Hawa ndugu zetu CHADEMA ni watu wasioeleweka. Wana tabia ya kwenda mahakamani wakiwa na majibu yao mfukoni, wao hujitia ujuzi wa sheria kuliko mtu yeyote yule.
Kwenye shauri la Mbowe, Jaji Siyani katoa hukumu kwa kesi ndogo katika ya Mbowe, wao wanadai hawajaridhika na tayari wameanza kuitishia Mahakama (rejea kauli za Mnyika leo)
Kama haitoshi wanapiga kelele wakijaribu kumshinikiza Rais Samia eti aingilie kati kesi hiyo...JAMANI. Watu wale wale wanaotaka Mahakama iwe huru ndio wanataka Rais aingilie kati?
Kama ujumbe huu utafika kwa Rais Samia, tunamuomba aendelee kutowajibu chochote watu hawa. Atulie hivyo hivyo na kuacha Mahakama ifanye kazi yake. Kama Mbowe ana hatia ataenda zaidi ya miaka 15 jela, kama hana hatia atarudi mtaani ila sio kwa amri ya Samia.
Bi Samia Rais wetu, wewe chapa kazi, hili la kina Mbowe waala lisicheze mishipa yako.