Wanabodi,
Hivyo huu ni ushauri wangu kwa Chadema, Its do or die! Chadema is left with only two options, kuchagua kufa, au kuchagua kuendelea kuishi. The choice is theirs.
Mbele ya macho ya jamii, hao ambao kwao ni wasaliti, kwa wengine hao ni makamanda mashujaa wapambanaji ambao ni wa kiwango cha makomandoo, ambao wameipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, na licha ya kufutwa uanachama wa CHADEMA, wataendelea kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ubunge wao sasa utakuwa ni ubunge wa Spika, Ubunge wa Taifa.
Nini Kifanyike, A Way Forward Kitaifa
[*]Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya na nchi nyingine zenye kuheshimu demokrasia ya kweli na sio hii demokrasia fake ya vyama!.
[*]Tubadili Katiba yetu na sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na wagombea binafsi.
[*]Tuibadili Tume yetu ya Uchaguzi iwe Tume huru zaidi na shirikishi, tujenge uwanja sawa wa ushindani wa haki kwa vyama vyote, uchaguzi uendeshwe kwa transparency ya hali ya juu kwa kuruhusu mawakala hadi kwenye tallying, na vyama au taasisi zozote ziwe free kuwa na tallying centers zake, kitu ambacho hakitaruhusiwa na talling centers hizo ni kutangaza matokeo, kama matokeo yote ya uchaguzi hadi wa rais yanahesabiwa kituoni na kubandikwa ukutani, kama hakuna jambo lolote la kificho, yaani nothing to hide, kwanini uzuie independent tallying?!. Uchaguzi wa 2025, kila mwenye uwezo wa kufanya tallying aruhusiwe afanye ila zisitangaze matokeo, hii itazuia bao la mkono!
[/LIST]
Hitimisho
Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kufanya siasa za ukweli,
Paskali