CHADEMA kuchangisha Milioni 350 ni maigizo na fedheha

Jera ni nini?
 
Kwa hiyo mkimtaja itakuaje? Mimi najiuliza kwa nini mhangaike Wakati nyie ndio mmewafunga????? Haaaaaaa mlishindwa kutumia akiri kila mbinu yenu mnayotumia mnajikuta mnakuwa Kama mmepiga chura teke, msitumie polisi na Mahakama mtakwama siasa ni sayansi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, hata tajiri mkubwa mtaani kwako akipata msiba nyumbani kwake, nenda tu na sh. elfu moja yako ukatoe rambirambi; si kwa sababu hana uwezo wa kuendesha msiba bila kuchangisha watu wakiwamo maskini, ila tu ni kwa kuonyesha kwamba mko pamoja katika kuomboleza janga hilo. Vivyo hivyo, watu wameamua kuchanga sh. mia mbili mia mbili ili kuwatia moyo kwamba wanatambua kuna janga kubwa la ubakaji demokrasia ikiwamo na muhimili mmoja kutoa maelekezo kwa mwingine kwa lengo la kukusanya fedha za ndani. Sasa kama ulikuwa hujui tunatekeleza miradi kwa fedha za ndani, basi hizi hapa zinazoelekezwa zitozwe kama adhabu ndio fedha za ndani zenyewe!
 
Nchi imerudi Nyuma zaid ya kipindi cha wakoloni, pesa nyiiingi zinatumika kunyamazisha watu pesa nyingi imewekezwa kufunga watu midomo, kufunga vyombo vya habari midomo, pesa nyingi inatumika kufanya biashara ya binadamu, na cheo ili upate unatakiwa utumie nguvu ya kusifia au kutukana upande wa pili kiukweli tumeingiliwa na Kwa kuwa wametambua kuwa hawakubaliki wanatumia garama ili kwenye Uchaguzi watu wasiende kupiga kura huku wanahamasishana wao kwa wao kwa kipita nyumba kwa nyumba Na kuandikisha watu haadi namba Ya Kadi Ya kupigia kura na Simu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Huyo mshahara si ndio wanautumia kuishi.
Je, sio kwamba labda akaunti zao zimechunguliwa na kukuta hawana hizo balances za kutosha kwa sasa na ndipo kupewa kiwango cha juu?
 
Sure wanaumiza masikini tu mtu kauza kamchicha kake afu anaenda kuchangia matajiri sio poa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna aliekulazimisha kuchanga, na watu wanaochanga ni wananchi hata hao viongozi wahajuani acha watu Wa change wewe ni Ccm ndio mmeyafanya hayo mmeishatimiza malengo yenu kwa nini mnalalamika tena? Tulia Dawa iwaingie, mbona mmekuwa Kama nyie ndio mmefungwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa wewe mwenye akili ndogo umafikiria kwamba Mbowe na hao wabunge hawana uwezo wa kulipa hiyo pesa. Sisi tunapendezwa kuchanga tunasukumu ujumbe kwa ubeberu unaoendelea
 
CCM mpo madarakani tangu 1961, lakini mpaka leo, tunapewa msaada wa vyandarua, ARV, fedha za REA, tunajengewa mpaka vyoo, bajeti yetu bila fungu la wafadhiri, hatutoboi!,
Idara ya magereza ina miriki ardhi kubwa, lakini chakula cha wafungwa mpaka msaada kutoka hazina,

Sasa anayetakiwa kuwa na fedheha nani hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole ndg,kwanza elewa kuchangiwa haimaanishi anayechangiwa hana kitu bali anaongezewa,lakini pia watu wanaonesha upendo na kukuamini.na wakati mwingine inakuwa kumpa somo aliyetengeza kesi.
 
We unaumia roho?hata kama wa gekuwa matajiri,wananchi tunataka tuwaonyeshe nyie jinsi tulivyo na MAHABA na wana demokrasia.

HAKI HUONDOA DHULMA NA KULETA AMANI NA FURAHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Luqman mohamedy, Hakuna sehemu viongozi wa Chadema waliomba kuchangiwa hiyo pesa ,kilichotokea ni wananchi na wapenda demokrasia ndio walioamua kuchangia na Chadema kama chama wakatoa namba za akaunt na simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…