CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Mayalla unatatizo la ushabiki, hao makamanda wako walifukuzwa chama kwa kosa la kuidharau CC iliyowaita wakajieleze, hivyo swala la kuapishwa halipo, lingekuwepo kama wangejieleza na chama kuwafukuza.
Anyway you will always hate Chadema and get nothing.
 
Mimi nina mashaka na akili zako, Mwinyi ni kibaraka tu wa Tanganyika wala hana uungwana wowote.

Kinachoendelea Zanzibar ni mambo ya Kikatiba na siyo hisani, kama uungwana basi Maalim Seif na wenzake ndio waungwana.
 
Mimi nina mashaka na akili zako, Mwinyi ni kibaraka tu wa Tanganyika wala hana uungwana wowote.

Kinachoendelea Zanzibar ni mambo ya Kikatiba na siyo hisani, kama uungwana basi Maalim Seif na wenzake ndio waungwana.
Nadhani tuna wajibu wa kutumia lugha ya staha kwa viongozi wetu, kumuita rais wa nchi kibaraka sio jina la staha. Vibaraka ni wale vibaraka wa mabeberu.
Viongozi wetu ni wazalendo.
P
 
Watanzania ,watanganyika na wazanzibar wanakatishwa tamaa na baadhi ya wanasiasa na maamuzi yao, hivyo wanaamua kuachana na mambo ya kufatilia Siasa!

Niwakumbushe tu ndugu zangu, sukari tunayokorogea Hot beverage ni siasa, mafuta tunayoweka kwenye automobile ni siasa, beer na condom tunazotumia ni siasa!

Tusiache, tuendelee kujadili SIASA, siasa ni maisha.
 
Tupo tayari chama kife lakini hatutakubali kutumika kama muhuri wa kuhalalisha mateso kwa Watanzania. DEMOKRASIA NI MUHIMU KULIKO UHAI WA CHADEMA, TANZANIA NA WATANZANIA NI MUHIMU KULIKO UHAI WA CHADEMA. Kikubwa zaidi hatusikilizi ushauri wa WANAFKI.
Nia ya huyu jamaa siyo ushauri ila anahangaikia uteuzi. Kinamuuma nini kwa Chadema kufa? Heri kufa shujaa kuliko kuishi mtumwa na kufa mtumwa.
 
Huu ndiyo uhuru wa habari, kila mtu ana haki ya kuandika matapishi yake ya asubuhi.
Unachofikiria kifanyike Chadema ndio kitakacho fanywa, ila tusuhiri kidogo hasira zipungue na wakat huo huo muda utatulazimisha nini cha kufanya.

Humu ndani bado kuna watoto wengi wa siasa, subiri tuu Mbowe atalazimishwa na uhalisia wa kisiasa kujiunga na Serikali kwa kupeleka Wabunge na kuchukua ruzuku ya kuendesha chama Chetu.

Sio maamuzi yote ya kisiasa unayafanya kwa kupenda au kuyachagua, kuna mengi tuu unalazimishwa na uhalisia wa kisiasa kwa wakati huo.
 

Km hauna chama kaa kimya!! Mkuu!!
 
Mkuu Gerald .M Magembe, asante sana kwa mchango wako wa ushauri huu mstari, "Sio maamuzi yote ya kisiasa unayafanya kwa kupenda au kuyachagua, kuna mengi tuu unalazimishwa na uhalisia wa kisiasa kwa wakati huo", ni maneno mazito sana, na ya ukweli mchungu. Naamini hasira zikipita, Chadema nao will do the right thing!.
P
 
Ni ushauri mzuri uliotoa. Tabia ya kususa haisaidii chochote. Chadema wameitumia sana tabia hii, matokeo yake Chadema si ile ya enzi za Slaa. CUF ya wakati ule walisusia uchaguzi wa marudio Zanzibar. Kuna jambo Maalim Seif kajifunza....ndo maana wakati huu akiwa ACT Wazalendo, hajataka susia serikali ya umoja wa kitaifa. Busara na hekima ni jambo muhimu katika uongozi. Ndo maana Malkia Mrembo toka Ethiopia ya wakati huo alimtembelea mfalme Suleiman walau kuchota hekima. Dhana ya kujiona kwakua weye ni mpinzani basi hukubaliani na lolote lile na kujiona weye ni kila kitu ujenga kiburi na kufanya mtu kuwa na maamuzi ya kukurupuka yasiyo na tafakuri. Chadema wanahitaji kuwa wajanja na kucheza kwa ustadi mkubwa ktk siasa za Tanzania. Wajifunze kwa Raila Ondiga. Aliwahi susia uchaguzi lkn aling'amua kitu. Akajirudi na sasa amewezesha kuwepo kwa mchakato wa BBI. Siasa hazihitaji hasira wala chuki. Siasa hazihitaji kujionesha weye ni mwamba kwani unaweza shupaza shingo ikavunjika ghafla. Chadema wakubali tu matokeo, kutokukubali haiwasaidii na haitowasaidia, zaidi ni kukififisha chama. Kwa wabunge hawa mtazamo wangu wangeonywa, kuonywa ni njia mojawapo katika kutatua mgogoro. Si kila kitu ni fukuza. Chadema miaka yote haijawahi kukubali matokeo. Lakini waliingia bungeni, kila mtanzania anajua. Hivyo kususa kwa sasa hakufanyi watu waione Chadema ni mashujaa bali inajichimbia kaburi lake yenyewe. Watanzania si wajinga. Ni wastaarabu na hawakurupuki ktk maamuzi. Watakushangilia lkn katika nafsi zao wanajua ukweli ni upi. Mandela alifungwa alinyanyaswa si yeyetu bali wafuasi wengi wa ANC wengi waliuliwa, je Mandela aliwahi susa, alikuwa wa kwanza kutangaza msamaha na maelewano, hakulipiza kisasi. Nasema hii kwani viongozi wengi wa Chadema na mashabiki zao upenda kujilinganisha au kumtolea mfano Mandela. Migogoro ya kisiasa ipo hata Ulaya na Marekani, lkn sijawahi sikia kususa, hii tabia wakati tunakua kule kwetu kanda maalum tuliambiwa ni tabia isiyofaa. Ni tabia inayoonesha udhaifu na kutojiamini. Nirejee kwako Pascal sijafurahishwa unapotumia neno Watanzania wanauelewa mdogo. Hii tabia ya baadhi ya watu kujidharau na kujitukana inazidi mea mizizi.Tusijidharau kama Watanzania. Tusjitukane kama Watanzania. Tuwe proud! Sijawahi ona Taifa watu wanajidharau kama Watanzania. Inaniuma sana. Nilisoma chuo kimoja nchi fulani ya jirani. Mwanafunzi mmoja tukiwa darasa moja aliniuliza ati Watanzania tunaiogopa nchi yao na watanzania hatujiamini kama wao. Jibu nililompa lilimbadili kufikiria alivyo fikiri. Pia nimezunguka nchi kadhaa raia wengi wako proud na hakuna anaejidharau au kudharau watu wa Taifa lake hata kama wanamigogoro ya ndani wako so proud na utaifa wao. Hivyo Pascal nakuomba utuombe msamaha watanzania kutuita wengi tunauelewa mdogo ktk complex issues kama ulivyosema. Sielewi umetumia kigezo kipi na katika utafiti wako una base yoyote ile kufikia kutudharau watanzania katika uelewa? Huoni umedharau kuanzia wazazi wako, ndugu zako, marafiki na jamii nzima ya watanzania. Ungeweza toa mada yako bila kuonyesha dharau au majivuno yoyote. Si kila mtu akuelewe, Lakini anaweza kukuelewa taratibu atakavyo eleweshwa zaidi. Unapowasilisha mada epuka "defensive mechanism" toa mada Swala la uelewa uja baadae ushawasilisha mada. Watu wakichangia ndo utaelewa kama wamekuelewa au la na wasipokuelewa pengine unanafasi ya kuelewesha kwa lugha nyepesi. Kuelewa au kutokuelewa si tu kwa mpokeaji mada hata mtoa mada anaweza kuwa kawasilisha mada isivyo takiwa na kufanya wapokea mada wasielewe. Kutoelewa kwao kunakuwa kumesababishwa na weye mwenyewe. So hapo nani kafail wewe mwasilishaji au wapokea mada?
 
Asante Wakudada, baeleze baelewe, ukisusa, sie twala. Kina Halima ni mashujaa!.

P
 
Sikio la kufa halisikii dawa. Kosa la kwanza lilikuwa la lowassa, hawakijunza, likaja la tundulissu, sasa hawaaminiwi tena.
 

Mpaka hapa tulipo naona CDM wapo ndani ya malengo na waendelee hivyo hivyo na ikiwezekana wasitrumie njia ya kususia tu waongeze na mbinu zingine ambazo wanaona zinafaa kwani vita ni vita tu, Kuhusu huyo Pascal wala usihangaike naye kwani hana tofauti na wenzie walamba viatu wa Lumumba
 
Wewe mataga unahangaika nini na cdm ambayo baba yenu jiwe alishawaambia kuwa cdm imekufa kisa kuwanunua wabunge na madiwani wa upinzani?
 
Umetisha sana kamanda
 
Hujawahi kuishauri kitu cdm, wewe endelea kujipendekeza kwa sukuma gang wenzio waliobakia
 
Yaani kaka Paskali tokea aitwe bungeni kwenye ile kamati ya maadili anaanidka minyuzi mirefu halafu haina chochote cha maana yaani; sijui tatizo huaga ni nini kwa kweli.
 
Nimeishia hapa we jamaa huna akili.kipindi sophia simba anafukuzwa alikua haja apa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…