CHADEMA inapokea ruzuku kama kawaida, hawajaigomea

Kwann usijikite kwenye kuisifia serikali kwa elimu bure? Achana na waliopo nje ya nchi.
 
We nani kwambia ruzuku inatokana na wabunge? Cdm imeshika nafasi ya pili, hivyo inachukua ruzuku kwa sababu hiyo. NCCR haina mbunge hata mmoja lakini inapewa ruzuku pia.

Ninadhani sasa utaacha ubishi kwamba ruzuku inapatikana kutokana na ubunge au udiwani. Wabunge au madiwani wanapopungua kwenye chama na ruzuku inapungua. Hii ilitokea sana kwenye chama cha chadema kipindi kilichopita ambacho kilikuwa na wimbi kubwa la madiwani na wabunge kukihama chama hicho na kuunga juhudi. Au wewe umesahau? Vivyo hivyo kama hao wabunge 19 wa viti maalum na hao madiwani wenu 80 wakiamua kujivua ubunge na udiwani wao huo kama ambavyo mnataka wafanye, ruzuku ya chadema itapungua kutoka hiyo Tsh 109 million kwa mwezi hadi kuwa Tsh 5 million kwa mwezi sawa na CUF. Wakina Mnyika na Mbowe watakosa hiyo mishahara yao minono ya chama na marupurupu kibao. Mwamba hatakubali hilo litokee. Stay tuned my friend. Pesa ni kitu kingine hasa kwa rafiki zetu wa mkoa ule!
 
Hahahahahaaa, kuthibitisha ulilosema hadi muda huu bado jamaa wanasugua kichwa waanzie wapi waitwe hao makomandoo 19 kwa ajili ya kuhojiwa kwa utovu wa nidhamu ili wavuliwe ubunge. Hapo wapenzi wa CDM watasubiri sana ili wapate hizo nafasi wanazodai zipo wazi kwa ajili ya uteuzi wa viti maalum
 
Njoo utuletee ushahidi kuhusu huu uongo wako.

 
Wametangaza kutoa ruzuku lakini bado fedha haijapokelewa na CHADEMA.Umeandika kishabiki na kijuha.Hiyo pesa haijatolewa bado na Karibu Mkuu JK Mnyika amegoma kwenda kwenye kikao kilichoitishwa na Msajili kuhusu masuala ya ruzuku.
 
Reactions: BAK
Uko sawa kabisa Mkuu.
Wametangaza kutoa ruzuku lakini bado fedha haijapokelewa na CHADEMA.Umeandika kishabiki na kijuha.Hiyo pesa haijatolewa bado na Karibu Mkuu JK Mnyika amegoma kwenda kwenye kikao kilichoitishwa na Msajili kuhusu masuala ya ruzuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…