CHADEMA isipowadhibiti vijana wake, itakuja kujuta

CHADEMA isipowadhibiti vijana wake, itakuja kujuta

Bado wako kwenye “uanaharati” siwatofautishi na EFF.
Kuna vitu chadema inapaswa kuiga CCM hata kwa jicho moja mfano kuwa na shule ya uongozi kuhusu falsafa na miiko ya chama. Hii itasaidia kukuza vipaji vya vijana wao wanaotarajiwa kuwa viongozi wao mbeleni.

Kama CCM wanachuo, basi ni hicho cha kupora uchaguzi. CDM wanaiga nini kwenye hilo? CCM ingekuwa na chuo cha maana tusingeona kiwango kikubwa cha kujikomba kwa vijana na wazee wake. Hicho chuo cha CCM hakifundishi ubora, bali kinafundisha zaidi hila, ukatili na jinsi ya kutumia dola kubaki madarakani kwa shuruti.
 
Nilikuwa mpinzani mkubwa wa Ben Sanane kwa hoja, Mola amuweke pema peponi.

PENGO LAKE CHADEMA NI KUBWA SANA
 
Hoja yako ni nini hapa?
Malalamiko ndiyo mengi, ni vizuri ukaelewa siku zote hamuwezi kuwa na mawazo sawa popote pale.
 
Mtu yupi? Msigwa? Fatma?
Hoja yangu ni kuwa Chadema inapaswa kujifunza kuvumilia wanapotofautiana kwenye baadhi ya mambo.

kuna mambo ya msingi ambayo wanatakiwa kukubaliana ila kuna mengine ambayo mtu anaweza kuwa na mtazamo tofauti na ikavumilika tu

Chadema kwenye mambo 10 ukikubaliana nao kwenye mambo 9 la 10 ukawa na mtazamo tofauti wewe ni msaliti umenunuliwa kwa mtazamo wa hao vijana wengi

Hebu ngoja kwanza maana naona unajichanganya,, hapa unaizungumzia Cdm au baadhi ya vijana wa CDM? Hebu weka vizuri hapo kwanza tujue tatizo lako ni CDM, au baadhii ya vijana wa Cdm kama kichwa chako cha habari kinavyosema?
 
Wote wapo responsible hapa, vijana wa CDM ndio sehemu kubwa ya CDM... Title inasema CDM isipodhibiti vijana wake, watajuta
 
Viongozi wetu wamepewa asali Sasa vijana wanaendeleza wanaendeleza Sela za chama za ulopokaji kama kawaida, ikiwezekana vijana nao wapewe asal [emoji847][emoji847][emoji847]
 
Wote wapo responsible hapa, vijana wa CDM ndio sehemu kubwa ya CDM... Title inasema CDM isipodhibiti vijana wake, watajuta

Wametumwa na CDM? Au ukibeba kilio cha Fatma ndio na ww unajigeuza mtetezi wake? Kama unaamini katika kutofautiana mawazo, sioni ni kwanini watu wakitofautiana upate shida boss.
 
CHADEMA inafanya siasa zake mtandaoni kwa kiasi kikubwa, kutokana na mazingira ya siasa nchini yalivyo tangu enzi za mwendazake

Sasa kuna vijana wa Chadema wamekuwa popular sana huko mtandaoni kuliko hata viongozi wao wa kitaifa, na waki push ajenda fulani inaonekana kama ni Chadema sababu wamebeba brand ya chama

Sasa tatizo kubwa la hawa vijana, nataka nimtolee mfano huyu anayeitwa Martin Maranja Masese, huyu alipata umaarufu mkubwa kutokana na ku tweet kuhusu kesi ya Mbowe

Kijana huyu yupo passionate na Chadema lakini hajui siasa, anafikiri siasa ni kupiga spana, ama kutukana ama kudhalilisha watu wenye mawazo tofauti basi.

Hajui kwenye siasa kuna muda unatakiwa kukaa kimya, saa nyingine hata kupongeza mahasimu wako, saa nyingine kukosoa

Believe me, kuna muda ukimsifia hasimu wako kisiasa inakupa heshima zaidi kuliko kulazimisha kumkosoa

Kipindi cha Magufuli ambacho ilikuwa ndio kipindi kibaya zaidi kwa upinzani nchini, wapo watu wengi waliteswa ili waunge mkono juhudi lakini wakabaki upinzani, side moja na Chadema

Sasa bana Watu hawa ikitokea wametofautiana na Chadema kidogo tu, iwe kwenye approach ya kudai Katiba mpya, ama kuhusu Wamasai Ngorongoro, ama mambo ya kikosi kazi na mengineyo wamekuwa wakishambuliwa na kudhalilishwa na sacrifice zote za nyuma kusahaulika, anayeongoza haya mashambulizi ni huyo Martin, sidhani kama chama cha siasa kinaweza kukua kama watu wake wana mtazamo huu

Fikiria mtu kama Msigwa ambaye kipindi cha Magufuli alinunuliwa akagoma akenda jela na kudhalilishwa pakubwa, na amekuwa pamoja na Chadema kwenye mambo mengi tu, leo hii unakuta anashambuliwa na kuitwa njaa ya kukosa ubunge imemshinda na amenunuliwa, kisa tu alikuwa na maoni tofauti kuhusu Ngorongoro na Royal Tour ambapo alieleza vizuri tu

Fikiria mtu kama Fatma Karume alivyompigania Lissu kabla na baada ya kupigiwa risasi na kupaza sauti kuhusu uonevu mwingi wa Magufuli na hata Mbowe alivyokuwa jela kwa kesi ya ugaidi

Fatma kaenda kutoa maoni kuhusu kikosi kazi imekuwa kosa kubwa anashambuliwa kuwa ni mdini na mkabila,
Aisee siasa za upinzani Tanzania ngumu sana
Kajinyonge
 
Upinzani...
Wao kila kitu ni kupinga tuuu.
Wewe ni kuramba miguu tu
2023275579.jpg
 
Wametumwa na CDM? Au ukibeba kilio cha Fatma ndio na ww unajigeuza mtetezi wake? Kama unaamini katika kutofautiana mawazo, sioni ni kwanini watu wakitofautiana upate shida boss.
Nimebeba kilio? Hakuna anayelia hapa, ni hoja tu,
kama ni kutofautiana mawazo sio kuitana wasaliti au mdini au mkabila
na kama wanachama wengi na viongozi wanaonyesha tabia fulani in public wawe wametumwa ama hawajatumwa inaonekana wanawakilisha chama
 
Huyo Fatma unayemtetea hapa hajawahi kuita mtu mkabila, au mdini?

Hata hivyo sio vibaya Fatma kaona mchango wako dhidi ya CDM, sasa kaa pembeni uangalie CDM itakavyojuta.
 
Huyo Fatma unayemtetea hapa hajawahi kuita mtu mkabila, au mdini?

Hata hivyo sio vibaya Fatma kaona mchango wako dhidi ya CDM, sasa kaa pembeni uangalie CDM itakavyojuta.
Fatma hanijui wala sijamtaja Fatma tu hapo, ni mifano miwili ninetoa
Halafu nyie watu kila anayekuwa na mtazamo tofauti dhidi ya siasa zenu anakuwa katumwa? 😂😂
 
Kama CCM wanachuo, basi ni hicho cha kupora uchaguzi. CDM wanaiga nini kwenye hilo? CCM ingekuwa na chuo cha maana tusingeona kiwango kikubwa cha kujikomba kwa vijana na wazee wake. Hicho chuo cha CCM hakifundishi ubora, bali kinafundisha zaidi hila, ukatili na jinsi ya kutumia dola kubaki madarakani kwa shuruti.
Mkuu tuwe kidogo objective, pamoja na yote lakini bado vijana kwa elimu zao na mengineyo bado wanatakiwa kupigwa msasa kuelewa miiko na falsafa japo siasa za afrika zinajulikana
 
Back
Top Bottom