CHADEMA kukataa mualiko wa NEC wakati wanasubiri mualiko wa Rais Samia ni kichekesho

CHADEMA kukataa mualiko wa NEC wakati wanasubiri mualiko wa Rais Samia ni kichekesho

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Iko wazi Chadema na vyama vingine vilivyokataa kuhudhuria Mualiko wa NEC kwenye kutoa ripoti ya Uchaguzi wa 2020 sababu ilikuwa ni malalamiko yao juu ya wanachokiita dhuluma kwenye uchaguzi huo. WAMEKWENDA mbali zaidi hata wengine kugomea ruzuku, kugoma kupeleka majina ya wabunge wa viti maalum na kugomea chaguzi za marudio.

Kwa uwazi kabisa mtazamo wa CDM ni kuwa chaguzi za S/M 2019 na MKUU 2020 zilikuwa ni batili na walioshinda hawawatambui. Ajabu ya CHADEMA ktk hili ni uleule undumilakuwili wa "Sizitaki mbichi hizi" kwani inaonekana wako tayari kukutana na Rais Samia kwa ajili ya kufanya mjadala wa kisiasa sijui maridhiano ya kitaifa, they know much.

SWALI hapa wanataka kukutana na Rais aliyetokana na uchaguzi waliouita batili, What does that mean?. Maana yake hawatambui ushindi wa JPM/SSH mwaka 2020. Je wanataka kukutana na SAMIA yeye kama nani?. Kama ni Rais ameupata kutokana na uchaguzi upi?, je kama wanamambua hivyo kuna haja kutoutambua huo uchaguzi? It is just a logical fact!

CHADEMA katika kususia jambo bado wamefeli na wanafeli, mwaka 2015 walisusa na kutotambua Urais wa JPM na walifika mbali wakamuita Lowassa kuwa "Rais wa Mioyo ya Watanzania" (Sitaki kuongelea tena huu upuuzi wao maana huyu Rais amerudi kwao kumenoga). In the end bado walikuwa wanajipendekeza kutaka maridhiano mara kutaka kuonana na JPM ili kusikilizwa kilio chao wakati hawakumtambua kama Rais. Funny indeed

Kuna mawili ambayo CDM yanawashinda na wataendelea kuwa Ndumilakuwili mpaka kesho baada ya kuamua moja:-
1. Kama unasusa basi susa mazima ijulikane UMESUSA KIUME NA UNA MSIMAMO kisha dai tume huru KWA NGUVU ZOTE.
2.Show some respect kisha omba kukutana na RAIS ufikishe kilio chako awasikilize shida zenu.

Zaidi ya hapo ni Undumilakuwili na kuendelea kuonekana hawana msimamo . UNAMSUSIA KUKU WAKATI MAYAI YAKE YANAKUTOA MATE.

 
UPUUZI MTUPU!!! unakutana na NEC wakitangaza uhuni wao waliofanya 2020 ili iweje!? Ukasikilize wakizungumza kuhusu wizi wao kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki wakati ukweli tunaujua?
 
Bwashee, hata huko kwa rais wameshaghairi asipokutana nao peke yao. Akiwaweka kwenye kundi la vyama vyote basi hawaendi!
Ujinga uliomo chadema sasa hivi hata kwa fimbo hatuwezi kuutoa.

Na hilo la kujiona wao ni bora na muhimu kuliko vyama vingine vyote vya upinzani litaendelea kuwakwamisha miaka nenda rudi, kwasababu vyama vingine vitaendelea kutowapa ushirikiano katika madai yao yote. Hiki ni chama ambacho hakina political strategists kabisa; kimejaa watu wa mitulinga tu. Utadhani Jeshi la Sungusungu!
 
Kumbuka kuna "cause and effect"--- Samia kuwa Rais ni effect lakini Cause yake ni NEC, sasa Chadema watakuwa wajinga kulaumu effect na kuacha kulaumu Cause na kutafuta njia ya kudumu kudhibiti cause kama hiyo ili effect ya aina hiyo isijetokea tena.

Mfano ni huu; huwezi kuwalaumu wote mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa na wazazi waliomzaa bali wazazi ndio wa kulaumiwa, sasa hatuwezi kuwalaumu Wote Samia aliyepewa urais na NEC bali NEC ndio mlaumiwa kwa kukiuka wajibu wake kisheria na njia mojawapo iliyopo ya kudai na kulalamika ni kupitia huyo huyo mtoto wa NEC Rais Samia.
 
Ni kwa mwenye ufinyu wa akili tu ndiyo anaweza kuandika hivi. Mpaka hapo nchi itakapoingia kwenye machafuko ya kutisha kwa UCHAFUZI wa uchaguzi ndiyo mtatia akili kichwani.


machafuko si mnayaombea kila siku? Mbowe yuko ndani nani anaandamana kumtoa?

usiwasemehe watanzania, wako tofauti mno na a akili yako..

machafuko??? my foot
 
Na hilo la kujiona wao ni bora na muhimu kuliko vyama vingine vyote vya upinzani litaendelea kuwakwamisha miaka nenda rudi, kwasababu vyama vingine vitaendelea kutowapa ushirikiano katika madai yao yote. Hiki ni chama ambacho hakina political strategists kabisa; kimejaa watu wa mitulinga tu. Utadhani Jeshi la Sungusungu!

Lissu anajiita mandela, mbowe sijui mugabe, na Lema anajiona ni Gandhi
 
UPUUZI MTUPU!!! unakutana na NEC wakitangaza uhuni wao waliofanya 2020 ili iweje!? Ukasikilize wakizungumza kuhusu wizi wao kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki wakati ukweli tunaujua?
Samia si katokana na huo uchaguzi batili? Hiyo ina maana urais wake ni batili pia, then why mnataka kuonana na Rais batili?
 
Back
Top Bottom