CHADEMA: Katiba mpya serikali 3 ruksa, Katiba Tanganyika mchakacho uanze mara moja!

CHADEMA: Katiba mpya serikali 3 ruksa, Katiba Tanganyika mchakacho uanze mara moja!

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
images
SAID%20ISSA%20MOHAMED.jpg

Chadema waweka msimamo serikali tatu, mabomu Arusha
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imekutana kwa dharura kujadili muundo wa serikali tatu na hatma ya Muungano wa Tanganyika na Zanziba, na leo chama hicho kinatarajia kutoa taarifa rasmi ya msimamo wake.

Halikadhalika, suala la Tume huru ya uchaguzi limejadiliwa kwa kina na wajumbe hao huku wengi wakiwa na hofu kuwa kulingana na ilivyopendekezwa kwenye rasimu hakuna uwezekano wa Tanzania kuwa na tume huru kama ilivyo nchini Kenya.

Hayo yalisemwa jana na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohamed,wakati akizungumza na NIPASHE kuhusu yaliyojiri kwenye mkutano huo wa dharura. Alisema Chadema itatoa msimamo wake leo mbele ya waandishi wa habari ili Watanzania waweze kujua kwa uwazi kuhusu masuala ambayo yameonekana kuwa mapya.

Katiba mpya

Alisema kikao hicho kilianza Julai 06, mwaka huu, na suala kubwa lilikuwa ni kujadili kipengele kwa kipengele rasimu ya Katiba, na wajumbe wengi walizungumzia kinagaubaga suala la serikali tatu na hatima ya Muungano.
“Wajumbe wengi wameonekana kulizungumzia kwa kina suala la Muungano, suala la serikali tatu ilikuwa ni moja ya mapendekezo ya Chadema kwa Tume, muundo wake ndio tunaujadili kwa kina,” alisema.

Tume huru ya Uchaguzi
Mohamed alisema suala la tume huru ya uchaguzi limechukua nafasi kubwa katika kikao hicho na huku wajumbe wengi wakionyesha hofu iwapo kutakuwa na Tume huru itakayotenda haki wakati wa chaguzi.

Katiba ya Tanganyika
Alisema msimamo wa Chadema ni kutaka ipatikane Katiba inayotengeneza viongozi na si watawala.Alibainisha kuwa suala lingine ni kuanza mchakato wa uundaji Katiba ya Tanganyika kwa kuwa Zanzibar tayari kuna Katiba na itakapokamilika ya Muungano ni wazi kuwa Tanganyika itashindwa kuendesha shughuli zake.

Shambulio la Bomu Arusha
Aidha, Mwenyekiti huyo, alisema kikao hicho pia kilijadili hali ya kisiasa nchini ikiwamo tukio la kulipuliwa kwa bomu katika kampeni za Chadema mkoani Arusha na uchaguzi katika kata 26 nchini.Tukio la shambulio la bomu lilitokea mwezi Juni, mwaka huu, na kuua watu watatu, akiwamo kiongozi wa Chadema, na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kaloleni.

 
Ngoja tusubiri msimamo rasmi utakaotolewa na viongozi wakuu wa chama au msemaji wa chama mh J J Mnyika
 
vipi, walionyesha na ule mkanda/video ya kujilipua kwa bomu arusha?
 
Kwa hiyo wao wanataka kujipanga ktk mbio za kutafuta urais upi ? Watanganyika au shiririkisho
 
Mbona hawasemi kuhusu wao kupinga mgombea binafsi?
 
Mbona hawajasema chochote kuhusu mualiko wa Mbowe Ikulu.
 
Soma vizuri acha kukurupuka ametaja NIPASHE au wewe unataka source gani Chili au Tomato?

Umeona Ritz,
Wengi wa wachangiaji wana hulka yakusoma kichwa cha habari tu bila kuipitia habari yote kwa kina, huwa tunaweka source kama ndani ya habari hakuna taarifa inayopambanua chombo kilicho-publish habari husika. Ndani ya habari mtu unaweza kupata mengi zaidi.
 
Mbona hawajasema chochote kuhusu mualiko wa Mbowe Ikulu.

Ritz wewe ni msengerema nn?mbona una shadadia sana swala la mualiko ikulu linakuhusu nn wewe pimbi?watu wanajadili mambo nyeti ya kimaslah kwa taifa wewe unaongea upumbafu wako hv umesoma shule ya wapi wewe akili yako kama ya kuku,pumbafu wahed
 
1+1=2 Hii formula ya nyerere kuhusu muungano kati ya tanganyika na zanzibar ni fumbo la siri haikwepeki. Wanaopenda muungano zenj ni wengi, wanaopinga ni wachache ila wanapiga vuvuzela mpaka wenzao wanaogopa. Serikali 3 itawarahisishia kazi wapiga vuvuzela.
 
matamko yanaendelea

Kukutana mara kwa mara na kupanga mikakati ni dalili nzuri ya umoja katika vyama vya siasa. Tofauti ninayoiona kati ya NCCR Mageuzi kipindi chama hicho kilipokuwa na nguvu nchini chini ya Lyatonga Mrema mzee wa Kiraracha ni hii ya chama Chadema kuwa na mikutano ya mara kwa mara na tamko kuwa la pamoja tofauti na kipindi cha Mrema yeye ndiye aliyekuwa kila kitu. CCM ilipopitisha mambo yao kukisambaratisha hawakutumia nguvu nyingi kama wanavyohaha sasa kupunguza kasi ya Chadema.

Mikutano ni muhimu, hata katika mapambano ya majeshi katika vita lazima kukutana mara kwa mara kuelezana mikakati ya adui na kupanga mbinu ya kupambana, la sivyo itakuwa kila mmoja kupigana kivyake tu na ikawa njia nyoofu kwa adui kushinda.
 
Acha kiitwe chama cha matamko,chama cha kidini,chama cha wachaga,mara saccoss mara kikundi cha wapiga deal,ila mwisho wa yote hiki ndiyo Chama pendwa hapa Tanzania,chama kinachoihenyesha ccm,kimeipumbaza ikapumbazika na mpk kuamua kuja na kila aina ya vitisho bila mafanikio na tunakoelekea mtaanza kuana wenyewe kwa wenyewe nakuisingizia cdm...

mwanaume unakuwa na roho mbaya kama kalai ya kukaangia karanga
 
Chadema walikuwa wamejipanga kuhusu muundo huu toka kwenye ilani yao ya uchaguzi ya 2010, copy and paste ya CCM ndiyo tatizo tulilonalo; nachoshukuru mimi ni JK kumchagua mzee Warioba, kawaida Mkurya ukimkabidhi madaraka utakoma. hongera zangu za moyoni zimfikie mzee wangu Warioba.....simamia haki za nchi hii kwa miaka mingine 100, okoa kizazi kijacho sisi wa sasa washatugeuza vitumbua.
 
Back
Top Bottom