issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,788
- 5,217
Kama mnaamini/mnajua kuwa ni ngumu kwa CHADEMA kushika/kuingia madarakani kwa sanduku la kura naomba kukuuliza maswali yafuatayoWana bodi,
NI jambo la kujiuliza kama kweli wananchi ndio wanaodai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi au ni wanasiasa wanao tumia mbinu tofauti tofauti ku tekeleza wanacho hitaji. Vile vile ni vyema kama tukiji uliza swali lingine. Tangia mfumo wa vyama vingi ku anza Tanzania, je ilishawahi kutokea kwa chama cha upinzani kushindwa uchaguzi kwa sababu ya katiba au tume tuliyo nayo ya uchaguzi?
Nafikiri tukitafakari na kujiuliza maswali haya, tuta gundua kwamba kwa kiasi kikubwa, wahusika wote hawaku pata ridhaa ya wananchi.
Tuki jaribu kuangalia kama chama chenyewe kina kubalika na watanzania walio wengi tuna gundua kwamba kuna mambo mengi muhimu zaidi kuliko tume huru au katiba mpya vinavyo weza kuwa saidia kuwa na msingi nchini kwote. Ni muhimu kwa wao ku elekeza nguvu kazi kwenye kujenga chama chao kwanza
- Kwanini hamtaki kuruhusu uchaguzi huru na wa haki?
- kwanini mnaogopa kuwa na tume huru ya uchaguzi?
- Kwanini mnatumia nguvu kubwa yaJWTZ, Polisi, TISS, RCs, DCs, DEDS kupambana na chama kisicho na ushawishi?
- Kwanini mnaogopa kuruhusu mchakato w akatiba mpya?
- Kwanini mnaogopa hadi mnazuia vyama kufanya mikutano na shughuli za vyama zilizoko kisheria?