CHADEMA: Katiba mpya serikali 3 ruksa, Katiba Tanganyika mchakacho uanze mara moja!

CHADEMA: Katiba mpya serikali 3 ruksa, Katiba Tanganyika mchakacho uanze mara moja!

Ritz peopleeeeeeeeeeeeeeeeesssssssssssssssssssss
998343_218766928270485_1759816244_n.jpg

mungu atatushindia.
 
kama ni Kweli, CHADEMA mmewahi sana! CCM wanacheza mchezo wa kusubiri waone wengine mnasemaje ili waweze kujua upepo unaelekea wapi. Uisahau wao lengo lao ni kushinda, na kwa hili kama ni kweli, basi watakuwa na hoja ya kusimamia. Tusubiri tuone misimamo rasmi
 
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imekutana kwa dharura kujadili muundo wa serikali tatu na hatma ya Muungano wa Tanganyika na Zanziba, na leo chama hicho kinatarajia kutoa taarifa rasmi ya msimamo wake.

Halikadhalika, suala la Tume huru ya uchaguzi limejadiliwa kwa kina na wajumbe hao huku wengi wakiwa na hofu kuwa kulingana na ilivyopendekezwa kwenye rasimu hakuna uwezekano wa Tanzania kuwa na tume huru kama ilivyo nchini Kenya.

Hayo yalisemwa jana na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohamed,wakati akizungumza na NIPASHE kuhusu yaliyojiri kwenye mkutano huo wa dharura.

Alisema Chadema itatoa msimamo wake leo mbele ya waandishi wa habari ili Watanzania waweze kujua kwa uwazi kuhusu masuala ambayo yameonekana kuwa mapya.

Alisema kikao hicho kilianza Julai 06, mwaka huu, na suala kubwa lilikuwa ni kujadili kipengele kwa kipengele rasimu ya Katiba, na wajumbe wengi walizungumzia kinagaubaga suala la serikali tatu na hatima ya Muungano.

“Wajumbe wengi wameonekana kulizungumzia kwa kina suala la Muungano, suala la serikali tatu ilikuwa ni moja ya mapendekezo ya Chadema kwa Tume, muundo wake ndio tunaujadili kwa kina,” alisema.

Mohamed alisema suala la tume huru ya uchaguzi limechukua nafasi kubwa katika kikao hicho na huku wajumbe wengi wakionyesha hofu iwapo kutakuwa na Tume huru itakayotenda haki wakati wa chaguzi.

Alisema msimamo wa Chadema ni kutaka ipatikane Katiba inayotengeneza viongozi na si watawala.

Alibainisha kuwa suala lingine ni kuanza mchakato wa uundaji Katiba ya Tanganyika kwa kuwa Zanzibar tayari kuna Katiba na itakapokamilika ya Muungano ni wazi kuwa Tanganyika itashindwa kuendesha shughuli zake.

Aidha, Mwenyekiti huyo, alisema kikao hicho pia kilijadili hali ya kisiasa nchini ikiwamo tukio la kulipuliwa kwa bomu katika kampeni za Chadema mkoani Arusha na uchaguzi katika kata 26 nchini.

Tukio la shambulio la bomu lilitokea mwezi Juni, mwaka huu, na kuua watu watatu, akiwamo kiongozi wa Chadema, na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kaloleni.
 


Katiba ya Tanganyika
Alisema msimamo wa Chadema ni kutaka ipatikane Katiba inayotengeneza viongozi na si watawala.Alibainisha kuwa suala lingine ni kuanza mchakato wa uundaji Katiba ya Tanganyika kwa kuwa Zanzibar tayari kuna Katiba na itakapokamilika ya Muungano ni wazi kuwa Tanganyika itashindwa kuendesha shughuli zake.

Nini msimamo rasmi wa Chadema kuhusiana na umuhimu wa Katiba ya Tanganyika? Kwa tamko la hapo juu, its not clear - je hoja ni kwamba katiba ya Tanganyika lazima ianze kabla ya katiba za Muungano? au hoja ni kwamba mchakato wa Katiba ya Tanganyika na ya Muungano ni muhimu iende sambamba? Lakini muhimu zaidi, tamko la chadema halielezei kwa uwazi bila kujiuma uma iwapo tumekosea kukimbilia katiba ya Muungano kabla ya kukamilisha kwanza Katiba ya Tanganyika;
 
Sio issue ya kuanza mara moja! Inabidi kusikiliza mawaidha ya wote na kuyatafakari.
 
Matola ameongeza jina langu kati ya watu wapokeao buku saba....iwe kweli sasa! sio porojo..nasubiri buku saba zangu!
 
Nini msimamo rasmi wa Chadema kuhusiana na umuhimu wa Katiba ya Tanganyika? Kwa tamko la hapo juu, its not clear - je hoja ni kwamba katiba ya Tanganyika lazima ianze kabla ya katiba za Muungano? au hoja ni kwamba mchakato wa Katiba ya Tanganyika na ya Muungano ni muhimu iende sambamba? Lakini muhimu zaidi, tamko la chadema halielezei kwa uwazi bila kujiuma uma iwapo tumekosea kukimbilia katiba ya Muungano kabla ya kukamilisha kwanza Katiba ya Tanganyika;

Msimamo wao nadhani utajulikana watakapotoa taarifa rasmi ya kikao hicho cha Kamati Kuu. Huu ulikuwa ni utangulizi kuhabarisha kinachoendelea ndani ya kikao kuongosa wasiwasi wa wengi kutojua kikao kinajadili nini. Nataraji hivyo, vinginevyo wakija na single kama ya hapo juu naona watakuwa wamejikanganya.
 
Swali: Ina maana ya kuwa mambo mengine yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba Mpya wanakubaliana nayo isipokuwa timing ya Katiba ya Tanganyika?

Swali la Nyongeza: Kama hakutakuwa na tume huru ya uchaguzi kabla ya wakati huo msimamo wa CDM ni nini?
 
..vipi kuhusu kura ya maoni Znz?

..wa-Znz wapewe nafasi ya kuamua kama wanataka kuwa ktk muungano kupitia kura ya maoni.

..vingenevyo hatutaishi kwa amani hata ktk hizo serikali 3 zinazopendekezwa.

Siyo Wazanzibari tuu. Kila Mtanzania kutoka Bara na Visiwani apewe nafasi ya kuamua kama anataka muungano kupitia kura ya maoni.
 
..vipi kuhusu kura ya maoni Znz?

..wa-Znz wapewe nafasi ya kuamua kama wanataka kuwa ktk muungano kupitia kura ya maoni.

..vingenevyo hatutaishi kwa amani hata ktk hizo serikali 3 zinazopendekezwa.

cc: Dr.W.Slaa, Zitto, Molemo, Tumaini Makene, Mwita Maranya, Mchambuzi, GHIBUU, Ngekewa, Nguruvi3, Gaijin, EMT, Kobello
Hapa ndipo tulimuonya Warioba mapema sana kuwa lazima wzn waamue kama wanataka muungano au la.
EMT nadhani wao ndio wenye malalamiko, na kupunguza gharama wao waamue kwasababu ni rahisi sana,
Iwe kama ilivyokuwa Quebec, north ireland, Timor, South Sudan na hata kule Puerto rico.

Tayari kuna uhasama waliojenga wzn kiasi kwamba hata muungano ukilazimishwa hakuna atakayekuwa na raha kuishi nao kama rai wa nchi moja. Zaidi ya hapo watazidi kudai kila kisicho chao kila siku. Nadhani tumechoka sasa.

Njia nzuri na rahisi tukutane EAC basi. Hatuhitaji kuishi katika mazingira haya yasiyo ya kuaminiana tena, yaliyojaa uhasama na chuki. Kila mtu akae kwake.
 
Last edited by a moderator:
Too low for you, yaani hata wewe unadhani Ritz wa JF ndio Ridhiwani Kikwete!? Ridhiwani akeshe hapa JF kwa shida gani na mipesa aliyotuibia kwa mgongo wa Baba yake atatumbuwa saa ngapi?

Ritz wa JF ni majobless wa Lumumba ambao wanaishi kwa ujira wa buku sabasaba na ndio maana muda wote wapo online hapa JF maana ni sehemu ya ajira yao.

Umeshawahi kujiuliza Mbowe aliipataje Bilicanas na Baba'ke alikuwa ni nani na ana wadhifa upi Serikalini?
 
rasimu ya katiba ni feki na serikali tatu ni feki. Genuine ni kila nchi kurudisha heshima yake na kuua muungano, ndipo kelele zitakwisha. Serikali tatu zitaleta makelele mengi zaidi.....nani atakuwa na hadhi ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la kijeshi....? who will be the head of state? mkuu wa muungano wa serikali ya muungano ataitwa nani, na wa tangani\yika ataitwa nani? Tangu 1962 tanganyika ilikuwa na rais wake....so is zanzibar on Jan 1964.
 
Back
Top Bottom