GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hakuna chadema waliosusia uchaguzi, mlitafakari sana hilo kwa mapana yake.
Mzitafakari kwanza hoja zao ndio mje na majibu yenu
 
Lowassa nguvu aliikuta cdm, kama yeye ndio alileta viti vile akiwa na miezi miwili, alileta viti vingapi akiwa na miaka miwili? Ama unadhani hatuujui ukweli? Baada ya uchaguzi wa 2010, cdm ndio chama kilichofanya siasa za hamasa kuliko chama chochote. Na wakati hayo yakifanyika Lowassa alikuwa ccm. Lowassa awe na nguvu wakati hata kusimama jukwaani alikuwa hawezi. Utakuwa unaumwa ww.

Baada ya uchaguzi wa 2015, hakukuwa na siasa za ushindani tena, maana mlevi wa madaraka na asiyeweza siasa za ushindani alikuwa madarakani. Na ushahidi kuwq dhalimu magu alikuwa hawezi ushindani ni ule uchaguzi wa kihayawani wa 2020.
hehehe Tindo najua hupendi kuskia ukwel ila chadema haijawahi kua na nguvu kwenye siasa za tanzania na haiwezi kua na nguvu kwa sababu hakina dira ya siasa zake, nyie ni wanaharakati, ikitokea corona mpo nayo, saahv gwajima mpo nae ieleweke kuna tafauti ya siasa na harakati, ccm kazi yake ni kuhakikisha anashinda uchaguzi nyie kazi yenu ni kufoka 🤣 🤣

turudi kwenye mada, kipindi cha 2015 ni kwa sababu ccm kulikua na rushwa nyingi sana ila sio kwamba mlikua na dira ya siasa, hivo basi hilo tatizo lishaisha kwahio kilichobaki ni nyie kudandia kila trend saahv, siasa haiko ivo and tunafurahi jinsi hamna dira
 
Tulia dada angu acha hii mada wachangie watu wenye akili timamu
Sawa mama angu lakini kuuweka uwanja level rudisheni familia zenu hapa ili mkikinusha sisi wote tupo hapahapa tz. Kama mtu akitangazwa kuwa kafa kwenye no reforms no erection lazima tutawasaka akina naniliu pia.
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
kataa ujinga kubali maarifa
 
Hakuna chadema waliosusia uchaguzi, mlitafakari sana hilo kwa mapana yake.
Mzitafakari kwanza hoja zao ndio mje na majibu yenu
Kosa kubwa la cdm ni kumlaumu sana Samia kuhusu Katiba hii na tume hii ya uchaguzi badala ya kuwalaumu saaaana Mwl Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, Mzee Kikwete, UKAWA na Mzee Magufuli kwa kuandika Katiba kama hii, kuitumia na kushindwa kuandika Katiba mpya hadi Le. , hoja ya muungano waliokujamayo UKAWA ndiyo iliyosimamisha uwandishi ya katipa mpya. Kama UKAWA watatushupalia tena muungano wa mkataba au serikali tatu katiba itakwana tena.

Huyu mama anatekeleZa amepatikana na anatenda kwa mujibu wa Katiba aliyoiacha Mwl Nyerere, mtanganyika. Katiba yetu Ina vionjo kutoka kwenye Katia ya china na Soviet, msilisahau hilo.Hata wanausalama wetu wamejifunza namna ya kuilinda nchi yao kutoka China, Urusi, Korea, Cuba, Ulaya mashariki na Magharibi kidogo sana. Kwani China demokrasia yao Iko kama ya ubelgiji? Mama mkanye mwanao.
 
Lakini mkuu wakigombea wanaanza kuuliwa na kutekwa
Mkuu Wacha uongo. Nani aligombea akauwa? Wote unaowaona wanatukana serikali walishawahi kuwa wabunge na wengine waligombea Urais mara dhaa na bado wapo tu, mbona hawakuuliwa. Kuna watu wanajiita wakimbizi huko nje na madai yao ni kwamba tz hakuko salama. Ili wazunguzu waamini kuwa tz sio salama lazima Kuna jambo watapenda litokee mbele ya camera . Wanashiriki kuteka na kuua watu ili kuhalalisha kuendelea kuwa wakimbizi. Kuna wakati wanaichokoza serikali makusudi ili wapigwe mbele ya camera
 
Chadema ni brand kubwa hata magazeti hayatauza saana
 
Mkuu Wacha uongo. Nani aligombea akauwa? Wote unaowaona wanatukana serikali walishawahi kuwa wabunge na wengine waligombea Urais mara dhaa na bado wapo tu, mbona hawakuuliwa. Kuna watu wanajiita wakimbizi huko nje na madai yao ni kwamba tz hakuko salama. Ili wazunguzu waamini kuwa tz sio salama lazima Kuna jambo watapenda litokee mbele ya camera . Wanashiriki kuteka na kuua watu ili kuhalalisha kuendelea kuwa wakimbizi. Kuna wakati wanaichokoza serikali makusudi ili wapigwe mbele ya camera
Kwanini usimwambie mumeo agombee kupitia upinzani tuone?
 
Sawa mama angu lakini kuuweka uwanja level rudisheni familia zenu hapa ili mkikinusha sisi wote tupo hapahapa tz. Kama mtu akitangazwa kuwa kafa kwenye no reforms no erection lazima tutawasaka akina naniliu pia.
Poa dada angu
 
Hivi chadema ni wakumpokea tena Dr.slaa? Mtu aliyekisulibu chama na kuhamia CCM na kupewa ubalozi!!!
Amepokelewa baada ya kuomba msamaha, tena kaomba hadharani. Na amepokelewa na kuwa mwanachama wa kawaida na sio kiongozi. Huko ccm mbona mnawapokea wengi tu waliohama na kuamua kurudi?
 
hehehe Tindo najua hupendi kuskia ukwel ila chadema haijawahi kua na nguvu kwenye siasa za tanzania na haiwezi kua na nguvu kwa sababu hakina dira ya siasa zake, nyie ni wanaharakati, ikitokea corona mpo nayo, saahv gwajima mpo nae ieleweke kuna tafauti ya siasa na harakati, ccm kazi yake ni kuhakikisha anashinda uchaguzi nyie kazi yenu ni kufoka 🤣 🤣

turudi kwenye mada, kipindi cha 2015 ni kwa sababu ccm kulikua na rushwa nyingi sana ila sio kwamba mlikua na dira ya siasa, hivo basi hilo tatizo lishaisha kwahio kilichobaki ni nyie kudandia kila trend saahv, siasa haiko ivo and tunafurahi jinsi hamna dira
Matamania yako ndio ukweli? Inaonekana hujui tofauti ya chama na mashabiki wa mitandaoni, ndio maana una hoja hizi zilizochoka. Chama ni vikao, ni wapi umeona cdm kama chama wamekaa na kuongelea hayo mambo unayosema? Jifunze kutofautisha chama, na mashabiki wa mitandaoni. Ukishajua uje tuendelee na mjadala.

Ccm ingekuwa na dira, nchi hii isingekuwa moja ya nchi masikini duniani. Huenda hujui unaongea nini zaidi ya kuwa bendera fuata upepo.
 
ukwel unauma ila unatakiwa ubebe kama ulivo, chadema lengo lake ni ruzuku hakina mpango wa kuongoza nchi na pia kama mlikua na nguvu kuliko lowasa kwann mlimfitini slaa ambae mlitoka nae mbal?

kwann mlisubiri mgombea wa ccm atangazwe na nyiie ndo mtangaze mgombea kama sio mlikua mnasubiri nguvu yake 🤣 , na mbna jimbo la lissu mpaka leo halina maendeleo kama alikua anauweza ubunge 🤣🤣! finished party
 
CHADEMA hawawezi kukiri eanashindwa kwa sera za matusi za Liddi. Mbona Dr Slaa na Lowassa walipata kura nyingi you mfumo huu huu? Tatizo no Lissu kutokukubalika.
 
ukwel unauma ila unatakiwa ubebe kama ulivo, chadema lengo lake ni ruzuku hakina mpango wa kuongoza nchi na pia kama mlikua na nguvu kuliko lowasa kwann mlimfitini slaa ambae mlitoka nae mbal?

kwann mlisubiri mgombea wa ccm atangazwe na nyiie ndo mtangaze mgombea kama sio mlikua mnasubiri nguvu yake 🤣 , na mbna jimbo la lissu mpaka leo halina maendeleo kama alikua anauweza ubunge 🤣🤣! finished party
Kama lengo lake ni ruzuku si wangekubali kushiriki huu uhuni uitwao uchaguzi sasa? Ama hujui unaongea nini? Nilishakuambia si kila mfuasi wa cdm alikubaliana na ujio wa Lowassa, Mbowe na genge lake ndio walimpokea kwa maslahi yao binafsi.

Kutangaza mgombea kila chama kina utaratibu wake. Nakuuliza Lowassa alikuwa na nguvu gani, maana hata kusimama jukwaani dakika 5 alikuwa hawezi. Nimekuambia kama aliwezesha cdm kupata viti vingi akiwa na miezi miwili, alipokuwa na miaka miwili alileta vingapi? Sioni jibu, naona unajichekesha tu.

Ukiona hilo jimbo lina umasikini basi ujue tatizo ni serekali na sio mbunge. Mbunge hapeleki maendeleo popote maana maendeleo sio kazi ya mbunge. Ukipenda naweza kukusaidia kazi za mbunge ni zipi. Isitoshe Tanzania ina miaka zaidi ya 60, Lisu amekuwa mbunge kwa miaka 10 tu, hiyo 50 ilikuwaje hilo jimbo lisipate maendeleo?
 
Ni sawa tu, kwa yaliyotendeka ktk uchaguzi wa serikali za mitaa ni bora kukaa miaka 50 bila uchaguzi.
 
TANU haijawahi kususia uchaguzi hata kama walikuwa wanajua kuwa wakoloni hawatawatendea haki kwenye chaguzi. Kushiriki mara nyingi kunasababisha yule anaeshiriki na kushindwa kugundua njia mpya za kuziba mianya ya kushindwa kwake na yule anaeshinda kila siku kusahau kuziba mianya yote ya kushindwa.

Mwanasaikolojia B.F. Skinner alikuja na falsafa yake ya kujaribu sana mara nyingi ili kufanikisha (operant conditioning). Ukijaribu kitu maranyingi iko siku utafanikisha tu. TANU ilijaribu mara nyingi kuingia kwenye chaguzi zilizokuwa zikisimamiwa na wakoloni na siku moja wakafanikiwa.

Misemo ya Mvumilifu hula mbivu, subira huvuta heri, mwenda pole hajikwai, hasira za mkizi tijara kwa mvuvi na hasira hasara ni kielelezo kuwa harakaharaka haina mbaraka.

Sheria, sera na mipango yote huwa inapitishwa bungeni. Bungeni ndiyo sehemu ambayo inatakiwa iwe na nguvu kubwa ya wabunge kutoka upinzani, sio Ikulu (kwa sasa). Kususia uchaguzi sio tu ni hasira za mkizi lakini hata wananchi wataumia sana kwa CCM kubaki wenyewe bungeni kupitisha chochote bila hofu.

Nani alipendekeza wazo la kususia uchaguzi pale chedema?
Umenena vyema. Hivi Chadema Wana ubavu gani wa kusema Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ulikuwa mbivu wakati hawajashiriki?
 
Back
Top Bottom