Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Taarifa kwa Umma
Jeshi la Polisi maeneo mbalimbali ya nchi yetu limepeleka barua kwa viongozi wetu ngazi za Wilaya wakiwataka kuwapelekea Majina ya Wagombea wetu ndani ya Chama wa nafasi ya Ubunge.
Barua hizo ambazo zimesainiwa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya hazitaji sababu za kuhitaji Majina ya Wagombea wetu wala kuelezea Nia na misingi ya kisheria ya kutaka kupelekewa Majina hayo.
Kwa hatua za sasa tumewaelekeza viongozi wetu nchi nzima kuwa wasipeleke Majina hayo hadi hapo Polisi watakapotoa sababu na misingi ya kisheria za kuhitaji Majina ya watia Nia na Wagombea wa Chama chetu.
Pili tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi awachukulie hatua mara moja wakuu wa polisi wa Wilaya ambao wameandika barua hizo huku wakijua kuwa hawana mamlaka ya kisheria ya kuingilia michakato ya uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa.
Aidha tunamtaka IGP atengue barua hizo na aliongoze Jeshi la Polisi Kwa mujibu wa sheria na weledi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Octoba.
Mwisho tunaendelea kufuatilia kwa karibu hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi ya watia nia na wagombea wetu maeneo mbalimbali nchini kama vile kuwakamata, kuwalaza mahabusu na wengine wanatakiwa kusalimisha magari yao binafsi Polisi bila kuelezea sababu za hatua hiyo.
Tunalitaka Jeshi la Polisi litimize wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na liache Mara moja tabia ya kukandamiza Chama chetu kwa kushusha bendera za Chama chetu kama ilivyofanyika kule Same,Mkoani Kilimanjaro.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Limetolewa Leo Alhamisi 16 Julai,2020.
View attachment 1508520