Uchaguzi 2020 CHADEMA: Jeshi la polisi limeomba majina ya wagombea wetu

Tofauti ya T-shirt mbili yaani ya Magufuli na Lissu ni kwamba za Magufuli zitagawiwa bure au ikiwezekana T-shirt unapewa na hela juu lakini T-shirt ya Lissi itauzwa na zitamwagika za kutosha nchi nzima najua wapo askari watakuwa wanazitamani kuzivaa ila kwakuwa waliuvaa usisiemu watakuwa hawana namna.
 
Ndo mmemaliza?
Kwa hatua hizi za kidemokrasia wamebakiza kipi ili muiite chadema ni chama cha kigaidi au wavunjifu wa amani?

On my note above !

Maaskofu wetu wanasubiri sadaka jumapili ? Au wanadhani sisi nimisule Yao ya kuwapelekea sadaka?
 
Huyu nae
Hivi jeshi la Polisi Tanzania mbona linetawaliwa na ujinga wa hali ya juu hivyo?
Huyu nae aliyeandika Taarifa kwa vyombo vya habari na Uma mbona hajataja polisi wa wilaya gani walioandika barua hizo vinginevyo taarifa ni bogus
 
Huu ndo mda wa sisi wanyonge kwenda kuwaponda tanipoli kule twitter
 
Maelezo kuwa imetolewa leo tarehe 16 Julai 2020 Alhamisi ila picha ya barua imetolewa leo tarehe 17 Julai, 2020 Alhamisi!
 

Attachments

  • Screenshot_20200717-012723~2.png
    94.1 KB · Views: 2
Hivi jeshi la Polisi Tanzania mbona linetawaliwa na ujinga wa hali ya juu hivyo?

Huyu IGP Zero hatoshi kwene nafasi hii! Huyu jamaa anafanya kazi Zake kwa maelekezo ya JIWE....pambaf zake!
Kutaka majina ya Watia Nia toka CHADEMA inaonesha Kuna Agenda ya Siri na lazima CHADEMA wafuatilie na kujua Kulikoni! IGP ajitokeze atoe ufafanuzi au la atoe Maagizo kwa RPCs na DPCs wakome Mara moja kufuatilia majina ya Watia Nia.,.. !!
Maana kama ni kutaka majina ya Watia Nia/Wagombea wa CHADEMA kwa kuwapa Ulinzi, Basi Jeshi la Polisi waombe majina ya Watia Nia wote wa vyama vyote including CCM...!!
Vinginevo Polisi Kuna kitu wanakijua nyuma ya pazia!!
 
Yaani watia nia wa ubunge Tanzania nzima watakua wengi kuliko kura za Chadema, ACT WAZALENDO kwa pamoja!

Mungu warehemu wanachadema, Mungu irehemu Chadema.
 
Polisi kwa kawaidà hutekeleza majukumu yake kutokana na Sheria,taratibu zilizo wazi au kwa maagizo toka juu ndo maana tunashuhudia matukio mengi yasiyo ya kawaidà yanatokea mara kwa mara kuhusisha jeshi hilo lakini Serikali, mwajiri, inakaa kimya. Kwa hiyo kama kweli kuna barua hizo toka polisi basi wahusika wajitahadhari kwa usalama wao maana amri toka juu huwa haihojiwi kabla ya utekelezaji na baada ya utekelezaji ni kusubiri tuzo. Kama hali ndo hiyo, tujiandae kuona mengi wakati wa kampeini na mengi zaidi siku ya uchaguzi.
 

Huu ni uhuni uliovuka mipaka na wala hauwezi kuvumilika, hivi Mbowe yuko wapi mbona leadership imekosekana. Yani hadi unaandikiwa barua za ajabu kama hizi alaf mwneyekit kajifungia chumbani akiwaza urais. Shameful
 
Chadema inafutika Octoba labda ACT wataibuka nao kwa muda wa miaka mitano baada ya hapo nao wanafia mbali

Kumbe bado haijafutika, mi nilijua Chadema imefutika kipind kile cha corona hahahah
 
Hebu tutajie hicho kifungu ?
 
Hivi jeshi la Polisi Tanzania mbona linetawaliwa na ujinga wa hali ya juu hivyo?
sifa kuu ya kuajiriwa kama polisi ni urefu na mbio. hakuna nahusiano ya moja kwa moja kati ya urefu na AKILI
 
good.

pamoja na tamko hili... jee mmewasilisha rasmi malalamiko yenu kwenye mamlaka husika (i.e msajili wa vyama & tume ya uchaguzi?) kuhusu haya?

kumbukeni taarifa kwa umma pekee haijitoshelezi ku trigger legal proceedings huko mbeleni. taarifa kwa umma zaidi zaidi ni sympathy seeker tu.
 
pelekeni majina kwa usalama wenu nyie chadema ni wehu nini! hamtaki wagombea wenu walindwe na tume ya uchaguzi?
 
Hii barua mbona haijasainiwa hata kama imekuwa "scanned"? Kabla hatujaanza kulishutumu Jeshi la Polisi ni vyema makada wa CDM kutoka Makao Makuu waliipo hapa jukwaani wakatueleza ukweli wa tuhuma hizi na uhalisia wa barua hii.
Baada ya hapo ndo utachukua hatua gani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…