GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?

Acha propaganda Uchwara. Bora Mkoloni alikuwa walikuwa na huruma. MaCCM hayafanyi uchaguzi bali uchafuzi na hayana huruma, wala haya. Yanajitangaza tu kama yanayotaka hata kubalance kura yanashindwa.
 
Kila mwaka wa uchaguzi Chadema wana;
1. Uwawa.
2. Wanatekwa.
3. Wanaharibiwa Mali zao.
4. Wanapewa kesi za uongo.
Halafu Bado washiriki uchaguzi huo bila mabadiliko!? Hapana aisee chadema wako sahihi wamewaepusha watu wao na madhila hayo.
 
Ni mpumbavu tu atakaye weza kushiriki kupiga kura ambayo haina thamani mbele ya TISS na POLISI WA CCM
Mbele ya DEDs wana ccm
No reforms no election
Ila upumbavu huu tumeuruhusu sisi wenyewe! Hawa ma-DED na hao wengine tunakaa nao mtaani tungekuwa tumetoa fundisho wasingerudia!
 
Good si mnataka kumsikiliza Lissu.

Ambae serikali imemuonea kumpa kesi ya uhaini.

Lakini angekuwa na kesi ya msingi ya icho jęzor na kumfunga kabisa atie akili kwa uropokaji wake.

Movement ya NRNE lengo lake ni kuzuia uchaguzi, haya tuone hiyo support ya CDM ya kuzuia uchaguzi.

Asilimia kubwa ya watanzania wanaona CDM ni mataahira tu, sio kwamba wanaifurahia CCM.
 
Kaka inatia hasira sana kwasisi ambao hatuna hata passport za kusafiria kumsikia na kumuona mtu anapiga bomu ambalo litaumiza na kuua watanzania wenzake huku yeye akiwa ameificha familia yake sehemu salama nje ya nchi. Taifa limelazimika kuajiri askari wengi sana wakati huu na hata waliostaafu wamezuiwa kistaafu hadi uchaguzi upite, utawezaje kuzuia uchaguzi usifanyike bila watoto wa wenzenu kuumia sana?

Kaka hawawezi hawa, kama wangeweza wangeshamtoa mwenyekiti wao kule aliko . Kama makaburu, wareno na alshabab walishindwa kututikisha sembuse hawa wakina naniliu?
 
Acha ptopsganda Uchwara. Bora Mkoloni alikuwa. MaCCM hayafanyi uchaguzi bali uchafuzi. Yanajitangaza tu kama yanayotaka hata kubalance kura yanashindwa.
Hata wakishinda wanarudi CCM kuunga juhudi, hawaaminiki. Kwani akina Nasari, Prof mkumbo, mtolea, Kafulila, Dr. Slaa na wengi tu si wamerudi CCM na wengine walirudi wakiwa wabunge? Upinzani bado kabisaaa. Wanadhani upinzani ni kupinga Kila kitu na Kila jambo la serikali. Kama yupo mtu ambae wapinzani walipaswa kumlaumu kuhusu Katiba hii ni Nyerere aliyetuachia hii Katiba na UKAWA waliosababisha Katiba mpya yenye nafuu isipatikane.
 
Hivi taja wakoloni wakati wa TANU waliteka watu wangapi, waliua watu wangapi, yaani huu unyama wewe hujauona tu? Unalingasha hawa wauaji na wakoloni?
Mimi Sina uhakika nani aliwateka na sababu ya kuwateka. Lakini kama aliyewateka alikuwa anazuia mipango ya watu kuiingiza Tanzania pia iwe kama DRC, Somalia, Sudan, msumbiji, Niger, Nigeria, Mali, Burkina Faso, au Ethiopia ni sawa tu NAMI nampongeza.

Tupende amani na maendeleo zaidi kuliko demokrasia pata isiyokuwa na tija. China na uarabuni hakuna demokrasia pana sana lakini nchi zao zinaendelea na watu wao wanakula Bata.
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
Serikali ya kikoloni ilikua na tume huru kuliko hii ya sasa. Hata wakoloni walijenga Barabara, reli, shule, mahospitali, miundombinu ya maji na umeme kuliko hawa wa sasa.
 
cdm haijawahi kua na nguvu bila lowasa, kipindi mmepata wabunge wengi ilikua kipindi icho icho cha lowasa na alivoondoka mlidhoofika sana, mule mule watu walianza kuhama na baada ya JPM kuanza kazi ndo kabisaa mlivua non existent, najua tunafanya siasa utajitahidi kupindisha ukwel
Lowassa nguvu aliikuta cdm, kama yeye ndio alileta viti vile akiwa na miezi miwili, alileta viti vingapi akiwa na miaka miwili? Ama unadhani hatuujui ukweli? Baada ya uchaguzi wa 2010, cdm ndio chama kilichofanya siasa za hamasa kuliko chama chochote. Na wakati hayo yakifanyika Lowassa alikuwa ccm. Lowassa awe na nguvu wakati hata kusimama jukwaani alikuwa hawezi. Utakuwa unaumwa ww.

Baada ya uchaguzi wa 2015, hakukuwa na siasa za ushindani tena, maana mlevi wa madaraka na asiyeweza siasa za ushindani alikuwa madarakani. Na ushahidi kuwq dhalimu magu alikuwa hawezi ushindani ni ule uchaguzi wa kihayawani wa 2020.
 
Back
Top Bottom