CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Wewe mzee umezeeka vibaya Sana na sizani hizo teuzi unazozifukuzia utazipata. Chadema imesha wafukuza uanachama hao ndugu zenu ninyi mmewang'ang'ania hao Wana wa haramu kwa mapenzi yapi? Mbona walipo fukuzwa wabunge wa CUF na Lipumba hamkusubiria Mkutano mkuu uitishwe ili hali walipinga kufukuzwa?

Hiyo huruma ya kuwa na wabunge wa Chadema mnaitoa wapi ili hali mmewatandika Risasi na kuwavunja miguu na mikono? Kazi ya kuthibitisha jinai ni ya Chadema au Serikali? Mbona ktk kesi ya urongo ya michongo ya Ugaidi hewa mmeichangamkia kufungua kesi wakati ushaidi ni wa kubumba? Mmeshindwa nini kufungua kesi dhidi ya madai ya Chadema kuwa imefanyika fojari za hao wabunge hewa?
 
Hata hueleweki, Badala ya kukihoji chama chako chenye matumizi hewa mpaka mnashindwa kufanya mkutano unataka pasco awafungulie kesi?
 
Chadema imesha wafukuza uanachama hao ndugu zenu ninyi mmewang'ang'ania hao Wana wa haramu kwa mapenzi yapi?

Mmeshindwa nini kufungua kesi dhidi ya madai ya Chadema kuwa imefanyika fojari za hao wabunge hewa?
Mkuu Lituye, kuna jinai za aina mbilil, public crimes na private crimes, public crimes ni pale jinai inapofanyika against the public, ndipo jeshi la polisi linajichukulia sheria to act lenyewe.

Lakini kwa private crimes zote, lazima mtendewa akaripoti police ndipo hatua zichukuliwe. Kwani Lissu alipoitisha press conference kutangaza kuwa anafuatiliwa na hadi kutaja number za gari, jeshi la polisi walifanya nini?. They did nothing kwasababu Lissu was supposed kuripoti polisi na sio kuitisha press conference!.

Polisi wa doria wakisikia unampiga mkeo nae analia kwa sauti kubwa, hawatabisha hodi kwako kuingilia kati unless mtu toka ndani kwako aripoti ndipo polisi waingilie.

Hata ukiingiliwa na majambazi ukavunjiwa ukaibiwa, ni jukumu lako wewe uliyeibiwa kwenda kuripoti polisi!. Hata police wakipita nje wakaona mlango wa nyumba yako umevunjwa kwa fatuma, hawaji kuuliza au kuchunguza shurti uripoti ndipo hatua zichukuliwe!.

Forgery ni public crime na private crime, ukifanya forgery ya public, police itaingilia kati na kuchunguza, lakini kwa private forgery kama hiyo forgery ya wabunge wanawake 19 wa viti maalum Chadema, ni private forgery, Chadema ilipaswa kuripoti police ndipo uchunguzi uanze!.
Chadema msilee incompetence under any excuses, ndio maana watu wenye akili zao timamu kamwe hawawezi kuwapa nchi!. Niliwahi kuuliza humu.

Ukiwa na madai ya tuhuma yoyote kama hii tuhuma ya Chadema kudai majina ya wabunge wake 19 wa viti maalum yamepelekwa kwa forgery, then kanuni ya "the one who alleges, must prove" inatumika!. Siku watu mkionyeshwa hiyo barua iliyowapeleka Bungeni imeandikwa na nani na imesainiwa na nani, watu mtabaki midomo wazi!.

Kiukweli kabisa Chadema, bado ni chama cha kiharakati, safari ya kuja kuwa chama tawala, bado sana!.
P
 
Mayala = Njaa
 

P Ni mtu wa hovyo sana
 
Spika ccm,police ccm,rais ccm,jaji ccm,wewe ccm ulitegemea nini???? Kwa nini uwape CHADEMA lawama wakati hawahusiki kwa chochote na lolote.Hiyo ni laana ndugu yangu sema ccm chini ya nduli mwendazake walishajipanga kisawasawa kwa sababu ya udhaifu wa donor countries kuwapendelea pendelea wanawake ndiyo maana walipenya kirahisi kwa sababu ya pesa.
 
Hili likifanyika ni jambo jema, hivi ndivyo nilivyoshauri hapa katika uzi huu.
P
 
kipigo kitakatitifu kipi?uchaguzi haukuwa uhuru..unakuja tu hapa na mitako yako unatingisha eti kipigo.....nenda katingishe mitako yako huko uje hoja za maana..nyau we
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kwamba tayari wanachama wake 19 waliofukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho wameshapelekewa wito wa kwenda kusikiliza matokeo ya rufaa yao waliyoikata siku ya Mei 11, 2022.
Hiki ni kikao muhimu sana, na kitakwenda kujenga heshima kubwa kwa Chadema kama chama cha siasa chenye vikao,kinachoendesha mambo yake kwa kufuata katiba yake!. Haiwezekani chama, an established party kukaa kama a kangaroo court na kufanya maamuzi ya kiajabu ajabu !.
P
 
Rufaa ni 6 tu so 13 mpaka sasa wamekubali matokeo!!! However wakija mbele ya Baraza kuu na kupiga magoti na kuomba msamaha kama Kafulila au Zitto 2011 basi watasemehewa ila ubunge watapisha tu maana hawakuingia kisheria kiufupi jinai ipo!!!

Walikubali huo mfumo wataleta precedence mbaya sana huku mbele, itafika siku watu watachukua fomu ya Urais na kuipeleka kimya kimya NEC bila hata kupigiwa kura na Kamati kuu!!! Ukiuliza utaambiwa Mbona kina Mdee walifoji fomu za ubunge mkawabariki!!

Wasamehewe ila ubunge wavuliwe.
 
Ubunge wa Spika mwisho Leo, kuanzia kesho ama wafungue kesi na kuendelea kuwa wabunge wa mahakama, ama wakubali matokeo na kuisubiria karma.
P
 
Ubunge wa Spika mwisho Leo, kuanzia kesho ama wafungue kesi na kuendelea kuwa wabunge wa mahakama, ama wakubali matokeo na kuisubiria karma.
P
Bwana P. Umezingumzia sana kuhusu Karma. Na umeonyesha wengi wa waliofukuzwa ktk Cdm kwa makosa mbalimbali walivyokumbatiwa na serkali na ccm kwa kuzawadiwa nyadhifa mbalimbali au ulaji, na umetabali na hao Covid 19 nao watazawadiwa udc,Rc na hata ubalozi na nafasi nyinginezo, KWAKO UNAONA NI KARMA INAWALIPA HUKU UKISAU KUWA ALIYEKUTUMA KUTENDA UOVU KWA MAKUBALIANO ATAKUPA VIPANDE 30 MLIVYOKUBALIANA, WEWE HUO KWAKO NI USHUJAA. Nimesikitishwa sana nawewe ulisaliti hapo uko unasubilia uteuzi, . Huo ni ubinafisi. Watazawadiwa lakini Cdm wamelinda heshima ya chama Chao. Wabinafsi kama wewe na hao COVID 19 hamfai, endeleeni kusubili VIPANDE 30
 
  1. Sakata la wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema ni Chadema wenyewe ndio walilianzisha kwa kugomea nafasi 18 za viti maalum walizopewa na NEC.
  2. Kwa msaada wa kiongozi mmoja mkubwa wa Chadema, Halima Mdee akiwa na Esta Bulaya, wakam convince umuhimu wa nafasi hizo kwa Chadema, akawakubalia kwa shurti wasimtaje.
  3. Halima akawaorganize Wanawake wa Chadema kwa kuanzia na waliokuwa wabunge, wengine wakikubali, wengine walikataa, kwa waliokubali wakaunda a coalition of the willing
  4. Barua bonafide genuine ikaandikwa, mnene akawasainia in return na yeye kuchomekea hapo kakidumu chake, yakaenda NEC, watu wa fursa wakaichangamkia fursa.
  5. Hivyo ni Chadema wenyewe ndio walilianzisha na hizi kati ni Chadema wenyewe wamelimaliza Kwa kikao cha Baraza Kuu kuyabariki maamuzi batili ya CC ya Chadema iliyo wafukuza.
  6. Walipopewa fursa ya kujitetea kwenye kikao cha Baraza Kuu, Halima Mdee akafanya kitendo kingine cha kishujaa kweli kweli kwa kutounguza picha ya Kilichopelekea kwa natumaini mnene yule angewaombea msamaha angalau wabaki wanachama wa kawaida!. Hili halikufanyika hivyo kilichofanywa na Baraza Kuu kuyabariki maamuzi batili ya CC ni uhuni.
  7. Sasa baada ya kuwatimua, ushauri wa bandiko hili bado uko valid, Chadema lazima sasa wautambue uchaguzi, wakubali matokeo, wafanye uteuzi wa wabunge wapya wakaapishwe maisha yaendelee.
  8. Kikwazo ni kimoja, utimuaji uliofanywa na CC ya Chadema ni batili, na baada ya kuonja fursa, jee watakubali matokeo, jee wataukubali ubatili huu au watakwenda mahakamani kutafuta haki yao?.
Jibu litapatikana on Monday.

This is my own recollection.
P.
 
Labda kiongozi huyo ni wewe
 
Magufuli alitueleza maana ya Mayalla ni njaa, ingawa Magufuli alikuwa ni baba wa uongo ila kwa hili la Mayalla alitueleza kweli tupu.
kabisa aiseee wanamjua vizuri sana jamaa nasikia anagongea hadi beer siku hizi siku hiyo kalewa kaanguka na pikipiki hadi leo mkono mmoja mbovu
 
Yani wajumbe wa baraza kuu la Chadema zaidi ya 400 hawana akili ila wewe mjanjamjanja mmoja magumashi misheni town ndio una akili kuwazidi waliojitengezea wenyewe katiba yao.

Nakushauri si kila jambo ni la kudandia mengine jaribu kukaa kimya halafu soma mabandiko ya manguli waliotetea PhD zao darasani kama Askofu Dr Bagoza ndio utajifunza matumizi mazuri ya akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…