GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
nadhan NCCR yuko juu zaidi maaana chadema peak yake ni lowasa ambae alitoka ccm sio kwamba chadema iliandaa mtu
Cdm ilikuwa na nguvu kabla ya Lowassa kumuhonga Mbowe. Na cdm imeendelea kuwa na nguvu baada ya yule mzee taplii kuondoka. Toka 2016 hadi sasa huwezi kupima maana siasa za sasa zinafanywa na vyombo vya dola, na chaguzi ni za kishenzi.
 
Huyu alikuwa mkurugenzi wa tume ya uchaguzi uchafuzi 2020.

Halafu bado mwanalumumba mwingine unasema CHADEMA imekuumiza kwa kutoshiriki upuuzi.

4R za mama yenu mojawapo ni REFORMS.

Ila ajabu kwenye kufunga bunge anawaambia polisi ndio wajiandae, kwani ndio wapiga kura?
IMG-20250629-WA0000.jpg
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
Wanaweza kubadili gia Agani!
 
Je huko Marekani aliyetakakumuua alikamatwa au aliachiwa? Umewahi kusikia kuna mpinzani ametekwa na kuuliwa kisa kukosoa serikali? Twende Tanzania hayo ya watu kutekwa na kuuliwa kila kukifikia kipindi cha Uchaguzi huyaoni toka 2017 mpka sasa yanaendelea ni nani aliwajibishwa kwa makosa ya utekaji hapo Tanzania?
Marekani ni habari ingine... kumbuka Epstein aliuawa akiwa cell. Wanawaua sema kwa akili au unatengenezewa kesi ya kukuweka jela maisha
 
Hata Trump alidai uchaguzi uliibwa lakini hakususa akajitosa tena ingawa mara hii alikoswakoswa kuawa. Kama USA wanauana unashangaa nini Afrika kuyaona hayo? Siasa hamziwezi bhna mmevamia tu mtumbwi wa vibwengo.
Usilinganishe hakuna na hakuna kabisa kwani jibu ni hakuna! Kama nafsi yako ni safi hebu niambie ungekuwa wewe ndiye cdm ungepeleka wagombea wako wakatekwe, wakauawe na hata kudhulumiwa kimwli kwa sababu ya kugombania ubunge, urais na udiwani? Na kwa Sheria hizi za sasa umezisoma na kuzielewa? Na hiyo tume ya uchaguzi si ni mali ya mgonbea urais? Hebu jitambue na uache kusumikiza watoto wa watu kwenye tanuru la moto! Kuwa na huruma kidogo.
 
Cdm ilikuwa na nguvu kabla ya Lowassa kumuhonga Mbowe. Na cdm imeendelea kuwa na nguvu baada ya yule mzee taplii kuondoka. Toka 2016 hadi sasa huwezi kupima maana siasa za sasa zinafanywa na vyombo vya dola, na chaguzi ni za kishenzi.
cdm haijawahi kua na nguvu bila lowasa, kipindi mmepata wabunge wengi ilikua kipindi icho icho cha lowasa na alivoondoka mlidhoofika sana, mule mule watu walianza kuhama na baada ya JPM kuanza kazi ndo kabisaa mlivua non existent, najua tunafanya siasa utajitahidi kupindisha ukwel
 
Mbona term hii inayoisha walibali ccm tu kwani chadema ilisusia 2020!? Na maamuzi yote ccm wameyafanya. Kumbe raha ya uchaguzi ni kuwana chadema wanapigwa kata funua, safari hii wameamua kupumzika wasubirini 2030 wakati urais hauna mwenyewe.
Shida ni pale hata kama wakishinda wanahamia CCM kwenda kuunga juhudi na kusababisha taifa kuendesha chaguzi ndogo kwa gharama nyingine. Kwakuwa haifahamiki nani ataenda CCM kuunga juhudi ni heri kuwaengua wagombea wote hadi hapo watakapotajana.
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
Una uhakika kabisa ulichokiandika.Hv unajua kwamba NO REFORMS NO ELECTION NDIO DAWA PEKEE YA KURUDISHA IMANI YA WANANCHI KTK KUCHAGUA VIONGOZI.
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
Hata kama wangeshiriki si rahisi kushinda kwa sheria za tume huru ya uchaguzi ya mwaka 2024.Ukiwa wakala katika kituo cha kura huruhusiwi hata kuwa na simu ya kumjulisha mgombea wako kiasi alichopata.Nakala ya matokeo utapewa iwapo tu kutakuwa na nakala za kutosha.Inachekesha sana
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi.
Wakati wa ukoloni TANU walishiriki uchaguzi gani? Ufafanuzi please?!
 
Hata kama wangeshiriki si rahisi kushinda kwa sheria za tume huru ya uchaguzi ya mwaka 2024.Ukiwa wakala katika kituo cha kura huruhusiwi hata kuwa na simu ya kumjulisha mgombea wako kiasi alichopata.Nakala ya matokeo utapewa iwapo tu kutakuwa na nakala za kutosha.Inachekesha sana
Na kushangaza pia
 
Wakoloni hawakuiba kura, walishawishi vyama wavitakavyo kuungana dhidi ya chama wasichokitaka.
Wanaiba bwana. Kule Ulaya Sasa hivi wakiiba kura wanasingizia Urusi imeingilia mifumo yao ya uchaguzi na kugomea matokeo. Dunia nzima Kuna shida kwenye chaguzi hata kule ambako demokrasia imeota mizizi.
 
Unamlinganisha mkoloni na ccm? Mkoloni alikuwa malaika mbele ya ccm.

Ukitaka kuamini mrudisheni mkoloni mwingereza au mjerumani aje agombee uongozi apambane na ccm uone nani atachaguliwa kwa kishindo.!
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
Wakoloni walikuwa hawawaengui wapinzani wao kwahiyo wakoloni walikuwa ni bora zaidi chaguzi zao kuliko hizi
 
OLE WAKE MWANANCHI ATAKAYE ENDA KUPIGA KURA
OLE WAKE MWALIMU ATAKAYE SIMAMIA UCHAGUZI
OLE WAKE MGAMBO ATAKAYE SIMAMIA UCHAGUZI

NO REFORMS NO ELECTION
Labda itakuwa no erection
 
Je huko Marekani aliyetakakumuua alikamatwa au aliachiwa? Umewahi kusikia kuna mpinzani ametekwa na kuuliwa kisa kukosoa serikali? Twende Tanzania hayo ya watu kutekwa na kuuliwa kila kukifikia kipindi cha Uchaguzi huyaoni toka 2017 mpka sasa yanaendelea ni nani aliwajibishwa kwa makosa ya utekaji hapo Tanzania?
Siamini kama Kila anaekosoa serikali anatekwa na kuuliwa. Heche, Lissu, zitto, mnyika, mbatia, rungwe, nk mbona wako hai hata baada ya kuikosoa serikali?
 
Back
Top Bottom