Kiranga,
Just to get kile unachoengelea hapa, hivi kuna tofauti kati ya kuvipa vyama uhuru wa kuchagua (na kuwapa wanachama wa vyama hivyo uhuru wa kuchagua)?
Big difference,
Kwa mfano, watu wa higher level katika chama kwa kutumia intelligence network yao wanaweza kujua mambo mabaya ya mgombea ambayo wanachama wa kawaida hawayajui, na labda hayawezi kuthibitishwa kirahisi na kwa hiyo hayawezi kusemwa wazi. Kukipa chama uwezo wa ku veto watu kutahakikisha chama kina uwezo wa kumuondoa mtu ambaye anajulikana kuwa na scandals fulani hatari kwa stability ya chama ambazo hazijulikani kwa wanachama wa kawaida. Lakini ukiwapa wanachama wa kawaida uwezo wa kuamua moja kwa moja kwa kutumia popular vote, unaweza kabisa kujikuta una mgombea gendaeka. Kwa hiyo big difference.
Chukulia mfano wa Malecela alivyokuwa anawa manipulate CCM, kama CCM isingekuwa na mechanism ya kum stop Malecela alikuwa anaweza hata kuununua urais, lakini wajanja wa CCM kina Nyerere wakatumia influence kwenye chama kumuondoa. Now unaweza kupinga hili kwa kusema kwamba ni counter-democratic means, lakini democracy inaweza kufanya system iwe gullible pia, hapo ndipo unahitaji means za kuvipa vyama autonomy.
Kumbuka, kuna the whole argument ya kumruhusu Shibuda aingie Chadema, na kisha wanachadema (wana chama wa chama cha chadema) wakapata nafasi na uhuru wa kumchagua au kumtosa - unakumbuka position yako kwenye hili?
Position yangu ilikuwa CHADEMA wasimpe Shibuda nafasi ya kugombea kiti sasa hivi, kwa sababu hajajiprove chamani, hajakaa na watu kueleweka chamani etc. Kujiingiza kwake CHADEMA mara tu baada ya kuondoka CCM (If at all that is the case) kunaonyesha kwamba anapenda ubunge zaidi ya anavyoipenda CHADEMA, if anything kama anataka angojee 2015 wakati atakuwa kashaji prove chamani.
Nikaongeza kumpa nafasi sasa hivi ni CHADEMA kujionyesha hakina principles wala wagombea na kipo desperate kuchukua makapi yeyote yaliyoshindwa CCM huko.
Hapa kuna suala la wanachama wa chadema wamechagua mtu wanayempenda, kisha chama (nikiongelea viongozi au whoever anamiliki chama) wanamkataa mtu huyo na kutaka kupendekeza mwingine - unaijua position yako kwenye hili pia.
Position yangu ni kwamba chama ni lazima kiwe na autonomy, hii ndiyo relevancy ya chama, as much as I believe in grassroot involvement and the bottom up system, chama pia -ngazi za juu- kinatakiwa kuonyesha leadership kwa wananchama wake, kuwapa muongozo. Kama tunataka wanachama ndio wawe wanaamua kila kitu itakuwa anarchy, wala si democracy.
Kama chama -uongozi wa juu- kina abdicate kila kitu kwa wanachama, then chama kinakosa relevancy, na we might as well abandon parties.
The idea is, if you have legitimate leadership, the leadership will operate with the interest of the members. And if you don't believe in this leadership, you vote it off or get off the ship. Hii ndiyo Msuya alisema, huwezi kusema wewe mkatoliki halafu humuamini papa, utakuwa umeanzisha faction nyingine.
Tofauti ya hayo mawili (katika context ya Shibuda, Nape, na hii thread) ni ipi kwa mtizamo wako?
Sina tofauti significant, kote nataka chama kiwe na autonomy, uongozi wa juu wa chama usiwe forced kufanya maamuzi, uwe na uwezo wa kuamua, usiwe forced na wanachama.Ila ningependa kuona uongozi wa juu haumpi mtu kama Shibuda nafasi ya kugombea ubunge right away.
My philosophy is simple, vipe vyama meno, au viue usiwe na vyama kabisa.