Chadema kuhamasisha watu kwenda mahakamani ni kutumia watu kama ngao, wataumizwa.

Nimewasikia viongozi wa cdm wakihamasisha wafuasi nchi nzima waende kwa wingi Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu, lengo hasa ni nini kuita watu wengi wakusanyike kwenye eneo dogo sana la mahakama ambalo liko kwenye maeneo yenye pilikapilika nyingi za watu? Tunafahamu kuwa chadema ina wafuasi wengi nchi nzima, vipi kama wote wataitikia wito wenu wa kwenda kusikiliza kesi Kisutu? Je, Kisutu ina eneo kubwa kiasi gani kutosha wafuasi wote wa chadema kukusanyika?

Ni serikali gani duniani itaruhusu jambo kama hilo litokee? Bila shaka mnajua kuwa watu wengi wataumizwa mbele ya camera za vyombo vya habari vya ndani na nje, je, lengo ni hilo? Hamuoni kama watu wakifa na kuuawa kwenye msongamano huo mtakuwa mmehusika moja kwa moja na kadhia hiyo?

Binafsi nimeamini ule msemo wa Rais Ali Hassani Mwinyi (RIP) kuwa "kunguru hana kibyongo, ukiona kibyongo kainama anaokota kitu, muwahi mapema kunguru kabla hajaruka nacho". Ukichelewachelewa huenda akaruka na kifaranga, kijiko na hata nguo yako ya ndani.

Lengo kuu nadhani ni kuichafua nchi mbele ya camera za wafadhili, maana walijua polisi itawatawanya kwa nguvu. Tusipoziba ufa tutapata M23 Tanzania..
Nimesoma bandiko lote ili nione umeweka kifungu cha sheria kinachikazuia raia wasiende sikiliza kesi sijaona, hebu tuwekee kifungu cha katiba hapa..
 
Kaka unahatarisha maisha ya watoto wa wanaume wenzako bure. Afrika yote inafahamika kuwa hata yaliyoko kwenye Katiba na sheria hayafuatwi. Nyie mlizuiwa kufanya siasa kwa takribani miaka 6 mfululizo ingawa kufanya siasa na maandamano vimo kwenye Katiba yetu. Viongozi wa chadema wana hatia kusababisha wafuasi wao kuumizwa, kwakuwa wana uzoevu wa matukio mengi ya aina hiyo. Kifupi akina Lissu, Lema na Heche walikuwa na uhakika wa 100% kuwa kuna watu watapigwa na kuumizwa na vyombo vya dola kama wataenda Kisutu kwa maelfu. Viongozi hawa wanawatumia watu hawa kufanikisha agenda zao, wanawatumia watu hawa wanaoumizwa kwaajili ya kupata uhalali wa watoto wao kuendelea kuwa wakimbizi Ulaya na Marekani. Wanatumia maandamano na watu kuumizwa na kuuawa kwaajili ya kujustify matuzi ya fedha za wafadhili wanazopewa na wanazotaka kuomba wapewe.

Hii ni mbaya sana alooooo!!
 
siku moja wekeni polisi pembeni,tume pembeni.
alafu wekeni uchaguzi mjipime ubavu.mtategemea wizi wa kura hadi lini?
 
Nimewasikia viongozi wa cdm wakihamasisha wafuasi nchi nzima waende kwa wingi Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu, lengo hasa ni nini kuita watu wengi wakusanyike kwenye eneo dogo sana la mahakama ambalo liko kwenye maeneo yenye pilikapilika nyingi za watu? Tunafahamu kuwa chadema ina wafuasi wengi nchi nzima, vipi kama wote wataitikia wito wenu wa kwenda kusikiliza kesi Kisutu? Je, Kisutu ina eneo kubwa kiasi gani kutosha wafuasi wote wa chadema kukusanyika?

Ni serikali gani duniani itaruhusu jambo kama hilo litokee? Bila shaka mnajua kuwa watu wengi wataumizwa mbele ya camera za vyombo vya habari vya ndani na nje, je, lengo ni hilo? Hamuoni kama watu wakifa na kuuawa kwenye msongamano huo mtakuwa mmehusika moja kwa moja na kadhia hiyo?

Binafsi nimeamini ule msemo wa Rais Ali Hassani Mwinyi (RIP) kuwa "kunguru hana kibyongo, ukiona kibyongo kainama anaokota kitu, muwahi mapema kunguru kabla hajaruka nacho". Ukichelewachelewa huenda akaruka na kifaranga, kijiko na hata nguo yako ya ndani.

Lengo kuu nadhani ni kuichafua nchi mbele ya camera za wafadhili, maana walijua polisi itawatawanya kwa nguvu. Tusipoziba ufa tutapata M23 Tanzania..

Sheria zikoje watu wanaruhusiwa au hawaruhusiwi kwenda mahakamani
 
Huwezi kusema kwamba viongozi wa chadema hawakujua kama watapigwa na polisi kwenye sakata la jana. Hawa viongozi lazima wahojiwe kuhusu dhamira yao ya kuwaita watu kuivamia mahakama ya kisutu.

View: https://www.youtube.com/watch?v=nqE4QoiAn3A

wapigwe kwasababu ya kwenda kusikiliza kesi. Hivi mnatetea nini hasa? Mlitaka viongozi wa Chadema wasiende kusikiliza kesi ya uhaini ya mwenyekiti wao! tuwe tunafikiria vizuri na sio kuweka uchama na ushabiki. Wasingeenda wanachama ambao wamewachagua wange waonaje?
 
Nimewasikia viongozi wa cdm wakihamasisha wafuasi nchi nzima waende kwa wingi Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu, lengo hasa ni nini kuita watu wengi wakusanyike kwenye eneo dogo sana la mahakama ambalo liko kwenye maeneo yenye pilikapilika nyingi za watu? Tunafahamu kuwa chadema ina wafuasi wengi nchi nzima, vipi kama wote wataitikia wito wenu wa kwenda kusikiliza kesi Kisutu? Je, Kisutu ina eneo kubwa kiasi gani kutosha wafuasi wote wa chadema kukusanyika?

Ni serikali gani duniani itaruhusu jambo kama hilo litokee? Bila shaka mnajua kuwa watu wengi wataumizwa mbele ya camera za vyombo vya habari vya ndani na nje, je, lengo ni hilo? Hamuoni kama watu wakifa na kuuawa kwenye msongamano huo mtakuwa mmehusika moja kwa moja na kadhia hiyo?

Binafsi nimeamini ule msemo wa Rais Ali Hassani Mwinyi (RIP) kuwa "kunguru hana kibyongo, ukiona
Nimewasikia viongozi wa cdm wakihamasisha wafuasi nchi nzima waende kwa wingi Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu, lengo hasa ni nini kuita watu wengi wakusanyike kwenye eneo dogo sana la mahakama ambalo liko kwenye maeneo yenye pilikapilika nyingi za watu? Tunafahamu kuwa chadema ina wafuasi wengi nchi nzima, vipi kama wote wataitikia wito wenu wa kwenda kusikiliza kesi Kisutu? Je, Kisutu ina eneo kubwa kiasi gani kutosha wafuasi wote wa chadema kukusanyika?

Ni serikali gani duniani itaruhusu jambo kama hilo litokee? Bila shaka mnajua kuwa watu wengi wataumizwa mbele ya camera za vyombo vya habari vya ndani na nje, je, lengo ni hilo? Hamuoni kama watu wakifa na kuuawa kwenye msongamano huo mtakuwa mmehusika moja kwa moja na kadhia hiyo?

Binafsi nimeamini ule msemo wa Rais Ali Hassani Mwinyi (RIP) kuwa "kunguru hana kibyongo, ukiona kibyongo kainama anaokota kitu, muwahi mapema kunguru kabla hajaruka nacho". Ukichelewachelewa huenda akaruka na kifaranga, kijiko na hata nguo yako ya ndani.

Lengo kuu nadhani ni kuichafua nchi mbele ya camera za wafadhili, maana walijua polisi itawatawanya kwa nguvu. Tusipoziba ufa tutapata M23 Tanzania..

kibyongo kainama anaokota kitu, muwahi mapema kunguru kabla hajaruka nacho". Ukichelewachelewa huenda akaruka na kifaranga, kijiko na hata nguo yako ya ndani.

Lengo kuu nadhani ni kuichafua nchi mbele ya camera za wafadhili, maana walijua polisi itawatawanya kwa nguvu. Tusipoziba ufa tutapata M23 Tanzania..
Nikisema huna akili pengine nitakuwa nimekosea sana, inawezekana wewe kachawa katoto, mwaka 1982/1983 kulikuwa na kesi ya uhaini iliyohusisha wanajeshi wengi wakiwa makomdoo(JWTZ). Ni kesi iliyovuta hisia za wengi maana mpaka baadhi ya majenerali walitajwa kuhusika na hayo mapinduzi.
Kwa taarifa yako nyakati hizo maisha yalikuwa magumu sana,haswa ukizingatia nchi ilikuwa imetoka vitani kupambana na nduli Idd Amin aliyekuwa Rais wa kiimla Uganda,Na hii ni baada ya Idd Amin mwaka 1978 kuivamia Tanzania na kuteka eneo la kuanzia mto Kagera mpaka kwenye mpaka wa Uganda na Tanzania.
Sasa baada ya vita hivyo vilivyomalizika 11/04/1979 ulipotekwa mji wa Kampala na Idd Amin kuikimbia nchi yake,tulitangaziwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Hayati Mwalimu Nyerere,kuwa Tujipange kwa miezi 18,ya kujifunga mikanda maana uchumi ulikuwa umeporomoka sana. Wananchi wengi kutokana na ugumu wa maisha waliichukia sana serikali.
Hivyo basi hata hao wanajeshi na wananchi wa kawaida waliojaribu kuipindua serikali wapo waliowaunga mkono kwani pamoja na kashindwa kwenye jaribio lao, hata sababu walizozitoa kama motive ya kuipindua nchi kwa sehemu kubwa ilikuwa ni ugumu wa maisha kitu ambacho ilikuwa ni kweli.
Pamoja na yote hayo,ile kesi iliendeshwa kwa uwazi na kutangazwa na vyombo vya habari vya serikali na taasisi zingine kama chama cha wafanyakazi nao walikuwa na gazeti lao nyakati hizo.
Ilikuwa siyo rahisi ukakosa kununua gazeti siku ya kesi na baada yake.
Kwa teknolojia duni ya wakati ule kwa polisi wetu enzi hizo najiuliza iliwezekanaje kesi kuendeshwa Kwa amani pasipo na woga!!!.
Watu walihudhuria mahakamani kwa wingi na kukaa nje kando ya barabara. Huyo Rpc wa Dar es Salaam alisomea wapi,sijui. Hakuna aliyepigwa au kusukumwa na polisi. Labda itoshe kusema, pamoja na mapungufu yote ya Mwalimu Nyerere alichukia sana kusikia kuuawa kwa mtanzania,labda niseme alithamini sana uhai wa mtu.
Nimalizie kwa kusema,ukweli unabakia awamu ya tano na hii inayojiita ya sita hawakuwa walijiandaa kukamata dola,japo angalau yule Hayati alikiri wazi kuwa ni kweli hakujipanga,ilitokea tu alipojaribu akawa yeye. Na huyu sote tunajua ilitokeaje amekuwa japo aliapishwa baada ya kupita masaa 60. toka mtangulizi wake afariki,heko kwa Gen. Mabeyo aliyeikumbuka katiba ya nchi inasemaje, kwa nini hao waliohusika na hizo itifaki walisita kumuapisha mapema hatujui. Naweza kufikiri halikuwa kosa lao kwani nafasi ya makamu ilichukuliwa kama haina madhara huko nyuma, kwani mwaka 2010 hata Mzee Kikwete aliitumia nafasi hiyo kuzima mgogoro wakati wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar alipomteua Dr. Ghalib Bilali kuwa makamu sijui atakuwa aliwaza nini ingekuwa kwa nchi hii,kama ilivyotokea mwaka 2021 march,ingetokea kwake.
Mahakamani ni mahali ambapo uwe na kesi au usiwe nayo unaruhusiwa kwenda.
Tundu Lisu anapaishwa na watawala waliokosa maarifa.
 
siku moja wekeni polisi pembeni,tume pembeni.
alafu wekeni uchaguzi mjipime ubavu.mtategemea wizi wa kura hadi lini?
Hiyo ni ile demokrasia ya kama mtoto hapendi kumeza dawa mwacheni, ni haki yake kukataa dawa. Mwacheni kama anataka kujinyonga.
 
Nimewasikia viongozi wa cdm wakihamasisha wafuasi nchi nzima waende kwa wingi Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu, lengo hasa ni nini kuita watu wengi wakusanyike kwenye eneo dogo sana la mahakama ambalo liko kwenye maeneo yenye pilikapilika nyingi za watu? Tunafahamu kuwa chadema ina wafuasi wengi nchi nzima, vipi kama wote wataitikia wito wenu wa kwenda kusikiliza kesi Kisutu? Je, Kisutu ina eneo kubwa kiasi gani kutosha wafuasi wote wa chadema kukusanyika?

Ni serikali gani duniani itaruhusu jambo kama hilo litokee? Bila shaka mnajua kuwa watu wengi wataumizwa mbele ya camera za vyombo vya habari vya ndani na nje, je, lengo ni hilo? Hamuoni kama watu wakifa na kuuawa kwenye msongamano huo mtakuwa mmehusika moja kwa moja na kadhia hiyo?

Binafsi nimeamini ule msemo wa Rais Ali Hassani Mwinyi (RIP) kuwa "kunguru hana kibyongo, ukiona kibyongo kainama anaokota kitu, muwahi mapema kunguru kabla hajaruka nacho". Ukichelewachelewa huenda akaruka na kifaranga, kijiko na hata nguo yako ya ndani.

Lengo kuu nadhani ni kuichafua nchi mbele ya camera za wafadhili, maana walijua polisi itawatawanya kwa nguvu. Tusipoziba ufa tutapata M23 Tanzania..
Kavulata ni investors gani hao? Waarabu na Wachina wanaoiba mali zetu?

Muwekezaji wa kweli anakuja kama nchi ina amani na haina corruption.

Polisi kazi Yao ni kulinda watu au ukiwashika washitaki huna mamlaka ya kuwapiga na kuua na kutupa polini.

You are another fucking asshole
 
Nimewasikia viongozi wa cdm wakihamasisha wafuasi nchi nzima waende kwa wingi Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu, lengo hasa ni nini kuita watu wengi wakusanyike kwenye eneo dogo sana la mahakama ambalo liko kwenye maeneo yenye pilikapilika nyingi za watu? Tunafahamu kuwa chadema ina wafuasi wengi nchi nzima, vipi kama wote wataitikia wito wenu wa kwenda kusikiliza kesi Kisutu? Je, Kisutu ina eneo kubwa kiasi gani kutosha wafuasi wote wa chadema kukusanyika?

Ni serikali gani duniani itaruhusu jambo kama hilo litokee? Bila shaka mnajua kuwa watu wengi wataumizwa mbele ya camera za vyombo vya habari vya ndani na nje, je, lengo ni hilo? Hamuoni kama watu wakifa na kuuawa kwenye msongamano huo mtakuwa mmehusika moja kwa moja na kadhia hiyo?

Binafsi nimeamini ule msemo wa Rais Ali Hassani Mwinyi (RIP) kuwa "kunguru hana kibyongo, ukiona kibyongo kainama anaokota kitu, muwahi mapema kunguru kabla hajaruka nacho". Ukichelewachelewa huenda akaruka na kifaranga, kijiko na hata nguo yako ya ndani.

Lengo kuu nadhani ni kuichafua nchi mbele ya camera za wafadhili, maana walijua polisi itawatawanya kwa nguvu. Tusipoziba ufa tutapata M23 Tanzania..
Watakao enda wahakikishe wanalipwa na chadema kama wakina Lisu,pambalu,mnyika nk unaweza vipi kwenda kumsaidia mtu KAZI yake anayolipwa moja Kwa moja ?
 
wapigwe kwasababu ya kwenda kusikiliza kesi. Hivi mnatetea nini hasa? Mlitaka viongozi wa Chadema wasiende kusikiliza kesi ya uhaini ya mwenyekiti wao! tuwe tunafikiria vizuri na sio kuweka uchama na ushabiki. Wasingeenda wanachama ambao wamewachagua wange waonaje?
Viongozi na wafuasi wa chadema wote walikuwa wanajua kuwa kiongozi wao Lissu amekamatwa na nani kwa kosa gani na kesi imekwenda mahakamani na itasikilizwa lini kwenye mahakama ipi. Je.. Heche.. Mnyika na Lema walihitaji kufanya mikutano ya hadhara ya kuhamasisha watu waende Kisutu kusikiliza kesi.. uliona wapi watu wanahutubiwa kwenda kusikilizakesi kwa wingi mahakamani? Je. Idadi kubwa ya watu mahakamani wanaosiliza kesi inasaidia nini kisheria kushinda kesi?

Je. Kwa uzoefu wa akina Heche.. Mnyika.. Lema.. Lissu.. Mbowe kwenye siasa hawakujuwa kuwa kuita watu wengi kwenda mahakamani kingesababisha watu kupigwa na kuumizwa? Kama walijua hivyo kwanini waliwaita waende Kisutu?

Kwani Wana agenda gani?
 
Nikisema huna akili pengine nitakuwa nimekosea sana, inawezekana wewe kachawa katoto, mwaka 1982/1983 kulikuwa na kesi ya uhaini iliyohusisha wanajeshi wengi wakiwa makomdoo(JWTZ). Ni kesi iliyovuta hisia za wengi maana mpaka baadhi ya majenerali walitajwa kuhusika na hayo mapinduzi.
Kwa taarifa yako nyakati hizo maisha yalikuwa magumu sana,haswa ukizingatia nchi ilikuwa imetoka vitani kupambana na nduli Idd Amin aliyekuwa Rais wa kiimla Uganda,Na hii ni baada ya Idd Amin mwaka 1978 kuivamia Tanzania na kuteka eneo la kuanzia mto Kagera mpaka kwenye mpaka wa Uganda na Tanzania.
Sasa baada ya vita hivyo vilivyomalizika 11/04/1979 ulipotekwa mji wa Kampala na Idd Amin kuikimbia nchi yake,tulitangaziwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Hayati Mwalimu Nyerere,kuwa Tujipange kwa miezi 18,ya kujifunga mikanda maana uchumi ulikuwa umeporomoka sana. Wananchi wengi kutokana na ugumu wa maisha waliichukia sana serikali.
Hivyo basi hata hao wanajeshi na wananchi wa kawaida waliojaribu kuipindua serikali wapo waliowaunga mkono kwani pamoja na kashindwa kwenye jaribio lao, hata sababu walizozitoa kama motive ya kuipindua nchi kwa sehemu kubwa ilikuwa ni ugumu wa maisha kitu ambacho ilikuwa ni kweli.
Pamoja na yote hayo,ile kesi iliendeshwa kwa uwazi na kutangazwa na vyombo vya habari vya serikali na taasisi zingine kama chama cha wafanyakazi nao walikuwa na gazeti lao nyakati hizo.
Ilikuwa siyo rahisi ukakosa kununua gazeti siku ya kesi na baada yake.
Kwa teknolojia duni ya wakati ule kwa polisi wetu enzi hizo najiuliza iliwezekanaje kesi kuendeshwa Kwa amani pasipo na woga!!!.
Watu walihudhuria mahakamani kwa wingi na kukaa nje kando ya barabara. Huyo Rpc wa Dar es Salaam alisomea wapi,sijui. Hakuna aliyepigwa au kusukumwa na polisi. Labda itoshe kusema, pamoja na mapungufu yote ya Mwalimu Nyerere alichukia sana kusikia kuuawa kwa mtanzania,labda niseme alithamini sana uhai wa mtu.
Nimalizie kwa kusema,ukweli unabakia awamu ya tano na hii inayojiita ya sita hawakuwa walijiandaa kukamata dola,japo angalau yule Hayati alikiri wazi kuwa ni kweli hakujipanga,ilitokea tu alipojaribu akawa yeye. Na huyu sote tunajua ilitokeaje amekuwa japo aliapishwa baada ya kupita masaa 60. toka mtangulizi wake afariki,heko kwa Gen. Mabeyo aliyeikumbuka katiba ya nchi inasemaje, kwa nini hao waliohusika na hizo itifaki walisita kumuapisha mapema hatujui. Naweza kufikiri halikuwa kosa lao kwani nafasi ya makamu ilichukuliwa kama haina madhara huko nyuma, kwani mwaka 2010 hata Mzee Kikwete aliitumia nafasi hiyo kuzima mgogoro wakati wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar alipomteua Dr. Ghalib Bilali kuwa makamu sijui atakuwa aliwaza nini ingekuwa kwa nchi hii,kama ilivyotokea mwaka 2021 march,ingetokea kwake.
Mahakamani ni mahali ambapo uwe na kesi au usiwe nayo unaruhusiwa kwenda.
Tundu Lisu anapaishwa na watawala waliokosa maarifa.
Twende mahakmni wenyewe bila kuhasishwa na upande wenye maslahi na mkusanyiko huo. Leo hii technology ya habari imeendelea sana. Hivi Iko sababu Gani watu watoke mwanza, Musoma, sumbawanga, Tanga, singida, songea kuja kisutu kusikiliza kesi. Inasaidia nini hiyo?

Hata kwenye hizo kesi za wanajeshi hakukua na watu waliokuwa wanaitisha mikutano ya hadhara kuambia watu waende kwa wingi mahakamani kusikiliza kesi ya makomandoo wahaini, kesi ilikuwa ikichapishwa kwenye magazeti na sisi tulinunua magazeti hayo . Leo hii technology Iko juu lakini lissu hataki itumike kbisaa. Ni rahisi kudhani Kuna jambo kweye jambo
 
Watakao enda wahakikishe wanalipwa na chadema kama wakina Lisu,pambalu,mnyika nk unaweza vipi kwenda kumsaidia mtu KAZI yake anayolipwa moja Kwa moja ?
Faida yao pekee ni kupata nafasi y kugombea ubunge. Hii no reforms no election inawachanganya wengi, Lissu na Lema ndio peke yao wanaofaidika na NO election.
 
Nimewasikia viongozi wa cdm wakihamasisha wafuasi nchi nzima waende kwa wingi Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu, lengo hasa ni nini kuita watu wengi wakusanyike kwenye eneo dogo sana la mahakama ambalo liko kwenye maeneo yenye pilikapilika nyingi za watu? Tunafahamu kuwa chadema ina wafuasi wengi nchi nzima, vipi kama wote wataitikia wito wenu wa kwenda kusikiliza kesi Kisutu? Je, Kisutu ina eneo kubwa kiasi gani kutosha wafuasi wote wa chadema kukusanyika?

Ni serikali gani duniani itaruhusu jambo kama hilo litokee? Bila shaka mnajua kuwa watu wengi wataumizwa mbele ya camera za vyombo vya habari vya ndani na nje, je, lengo ni hilo? Hamuoni kama watu wakifa na kuuawa kwenye msongamano huo mtakuwa mmehusika moja kwa moja na kadhia hiyo?

Binafsi nimeamini ule msemo wa Rais Ali Hassani Mwinyi (RIP) kuwa "kunguru hana kibyongo, ukiona kibyongo kainama anaokota kitu, muwahi mapema kunguru kabla hajaruka nacho". Ukichelewachelewa huenda akaruka na kifaranga, kijiko na hata nguo yako ya ndani.

Lengo kuu nadhani ni kuichafua nchi mbele ya camera za wafadhili, maana walijua polisi itawatawanya kwa nguvu. Tusipoziba ufa tutapata M23 Tanzania..

Inabidi waende wengi ikiwezekana nchi nzima kwa sababu wale wachache waliokwenda ambao ni viongozi wao tu wa Kanda na makao makuu .Walipoenda wao peke yao mkawapiga na wengine kuwaua na wengine mpaka sasa hawaonekani walipo.
Sasa mnataka nini kama sio kuua wengi na kuumiza wengi na kukamata wengi . Huenda umaarufu wa Polisi ili apate uteuzi ni kukamata Chandema wengi ,kuua Chandema wengi na kutesa na kujeruhi Chasema wengi na kuisababishia hasara serikali na jamii kwa kupoteza mabomu na risasi nyingi kwa manufaa ya yule MwanaCCM mmoja na familia yake kwa sababu tu katiba imempa Mamlaka ya kuua na kufanya anachotaka . Mamlaka aliyonayo anayatumia kuangamiza upinzani na wapinzani .

Sasa ili wamkamate na kuua wengi basi watakwenda wengi ili ama washinde au washindwe uhuru upatikane . Hakuna namna .
Huwezi kuwazuia viongozi wa Chadema kwenda kusikiliza Kesi ya mwenyekiti wao . Haijawahi kutokea Kokote hata kwa watu wabaya kama wakoloni labda wakoloni waarabu maana wao ndio hawana kumbukumbu popote ya waliyoyafanya mpaka wakafanikiwa kushika soko la kununua na kuuza binadamu . Yaani hatujui kabisa ilikuwaje mpaka Waafrika wakakubali kuwafanya ndugu zao kuwa bidhaa,Huku pembe za ndovu ,Madini vikibebwa na waarabu . Bila shaka walitumia rushwa kama CCM inavyofanya leo . Ardhi inauzwa ,Madini yanauzwa mpaka katikati ya hifadhi za wanyama ,umeme inanunuliwa kutoka nje wakati ndani upo , na utakosa wateja ,Bandari inauzwa na sasa Wataganyika wanauawa na kutishwa ili waifurukute huku rushwa ikitembiea kwa wataganyika ili waue na kufunga ndugu zao kama babu zao walivyofanywa na hao hao waarabu na sasa ni mjukuu wao anafanya haya ndani ya ardhi ya Tanganyika kwa Mamlaka aliyopewa na anayempinga anakula jambia la shingo .

Waafrika kama maana ya hizi dini na itikadi za kigeni ndio hizo za kuuana kwa sababu ya familia ya mtu mmoja hata kama anavuruga maendleo na ustaarabu wa taifa basi hizo dini ni ushetani mtupu na uovu usio faa popote mbingun na duniani.

Huwezi ukauwa watu wasio na hatia .
Kumwaga damu isiyo na hatia ni dhambi kubwa sana tangu mababu zetu mpaka Ukrsto japo usilam sijui kama kuua mtu asiye na hatia ni sawa au ni thawabu.

Watu hawarusha hata jiwe kwa polisi unawavunjaje miguu mpaka unaua ?
Hivi CCM imekua na watu au majini na mashetani wasioona hayo ?

Yaani kwa akili ya kawaida yule Mama polisi angepigwa jiwe na wananchi wale si angepiga bomu la nyuklia nakuua halaiki nzima kama anaua watu wasio rusha hata ngumi ?

Wakati CUF iliyokua inasadikiwa kuwa ni chama cha kiislam inapinga dhulma ni wazi kuwa Ilikua ni jino kwa jino na mapanga Shaa . Polisi kule Zanzibar walikua wanakatwa vichwa kama kuku . Wakahamia Mkuranga kwa mchengerwa wakati huo naye ni mkereketwa wa mapanga Shaa kabla ya kujitokeza kama CCM ,kule napo waliua polisi sana na wananchi wengi wa CCM na viongozi wao .

Leo Chadema inasubiri Haki na kuondoa sheria zenye kupendelea upande mmoja bila kutumia hata nyembe ,tena ,miongoni mwao kuna mpaka askofu Mwamakula bila kudhuru mmtu kwa amani kabisa kama Kristo alivyoagiza cha ajabu polisi na watawala wanaagiza wauawe tena . SASA CCM na Samia wanataka upinzani wa namna gani ? Wanataka siku CCM ikiondoka madarakani magereza yote yageuke kuwa nyumba za Makada wa CCM na wale waliosimamia ukatili wao ?

Ni wazi CCM haikubaliki kama Mwanzo . Samia hana mvuto wowote wa kisiasa hata kijamii .
Rais anafika mahali watu wanakwenda kwenye mkutano wake wa hadhara kwa rushwa !! Halafu Intelijensia yake haimwambii ukweli wala kuwaambia watu wake kuwa chama kitakufa na kuondoka na utawala wa Samia .

Chadema waende ikiwezekana wafikie hata milioni tano wajaze jiji la Dar es salaam wazunguke kila pahali sio barabara moja bali watawanyike barabara zote polisi wajikute wapo katikati mabomu wajirushie wenyewe.

Mikakati ya Chandema ndiyo ya kizembe ndio maana wanalia lia ,yaani wanawalilia wauaji . Yaani unamlilia na kudeka kwa mama wa kambo .
 
Ni HAKI yetu kwenda kusikiliza kesi 28-04-2025.
 
Faida yao pekee ni kupata nafasi y kugombea ubunge. Hii no reforms no election inawachanganya wengi, Lissu na Lema ndio peke yao wanaofaidika na NO election.

Ananufaika vipi gerezani na risasi mwilini na ulemavu wake ,

Kwa nini usiweme kuwa polisi anayemufaika na kuua watu ni Mulilo na Wambura? Hao wengine watakuja kupata hasara kubwa sana maana wanawaumiza vijana wadogo ambao watakutana nao huko mbeleni .
Hakuna namna ya kuwanyamazisha watu kwenye nchi yao tena watu wasio na ajira . Leo kuna wale polisi wema wanaotoa elimu juu ya haki na kushirikiana na polisi kudhibiti uhalifu ambayo ni sera ya Chama cha mapinduzi inayojulikana kama polisi kwenye jamii . Sasa je,watatoa Elimu gani kwa jamii inayoona wazi kuwa polisi ndio wanaosaidia watawala kuvunja sheria na haki za watu? Hivi kwa sasa ni wapi Tanzania hakuna watu wa vyama vya upinzani ? Je,wanayoyafanya Polisi tangu kuanzishwa kwa vyama vingi yamekiimarisha chama cha mapinduzi au yamekidhoofisha ? Kama yamekiimarisha kwa nini hakiwezi kushindana kwa hoja na kupigiwa kura kwa haki?

Ni wazi polisi wameshindwa kuwa nyutro kwenye mfumo wa vyama vingi kabla na hata kwenye uchaguzi sasa nani ataingia kwenye uchaguzi wa watu wanaotumia polisi ili kushinda?

Je, ni ,mwanaChama yupi wa Chandema wa kawaida aliandamana juzi ?

Lakini Mwisho ni kwamba wasilie lie tu KWA SABABU ya ubaya wanaofanyiwa . Nchi za kiafrika zina mila zake za kulipa wanaofanya dhulma .

Mtu hawezi akamuumiza ndugu yangu bila kosa nikakaa kimya wakati kuna waganga ukimpa mil. moja tu anasambaratisha familia nzima ya aliyetenda ubaya yeye kama yeye. Amazika mpaka anakata tamaa na mwisho anaondoka yeye mwenyewe bila kuacha hata ndugu wa kusingiziwa.
Bila kulipa kisasi kamwe watenda mabaya hawataacha labda Mungu mwenyewe aingilie kati.
 
Inabidi waende wengi ikiwezekana nchi nzima kwa sababu wale wachache waliokwenda ambao ni viongozi wao tu wa Kanda na makao makuu .Walipoenda wao peke yao mkawapiga na wengine kuwaua na wengine mpaka sasa hawaonekani walipo.
Sasa mnataka nini kama sio kuua wengi na kuumiza wengi na kukamata wengi . Huenda umaarufu wa Polisi ili apate uteuzi ni kukamata Chandema wengi ,kuua Chandema wengi na kutesa na kujeruhi Chasema wengi na kuisababishia hasara serikali na jamii kwa kupoteza mabomu na risasi nyingi kwa manufaa ya yule MwanaCCM mmoja na familia yake kwa sababu tu katiba imempa Mamlaka ya kuua na kufanya anachotaka . Mamlaka aliyonayo anayatumia kuangamiza upinzani na wapinzani .

Sasa ili wamkamate na kuua wengi basi watakwenda wengi ili ama washinde au washindwe uhuru upatikane . Hakuna namna .
Huwezi kuwazuia viongozi wa Chadema kwenda kusikiliza Kesi ya mwenyekiti wao . Haijawahi kutokea Kokote hata kwa watu wabaya kama wakoloni labda wakoloni waarabu maana wao ndio hawana kumbukumbu popote ya waliyoyafanya mpaka wakafanikiwa kushika soko la kununua na kuuza binadamu . Yaani hatujui kabisa ilikuwaje mpaka Waafrika wakakubali kuwafanya ndugu zao kuwa bidhaa,Huku pembe za ndovu ,Madini vikibebwa na waarabu . Bila shaka walitumia rushwa kama CCM inavyofanya leo . Ardhi inauzwa ,Madini yanauzwa mpaka katikati ya hifadhi za wanyama ,umeme inanunuliwa kutoka nje wakati ndani upo , na utakosa wateja ,Bandari inauzwa na sasa Wataganyika wanauawa na kutishwa ili waifurukute huku rushwa ikitembiea kwa wataganyika ili waue na kufunga ndugu zao kama babu zao walivyofanywa na hao hao waarabu na sasa ni mjukuu wao anafanya haya ndani ya ardhi ya Tanganyika kwa Mamlaka aliyopewa na anayempinga anakula jambia la shingo .

Waafrika kama maana ya hizi dini na itikadi za kigeni ndio hizo za kuuana kwa sababu ya familia ya mtu mmoja hata kama anavuruga maendleo na ustaarabu wa taifa basi hizo dini ni ushetani mtupu na uovu usio faa popote mbingun na duniani.

Huwezi ukauwa watu wasio na hatia .
Kumwaga damu isiyo na hatia ni dhambi kubwa sana tangu mababu zetu mpaka Ukrsto japo usilam sijui kama kuua mtu asiye na hatia ni sawa au ni thawabu.

Watu hawarusha hata jiwe kwa polisi unawavunjaje miguu mpaka unaua ?
Hivi CCM imekua na watu au majini na mashetani wasioona hayo ?

Yaani kwa akili ya kawaida yule Mama polisi angepigwa jiwe na wananchi wale si angepiga bomu la nyuklia nakuua halaiki nzima kama anaua watu wasio rusha hata ngumi ?

Wakati CUF iliyokua inasadikiwa kuwa ni chama cha kiislam inapinga dhulma ni wazi kuwa Ilikua ni jino kwa jino na mapanga Shaa . Polisi kule Zanzibar walikua wanakatwa vichwa kama kuku . Wakahamia Mkuranga kwa mchengerwa wakati huo naye ni mkereketwa wa mapanga Shaa kabla ya kujitokeza kama CCM ,kule napo waliua polisi sana na wananchi wengi wa CCM na viongozi wao .

Leo Chadema inasubiri Haki na kuondoa sheria zenye kupendelea upande mmoja bila kutumia hata nyembe ,tena ,miongoni mwao kuna mpaka askofu Mwamakula bila kudhuru mmtu kwa amani kabisa kama Kristo alivyoagiza cha ajabu polisi na watawala wanaagiza wauawe tena . SASA CCM na Samia wanataka upinzani wa namna gani ? Wanataka siku CCM ikiondoka madarakani magereza yote yageuke kuwa nyumba za Makada wa CCM na wale waliosimamia ukatili wao ?

Ni wazi CCM haikubaliki kama Mwanzo . Samia hana mvuto wowote wa kisiasa hata kijamii .
Rais anafika mahali watu wanakwenda kwenye mkutano wake wa hadhara kwa rushwa !! Halafu Intelijensia yake haimwambii ukweli wala kuwaambia watu wake kuwa chama kitakufa na kuondoka na utawala wa Samia .

Chadema waende ikiwezekana wafikie hata milioni tano wajaze jiji la Dar es salaam wazunguke kila pahali sio barabara moja bali watawanyike barabara zote polisi wajikute wapo katikati mabomu wajirushie wenyewe.

Mikakati ya Chandema ndiyo ya kizembe ndio maana wanalia lia ,yaani wanawalilia wauaji . Yaani unamlilia na kudeka kwa mama wa kambo .
Wakoloni wanapenda sana watu wa afrika wanaowaza kama wewe. Ulaya na Marekanani wanaogopa sana nchi za China, NKorea na uarabuni ambako hakuna uhuru mpana wa kijinga wa kusema na kuchaguana kama vile wakoloni hawapo nyuma ya milango yao. Kupitia demokrasia pana ndimo wanapotumia kupenyeza vibaraka wao. Urusi ya Kisoviate walijaribu hilo wakakiona.

Afrika tusikubali demokrasia pana kama ya Ulaya na Marekanani maana gharama na hasara zake ni nyingi na kubwa sana. Ulaya bado inazihitaji rasilimali zetu saaaana, na bado wanahitaji masoko yetu kuuza bidhaa zao na bado wanahitaji nguvukazi yetu tangu Jana, Leo na hata kesho.
 
Nimewasikia viongozi wa cdm wakihamasisha wafuasi nchi nzima waende kwa wingi Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu, lengo hasa ni nini kuita watu wengi wakusanyike kwenye eneo dogo sana la mahakama ambalo liko kwenye maeneo yenye pilikapilika nyingi za watu? Tunafahamu kuwa chadema ina wafuasi wengi nchi nzima, vipi kama wote wataitikia wito wenu wa kwenda kusikiliza kesi Kisutu? Je, Kisutu ina eneo kubwa kiasi gani kutosha wafuasi wote wa chadema kukusanyika?

Ni serikali gani duniani itaruhusu jambo kama hilo litokee? Bila shaka mnajua kuwa watu wengi wataumizwa mbele ya camera za vyombo vya habari vya ndani na nje, je, lengo ni hilo? Hamuoni kama watu wakifa na kuuawa kwenye msongamano huo mtakuwa mmehusika moja kwa moja na kadhia hiyo?

Binafsi nimeamini ule msemo wa Rais Ali Hassani Mwinyi (RIP) kuwa "kunguru hana kibyongo, ukiona kibyongo kainama anaokota kitu, muwahi mapema kunguru kabla hajaruka nacho". Ukichelewachelewa huenda akaruka na kifaranga, kijiko na hata nguo yako ya ndani.

Lengo kuu nadhani ni kuichafua nchi mbele ya camera za wafadhili, maana walijua polisi itawatawanya kwa nguvu. Tusipoziba ufa tutapata M23 Tanzania..
CHADEMA KUKATAA UCHAGUZI IS A HISTORICAL MISCALCULATION. BAADA YA UCHAGUZI AMBAO HAWAKUSHIRIKI HAITAKUWA RAHISI KWA CHADEMA KURIKAVA MAANA KUNA UWEZEKANO MKUBWA KUTOKEA KWA MAKUNDI NAICHAFUKO YA NDANI YA CHAMA..DEAD END!!!
 
Back
Top Bottom