CHADEMA isipowadhibiti vijana wake, itakuja kujuta

CHADEMA inafanya siasa zake mtandaoni kwa kiasi kikubwa, kutokana na mazingira ya siasa nchini yalivyo tangu enzi za mwendazake

Sasa kuna vijana wa Chadema wamekuwa popular sana huko mtandaoni kuliko hata viongozi wao wa kitaifa, na waki push ajenda fulani inaonekana kama ni Chadema sababu wamebeba brand ya chama

Sasa tatizo kubwa la hawa vijana, nataka nimtolee mfano huyu anayeitwa Martin Maranja Masese, huyu alipata umaarufu mkubwa kutokana na ku tweet kuhusu kesi ya Mbowe

Kijana huyu yupo passionate na Chadema lakini hajui siasa, anafikiri siasa ni kupiga spana, ama kutukana ama kudhalilisha watu wenye mawazo tofauti basi.

Hajui kwenye siasa kuna muda unatakiwa kukaa kimya, saa nyingine hata kupongeza mahasimu wako, saa nyingine kukosoa

Believe me, kuna muda ukimsifia hasimu wako kisiasa inakupa heshima zaidi kuliko kulazimisha kumkosoa

Kipindi cha Magufuli ambacho ilikuwa ndio kipindi kibaya zaidi kwa upinzani nchini, wapo watu wengi waliteswa ili waunge mkono juhudi lakini wakabaki upinzani, side moja na Chadema

Sasa bana Watu hawa ikitokea wametofautiana na Chadema kidogo tu, iwe kwenye approach ya kudai Katiba mpya, ama kuhusu Wamasai Ngorongoro, ama mambo ya kikosi kazi na mengineyo wamekuwa wakishambuliwa na kudhalilishwa na sacrifice zote za nyuma kusahaulika, anayeongoza haya mashambulizi ni huyo Martin, sidhani kama chama cha siasa kinaweza kukua kama watu wake wana mtazamo huu

Fikiria mtu kama Msigwa ambaye kipindi cha Magufuli alinunuliwa akagoma akenda jela na kudhalilishwa pakubwa, na amekuwa pamoja na Chadema kwenye mambo mengi tu, leo hii unakuta anashambuliwa na kuitwa njaa ya kukosa ubunge imemshinda na amenunuliwa, kisa tu alikuwa na maoni tofauti kuhusu Ngorongoro na Royal Tour ambapo alieleza vizuri tu

Fikiria mtu kama Fatma Karume alivyompigania Lissu kabla na baada ya kupigiwa risasi na kupaza sauti kuhusu uonevu mwingi wa Magufuli na hata Mbowe alivyokuwa jela kwa kesi ya ugaidi

Fatma kaenda kutoa maoni kuhusu kikosi kazi imekuwa kosa kubwa anashambuliwa kuwa ni mdini na mkabila,
Aisee siasa za upinzani Tanzania ngumu sana
Naunga mkono hoja,hata huyu Mdude Nyagali naye anakosea sana, siasa ni sayansi na hekima pia. Natoa mwito kwa uongozi wa Bavicha uwaonye hawa wenzao. Rais Samia ameonyesha uungwana katika kufanya siasa Kwa kuachana na siasa za kishenzi alizoasisi yule dhalim,basi ni wajibu wa wapinzani pia kubadilisha aina ya kufanya siasa. Kama kukosoana basi itumike lugha ya staha.
 
Kwa nini sasa unaleta hapa na usiwaambie huko huko ulikowatoa ? Hao unaowataja wengine hatujawahi hata kuwasikia, ungejibizana nao huko huko walipo ingekusaidia zaidi labda kwa maoni yangu!
Kwani kila mada lazima uelewe? Kama huelewi si upite kushoto utafute unazoelewa uchangie, acha nafasi kwa wanaoelewa wachaangie
 
Fatma Karume alikuwa hampendi Magufuli kwa sababu ni Mkristo ,sasa hivi Mzanzibar mwenzake mwislam basi anasifia tu
 
CHADEMA inafanya siasa zake mtandaoni kwa kiasi kikubwa, kutokana na mazingira ya siasa nchini yalivyo tangu enzi za mwendazake

Sasa kuna vijana wa Chadema wamekuwa popular sana huko mtandaoni kuliko hata viongozi wao wa kitaifa, na waki push ajenda fulani inaonekana kama ni Chadema sababu wamebeba brand ya chama

Sasa tatizo kubwa la hawa vijana, nataka nimtolee mfano huyu anayeitwa Martin Maranja Masese, huyu alipata umaarufu mkubwa kutokana na ku tweet kuhusu kesi ya Mbowe

Kijana huyu yupo passionate na Chadema lakini hajui siasa, anafikiri siasa ni kupiga spana, ama kutukana ama kudhalilisha watu wenye mawazo tofauti basi.

Hajui kwenye siasa kuna muda unatakiwa kukaa kimya, saa nyingine hata kupongeza mahasimu wako, saa nyingine kukosoa

Believe me, kuna muda ukimsifia hasimu wako kisiasa inakupa heshima zaidi kuliko kulazimisha kumkosoa

Kipindi cha Magufuli ambacho ilikuwa ndio kipindi kibaya zaidi kwa upinzani nchini, wapo watu wengi waliteswa ili waunge mkono juhudi lakini wakabaki upinzani, side moja na Chadema

Sasa bana Watu hawa ikitokea wametofautiana na Chadema kidogo tu, iwe kwenye approach ya kudai Katiba mpya, ama kuhusu Wamasai Ngorongoro, ama mambo ya kikosi kazi na mengineyo wamekuwa wakishambuliwa na kudhalilishwa na sacrifice zote za nyuma kusahaulika, anayeongoza haya mashambulizi ni huyo Martin, sidhani kama chama cha siasa kinaweza kukua kama watu wake wana mtazamo huu

Fikiria mtu kama Msigwa ambaye kipindi cha Magufuli alinunuliwa akagoma akenda jela na kudhalilishwa pakubwa, na amekuwa pamoja na Chadema kwenye mambo mengi tu, leo hii unakuta anashambuliwa na kuitwa njaa ya kukosa ubunge imemshinda na amenunuliwa, kisa tu alikuwa na maoni tofauti kuhusu Ngorongoro na Royal Tour ambapo alieleza vizuri tu

Fikiria mtu kama Fatma Karume alivyompigania Lissu kabla na baada ya kupigiwa risasi na kupaza sauti kuhusu uonevu mwingi wa Magufuli na hata Mbowe alivyokuwa jela kwa kesi ya ugaidi

Fatma kaenda kutoa maoni kuhusu kikosi kazi imekuwa kosa kubwa anashambuliwa kuwa ni mdini na mkabila,
Aisee siasa za upinzani Tanzania ngumu sana

Hoja yako ilikuwa ni kwenye hilo hitimisho la paragraph ya mwisho. Umeshindwana nao huko unakuja kutuletea huku! Na kwa bahati mbaya unaside na upande fulani kiasi kwamba unadhani hatuna uwezo wa kupima. Unasema cdm itajuta kwasababu wafuasi wake baadhi wanatofautiana na mtu fulani unayemkubali.
 
Mtu yupi? Msigwa? Fatma?
Hoja yangu ni kuwa Chadema inapaswa kujifunza kuvumilia wanapotofautiana kwenye baadhi ya mambo.

kuna mambo ya msingi ambayo wanatakiwa kukubaliana ila kuna mengine ambayo mtu anaweza kuwa na mtazamo tofauti na ikavumilika tu

Chadema kwenye mambo 10 ukikubaliana nao kwenye mambo 9 la 10 ukawa na mtazamo tofauti wewe ni msaliti umenunuliwa kwa mtazamo wa hao vijana wengi
 
Back
Top Bottom