CHADEMA kupoteza halmashauri zote inazoziongoza kabla ya mkesha wa mwaka mpya mamia ya madiwani wake kuhamia CCM

Baada ya hapo mwananchi wa kawaida anayetembea Km 6 kutafuta maji ndo atayapata bila shida?

Au leta faida atakazozipata mwananchi wa kawaida ambazo amezikosa kutokana na hizo Halmashauri kuwa chini ya Chadema.
 
Lkn kwa vyovyote iwavyo siyo rahisi madiwani na wabunge wa upinzani kuhimili vitisho na mipango ya kuwafukarisha wanayo fanyiwa kila uchwao. Ni vema waunge mkono juhudi za jiwe a.k.a kichwa korosho
 
Kauli hizo mbili zinakinzana. Panga upya ngano na soga zako kisha urudi tena hapa.
Wewe ndio unayejichanganya madiwani wanaanza kuhamia CCM kuanzia kesho.......wabunge ndio wanaosubiri assessment ya bungeni mwezi April 2020!

Uwe unaelewa bwashee!
 
Baada ya hapo mwananchi wa kawaida anayetembea Km 6 kutafuta maji ndo atayapata bila shida?

Au leta faida atakazozipata mwananchi wa kawaida ambazo amezikosa kutokana na hizo Halmashauri kuwa chini ya Chadema.
Waulize jimbo la Kinondoni au Singida mashariki watakushuhudia!
 
Hahahaaa........ Chadema ndio inaishia hiyo!

Mngeumaliza umaskini,ujinga na maradhi ,Watanzania wangewaelewa.

Tatizo mmewekeza sana kwenye kuua upinzani kitu ambacho hamtoweza kamwe,,liwake jua mvua inyeshe upinzani upo tu, hata ndani ya familia yako.
 
Wewe ndio unayejichanganya madiwani wanaanza kuhamia CCM kuanzia kesho.......wabunge ndio wanaosubiri assessment ya bungeni mwezi April 2020!

Uwe unaelewa bwashee!
Hill fungu litakuwa kubwa sana, maana hakuna uchaguzi tena hadi mwakani
 
Usilifurahie hili jambo. Kama lipo kwanza ni aibu kwa chama dume ka ccm kuua upinzani kwa vyovyote vile. Chama kikubwa hivi kingewakatalia hao wanaotaka kujiunga nao kiwape ruhusa kuanzisha chama kipya halafu kiwe kinawapinga hao CDM.
Kiwaruhusu wajinyonge wenyewe. Kiongozi mzuri ni yule awezaye kubuni mbinu za kumwongoza mpinzani akiwa mnyonge daima.
 
Mngeumaliza umaskini,ujinga na maradhi ,Watanzania wangewaelewa.

Tatizo mmewekeza sana kwenye kuua upinzani kitu ambacho hamtoweza kamwe,,liwake jua mvua inyeshe upinzani upo tu, hata ndani ya familia yako.
Upinzani wa kweli siyo rahisi kuuliwa lakini huu wa ruzuku mbona simple tu!
 
JB, tuachane kidogo na siasa zetu hizi...... unadhani hii ina tija kwa maendeleo yetu kama watanzania!?......
 
Siyo kwamba nafurahia mkuu...... Sasa wewe unaelewa historia ya JJ Mnyika kwa mfano hadi umtake aanzishe chama chao?!
 
Ni jambo jema sana hili!

CHADEMA itajifunza kupitia hili, wengi wa hao watakua ni wale waliovutwa na nguvu ya mabadiliko mwaka 2015 ambapo CDM ilivamiwa na wimbi kubwa la watu wachumia tumbo ambapo ilikua ni ngumu kwa CHADEMA kuwatambua kwa haraka kutokana na vuguvugu lile, hivyo wanapoamua kurejea kwao walipotoka maana yake ni kwamba CHADEMA inarudi kujijenga upya kwa kupata wanachama halisi watakaokubaliana na joto la kisiasa lililopo wakati huu na hawa ndio watakua makamanda halisi.

Ni hasara kwa wanachama wa CCM waliokaa ndani ya chama kwa kipindi kirefu wakipigania chama kwani itabidi wao waendelee kukipigania chama na kukubali kupisha fursa kwa wageni hawa wanaokuja.

Iwapo kutakua na uchaguzi, taifa litaingia hasara tena lakini nafurahi kwa vyama vya upinzani kususia ili kupunguza gharama hizo na kuokoa muda labda kwa hawa wabunge ndipo tutapata hasara kuwalipa watu fedha.
 
JB, tuachane kidogo na siasa zetu hizi...... unadhani hii ina tija kwa maendeleo yetu kama watanzania!?......
Kimsingi haina tija kabisa........ Lakini ni ujinga kuwa na Upinzani unaogharamiwa na serikali kwa kila kitu.

Kiongozi yoyote mwenye maono hawezi kulea aina ya upinzani kama huu wa Tanzania....... Yaani serikali ikupe ruzuku kwa kazi ya kuitukana na kuikwamisha?!
 
Itasaidia nini Taifa!!? Mbona huna furaha ka Bondia aliyepigwa na Mfilipino na kushinda yeye...mgosi vipi?
 

Mzee Mgaya na Mchungaji Erasto nao wamesemaje? Huo usiku wa mwaka mpya ni mbali, wahamie hata usiku huu, uzuri ni kuwa hatuko upinzani kwa ajili ya kuwafuata wao. Wanaweza kwenda ccm muda wowote, lakini msimamo wetu ni dhabiti na hatushawishiki kwa lolote na wao.
 
Kuna tofauti ya kuelimika kati ya wale wa awamu ya 4 na hii awamu ya tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…