LIMBOMAMBOMA
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 10,482
- 14,007
Polis wanafanya mambo kienyeji sana, wao walipaswa kuonesha sababu ya kuomba majina hayo, polis wanafanya kazi kienyeji sana...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa maOCD walipaswa kufutwa kazi Mara moja, wameshindwa kufanya kazi kiweledi.Igp siro ameliingiza jeshi kwenye siasa vibaya sana.wao majina ya wagombea yanawahusu nin
Hapo msajili hawezi kutia neno, yuko kiimyaWanataka majina ya nini hawa polisi CCM.?
Wamechukua majukumu ya Tume ya Uchaguzi ya CCM.
Tulishawazoea kwa kulalamika! Umesema hujui sababu badala ya kwenda kuwauliza sababu tayari eti unasema UNAMTAKA IGP .... Who are you?? Mnaanza kuleta sababu za kushindwa! Kama Polisi wanataka kuwajua wagombea wenu ili waimarishe ulinzi kwenye maeneo yao. Kila wakati kuwaza negativity tuuuu!!
Nashangaa!!simpeleke tu majina kwani watayafanya nini
Na kiongozi muongo, anayetekeleza kwa hila yale asemayo, hupata laana ya milele.Siasa siyo mchezo mchafu sema watu wanapofanya siasa ndiyo wachafu.
Na siasa ikijaa watu wachafu inakuwa haina lengo la kuleta mabadiliko yoyote kwa wananchi zaidi ya kuiba Mali za umma tu
simpeleke tu majina kwani watayafanya nini
Kazi imeanza tayariChama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Taarifa kwa Umma
Jeshi la Polisi maeneo mbalimbali ya nchi yetu limepeleka barua kwa viongozi wetu ngazi za Wilaya wakiwataka kuwapelekea Majina ya Wagombea wetu ndani ya Chama wa nafasi ya Ubunge.
Barua hizo ambazo zimesainiwa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya hazitaji sababu za kuhitaji Majina ya Wagombea wetu wala kuelezea Nia na misingi ya kisheria ya kutaka kupelekewa Majina hayo.
Kwa hatua za sasa tumewaelekeza viongozi wetu nchi nzima kuwa wasipeleke Majina hayo hadi hapo Polisi watakapotoa sababu na misingi ya kisheria za kuhitaji Majina ya watia Nia na Wagombea wa Chama chetu.
Pili tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi awachukulie hatua mara moja wakuu wa polisi wa Wilaya ambao wameandika barua hizo huku wakijua kuwa hawana mamlaka ya kisheria ya kuingilia michakato ya uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa.
Aidha tunamtaka IGP atengue barua hizo na aliongoze Jeshi la Polisi Kwa mujibu wa sheria na weledi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Octoba.
Mwisho tunaendelea kufuatilia kwa karibu hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi ya watia nia na wagombea wetu maeneo mbalimbali nchini kama vile kuwakamata, kuwalaza mahabusu na wengine wanatakiwa kusalimisha magari yao binafsi Polisi bila kuelezea sababu za hatua hiyo.
Tunalitaka Jeshi la Polisi litimize wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na liache Mara moja tabia ya kukandamiza Chama chetu kwa kushusha bendera za Chama chetu kama ilivyofanyika kule Same,Mkoani Kilimanjaro.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Limetolewa Leo Alhamisi 16 Julai,2020.
View attachment 1508520
Lisu kutwa anaomba ulinzi,.lakini hao policeccm wamekaa kimya,.sasa from no where wanaomba majina ya watia nia wa cdm, wamjibu kwanza lisu barua zake alizowatumia.Tuisome sheria ya uchaguzi kabla ya kuanza kulaumu.watia Mia wote na wagombea wanaitaji kulindwa hivyo wanapotaka kuwstambua ni kuwapatia ulinzi kwenye hiki kipindi kigumu ambacho kila mtu anaamini anaweza kuwa mbunge hivyo aina mpya ya uhalifu wa watiania kufanyiana njama mbaya waweza kuibuka
Barua zipo Tele wosap... Sema mambo yakiwa ovyo hawakawii kusema FAKEHivi Chadema ni wa kuandika barua ya hivi kweli asee? Au ni mkakati wa kuichafua chadame ionekane kutoa tuhuma za ovyo?
Na kama ni kweli hii ni ya Chadema mbona hawakuweka ushahidi wa hizo barua za polisi zinazolalamikiwa hapa?
Wasipo ziweka hizo barua tutaamini kuwa hizo ni propaganda tu kama ilivyokuwa kwenye tukio la kupigwa na kuvunjwa kwa KUB huku watu wakitamka "tumetumwa kukuvunja mkuu na unamsumbua Rais".
Mnapomshirikisha mungu kwenye mambo ya uongo, ndo maana chama chenu kimepata laanaSirro hata kama amewekewa kinga na bunge lakini Naapa kwa Jina la Mungu aliye hai ni lazima atafungwa tu
Kwa waandishi wa habari mnapelela list ya majina yote, lakini kwenye vyombo vya ulinzi na usalama hamtaki....yaani kati ya zero strategy hii imefunga mwaka.Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Taarifa kwa Umma
Jeshi la Polisi maeneo mbalimbali ya nchi yetu limepeleka barua kwa viongozi wetu ngazi za Wilaya wakiwataka kuwapelekea Majina ya Wagombea wetu ndani ya Chama wa nafasi ya Ubunge.
Barua hizo ambazo zimesainiwa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya hazitaji sababu za kuhitaji Majina ya Wagombea wetu wala kuelezea Nia na misingi ya kisheria ya kutaka kupelekewa Majina hayo.
Kwa hatua za sasa tumewaelekeza viongozi wetu nchi nzima kuwa wasipeleke Majina hayo hadi hapo Polisi watakapotoa sababu na misingi ya kisheria za kuhitaji Majina ya watia Nia na Wagombea wa Chama chetu.
Pili tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi awachukulie hatua mara moja wakuu wa polisi wa Wilaya ambao wameandika barua hizo huku wakijua kuwa hawana mamlaka ya kisheria ya kuingilia michakato ya uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa.
Aidha tunamtaka IGP atengue barua hizo na aliongoze Jeshi la Polisi Kwa mujibu wa sheria na weledi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Octoba.
Mwisho tunaendelea kufuatilia kwa karibu hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi ya watia nia na wagombea wetu maeneo mbalimbali nchini kama vile kuwakamata, kuwalaza mahabusu na wengine wanatakiwa kusalimisha magari yao binafsi Polisi bila kuelezea sababu za hatua hiyo.
Tunalitaka Jeshi la Polisi litimize wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na liache Mara moja tabia ya kukandamiza Chama chetu kwa kushusha bendera za Chama chetu kama ilivyofanyika kule Same,Mkoani Kilimanjaro.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Limetolewa Leo Alhamisi 16 Julai,2020.
View attachment 1508520
If that's the case then, hatuna tena Jeshi la Polisi Tanzania bali tuna Jeshi la Polisi la ki CCM.Wakipotea tu tunajua ni wao .View attachment 1508586