CHADEMA: Katiba mpya serikali 3 ruksa, Katiba Tanganyika mchakacho uanze mara moja!

CHADEMA: Katiba mpya serikali 3 ruksa, Katiba Tanganyika mchakacho uanze mara moja!

..vipi kuhusu kura ya maoni Znz?

..wa-Znz wapewe nafasi ya kuamua kama wanataka kuwa ktk muungano kupitia kura ya maoni.

..vingenevyo hatutaishi kwa amani hata ktk hizo serikali 3 zinazopendekezwa.

cc: Dr.W.Slaa, Zitto, Molemo, Tumaini Makene, Mwita Maranya, Mchambuzi, GHIBUU, Ngekewa, Nguruvi3, Gaijin, EMT, Kobello

Wazanzibari wanaenda kwa hatuwa hawahitaji haraka! Hapo mwanzo waliomba hili la kura ya maoni sana lakini ikashindikana. wakataka serikali tatu nayo ikashindikana wakaona waaim juu zaidi ili wapate la chini. Watatishia kuukataa muungano kwa harakati za uamsho wakijuwa kuwa lolote litakalofanywa mwisho wake ni kuvunjika klwa muungano kwa vile upande wa pili wanachukulia huu muungano kama nguvu ya kuitawala zanzibar.
Wazanzibari iwapo serikali tatu zitapita hatuhitaji kura ya maoni kwani tunajuwa hiyo ni transition kuelekea mgawanyiko. angalau mgawanyiko huu utakuwa wa amani kwani Tanganyika na hasa kwa nguvu ya CDM hawahimili kukaa meza moja na zanzibar kwa misingi ya usawa! Viongozi wao mara nyingi wameshaonyesha hilo. Kiburi chao na dharau kitapelekea Tanganyika kwa hiari yao wavunje muungano!
 
Ngekewa,

..wewe unaona kiburi upande wa wa-Tgk tu.

..hivi huoni ni kiburi, dharau, choyo, na ubinafsi, kwa wa-Znz ambao ni 3% ya population ya muungano, kudai usawa na wa-Tgk ambao ni 97% ya muungano.

..halafu usawa mnadai wakati wa kugawana tu, wakati wa kuchangia hamdai usawa.

..tafadhali usitumie mfano wa uanachama wa UN, au kwamba tuliungana mataifa mawili huru. hata huko UN kuna wanachama wa kawaida, na mataifa makubwa members wa security council. pia tuliungana mataifa mawili huru, lakini mmoja ni mkubwa kuliko mwenzake.

NB:

..baraza la wawakilishi lilipitisha azimio la kura ya maoni kuamua suala la serikali ya umoja wa kitaifa.

..kwa msingi huo baraza la wawakilishi linaweza kupitisha mswada wa-Znz mkapiga kura ya maoni kuamua kama mnataka muungano au la.

cc: Nguruvi3, Mchambuzi, gombesugu
 
Last edited by a moderator:

Joka Kuu napenda kubadilishana mawazo nawe kwa vile umuwazi na naamini unachokisema ndio kilcho akilini mwako hasa!
Kuhusu dharau, unafikiri dharau inatoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa? La ni kinyume chake. Watanganyika wengi wanadharau kwa Wazanzibari kwa sababu tu wanafikiri kuwa wao bora kuliko wenzao. Mfano wewe unadharau idadi ndogo ya Wazanzibari lakini nikuulize mtu kumiliki chake kunataka ukubwa na udogo. Wazanzibari nchi yao ni zanzibar sio Tanganyika, sasa unataka tujidharau na tukubali kudhulumiwa eti kwa kuwa sisi ni wachache, au tuanze kujifanya kuwa tuna haki na Tanganyika eti tu ni nchi yenye watu wengi kuliko sisi? Sijui kama unaiona level ya dharau yako juu yangu lakini kwa mie nahisi kikubwa chako ni chako na kidogo changu ni changu na ndicho nitakachojivunia. Sasa dharau hiyo iko kwenye kila nyanja pengine elimu, rasilimali na vyenginevyo.
Kuhusu kuchangia, tatizo ni kwamba Huu muungano ulifanywa kwa njia za kilahai na faida yake wanaijuwa hao waliofanya hila hizo. Iwapo Tanganyika inachangia kikubwa, hili halikueleweka hapo mwanzo? Hata hivyo Joka Kuu unapofikiri suala la kuchangia sijuwi pia unafikiri utumiaji wa huduma? Polisi wangapi wanaohudumia Zbar ukilinganisha na wale wa Tanganyika? Urefu wa mipaka ya kulindwa na jeshi iko vipi kati ya nchi mbili hizi,mbali ya kuwa zanzibar jirani wake ni mmoja tu Kenya. Elimu ya juu wanafunzi wa ngapi wanasoma elimu ya juu kutoka Zanzibar na elimu ya msingi na sekondari nani analipa kwa Tanganyika na nani analipa kwa zanzibar? Mambo ya nje, Zanzibar hawazidi watu 20 wanaotumikia wizara hiyo na Ziara ngapi za marais na wakuu waq nje zinakwenda zanzibar(tukiaminikuwa ziara hizo huwa na tija). Msururu wa kutokuwepo usawa ni mrefu ndugu yangu!

Hilo la Baraza kuamuwa ni kusadikika kwani walipobadilisha katiba tu mliruka ohh1 wanavunja Katiba. Kuweni wakweli na mtueleze nini hasa kinakufanyeni mtubane ili tusiendelee.
 
Back
Top Bottom