kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 239
(1) Rachel au Regia wamelalamika? Hapana. Wameelewa na kukubaliana na maamuzi ya chama chao. Tuwaunge mkono basi.
(2) Lengo ni kuleta mabadiliko Tanzania mwaka huu. Wananchi wamechoshwa sana na utawala wa miaka 49 wa TANU na CCM. Wengi hapa tunamkubali Slaa aongoze hayo mapambano. Mbona wengine mnatafuta namna ya kutugawa tena? Tuungane ili kushinda kwa sasa, na tukubali maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA.
(3) Watanzania wataunda Katiba Mpya ya Tanzania na hata ya CHADEMA, baada ya kuing'oa CCM.
(4) Wale wanaoutumia muda wao hapa kuikosoa CHADEMA kwa namna ya kutaka kuiongezea nguvu wanafanya vyema. Wale wanotaka kuidhoofisha wanapigania CCM ibaki madarakani.
(5) Nadhani CCM wanapata ahueni wanopoona namna akina MMKJ wanavyojitahidi kupooza nguvu ya CHADEMA.
Nikiwa mwanachama hai wa Chadema siamini mawazo ya mwanachama au mwananchi yana nia ya kuua Chama. Mtazamo na maoni ya mtu yeyote hayana nia ya kuua chama. Maswali au mshangao hauna nia ya kuua chama.
Chama cha siasa kinajiiua chenyewe kwa matendo, sera, maadili na mwendesho wake. naichukia CCM kwasababu ya umangimeza, imekataa kusikia kilio cha wananchi na kero zake kwa kukumbatia chama zaidi ya sera na kanuni zake.
Nikiwa mmoja wa wanaCHADEMA napenda kukosolewa kuulizwa na kuhojiwa kwani hii yote kwa Chama watu na viongozi makini ndiyo misingi ya kufanya sahihi. Sera ya zidumu fikira sahihi imekufa haipo na haitakuja. Yeyote mwenye mawazo, yanayofanana na yasiyofanana anakaribishwa kwani wote wanatoa changamoto kujenga chama imara na chenye misingi bora kwa wanachama na wananchi.
kama kunamakosa ni haki ya wanachama wananchi kuuliza, kuhoji na kutaka maelezo bila ya vitisho kwamba kila mwenye hoja tofauti anawalakini. Hiki ni chama cha siasa sio kampuni. Naungana na wote wenye mawazo chanya na wale wenye mawazo hasi kwa manufaa ya chama. CCM inakufa kwa sababu kilaanayewakosoa anaonekana adui na kutupwa kuzimu, sitaki chama changu kirithi huu upupu.