Huku sasa kwa wanaCHADEMA ni kupaniki na hii ni baada ya Caution statement za mmoja wa watuhumiwa wenzake na Mbowe kupokelewa kama ushahidi mahakamani.
Kwa nini Mnyika J, anasahau na kutoa kauli za ajabu ambazo hazina mashiko? Kesi ipo mahakamani na rais hana mamlaka ya kuingilia muhimili wa mahakama. Lakini Mnyika anaomba rais atoe neno ili kesi ifutwe. Hii ni sawa?
Kama chama makini nilitegemea kipambane Mahakamani ili kuwashinda Jamhuri, lakini sio kuomba msaada kwenye tuta wakati wanajua mhimili wa mahakama upo huru. Hii inaanza kutia shaka huenda watuhumiwa wanakosa.
My take: Mambo ya Mahakama tuwaachie mahakama.
Mahakama hazipo huru Tanzania,hukumu kama Zina maslahi na Serikali,mahakimu,majaji huwa hawafati sheria,husubili maelekezo ya Serikali,sasa watu kama wewe kujifanya Hilo hamlijuhi,na kutaka kutuaminisha kwamba mahakama zetu zipo huru kama za nchi zingine,mfano Israel,South Afrika,Zambia,USA,au UK,ni ukichaa.
"Mkurugenzi,nikupe ajira, nikupe gari,harafu umtangaze mpinzani kwamba kashinda"hayo ni maneno aliyoyasema Shetani Jiwe(JPM),wote tunajua kilichofuata kwenye uchaguzi,wizi na ubakaji wa demokrasia.
Harafu mpuuzi mmoja anakuja hapa anataka atuaminishe mahakama zinatenda haki pale ambapo serikali ina maslahi na kesi husika.
Serikali Haina maslahi na kesi ya Sabaya,inataka ashindwe na afungwe,
Kwenye kesi ya Mbowe,serikali inataka kushinda kwa lazima,lazima itacheza lafu tu