CHADEMA inazuia Watanzania kuanzisha vyama vingine vya Siasa?

CHADEMA inazuia Watanzania kuanzisha vyama vingine vya Siasa?

Mkuu waonekana kuuzunguka mbuyu kisomi ukiwaepuka wale nguli wengine kiaina.
Kwanza hakuna mtu anayezungukwa. Hii hoja wao ndiyo wanazunguka. Kwao hakuna jema linalofanywa na CHADEMA lakini kwenye mapambano huwa upande wa waonezi.
"Hoja yako hii ya watu kuanzisha vyama kama ni kuwalenga manguli wengine wenye mawazo tofauti vyamani, haina mashiko."
Hakuna mwanachadema anayelengwa. Ndani ya CHADEMA hakuna mtu anayetakiwa kuondoka Kwa kuwa ana mawazo tofauti na wenzie.

Hapa ni wale walio nje ya CHADEMA ambao kila uchao na uchwao huwa wanajifanya wanaitakia mema CHADEMA lakini ndani kabisa wanatani CHADEMA ife hata leo.

Kwani kama wewe unaona CHADEMA haifai si ujiunge na chama kingine au uanzishe kipya?

Yaani CCM wanavojifanya kuitakia mema CHADEMA tuwaamini? Au leo hii watu Wa NCCR-Mageuzi na ACT waseme CHADEMA ifanye jambo fulani Ili iwe imara tuwape haki ya kuaminika??

Hoja hii inawahusu watu wasio CHADEMA.
 
Kwanza hakuna mtu anayezungukwa. Hii hoja wao ndiyo wanazunguka. Kwao hakuna jema linalofanywa na CHADEMA lakini kwenye mapambano huwa upande wa waonezi.

Labda ungekuwa wazi hapa. "Kwao" - una maanisha kina nani? Kutokuwa wazi kunaileta dhana ya kuuzunguka mbuyu.

Hakuna mwanachadema anayelengwa. Ndani ya CHADEMA hakuna mtu anayetakiwa kuondoka Kwa kuwa ana mawazo tofauti na wenzie.

Hili ni jambo la kheri na afya sana.

Hapa ni wale walio nje ya CHADEMA ambao kila uchao na uchwao huwa wanajifanya wanaitakia mema CHADEMA lakini ndani kabisa wanatani CHADEMA ife hata leo.

Tutofautishe kuitakia mema nchi na kuitakia mema Chadema. Hapa hawezi kulaumiwa awaye yote kwa kuitakia mema nchi.

Ni wazi kuwa mema ya nchi si lazima yawe mema ya Chadema, kwa sababu nchi si Chadema na wala Chadema si nchi.

Tukumbuke pia kuheshimu haki za vyama vingine na agenda zao zozote. Vinginevyo ni nini tofauti nao?

Kwani kama wewe unaona CHADEMA haifai si ujiunge na chama kingine au uanzishe kipya?

Hapa ni muhimu kuwa bayana. Tutofautishe vilivyo kuwa na mawazo tofauti na kuona Chadema haifai.

Tamko la haifai ni zito ambalo binafsi sijalisikia kutamkwa hata na Lucas mwashambwa au hata johnthebaptist.

"Tukumbuke Mwigulu kwenye Tambo kama hIzi amewahi kutuhimiza kwenda Burundi jambo ambalo sidhani kama atathubutu tena."

Kuwa na ngozi ngumu ni sehemu ya maisha ya kisiasa. Kukosolewa hakuhalalishi majibu ya kifedhuli.

Yaani CCM wanavojifanya kuitakia mema CHADEMA tuwaamini? Au leo hii watu Wa NCCR-Mageuzi na ACT waseme CHADEMA ifanye jambo fulani Ili iwe imara tuwape haki ya kuaminika??

Vyama vingine vinayo haki ya kusema lolote dhidi ya vingine, overt na hata covert. Labda kama ni lengo lako kuwanyima haki hiyo?

Hapa niseme wazi ninashindwa kuiona hoja yako kuwa ni ipi hasa na
hata wapi.

Kwamba ni ushauri wa bure kwao, Chadema au unawaza mwenyewe kwa sauti?

Kwani yupo asiyeijua haki hiyo ndugu?

Hoja hii inawahusu watu wasio CHADEMA.

Haha ha ha ha .. kwamba kumbe unawapa ushauri wa bure kina Samia, Msukuma, Tulia, Kipi*imba, D*wani na wa namna hiyo, siyo?

Basi sawa.
 
Back
Top Bottom