio maana huwa nakuambia wewe sio mzalendo. Yaani mkoloni kujenga shule alafu Pamba,almasi na dhahabu akawa anapeleka bure unamsifia. Na shule zenyewe alijenga kwa ajili ya watu wachache na watoto wa wakoloni. Unafeli sana we dogo.
 
Ndio maana huwa nakuambia wewe sio mzalendo. Yaani mkoloni kujenga shule alafu Pamba,almasi na dhahabu akawa anapeleka bure unamsifia. Na shule zenyewe alijenga kwa ajili ya watu wachache na watoto wa wakoloni. Unafeli sana we dogo.

Sina uzalendo wa kiccm, mimi sina hata muda wa kujifanya mzalendo maana hizo ni approach za kikomunisti, kujifanya wana uzalendo kwa nchi ili wapate madaraka. Simsifii lolote mkoloni, nimekupa mfano wa majengo kuwa sio issue. Kama unatarajia nitajipendekeza kwa serikali ili uniite mzalendo, utasubiri sana. Sihitaji uzalendo wa kishamba boss.
 

Inaonekana ni jambo linaloruhusiwa ndani ya katiba ya CHADEMA.Kwa muda mrefu imekuwa hivyo.Lengo ni kwamba akikosa jimbo wamfikirie Viti Maalumu.Hoja ni kuwa na wabunge wanaoweza kujengewa uwezo jimboni,ikishindikana basi apewe viti maalumu kama chama ni kinaona anafaa kuwakilisha chama kwenye ngazi hiyo.Ni utaratibu ambao hata akina Halima Mdee wameupitia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…